A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, February 25, 2025

Benki ya Absa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya wanawake mahali pa kazi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto), akikabidhi cheti Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, kwa kutambua mchango wa benki hiyo kama mdau muhimu wa Programu ya Mwanamke Kiongozi inayoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), katika hafla ya maadhimisho na mahafali ya 10 ya programu hiyo, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

Benki ya Absa Tanzania imesema itaendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali zenye lengo la kuhakikisha wanawake wa Tanzania wanapiga hatua za kimaendeleo mahali pa kazi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wakati wa maadhimisho ya miaka 10 na mahafali ya 10 ya programu ya Mwanamke Kiongozi, inayoratibiwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Sisi Absa tuna kitu tunaita ahadi yetu ya chapa inayosema ‘Stori yako ina thamani’, kwa kuendana na ahadi yetu hii tunaamini kwamba story za wanawake wa Tanzania zina thamani na ndio maana tuliamua kuungana na ATE kusapoti jambo ili kama wadhamini, lakini pia tumekua wadau wa karibu sana na ATE kwa miaka 10 tumeweza kuweka wahitimu wengi, leo hii tukiwa na wahitimu kama wanne."

Sababu kubwa inayotufanya tuendelee kusapoti juhudi hizi ni kwamba kwenye miaka hivi karibuni tumekuwa na mafanikio makubwa sana katika utendaji, wale ambao mnafuatilia nadhani mtakuwa mashahidi na sababu kubwa ya kwanini tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu tumekuwa na viongozi wanawake kwenye timu ya uongozi."

Sisi Absa, tuna idara mbalimbali, tuna idara nne za biashara, kati ya hizo, tatu zinaongozwa na wakurugenzi wanawake, wamepata promosheni hivi karibuni kuingia katika ngazi ya ukurugenzi, hawa ndio wakurugenzi wa biashara, hivyo basi mafanikio ya benki yetu hayawezi kabisa kutenganishwa na uwepo wa viongozi wanawake”, alisema Bw. Laiser.

Mmoja wa wahitimu wa programu hiyo, kutoka Benki ya Absa, Ikunda Kishimbo, ambayo tokea ianzishwe jumla ya washiriki 462 kutoka sekta binafsi na umma wamehitimu alisema, programu hiyo imewajengea washiriki kujiamini na kuwapa uwezo wa kiutendaji katika maeneo yao ya kazi.

Mafunzo yanayotolewa kupitia Programu ya Mwanamke Kiongozi pamoja na kuwa na lengo la kuongeza ujuzi wa wanawake viongozi, lakini pia yanasaidia kuongeza msukumo wa suala la usawa wa kijinsia katika mahali pa kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akizungumza machache kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo na benki hiyo, wakati wa maadhimisho na mahafali ya 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi inayoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wahitimu wa Programu ya Mwanamke Kiongozi inayoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kutoka Benki ya Absa Tanzania, Ikunda Kishimbo na Vailet Ephata, wakipozi kwa picha katika hafla ya maadhimisho na mahafali ya 10 ya programu hiyo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan (katikati), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia kwake), wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na wadhamini na viongozi mbalimbali, muda mfupi mara baada ya kukamilika kwa hafla ya maadhimisho na mahafali ya 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi iliyoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Share:

Sunday, February 23, 2025

KAMPUNI YA YAS YAIBUKA KINARA TUZO ZA TEHEMA

Kampuni ya mtandao wa simu ya Yas Tanzania usiku wa kuamkia Leo imeibuka kinara wa jumla katika Tuzo za Tehama zilizoandaliwa na mamlaka ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano TEHAMA.

ambapo katika Tuzo hiyo YAS imeibuka mshindi wa jumla kwa makampuni yanayoongoza kwa matumizi ya Teknolojia ya habari Tehama,ambapo imekuwa ikishindanishwa na makampuni mengine yanayotoa huduma kwa jamii.

Yas imekuwa kinara kwenye matumizi Teknolojia ambapo imekuwa ikijikita Zaidi katika Kutoka huduma mbalimbali ikiwemo Data, Mawasiliano ya simu,pamoja na kumbe FUPI sms, 

Mwishoni mwa mwaka Jana kampuni ya Yas iliweza kuibuka kinara na hatimaye kutwa Tuzo ya mshindi wa jumla Africa Tuzo zinazoandaliwa na shirika la kimataifa la OOKLA lenye maskani yake Nchini MAREKANI ambapo Yas zamani Tigo ilifanikiwa kuibuka mshindi mara mbili wa Tazo hiyo

Share:

WATANZANIA WAIBUKA KIDEDEA MBIO ZA YAS HALF INTERNATIONAL MARATHON 2025

Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Mbio za Yas Half international Marathon kwa upande wa wanaume Mtanzania, Inyasi Sule, akimaliza mbio hizo ktika mashindano Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro

Hatimaye watanzania wamefanikiwa kung'ara kwenye mashindano ya mbio za Kili marathon 2025, zilizofanyika Jana Moshi mkoani Kilimanjaro.

Maofisa wa Kampuni ya Yas pamoja na washiriki wengine wakiwa Kwenye mbio za Yas Half international Marathon ktika mashindano ya Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika mbio hizo mtanzania Suleiman Inyasi aliibuka Mshindi wa kwanza wanaume kwenye mbio za km 21.

Ambapo nafasi nyingine 3 zilishikwa na watanzania wengine wa 4 huku nafasi ya 5 ikuenda Kenya kwa Bernard Kiplagat ambaye amemshinda,shumeli Said WA Tanzania na Theophile Rugamba wa Rwanda.

Inyasi amefuatiwa na Watanzania wenzake, Samhenda Sombi na Peter Mwangi huku washindani wawili kutoka nchi za Kenya na Rwanda wakiambulia kuingia kumi bora.

Mbio za Kili International Marathon zinazoshirikisha wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni ambapo kipengele cha km 21 maarufu kama Nusu Marathon kinadhaminiwa na Kampuni ya mtandao wa simu ya Yas kwa mwaka wa kumi sasa.
Kwa mwaka huu 2025 washiriki zaidi ya 2000 wameshiriki mbio za Yas Marathon. 
Yas imekuwa mdhamini wa mashindano ya Kili marathon kwa mwaka WA 10 sasa ambapo awali yalikuwa yakidhaminiwa na chapa ya Tigo kabla ya kubadirika kuwa Yas

Mapema hapo Jana Serikali ikishirikiana na kampuni ya Yas iliendesha kampeni maalum ya upandaji miti, ikumbukwe kwa hizi ni mbio maalum kwa ajili ya wanariadha Kutoka mataifa kadhaa hususani Yale ya afrika mashariki ambao nchi kama Kenya, Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania zilimeshiriki mbio hizo
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive