RC Makonda akishiriki Katika ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Ukonga zinazomaliziwa na SUMA JKT .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimsikiliza Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Julius Ntambala, wakati wa hafla ya Mkuu wa Mkoa kwenda kutembelea majengo yanayojengwa kwaajili ya makazi ya askari magereza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, (kulia) ni Brigedia Jenerali, Charles Mbuge, kutoka Makao Makuu ya JKT, ambae pia ni Mkuu wa mradi wa ujenzi wa nyumba za askari magereza na maofisa wengine kutoka jkt na magereza
Baadhi ya Majengo yanayojegwa na Jkt
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka watumishi wote wa Serikali kuacha majungu Pamoja na fitina na badala yake kufanya kazi kwa bidii ili waweze kupandishwa madaraja.
Akizungumza Leo na waandishi wa habari Katika mwendelezo wa Ziara yake Katika mkoa huo RC Makonda ametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Askari Magereza Pamoja na maafisa Ukonga yanayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwili,ambapo ujenzi huo walipewa SUMA JKT baada ya kampuni ya TPA kusuasua katika kujenga Nyumba hizo.
"Watumishi wa Serikali tunapasawa kuacha uzembe ,Tuache majungu tufanye kazi tukiacha hayo na kufanya kazi tutafika mbali hata ukitaka kupandishwa cheo fanya kazi kwahiyo Kama Kuna mtumishi yeyote anatamani kupanda daraja ndani ya serikali afanye kazi na kazi yake itamsemea" Amesema Makonda.
Amesema watumishi wengi wa Serikali wamekuwa na fitina na uzembe Katika kazi Jambo linalopelekea kuchelewa kwa maendeleo Katika nchi na hata wengine kushindwa kupanda madaraja.
Aidha ametoa pongezi kwa Mkuu wa Oparetion ya ujenzi huo Bregidia Mbuge kwa kusimamia vyema ujenzi huo ambao unaenda vizuri ambapo Amesema mradi huo utakuwa ni chachu ya kuongeza kazi nyingine zaidi kwa SUMA JKT.
Pia RC Makonda amesema lengo la Ziara hiyo Ni kuona maendeleo ya Miradi na kuhamasisha zaidi na mpango kabambe unaochelewesha maendeleo ya wananchi hivyo amezitaka kampuni nyingine kujifunza kutoka kwa wanajeshi ili kufikia malengo ya serikali kukuza maendeleo Katika nchi.
Katika hatua nyingine RC Makonda amemwomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuangalia kwa jicho la tatu mradi wa NSSF uliopo kata ya Toangoma Wilaya ya Temeke,ambao umekaa kwa muda mrefu bila kuendelezwa hivyo ameomba Majengo hayo yakabidhiwe kwa Suma Jkt ili yaweze kuendelezwa.
"Katika Ziara yangu hii nimeweza kuona Majengo ya NSSF yaliyojengwa tokea 2004 nitumie fursa hii kumwomba Mhe. Rais awakabidhi wanajeshi kwani huu Ni mradi mkubwa ulioachwa kwa takribani miaka 15 Sasa bila kufanyiwa kazi yoyote na kuonekana kutokuwa na tija yoyote kwa taifa" Amesema Makonda.
Amebainisha kuwa Majengo Yale yanaweza kusaidia watumishi, na wanaweza kulipa hata gharama kidogo na kuweza kuchangia Pato la taifa kwa kupitia Kodi hivyo amemwomba Mhe. Rais aweze kufanya linalowezekana kuhusu Majengo hayo.
0 comments:
Post a Comment