Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Kampuni ya Airtel Tanzania ikitambulisha filamu za kitanzania zaidi ya 100 ambazo wapenzi wa filamu wanaweza kuziangalia kupitia Airtel TV inayopatikana ndani ya aplikesheni ya Airtel App. Kati ya filamu hizo zimo za washindi na washiriki wa Tuzo za Filamu Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua na kushoto ni msanii nguli wa vichekesho nchini na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’.
Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua (kulia), akionyesha baadhi ya filamu za kitanzania zinazoonyeshwa katika Airtel TV, wakati Airtel Tanzania ikitambulisha filamu za kibongo zaidi ya 100 ambazo wapenzi wa filamu wanaweza kuziangalia kupitia Airtel TV inayopatikana ndani ya aplikesheni ya Airtel App. Kati ya filamu hizo zimo za washindi na washiriki wa Tuzo za Filamu Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo na msanii nguli wa vichekesho nchini na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’.
Msanii nguli wa vichekesho na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’ (kushoto0, akizungumza katika hafla hiyo huku akitoa hamasa kwa wasanii wenzake kupeleka kazi zao Airtel TV na pia kupakua Airtel App kwani Airtel imekuja kivingine katika kuwapa watanzania burudani za filamu za kibongo na kutoa fursa za kiuchumi kwa wasanii. Kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo na Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua.
*Ni fursa kwa wasanii pia kujiongezea kipato
WAPENZI wa filamu za kibongo, wana kila sababu ya kufurahia msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, mara baada ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, kupitia Aplikesheni yake ya (Airtel App), kuweka filamu zaidi ya 100 katika Airtel TV inayopatikana katika App hiyo inayowawezesha watanzania kuangalia filamu hizo kwa urahisi na kwa unafuu mahali popote walipo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kutambulisha filamu hizo ambayo pia ilihudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo, Meneja Bidhaa wa Airtel App, Bwana James Gua alisema filamu hizi 100 nzuri kwani kati yake zimo za washindi na washiriki wa Tuzo za Filamu Tanzania 2023 zilizofanyika jijini humo hivi karibuni.
“Tunayo furaha kubwa kuwajulisha wapenzi wa burudani za filamu za kitanzania kuwa sasa Kampuni ya Airtel kupitia Airtel App tumeweka filamu kali zaidi ya 100 za washiriki na washindi wa mwaka huu wa Tuzo za Filamu nchini pamoja na aina nyingine za burudani hivyo ni wakati mzuri kwa wazazi na familia kuwa na wakati mzuri wa kufurahia katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka."
“Airtel App ni rahisi kuipakua na kuanza kupata huduma mbalimbali zikiwemo huduma mbalimbali za Airtel Money kama vile kutuma na kutoa pesa kwa wakala, kufanya malipo ya huduma mbalimbali na sasa kwa kupitia Airtel TV inayopatikana ndani ya app hiyo tumewaletea burudani ya aina yake ya filamu za kitanzania zenye ubora ili kukonga nyoyo za wateja wetu wenye kiu ya kuangalia filamu za kikwetu”, alisema Bwana Gau.
Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dk. Kiagho Kilonzo aliishukuru Kampuni ya Airtel kwa udhamini wake katika tuzo za filamu za mwaka huu zikishindanisha filamu kutoka Tanzania na nje ya Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki akisema umechangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha tuzo hizo kufanyika katika viwango vyenye ubora wa kimataifa.
“Kwa niaba ya Bodi ya Filamu Tanzania ningependa kuchukua fursa hii kuishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kuthamini maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na kwa maendeleo ya wasanii wetu kwani kati ya filamu 565 zilizopokelewa mwaka huu, filamu 535 zilitoka nchini na 30 tu ndio zilitoka nje ya nchi."
“Natoa wito kwa wasanii wote nchini kuleta filamu zenu zenye vigezo na zilizopata kibali kutoka katika Bodi ya Filamu Tanzania ili ziweze kupakiwa katika Airtel App ziweze kutazamwa na kuwapa burudani wapenda filamu za kitanzania nchini lakini pia zitumike kama fursa ya kujiongezea kipato kwenu wasanii”, alisema katibu mtendaji huyo.
Naye mmoja ya wasanii nguli wa vichekesho nchini na Balozi wa Airtel Money, Lucas Lazaro Mhuville ‘Joti’ ambaye katika tuzo za mwaka huu alijinyakulia tuzo kwa miaka mitatu mfululizo ya Filamu Bora ya Uchekeshaji alitoa hamasa kwa wasanii kupeleka kazi zao Airtel TV na pia kupakua Airtel App kwani Airtel imekuja kivingine katika kuwapa watanzania burudani za filamu za kibongo na kutoa fursa za kiuchumi kwa wasanii.
0 comments:
Post a Comment