
Thursday, May 12, 2022
ABSA BANK TANZANIA PROFIT AFTER TAX SOARS 155% IN THE FIRST QUARTER OF 2022

Tuesday, April 26, 2022
ZAIDI YA WATOTO 62,155 KUNUFAIKA NA CHANJO YA POLIO IKUNGI
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Oliva Njoka akitoa taarifa kuhusu maandalizi ya chanjo hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo Mika Likapakapa akichangia jambo kwenye kikao hicho.
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jerry Muro ametoa onyo kwa mtu yeyote wilayani hapa kutokwamisha mchakato wa utoaji wa chanjo ya polio kitaifa utakaoanza Aprili 28 mwaka huu unaotarajiwa kuwafikia watoto 62,155 na atakayebainika akifanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Muro alitoa onyo hilo wakati akizungumza na maafisa mbalimbali, viongozi wa dini, wadau wa maendeleo na timu ya wataalamu watakaoratibu zoezi hilo wilayani hapa ambapo alihamasisha wananchi wote kujitokeza bila kukosa wakati zoezi hilo litakapoanza.
"Sisi hapa Ikungi tupo tayari mpaka sasa tumepokea jumla ya chanjo 71,400 na tumesambaza dozi 70,000 katika vituo vya kutolea afya na kuwa watalifanya kwenye vijiji vyote 101 na zaidi ya vitongoji 500" alisema Muro.
Alisema tayari wamewapanga wataalamu kwenye vituo 140 na watafika kwenye maeneo yote na kila mtoto aliopo kwenye wilaya hiyo watahakikisha anapata chanjo hiyo.
Muro alisema kwamba miundombinu yote pamoja na timu ya wataalamu kwa ajili ya kuwezesha ufanikishaji wa zoezi hilo yamekamilika kwa asilimia 100.
Aidha Muro alitoa mwito kwa wazazi wilayani humo kuacha tabia ya kuwapeleka watoto wao kwa waganga wa kienyeji kwani hawana uwezo wa kutoa chanjo ya polio badala yake wawapeleke kwenye vituo vya afya wakiwapeleka huko wanaweza kupigwa na ugonjwa huo na hata kupata kifo.
Muro aliwaomba wazazi hao kuanzia Aprili 28 hadi Mei Mosi kuwa ni kipindi cha mzazi kumpeleka mtoto wake kituo cha afya na yale maeneo yaliopo pembezoni kabisa mwa wilaya hiyo watayafikia kupitia kampeni ya nyumba kwa nyumba.
Muro alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku tabia ya wazazi ambao kila wakipewa elimu na kuambiwa umuhimu wa kuwapeleka watoto wao vituo vya afya kwa ajili ya kupewa chanjo wamekuwa mstari wa mbele kukahidi kwa sababu ya imani na mila potofu hivyo kuanzia jana mzazi yeyote watakaye mbaini anakendwa kinyume na maagizo ya kitaifa ya zoezi hilo atakamatwa na kuchuliwa hatua kali za kisheria na kuwa mfano kwa wengine wote katika wilaya hiyo.
"Tumepata taarifa kuwa kuna watu wamejipanga kukwamisha zoezi ili sasa mimi nawaambia kuwa kabla ya kuanza kukwama sisi watakwama wao na waomba watu wote wenye imani potofu dhidi ya chanjo hii watuache kwanza tufanye kazi nipo hapa kwa ajili ya kuwatoa mashaka wananchi wote wa wilaya ya Ikungi kuwa chanjo hizi ni salama zimedhibitishwa na wataalamu wa afya wa kimataifa na hapa nchini" alisema Muro.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Oliva Njoka alisema wamepokea maagizo kutoka wizarani kuwa kunakampeni ya kitaifa ya chanjo hiyo kwa nchi nzima ambapo watachanjwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kuwa tayari wamekwisha anza maandalizi kwa kupata mafunzo ngazi ya halmashauri kwa timu ya uendeshaji na pia watatoa mafunzo kwa wale wahudumu watakao kuwa wakichanja.
Mratibu wa Elimu ya Afya na Uhamasishaji Wilaya ya Ikungi Braison Shoo alisema hivi sasa wapo kwenye kampeni ambayo wanatarajia kuianza Aprili 28 hadi Mei Mosi ya chanjo ya matone kwa watoto waliochini ya miaka mitano ambapo aliwaomba wananchi wote wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao kupata chanjo.
Alisema lengo la chanjo hiyo ni kuongeza kinga katika jamii baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa huo nchi jirani ya Malawi hivyo aliendelea kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la chanjo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Mika Likapakapa walisema watakwenda kuwahimiza madiwani na viongozi wa chama na serikali ngazi za vijiji na kata kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Sunday, April 24, 2022
TANZANIA COMMERCIAL BANK SPONSORS FOR FREE HEALTH TESTING DAR ES SALAM
Tanzania Commercial Bank Bank Manager Edward Mwoleka (center), undergoing a blood test by Alliance Insurance Specialist Ravi Kumar, while Tanzania Commercial Bank teamed up with Alliance insurance to provide free diagnostic tests to the residents of Mbagala and its suburbs for free. Head of Alliance Insurance Group, KVA Krishnan. The ceremony took place today at the Tanzania Commercial Bank branch in Mbagala.
Tanzania Commercial Bank Bank Manager Edward Mwoleka and Alliance Insurance Group CEO KVA Krishnan watching one of Dar es Salaam's residents, Joseph John, receive a blood pressure test from Alliance Insurance Group Specialist Ravi Kumar, while Tanzania Commercial Bank teamed up with Alliance insurance to provide free diagnostic tests to the residents of Mbagala and its suburbs free of charge.
Some of the citizens who showed up at the TCB Mbagala branch in the provision of various diagnostic tests conducted by Alliance Insurance incorporation to various residents of Mbagala.
Tanzania Commercial Bank Bank Manager Edward Mwoleka, CEO of Alliance Insurance Group, KVA Krishnan and (name not found) greet each other at a special screening ceremony conducted by Alliance Insurance incorporation for various residents of Mbagala.
.Mbagala resident receiving a blood pressure check from Alliance Insurance Group Specialist Ravi Kumar, while Tanzania Commercial Bank teamed up with Alliance insurance to provide free diagnostic tests to residents of Mbagala and its suburbs free of charge.
Tanzania Commercial Bank Mbagala Branch Manager Edward Mwoleka witnessing one of the Dar es Salaam residents receiving a sugar test from Laboratory Laboratory Specialist Husna Hassan as Tanzania Commercial Bank teamed up with Alliance insurance to provide diagnostic tests for Mbagala residents and its free suburbs
Saturday, April 23, 2022
Absa Bank pledges to maintain quality services for sustainable growth

Friday, April 22, 2022
WANANCHI IKUNGI WAHIMIZWA KUTUNZA CHAKULA ILI KUJIKIGA NA BAA LA NJAA
Thursday, April 21, 2022
AKIBA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE DAR ES SALAM
Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc Silvest Arumas akizungumza wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali wateja wake Baadhi ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Akiba Commercial Bank ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali na kuwa karibu na wateja wao.

Wateja na wageni waalikwa wa Akiba Commercial Bank wakichukua mlo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali wateja wake
Akiba Commercial Bank tunatambua nakuheshimu imani za wateja na wadau wetu
Akizungumza katika halfla ya futari iliyoandaliwa na ACB Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc Bw. Silvest Arumas alisema benki hiyo imeweka mipango mikakati kwaajili ya wateja wake hasa katika kipindi hiki cha Ramadhan
Tunaupa umuhimu wa kipekee sana mwezi mtukufu wa Ramadhan sio tu kwa wateja na wadau bali ni kwa waislamu wote kwani kama benki tunadhamini nakujali kila dini hivyo hivyo tumejikita kikamilifu katika mwezi huu wa Ramadhan kwaajili ya kuwashika mkono ndugu zetu waislam.
Akiba Commercial Bank, umekuwa ni utaratibu wetu kama benki yenye kujali na kutambua umuhimu wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan tumekuwa tukiwaruhusu wafanyakazi kutoka kazini mapema kwaajili ya ibada na matayarisho ya futari.
Pia Akiba Commercial Bank, umekuwa pia ni utaratibu wetu kufanya hafla yakuandaa futari kwa wateja wetu kila mwaka kwaajili ya kuwaunga mkono ndugu zetu waislamu katika funga yao pia kudumisha mahusiano kati ya wateja na benki yao pendwa.
Wednesday, April 20, 2022
BENKI YA ABC YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 2 KUSAIDIA UJENZI WA CHOO CHA WAALIMU SHULE YA MSINGI MTAWALA MANISPAA YA MOROGORO.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga,(katikati), akikabidhi vifaa vya ujenzi wa Choo kwa Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya (wapili kutoka kulia), kulia Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akimkabidhi taarifa ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi , Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga akizungumza katika hafla hiyo.
Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati akisalimiana na waalimu waliojitokeza katika hafla hiyo.
Waalimu wa shule ya Msingi Mtawala.
BENKI ya ABC Kanda ya Morogoro, imekabidhi vitu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 2 katika kusaidia ujenzi wa Choo cha Waalimu katika Shule ya Msingi Mtawalaa Manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia kuondoa changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu hususani katika upande wa vyoo.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, imefanyika leo Aprili 20/2022 katika shule hiyo huku tukishuhudia Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro , Chausiku masegenya ,akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Masegenya, ameishukuru Benki ya ABC huku akibainisha kuwa msaada huo utagusa maisha ya Waalimu wengi kwa miaka mingi ijayo.
“Wadau wetu muhimu na washirika kama Benki ya ABC ndio nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao utasaidia katika kuweka mazingira rafiki kwa waalimu ya kupata huduma ya choo , lakini pia kuwaondolea adha ya kutoka nje kwa ajili ya kufuata huduma ya choo" Amesema Masegenya.
Mwisho, Masegenya, ametoa wito kwa taasisi zingine za kifedha na wadau wanaopenda kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya vyoo pamoja na mazingira ya kujifunzia katika shule za umma zilizopo Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi katika jitihada hizo.
Naye Diwani wa Viti Maalum anayetokana na Kata ya Mwembesongo, Mhe. Hadija Kibati, ameishukuru Benki ya ABC Kwa kuwaunga mkono kwenye sekta ya elimu kwa kuwapa vifaa hivyo ambayo yatasaidia kuondosha changamoto ya choo cha walimu shuleni hapo.
Kwa upande wa Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo, amesema kwamba utoaji wa misaada kwa jamii ni sehemu ya dhamira endelevu ya benki hiyo katika kusaidia sekta za elimu na kuona benki hiyo inachukulia kwa uzito sana suala la uwekezaji kwenye sekta ya elimu.
Kalinga,
amesema wametoa msaada huo ili kuunga mkono Serikali na juhudi za
wananchi na kurudisha kwao ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na hamasa ya
kutenegeneza miundombinu ya elimu kwa manufaa ya sasa na kizazi cha
baadae.
“Benki yetu inajivunia kuona Taifa linapiga hatua kubwa kwenye sekta ya elimu ambapo kupitia sera ya serikali elimu bure imeongeza idadi ya wanafunzi lakini pia ufaulu ambao maendeleo yake yanaakiisi hadi kiwango chetu cha uchumi ambapo mwaka jana nchi iliingia kwenye uchumi wa kati” Amesema Kalinga.
“Tumejitolea kuhudumia watu, biashara na jamii kwa ujumla. Benki yetu ya ABC, tumeguswa na changamoto ambayo iliwasilishwa kwetu , dhamira yetu kwa jamii ni kuona ni kuona tunaunga mkono na kusaidia juhudi za kielimu na ustawi wa wanafunzi wetu na shule kote nchini na sio kwa Manispaa hii ya Morogoro pekee, hivyo ni muhimu zaidi tukiweka jitihada katika kuboresha mazingira ya vyoo shuleni ili sasa Waalimu waweze kuwa na mahala rafiki kwa kutumia na kuacha kutoka eneo lao kwenda mbali na shule zao, ABC tutaendelea kushirikiana na Serikali kwa kadri tunavyoweza kuguswa na changamoto katika jamii ” Ameongeza Kalinga.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mtawala, Mwl. Godfrey Binagwa , ameishukuru Benki ya ABC kwa msaada huo ambao wameutoa ambao utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo za uhaba wa choo cha walimu.
Vifaa hivyo vya ujenzi ambayo walikabidhi benki hiyo ni Mifuko 50 ya saruji, mchanga Lori 1, Kokoto Lori 1, Mawe Lori 1, Milango 2 ya mbao, Fremu 2 za milango, Tofali za block 400 pamoja na Mabati 70.
Wednesday, April 13, 2022
TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKIANA NA TRC KUZINDUA UJENZI WA RELI TABORA
Tanzania Commercial Bank TCB) imesema itaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ili kuboresha uchumi wa Tanzania.
TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora mpaka Makutupora Mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya tatu leo Mkoani Tabora
“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC ni wenzetu hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio kwa mkoa wa Tabora,”amesema
“Kufanikiwa kwa mradi huu kutarahisha usafiri wa kutoka Tabora hadi Dar es Salaam kwa masaa sita, na treni ya mizigo kwa masaa kumi pia kutafungua fursa za kiuchumi kwa mikoa ya Tabora, Dodoma, Singida , Shinyanga hadi Mwanza,”amesema
Moshingi amesema, wananchi wa Tabora kwa sasa wataanza kukua kiuchumi, kwa kusafirisha mazao yao kwenda Dar es Salaam ambapo ndio soko kuu la biashara na usafiri utakuwani ni wa uhakika zaidi.