A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, December 27, 2023

BAYPORT YANOGESHA ROMBO MARATHON

Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko akikabidhi cheti cha shukurani kwa Meneja Rasilimali Watu wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport, Bi. Evalyn Hall (kulia), kutambua mchango wa kampuni hiyo kama mdhamini mkuu wa mbio za Rombo Marathon 2023 zilizotimua vumbi lake mjini Rombo mkoani Kilimanjaro jana. Kulia kwa Naibu waziri mkuu ni Waziri wa Elimu na Mbunge wa Rombo, Prof. Adolf Mkenda na kushoto kwake ni Waziri Biteko ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bwana Nurdin Babu.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport, Bwana Nderingo Materu (wa pili kushoto), Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo, Bwana Lugano Kasambala (kushoto kwake), pamoja na wakimbiaji wengine, wakishiriki mbio za Rombo Marathon mjini Rombo, Kilimanjaro jana. Mbio hizo zilizodhaminiwa na Bayport, zina lengo la kuhamasisha vivutio vya utalii mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bwana Nurdin Babu (kulia), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport, wakishiriki mbio za Rombo Marathon mjini Romb, Kilimanjaro jana. Mbio hizo zilizodhaminiwa na Bayport, zina lengo la kuhamasisha vivutio vya utalii mkoani humo.

Na mwandishi wetu, Rombo, Kilimanjaro

TAASISI ya Kifedha ya Bayport imenogesha na kufanikisha mbio za Rombo Marathon 2023 zilizofanyika mjini Rombo, Kilimanjaro jana, zikiwa na lengo la kuhamasisha vivutio vya utalii wilayani humo.

Ikiwa ni mwaka wa pili sasa Rombo Marathon imefanyika ikihudhuriwa na viongozi wa kiserikali, wageni, na watu mashuhuri huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dk. Doto Biteko.

Akizungumza wakati wa mbio hizo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bayport, Bwana Nderingo Materu alisema Bayport ilikubali kuwa mdhamini Rombo Marathon ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na muasisi wa mbio hizo, Waziri wa Elimu na Mbunge wa Rombo, Prof. Adolf Mkenda katika kukuza utalii pamoja na suala zima la uhifadhi wa mazingira.

Kama mnavyofahamu sisi Bayport tumekuwa namba moja katika suala la utunzaji wa mazingira kwa njia ya upandaji miti, leo hii tumeamua kudhamini Rombo Marathon na tutaendelea kuunga mkono juhudi zozote nchini zenye lengo la kukuza utalii na kuhifadhi mazingira."

Lakini pia kama inavyofahamika umuhimu wa kufanya mazoezi ya mwili kwa ajili ya ubora wa afya za wafanyakazi na familia zetu, tunaamini mbio hizi zitaleta hamasa pia kwa watanzania kutilia mkazo umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,” alisema Bwana Materu.
Katika hotuba yake, Naibu Waziri Mkuu, Mhe, Dk. Biteko alitoa pongezi kwa waandaaji na wadhamini wa mbio za Rombo Marathon akisema zimekuwa na mafanikio makubwa lakini kikubwa ikiwa ni kujifunza utamaduni wa wana Rombo pamoja ya vivutio vya utalii vinavyopatikana katika wilaya na mkoa huo.

Natoa pongezi nyingi kwa muasisi wa Rombo Marathon, Waziri wa Elimu na Mbunge wa Rombo, Prof. Mkenda, natoa pongezi kwa serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Rombo bila kuwasahau wadhamini wote waliojitolea rasilimali zao kufanikisha tukio hili."

Serikali chini ya Rais, Mhe, Dk. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuunga mkono juhudi yoyote inayofanywa yenye lengo la kuwaletea maendeleo watu wa Rombo na kwa watanzania kwa ujumla,” alisema Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu.

Naye Waziri wa Elimu, Mbunge wa Rombo na muasisi wa mbio hizo, Prof. Adolf Mkenda alitoa shukurani zake kwa Mhe. Naibu Waziri Mkuu, Dk. Biteko kwa kukubali kuwa mgeni rasmi pamoja na wadhamini wa mbio hizo Taasisi ya Kifedha ya Bayport kwa kufanikisha tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya watu wa Rombo na wananchi wa Kilimanjaro.

Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu kwa kuungana na wana Rombo katika kushiriki tukio hili, natoa pia shukrani kwa wadhamini wote waliowezesha kufanya tukio hili kuwa lenye ubora ikiwemo Taasisi ya Bayport Financial Services,” alisema Prof. Mkenda.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bwana Nurdin Babu, alichukua nafasi hiyo kuwakaribisha wageni wote wanaotoka ndani na nje ya Tanzania kwenda kuangalia vivutio vya utalii mkoani humo akisema Kilimanjaro ipo salama na wapo tayari kuwapokea na kuwahudumia.
Mbio za Rombo Marathon zinazofanyika kwa mwaka wa pili sasa zimeshirikisha mbio za Km 21, Km 10 na mbio za kujifurahisa za kilomita 5.
Share:

Thursday, December 21, 2023

Filamu za kibongo zote kali kuonekana kupitia Airtel TV

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Kampuni ya Airtel Tanzania ikitambulisha filamu za kitanzania zaidi ya 100 ambazo wapenzi wa filamu wanaweza kuziangalia kupitia Airtel TV inayopatikana ndani ya aplikesheni ya Airtel App. Kati ya filamu hizo zimo za washindi na washiriki wa Tuzo za Filamu Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua na kushoto ni msanii nguli wa vichekesho nchini na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’.
Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua (kulia), akionyesha baadhi ya filamu za kitanzania zinazoonyeshwa katika Airtel TV, wakati Airtel Tanzania ikitambulisha filamu za kibongo zaidi ya 100 ambazo wapenzi wa filamu wanaweza kuziangalia kupitia Airtel TV inayopatikana ndani ya aplikesheni ya Airtel App. Kati ya filamu hizo zimo za washindi na washiriki wa Tuzo za Filamu Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo na msanii nguli wa vichekesho nchini na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’.
Msanii nguli wa vichekesho na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’ (kushoto0, akizungumza katika hafla hiyo huku akitoa hamasa kwa wasanii wenzake kupeleka kazi zao Airtel TV na pia kupakua Airtel App kwani Airtel imekuja kivingine katika kuwapa watanzania burudani za filamu za kibongo na kutoa fursa za kiuchumi kwa wasanii. Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo na Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua.

*Ni fursa kwa wasanii pia kujiongezea kipato

WAPENZI wa filamu za kibongo, wana kila sababu ya kufurahia msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, mara baada ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, kupitia Aplikesheni yake ya (Airtel App), kuweka filamu zaidi ya 100 katika Airtel TV inayopatikana katika App hiyo inayowawezesha watanzania kuangalia filamu hizo kwa urahisi na kwa unafuu mahali popote walipo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kutambulisha filamu hizo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo, Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua alisema filamu hizi 100 nzuri kwani kati yake zimo za washindi na washiriki wa Tuzo za Filamu Tanzania 2023 zilizofanyika jijini humo hivi karibuni.

Tunayo furaha kubwa kuwajulisha wapenzi wa burudani za filamu za kitanzania kuwa sasa Kampuni ya Airtel kupitia Airtel App tumeweka filamu kali zaidi ya 100 za washiriki na washindi wa mwaka huu wa Tuzo za Filamu nchini pamoja na aina nyingine za burudani hivyo ni wakati mzuri kwa wazazi na familia kuwa na wakati mzuri wa kufurahia katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka."

Airtel App ni rahisi kuipakua na kuanza kupata huduma mbalimbali zikiwemo huduma mbalimbali za Airtel Money kama vile kutuma na kutoa pesa kwa wakala, kufanya malipo ya huduma mbalimbali na sasa kwa kupitia Airtel TV inayopatikana ndani ya app hiyo tumewaletea burudani ya aina yake ya filamu za kitanzania zenye ubora ili kukonga nyoyo za wateja wetu wenye kiu ya kuangalia filamu za kikwetu”, alisema Bwana Gau.

Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo aliishukuru Kampuni ya Airtel kwa udhamini wake katika tuzo za filamu za mwaka huu zikishindanisha filamu kutoka Tanzania na nje ya Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki akisema umechangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha tuzo hizo kufanyika katika viwango vyenye ubora wa kimataifa.

Kwa niaba ya Bodi ya Filamu Tanzania ningependa kuchukua fursa hii kuishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kuthamini maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na kwa maendeleo ya wasanii wetu kwani kati ya filamu 565 zilizopokelewa mwaka huu, filamu 535 zilitoka nchini na 30 tu ndio zilitoka nje ya nchi."

Natoa wito kwa wasanii wote nchini kuleta filamu zenu zenye vigezo na zilizopata kibali kutoka katika Bodi ya Filamu Tanzania ili ziweze kupakiwa katika Airtel App ziweze kutazamwa na kuwapa burudani wapenda filamu za kitanzania nchini lakini pia zitumike kama fursa ya kujiongezea kipato kwenu wasanii”, alisema katibu mtendaji huyo.

Naye mmoja ya wasanii nguli wa vichekesho nchini na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’ ambaye katika tuzo za mwaka huu alijinyakulia tuzo kwa miaka mitatu mfululizo ya Filamu Bora ya Uchekeshaji alitoa hamasa kwa wasanii kupeleka kazi zao Airtel TV na pia kupakua Airtel App kwani Airtel imekuja kivingine katika kuwapa watanzania burudani za filamu za kibongo na kutoa fursa za kiuchumi kwa wasanii.
Share:

Friday, December 8, 2023

Waziri Nape azipongeza Airtel, Jubilee Insurance na Axieva kuanzisha Afya Bima

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu huduma mpya ya Afya Bima inayotolewa na Airtel Money kwa ushirikiano na makampuni ya Jubilee Insurance na Axieva. Waziri Nape alisema Afya Bima itasaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi kiafya na kiuchumi. Wengine ni viongozi kutoka makampuni hayo.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Bwana Charles Rugambwa (kulia), akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo kuhusu huduma ya Afya Bima inayopatikana kwa wateja wote wa Airtel Money wenye simu janja na za kawaida.. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye na Mkurugenzi Mtendaji wa Jubilee Insurance, Dk. Harold Adamson.
Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano (kushoto), akizungumzia faida mbalimbali watakazozipata wateja wa Airtel Money kwa kujiunga na huduma mpya ya Afya Bima wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Axieva, Davrav Dhingra, akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwakwe ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Bwana Charles Rugambwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.

*Asema itaokoa maisha ya watanzania na kuwapunguzia umasikini.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amezipongeza kampuni ya Airtel Tanzania kwa ushirikiano wake na kampuni za Jubilee Insurance pamoja na Axieva kwa kuanzisha huduma Afya Bima, akisema huduma hiyo imekuja wakati muafaka katika kipindi hiki ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akisaini muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuwapa fursa watanzania wengi zaidi kunufaika na mpango huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati akitambulishwa rasmi huduma hiyo, Waziri Nape alisema, huduma ya Afya Bima itakayotolewa Airtel kwa kushirikiana na Jubilee Insurance pamoja na Axieva itaenda kuokoa maisha na uchumi wa watanzania wengi ambao hawakuwa katika mfumo wa bima ya afya hivyo kulazimika kutumia pesa taslimu na wakati mwingine kulazimika kuuza rasilimali zao ili kujitibu wao ama wategemezi wao.

Nichukue nafasi hii kuzipongeza Airtel Tanzania, Jubilee Insurance pamoja Axieva kwani huduma hii inapatikana kirahisi kwa njia ya kidigitali kupitia Airtel Money hivyo kuwafanya watanzania wengi zaidi kujiunga mahali popote walipo bila usumbufu."

Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika kuongeza miundo mbinu mingi ya kutoa huduma za afya, ujenzi wa zahanati katika ngazi ya vijiji, vituo vya afya katika ngazi ya kata, hospital za halmashauri, hospital za rufaa za mikoa, hospital za Kanda pamoja na hospital za kitaifa hivyo ujio wa Afya Bima utasaidia watanzania wengi kuweza kunufaika na huduma bora za afya zitolewazo katika hospitali za umma”, alisema Waziri Nape.

Waziri Nape aliongeza kuwa uwekezaji wa Serikali katika kutengeneza miundombinu ya afya hautakuwa na maana kama wananchi watakuwa wanapata huduma hizo kwa kusuasua na ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Sita ikaamua kusukuma ajenda ya Bima ya afya kwa wote.

Jambo kubwa ni kwamba Bima hii, imewalenga watanzani wote hasa ambao hawana uwezo wa kuweza kujigharamia matibabu pindi wakipata shida ya kuumwa kama madereva bodaboda na Mama ntilie kwa hiyo jambo hili ni suluhisho kubwa kwao kupata huduma za afya huku Maisha yao yakiendelea”, Alisema Waziri Nape.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Bwana Charles Rugambwa alisema huduma ya Afya Bima ni moja ya mikakati ya Airtel katika kuwaletea watanzania huduma bora za kiubunifu na rahisi kujiunga kwa njia ya kidigitali ambapo wateja wote wa Airtel Money wanaweza kujiunga kwa kutumia simu janja na ya kawaida.

Kwa kuwa huduma ya Afya Bima ni kwa ajili ya watu wote na hiki ni kipindi cha msimu wa sikukuu za kuelekea mwaka mpya, natoa wito kwa wateja wa Airtel Money kuwapa zawadi wapendwa wao kwa kuwalipia vifurushi ya Afya Bima, hii ni zawadi ya ukweli."

Ni rahisi kujiunga, mteja wa anachotakiwa kufanya ni kuingia katika menu ya Airtel Money kisha anaingia namba 6, Huduma za kifedha, kisha 2, Bima, kisha 2 tena, Afya Bima, kisha kuthibitisha na baadae kuchagua aina ya vifurushi ukitakacho”, alisema Bwana Rugambwa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Jubilee, Dk. Harold Adamson amesema kuwa wamefarijika kuwapata wadau ambao wameshirikiana nao katika kuongeza thamani ya tehama na kuhudumia moja kwa moja kwenye Maisha ya watanzania wote.

Sisi kama Jubilee tumefarijika kuweza kupata wadau wenzetu ili kuanzisha huduma na bidhaa hii mpya kwa watanzania hasa wanaotumia mtandao wa airtel, bidhaa hii ya afya bima inaunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kuhakikisha watanzania wote wanafikiwa na bima ya afya”, Alisema Dkt. Adamson.

Akitaja baadhi ya manufaa na Afya Bima, Dk. Adamson alisema, Afya Bima inakuja na bima za afya aina tatu ambazo ni Afya Poa, Afya Supa na Afya Dhahabu ambapo mteja ataweza kuchagua vifurushi tofauti kulingana na uhitaji wake.

Bima ya Afya Poa inalenga kurudisha mapato yaliyopotea wakati mgonjwa alipolazwa ambapo mgonjwa anapokuwa amelazwa atakuwa anarudishiwa gharama kati ya Tzs 20,000 mpaka Tzs 50, 000, vile vile, Afya Poa inatoa faida ya bima ya gharama za mazishi ya mpaka Tzs 1 milioni moja, ajali, ulemavu au kifo faida ya mpaka Tzs 500,000 na vifurushi vyake gharama yake kati ya Tzs 6,000, Tzs 7,000 mpaka Tzs 35, 0000 kulingana na uhitahitaji wake.

Kwa upande Afya Supa na Afya Dhahabu zinatoa faida kwa mteja kupata huduma za matibabu bila malipo, Afya Supa inampa mteja kupata gharama ya matibabu ya hadi Tzs 5 milioni na hii ni pamoja na mteja aliyelazwa au kupata matibabu ya bila kulazwa. Bima hii ina kufurushi cha kulipia kati ya Tzs 15,000 mpaka Tzs 45,000 kwa mwaka kulingana na mahitaji ya mteja, lakini pia Afya Supa inakuja na faida ya uzazi ya gharama ya hadi Tzs 2 milioni”, alisema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano amesema kuwa kampuni hiyo inatekeleza maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya kuhakikisha watoa huduma kupitia Tehama wanatumia ujuzi huo kuwasaidia wananchi wa aina zote na kuipa thamani sekta hiyo.

Alisema kuwa Huduma na Bidhaa mpya ya Afya Bima itakwenda kwa watanzania wapatao milioni 17.5 wanaotumia mtandao huo kuweza kupata matibabu kwa bei nafuu katika vituo zaidi ya 600 nchini na kuwawezesha wananchi kuwa na unafuu wakati wa shida ya kuumwa na kusimama kufanya kazi.

Mteja anayejiunga na Afya Bima ataweza kupata huduma ya matibabu kulingana na hospitali ambazo Wizara ya Afya Imesajili ambazo ni Hospitali za Umma, hospitali za kibinafsi na za Misheni kulingana na orodha iliyotolewa.
Share:

Wednesday, December 6, 2023

Benki ya Absa Tanzania yazindua mfumo wa malipo ya kadi za benki kupitia simu za mkononi

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (wa nne kutoka kushoto, mstari wa mbele), Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bwana Aron Luhanga (kushoto kwake), wakipozi kwa picha mbele ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi mfumo wa malipo ya kadi za benki kupitia simu za mkononi ‘Absa Tanzania Mobi Tap’ jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Mauzo na Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Frank Mboya (kushoto), akionyesha jinsi mfumo wa malipo ya kadi za benki kupitia simu za mkononi unavyofanya kazi kwa waandishi wa habari, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mfumo huo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bwana Aron Luhanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Lilian Swere na Meneja Bidhaa na Kadi, Bi. Elfrida Mruma.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mfumo wa malipo ya kadi za benki kupitia simu za mkononi 'Absa Mobi Tap' katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja Mauzo na Biashara, Bwana Frank Mboya, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Lilian Swere na Meneja Bidhaa na Kadi, Bi. Elfrida Mruma.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mfumo wa malipo ya kadi za benki kupitia simu za mkononi 'Absa Mobi Tap' katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja Mauzo na Biashara, Bwana Frank Mboya, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Bwana Aron Luhanga na Meneja Bidhaa na Kadi, Bi. Elfrida Mruma.

Absa MobiTap inawezesha wauzaji kupokea malipo ya kadi za benki kutoka kwa wateja kwa kutumia simu janja kama mashine ya kuchanjia kadi.

Benki ya Absa Tanzania imezindua Absa Mobi Tap – ambayo ni suluhisho la kwanza la aina yake nchini Tanzania ambalo linawawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati (SMMEs) kutumia simu zao kwa ajili ya kuchakata miamala ya kadi za benki na kuondoa hitaji la mashine za kuchanjia kadi, yaani POS.

Absa MobiTap inatarajiwa kuharakisha mchakato wa ulipiaji wa bidhaa kwa wanunuzi na wauzaji kwa kutumia simu janja kama mashine ya kuchanjia kadi. Wateja wanaweza tu kugusa kadi zao za benki kwenye simu ya muuzaji ya Android au kompyuta kibao ili kufanya malipo.

Kwa upande wa wafanyabiashara, wanachohitaji kufanya ni kupakua programu ya Absa Mobi Tap kutoka Play Store kwenye simu zao janja. Baada ya hapo wataweka taarifa zao na kuunganishwa na kuwa tayari kupokea malipo ya kadi za benki. Ili kuchakata malipo, mfanyabiashara ataingiza kiasi cha manunuzi kwenye program ya Absa MobiTap, kisha mteja atagusisha kadi yake nyuma ya simu hiyo na kuingiza PIN yake ikiwa inahitajika na kukamilisha malipo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ndabu Swere, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, alisema kuanzishwa kwa Absa Mobi Tap ni ushahidi wa mkakati wa benki hiyo kuendelea kujikita katika kujenga kampuni ya kisasa ya kidijitali ambayo inaenda na nyakati na mahitaji ya wateja.

Kama benki inayoongozwa kidijitali, tumejitolea kuongoza njia katika uvumbuzi wa kidijitali na tutaendelea kuzindua suluhisho nyingi za kidigitali za ubunifu wa hali ya juu ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja wetu ya sasa na ya baadae, na kuhakikisha kuwa bidhaa zetu zimeundwa kushughulikia changamoto ambazo wateja wetu wanakabiliwa nazo.

Absa MobiTap ni suluhisho la kwanza la aina yake hapa nchini na tunajivunia kuwa benki ya kwanza kuwaletea Watanzania suluhisho la malipo ya kidigitali la ubunifu huu wa kipekee.

Tunaamini suluhisho hili litaleta mapinduzi katika namna ambayo wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati nchini yanavyoendesha biashara zao, kwani itaondoa vizuizi na kupanua chaguzi katika upatikanaji wa huduma za malipo ya kidijitali.

Biashara nyingi ndogo ndogo hazikuweza kupata mashine za POS kwa sababu ya uwekezaji mzito unaohitajika kwaajili ya hizo mashine. Lakini Absa MobiTap amekuja kuleta ufumbuzi kwenye hili.

Sasa hata dereva wa Uber/Bolt anaweza kupokea malipo ya kadi kupitia simu yake ya mkononi ambayo ni njia salama, ya haraka, na rahisi kwa wote – wanunuzi na wauzaji. Dhama hii ya kuwezesha wafanyabiashara wa aina zote inaenda sambamba na kusudi letu la ‘Kuwezesha Afrika ya kesho, pamoja, …hatua moja baada ya nyingine’.

Kwa upande wake, Aron Luhanga, Mkuu wa Kitengo Mawasiliano, Masoko na Mahusiano, alisema suluhisho hili la Absa MobiTap ni moja ya mengi ambayo benki itaendelea kutoa katika ufumbuzi wa malipo ya kidijitali wakati Absa inaendelea kuimarisha nafasi yake kama kinara katika nyanja hiyo hapa nchini.

Alisema, “MobiTap inaruhusu wauzaji kutumia teknolojia ambayo tayari wanayo – simu janja, karibuni kila mfanyabiashara siku hizi ana simu janja. Hata hivyo, mtej wetu akiwa hana simu janja, na anahitaji kujiunga na Absa MobiTap, tutampatia simu bure ili kumfanikisha.

Kwa mujibu wa Aron, suluhisho hili kimsingi linalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), hasa wale ambao hapo awali walitegemea malipo kwa fedha taslimu au uhamishaji wa kielektroniki (EFT). Wafanyabiashara mbalimbali, kama vile madereva wa Uber/Bolt, migahawa, saluni, maduka ya vifaa, wakulima, wote wanaweza kutumia fursa hii ya uvumbuzi kuwasaidia kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.

Katika hotuba yake ya kuhitimisha, Ndabu, alitoa wito kwa wafanyabiashara wote – wafanyabiashara wa ukubwa wote (wadogo na wa kati) kutumia fursa ya Absa MobiTap kuwezesha biashara zao kupokea malipo ya kadi za benki kwa njia ya haraka, rahisi, na salama zaidi, ili kuwezesha kukuza jamii ya kidijitali, isiyotembea na pesa taslimu kwa faida ya wote.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive