A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, December 18, 2018

BENKI YA CBA NA VODACOM YAKABIDHI ZAWADI ZABAJAJI MPYA 5 KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA SHINDA NA M-PAWA

Mkurugenzi  Idara  Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani (kushoto),  akimkabidhi Mshindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na  M-PAWA  Bi.Mariam Balawa mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam, ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama  anaeshuhudia (kulia) ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya.
Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na  M-PAWA ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama, (katikati) ni Mkurugenzi  Idara  Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani na kulia ni Meneja Biashara Huduma yaM-PAWA Gloria Njiu.
Mkurugenzi  Idara  Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla yakuwakabidhi washindi wa Bajaji katika promosheni ya Shinda na  M-PAWA ambapo washindi watano walikabidhiwa bajaji zao na Bi Sophia mkazi wa Bukoba amekabidhiwa kitita cha Shilingi milioni kumi, hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika kwenye viwanja vya Benki hiyo Kijitonyama, (kushoto) ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya  na kulia ni Meneja Biashara Huduma ya M-PAWA Gloria Njiu.


Benki ya CBA na Vodacom imekabidhi zawadi kwa washindi wake wa promosheni ya SHINDA NA M-PAWA leo katika tawi la benki hiyo lililopo Kijitonyama.Zawadi hizo ni bajaji tano mpya. Promosheni hiyo iliyodumu wa wiki 6 ilifikia tamati hapo tarehe 14 mwezi huu.

Mshindi wa milioni kumi ni Mama Sophia Sarapion (54) ni mwenyeji wa Bukoba ambapo anaishi akijushughulisha na shughuli ya kilimo cha mihogo, Benki imepanga kumtembelea mshindi huyo mwezi ujao. Washindi watano wa bajaji ambao ni AbeidAbeid, Lucas Ngoye, MariamuBarawa, Hassan MsabilanaHamisiMpela wanatokea maeneo tofauti tofauti ya Tanzania ambayo ni Arusha (1),Chalinze (1) Dar Es Salaam (3).

Mama Sophia ambaye amefurahi sana ameishukuru benki ya CBA na Vodacom kwa kuunda promosheni hii akisema “M-Pawa haijanisaidia tu kwenye maisha yangu ya kila siku linapokuja swala la kutunza akiba na kupata mikopo inayoniwezesha kufanikisha mipango yangu bali imebadilisha maisha yangu kabisa.Nitatumia fedha hizi vizuri  katika kuboresha shughuli yangu ya kilimo”

Washindi watano wa bajaji wakiwa wamefurahia sana ushindi huo wameisifia benki ya CBA na Vodacom kwa mkakati wao wa kuirejeshea jamii fadhila kwa njia ya kuwezesha wananchi huku wakiwataka wateja wa M-Pawa kuendelea kutumia M-Pawa na kuwakaribisha ambao bado hawajaanza kutumia kujiunga.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya makabidhiano ya zawadi hizi kwa washindi,Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CBA Bwana Julius Konyani alieleza “Promosheni ya SHINDA NA M-PAWA ililenga kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki na kuwawekea mazingira ya kujiwekea akiba huku ikiwapa changamoto ya kurudisha mikopo yao kwa wakati pale wanapokuwa wamechukua mkopo.Mikopo yetu ina riba ndogo sana kwani lengo letu hasa ni kuwawezesha kiuchumi wateja wetu.Lengo letu jingine ilikuwa kuwashukuru na kuwazawaida wateja wetu msimu huu wa sikukuu.Tunafurahi washindi wetu wameweza kuwa ishara ya mafanikio yetu katika lengo hili

Benki ya CBA kwa ushirikiano na Vodacom tutaendelea kutoa huduma hii ya Mpawa kuweza kuwafikia watanzania wengi zaidi, wakiwemo wakulima na wajasiriamali kuweza kuwakwamua kwa kuwapa mikopo midogo midogo ya mpaka shilingi laki tano. Mbali na hayo M-Pawa inawapa fursa wateja kuhifadhi hela zao kwa malengo yao ya baadae, akiba yako ndio Malengo yako. Katika kipindi hichi cha promosheni tumefanikiwa kuwapata wateja wapya zaidi ya milioni moja wa M-pawa, hivyo Mpawa imekuwa na jumla ya watumiaji wa huduma hii wanayokaribia milioni nane.
Nawapongeza sana washindi wetu wote zaidi ya 1200 na pongezi za kipekee kwa mshindi mkuu na washindi watano waliojishindia bajaji wakawe mabalozi wetu popote watakapopita na waendelee kuhamasisha matumizi ya Mpawa.”

Kampeni ya SHINDA NA M-PAWA ilifanyika kwa muda wa wiki 6 kuanzia tarehe 8 Novemba hadi tarehe 13 Desemba ikilenga watumiaji wa huduma ya M-Pawa.Jumla ya washindi 1,296 walipatikana katika kipindi hicho cha promosheni.Huu ni Ushahidi kwamba jitihada za benki ya CBA na Vodacom katika kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki zinaendelea vyema.

Commercial Bank of Africa (CBA) is a commercial bank in Tanzania, regulated by bank of Tanzania. The bank is a subsidiary of the Commercial Bank of Africa Group.
Share:

Sunday, December 16, 2018

CHAMA CHA WAAJIRI ATE CHATOA TUZO ZA WAAJIRI BORA

Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jane Nyimbo akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa katika hafla ya kutoa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na chama hicho katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akiwa mgeni rasmi ilitoa tuzo kwa kutambua vipengele 17 kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji Tuzo kwa Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo Mh. Anthony Mavunde (MB), Mhe. Stella Ikupa (MP), wawakilishi wa balozi za Norway, Denmark, China  pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo TUKTA, ILO, na waajiri mbali mbali.

Mwakilishi kutoka kampuni ya utengenezaji Sigara  (TCC), akiwa amebeba Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya tatu katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) wapili (kulia) akikabidhi tuzo kwa Mwakilishi wa kampuini ya Bia Tanzania  (TBL), Lilian Makau wakati wakutoa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya Kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya pili katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa ATE Jane Nimbo watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho Dk. Aggrey Mlimuka.
Wafanyakazi wa Geita Gold Mine (GGM) wakifurahiya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) baada ya kampuni hiyo kuibuka kidedea nakushika nafasi ya kwanza  kwenye Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018e  hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani.

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Disemba 14 2018 kimeandaa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka
2018 zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Tangu kuanzishwa kwake
mwaka 2005, tuzo hizo zimejikita katika kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa
nguvu kazi na rasilimali watu kwa lengo la kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu na
kupelekea kukuza uzalishaji wa kibiashara. Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau mbali mbali
wakiwemo Mh. Jenista Mhagama, Mh. Anthony Mavunde, Mhe. Stella Ikupa, Mkuu wa Mkoa
DSM, Mhe. Paul Makonda, Balozi wa Norway nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark
nchini, Bw. Einer H. Jensen na Balozi wa China nchini Nd. Wang Fe, pamoja na taasisi mbali
mbali ikiwemo TUKTA na ILO.

Tuzo hizo zinazofanyika kila mwaka zimasaidia kuhamasisha wanachama kuchukulia masuala
ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama misingi muhimu katika kumwezesha mwajiri kuwa
na wafanyakazi wenye uwezo na ueledi ili kukidhi mahitaji ya ushindani katika biashara.
Sherehe ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa Mgeni Rasmi, zimekuwa
maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni
makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya
kufanya biashara nchini.

Tuzo hizo ambazo kwa mwaka 2017 ziliboreshwa kwa kuongezewa vipengele 12 vipya vya Hali
nzuri kwa Wafanyakazi (Employee Wellness), Kuvutia na kutunza wafanyakazi wenye ujuzi
(Attraction and Retention), Mahusiano Mazuri Mahali pa Kazi (Industrial Relations), Kujali kazi na
maisha nje ya Kazi (Work Life Balance), Mwajiri anayekubalika na Kufahamika (Employer
Branding), Usimamizi wa Wafanyakazi kwa kuzingatia Umri (Managing an Aging Workforce),
Uwekezaji katika Teknolojia (Technology Investment), Tuzo kwa ajili ya Sekta Binafsi (Private
Sector Award), Tuzo kwa Sekta ya Umma (Public Sector Award), Tuzo kwa Ajili ya Mashirika ya
Kijamii ( Civil Society Award) na Tuzo ya Mwajiri Mzawa (Indigenous Employer Award) ,
zitaendelea na vipengele hivyo vipya kwani vinatoa fursa kwa wanachama kufanyia kazi
vipengele hivyo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na ajira kulingana na mahitaji ya
waajiri nchini.

Akizumgumza na wageni waalikwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu alisema kwamba
serikali inatambua mchango wa waajiri kutoka sekta zote na itaendelea kushirikiana nao
pamoja na Vyama vya Wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika kutimiza azma ya nchi yetu
kujitegemea. Mhe. Jenista Mhagama aliongeza kuwa serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania, Dr. John Joseph Magufuli imebeba jukumu la kuboresha
miundombinu katika nyanja za usafirishaji wa anga, reli na maji, afya, nishati, elimu na
mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa zinaongeza uzalishaji wa nchi kupitia waajiri wa sekta
binafsi na umma.

Aidha Mh. Mhagama alipongea Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa shughuli zake mbali
ikiwemo Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Uongozi kwa Mwaka
2018, Mwanamke wa Wakati Ujao inayofanyika kwa ushirikiano na Shirikisho la Vyama vya
Waajiri nchini Norway (NHO) kutoa mafunzo kwa wanawake ili waweze kushika za juu za
uongozi katika makampuni na taasisi mbali mbali ambapo tangu kuasisiwa kwake mwaka 2016,
wanawake 66 wamehitimu mafunzo hayo.

Akiongea na wageni waalikwa, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jayne
Nyimbo Taylor alishukuru serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake katika kuboresha
mazingira ya kufanya biashara nchini kama punguzo la tozo inayolipwa na waajiri kwa ajili ya
kukuza ujuzi mahali pa kazi maarufu kama “Skills Development Levy (SDL)” kutoka 6% mpaka
kufikia 4.5% huku akiiomba serikali kuipunguza tozo hiyo hadi kufikia 2%. Pamoja na
mapendekezo hayo, Bi. Jayne Nyimbo pia aligusia changamoto mbali mbali zinazowakabili
waajiri kama ufuatiliaji wa vibali vya kufanya kazi nchini, utaratibu wa malipo ya Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo sekta binafsi wanalipa 1% huku waajiri wa umma wanalipa
0.5% ya mshahara anaolipwa mfanyakazi, aina mikataba ya ajira pamoja na tozo na faini
zinazotozwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Dkt.
Aggrey K. Mlimuka, alitoa shukrani zake za dhati kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wageni
waalikwa na wadau mbali mbali waliofanikisha Tuzo ya Mwajiri wa Mwaka 2018. “Naomba
nikushukuru tena Mhe. Mgeni Rasmi, na Washiriki wote kwa kuja kujumuika na sisi katika utoaji
wa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018, na naamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa
kushikiana na TUCTA pamoja na Serikali hasa tunapoendelea kujenga nchi yetu kuelekea
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Naomba kutumia fursa hii pia kuwashukuru na
kuwapongeza wanachama wote walioshiriki katika zoezi hili hasa kwa kujaza dodoso ili kupata
fursa ya kulinganisha utendaji wa makampuni yao na ya wengine.” Alisema Dkt. Mlimuka.
“Naomba kuhitimisha salamu zangu kwa kuwatambua uwepo wa baadhi ya wanachama na
wadau wetu kwa michango yao ambayo imetuwezesha kufanikisha utoaji wa tuzo hii ambao ni
wafuatao.” Alimalizia Dkt. Mlimuka.

Kuhusu Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ni chombo pekee cha waajiri kinachowawakilisha vema
nchini Tanzania. Kiliundwa mwaka 1960 ili kusimamia na kulinda maslahi ya waajiri katika
masuala ya kazi na ajira.

Kama sauti muhimu ya masuala ya kibiashara, Chama cha waajiri Tanzania kinawakilisha waajiri
katika sekta zote zinazohusu uchumi wa taifa isipokuwa zile za utumishi wa umma. ATE ina
jumla ya wanachama wa moja kwa moja wapatao 1500 waliosajiliwa na wengine zaidi ya 6000
wasio wa moja kwa moja wanaaotoka makampuni binafsi ya kibiashara na baadhi ya mashirika
ya umma.

Aidha zaidi ya mamlaka yake kuu ya kulinda maslahi ya waajiri na kuhakikisha mahusiano
mazuri baina ya waajiri na waajiriwa makazini, Chama cha Waajiri Tanzania pia kinahamasisha
na kuchochea mienendo mizuri ya usimamizi wa rasilimali watu na misingi bora miongoni mwa
waajiri ili kurahisisha uendeshaji wa biashara ambao ni muhimu katika uzalishaji na ushindani na
hivyo huandaa tuzo za waajiri kila mwaka ili kutambua na kuthamini makampuni yaliyofanya
vema katika kulinda misingi na mienendo ya usimamizi wa rasilimali watu.

Chama hutoa uanachama unaojumuisha makampuni makubwa, ya kati, madogo na madogo
zaidi kutoka sekta mbalimbali za uchumi wa taifa. Wanachama ni pamoja na makampuni binafsi
na ya umma, mashirika ya umma, vyama vya ushirika, balozi mbalimbali, vyama vya kibiashara,
taasisi za kidini, asasi binafsi (NGOs), na watu binafsi. Uanachama wa ATE upo kwa ajili ya waajiri
wote nchini Tanznia:- watu binafsi,vikundi, makampuni, mashirika ya umma, serikali za mitaa na
mamlaka zingine za nchi au vyama vya waajiri na kwa sasa chama kimegawanyika katika idara
8 ikiwemo kilimo, biashara, viwanda, ushirika na huduma, benki na fedha, madini, mafuta na
usalama binafsi.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na mratibu wa mradi wa tuzo za waajiri (EYA Project Coordinator)
Joyce Nangai kupitia +255 784 702670 au barua pepe nangai@ate.or.tz au wasiliana na Afisa
Mawasiliano (Communications Officer), Yunge Kanuda kupitia +255 657 453618 au barua pepe


kanuda@ate.or.tz


Share:

NBC yatoa elimu ya kifedha kwa mama na baba lishe soko la feri

Mkurugenzi wa wateja wadogo wa Benki ya NBC, Andrew Lyimo (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko, Sarah Laiser (kushoto), na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Alina Maria Kimaryo wakikabidhi msaada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa Mtendaji wa Soko la Samaki la Kivukoni, Mkuu Chanje (kulia), ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. Katika hafla hiyo iliyofanyika sokoni hapo juzi, NBC ilikabidhi pia tanki la maji vizibao kwa ajili ya baba na mama lishe na watoza ushuru pamoja pamoja na kutoa elimu ya masuala ya kifedha kwa wafanyabiashara sokoni hapo.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Alina Maria Kimaryo (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam juzi  ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (kushoto), akikabidhi vizibao kwa baadhi ya baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na tanki la maji sokoni hapo, Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao. 

Mkuu wa Kitengo cha Malalamiko wa Benki ya NBC ambaye pia alimwakilisha Mkurugenzi mtendaji wake, Sarah Laiser (wa tatu kushoto), akikabidhi msaada wa tanki la maji kwa Mtendaji wa Soko la Samaki la Kivukoni, Mkuu Chanje katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pia vizibao kwa baba na mama lishe pamoja na watoza ushuru sokoni hapo, Dar es Salaam juzi pamoja na vifaa vya kufanyia usafi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za benki hiyo katika kusaidia jamii. NBC pia ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao.

Nguli Wa masuala ya elimu za biashara na ujasiariamali, James Mwang’amba (kushoto), akizungumza na baadhi ya baba na mama lishe na wafanyabiashara wa Soko la Samaki la Kivukoni katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanyabiashara hao sokoni hapo. 

Baadhi ya baba na mama lishe na wachuuzi wengine katika Soko la Samaki la Kivukoni, wakifungua akaunti  kujiunga na Benki ya NBC kupitia huduma yao ya kufunguliwa akaunti mahali alipo mteja. NBC pia sokoni hao, Dar es Salaam, ilitoa elimu ya  masuala ya biashara na kifedha kwa wafanyabiashara hao pamoja na kuwapa msaada wa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na tanki la maji, vizibao na vifaa vya kufanyia usafi.

Mama lishe wa Soko la Kivukoni wakibeba pia la kuwekea takataka muda mfupi baada ya kukabidhiwa na benki ya NBC sokoni hapo juzi.
Share:

Friday, December 14, 2018

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Singida imetupilia mbali kesi ya rushwa iliyokuwa ikimkabili mfanyabiashara, Haidar Hussein Gulamali.


Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Consolata Singano ambapo amesema amezingatia ushahidi wa mashahidi 9 wa upande wa jamuhuri waliofika mahakamani hapo.

Katika uamuzi huo, Hakimu Singano amesema hakuna ushahidi unaomgusa Gulamali moja kwa moja.

Katika kesi hiyo ambapo  Mawakili wa Gulamali walikuwa Godfrey Wasonga, amesema moja ya sababu ni kutofautiana kwa mashahidi watatu kuhusu bahasha iliyobeba fedha. 

Katika ushahidi wao kila shahidi ametaja rangi tofauti ambapo mmoja ametaja Kaki, mwingine nyeupe, huku wa mwisho akitaja Brown jambo ambalo mahakama imeshindwa kuelewa  bahasha ipi ilibeba fedha.

Pia amesema hata mchakato wa ukamataji haupo vizuri kwani hakuna mahali iliyoonyesha Pesa ziliwahi kutaifishwa hadi zilipofikishwa mahakamani, pia namna zilivyotunzwa mpaka kuletwa kama ushahidi.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Singano amesema anatupilia mbali kesi hiyo na kumfanya Gulamali kuwa huru.
Share:

Thursday, December 13, 2018

Watanzania washauriwa kutumia huduma za kibenki za kidijitali


Meneja Masoko na Mawailiano wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera (kushoto), akikabidhi zawadi ya flat screen televisheni ya ukubwa wa inchi 40 kwa mshindi wa kampeni ya’fanya miamala ushinde’ ya benki hiyo, Darius Tebuka, jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni maofisa wa Barclays, Theresia Robert na Emmanuel Wangwe

WATANZANIA wametakiwa kutumia mifumo ya kibenki kwa njia za kidigitali badala ya fedha taslimu katika kufanya manunuzi hususani katika msimu huu wa sikukuu ili kujiepusha na vitengo vya wizi na unyang’aji.

Hayo yalisemwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendera jijini Dar es Salaam jana, wakati wakikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili wa kampeni iitwayo ‘fanya miamala ushinde’ inayoendeshwa na benki hiyo.

Kampeni hiyo ya miezi mitatu inahamasidha wateja wa benki hiyo katika kutumia huduma za kidigitali kama vile ATM,  na kupitia  simu za mkononi ili kufanya malipo mbalimbali kama vile, luku, bili za maji, ving’amuzi, kodi mbalimbali ama kuhamisha fedha kutoka katika akaunti ama kutoka kwenye akaunti kwenda katika mitandano ya simu za mkononi hivyo pia kupunguza muda wa kwenda katika matawi ya benki.

“Natoa hamasa kwa wateja wetu na kwa watanzania kuondokana na tabia ya kutembea na lundo la fedha mfukoni bali watumie huduma za Barclays za njia ya kidigitali kwani ni salama na za uhakika”, alisema.

Katika hafla hiyo, Darius Tebuka alikabidhiwa zawadi ya flat screen television yenye ukubwa inchi 40 aliwashauri watu kutokuwa na wasiwasi na matumizi ya huduma za kibenki kwa njia za kidigitali hapa nchini kwani ni salama na zinasaidia kuwapa muda wa kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali.

Share:

BENKI YA CBA NA VODACOM WATANGAZA MSHINDI MKUU WA KAMPENI YA M-PAWA NA WASHINDI WENGINE WATANO WALIOJISHINDIA BAJAJI KILA MMOJA.

Mkurugenzi  Idara  Usajili wa hazina wa Benki ya Biashara Afrika CBA Hakim Sheikh (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  kuchezesha  droo ya mwisho ya Promosheni iliyokuwa inakwenda kwa  jina la Shinda na  M-PAWA.  kushoto ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya pamoja na Sophet Mafuru hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  Idara  Usajili wa hazina wa Benki ya Biashara Afrika CBA Hakim Sheikh (kulia) akipiga simu kwa mmoja wa washindi wakati wa droo ya mwisho ya Promosheni iliyokuwa inakwenda kwa  jina la Shinda na  M-PAWA.  (Katikati)  ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya, pamoja na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Abdallah Hemedy

Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha  droo ya mwisho ya Promosheni iliyopewa jina la Shinda na  M-PAWA.  (wapilikushoto) ni Mkurugenzi  Idara  Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika CBA Julius Konyani ambae amemuwakilisha Mkurugenzi  Mkuu wa Benki hiyo,   Wengine  ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha  Jehud Ngolo pamoja na Sophet Mafuru.  hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam.


BENKI YA CBA NA VODACOM WATANGAZA MSHINDI MKUU WA KAMPENI
YA M-PAWA NA WASHINDI WENGINE WATANO WALIOJISHINDIA BAJAJI
KILA MMOJA.

Dar es Salaam, 13 Desemba 2018.

Benki ya CBA na Vodacom Tanzania waibua Mshindi Mkuu wa kampeni yao ya
‘‘SHINDA NA M-PAWA’’ iliyofikia tamati leo. Mshindi huyo aliyejinyakulia kitita cha
milioni kumi ni Sophia Sarapion wa Bukoba. Washindi wengine watano
waliopatikana kwenye droo hiyo kubwa waliojinyakulia bajaji moja moja ni Abeid
Abeid, Lucas Ngoye, Mariamu Barawa, Hassan Msabila na Hamisi Mpela.

Promosheni hii iliyowalenga, wateja wote wa M-PAWA nchini, imetengenezwa kwa
ajili ua kuwasaidia watumiaji kujiwezesha kifedha ili waweze kujiwekea utaratibu wa
kuweka akiba na kuwahimiza kurudisha mikopo mapema kwa riba za chini kabisa
kwa muda wa wiki 6 kuanzia tarehe 8 Novemba 2018 kukiwa na jumla ya wateja
1,296 wanaoshinda kwenye droo za kila wiki. Sambamba na draw ya washindi wa
mwisho droo hiyo imemalizia idadi ya wateja 200 waliongeza mara mbili ya amana
na wateja 15 walioweza kuchukua na kurejesha mikopo yao kabla ya wakati.

Wakizungumza kwenye muendelezo huo, washindi walitoa shukrani zao kwa Benki
ya CBA na Vodacom kwa kuwapa fursa hiyo ya kuwatuza na kuwawezesha wateja
kupitia kampeni ya “SHINDA NA M-PAWA’’.

Wakati akitoa tamko kwenye finali hizo za kampeni ya "SHINDA NA M-PAWA",
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CBA Bw. Hakim Sheikh alikiri
kwamba benki ya CBA imetimiza ahadi yao kwa wateja kwa kuwazawadia wote
walioshiriki na kufikia vigezo vya kampeni hiyo na wote walioshiriki katika droo zote
nne zilizopangwa wakati wa kampeni.

“Tunahimizwa na msisimko mkubwa wa ushiriki katika kampeni ya Shinda na MPAWA
na jinsi inavyoendelea kupokelea. Ukiacha zawadi mbalimbali walizoshinda
washiriki, ukweli ni kwamba kampeni hii imetupatia fursa kubwa ya kuwahamasisha
wateja wetu kuwa na utamaduni wa kujiweka akiba, ili kuwawezesha kifedha. Kwa
hiyo tunawahimiza Watanzania wasio wateja wa Benki ya CBA kujiunga na benki yetu
ili kufaidika na fursa mbalimbali za maendeleo zinazotolewa na Benki CBA”,
aliongeza Bw. Gift Shoko.

Katika maneno yake, Meneja Masoko wa M-PESA Vodacom, Bw. Noel Mazoya,
aliipongeza Benki ya CBA kwa kuendesha promosheni hiyo kwa uadilifu na uwazi.
Alithibitisha kuwa zoezi la kuchagua washindi hao lilifuata utaratibu toka mwanzo
wa kampeni Novemba 2018 hadi kuibuka kwa washindi mbalimbali. Aliwahimiza
wateja wenye bahati, hasa wale washindi, kutumia zawadi zao vizuri, na kusisitiza, ''
ni muhimu kuwekeza kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kukupa ushauri bure
unapohitaji''.

Commercial Bank of Africa (CBA) is a commercial bank in Tanzania. It is licensed by the Bank of Tanzania, the country's central bank and national banking regulator. The bank is a

subsidiary of the Commercial Bank of Africa Group.

Share:

Wednesday, December 12, 2018

VODACOM TANZANIA PLC YAWATUNUKU WATUMIAJI WA MTANDAO BOMBA POINTI ZA TUZO ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (katikati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom, points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu Noel na Mwaka Mpya, yenye kaurimbiu Nabaki mulemule na Vodacom “Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo Rosalynn Mworia na Kaimu Mkurugenzi wa biashara Linda Riwa.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo Rosalynn Mworia, akifafanua jambo kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, (hawapo pichani) juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom, points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu Noel na Mwaka Mpya, yenye kaurimbiu Nabaki mulemule na Vodacom. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Kaimu Mkurugenzi wa biashara Linda Riwa.
Kaimu Mkurugenzi wa biashara, Linda Riwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom, points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu Noel na Mwaka Mpya, yenye kaurimbiu Nabaki mulemule na Vodacom (katikati) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi pamoja na Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo Rosalynn Mworia.
Vodacom Tanzania yawatunukia watumiaji wa mtandao wake bomba kwa Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 Desemba, 2018 – Vodacom, kampuni ya simu nambari moja nchini, inagonga kengele za shangwe katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunukia wateja wake pointi za Tuzo zenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kama sehemu ya
mpango wa kampuni kuwashukuru wateja wao.

Programu hii ni ya kwanza kabisa iliyoletwa na kumpuni hiyo ambayo inawapatia wateja wake pinti za tuzo kila waongezapo salio au kufanya miamala ya M-Pesa. Wateja wanaweza kutumia pointi hizo kwa kuzibadili kupitia waleti zao za M-Pesa, kununua bando, na pia kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka ya Vodacom.

“Mapato ya Vodacom Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 6 katika mwaka huu, na ukuaji huu umechangiwa sana na wateja wetu. Hivyo Pointi za Tuzo ni njia ya kuonyesha shukrani zetu kwa watumiaji wetu na kwa moyo wa kutoa, tumeamua kufanya jambo la ziada katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunuku wateja wetu Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1,” alisema Hisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. “Ninawahimiza wateja wetu kuishi maisha ya ki-Tuzo, kununua muda wa maongezi na kufanya miamala mingi kadri inavyowezekana katika M-Pesa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na kujipatia pointi hapo hapo kila wafanyapo miamala hiyo,” aliongeza Hisham.

Wateja hao wanatunukia Pointi za Tuzo 50 kwa kila Shilingi 500 wanayotumia kununua salio. Pointi hizi za Tuzo zinaweza kulimbikizwa hadi miezi 12 tangu mtu aanze kujikusanyia na baada ya miezi hiyo 12 zisipotumiwa muda wake huisha. Wateja wa Vodacom wanaweza pia “Kulipa kwa Pointi” moja kwa moja kwa wafanyabiashara wanaopokea M-Pesa, kwa kupiga *149*01#>TUZO>TUZO POINTS>Vuna Pointi> (Nunua bando/Lipa/Badili kwa M-Pesa).

“Mwaka mzima, wateja wetu wamekuwa ndiyo walengwa na kiini cha ubunifu wetu –Vodacom Tanzania tumedhamiri kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kabisa,” alimalizia Hisham.
Share:

Tuesday, December 11, 2018

Benki ya Biashara ya DCB Yang’ara Tuzo za NBAA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya ushindi wa pili katika kitengo cha benki ndogo na za kati katika tuzo za Mwasilishi Bora wa Hesabu za Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi  wa Mahesabu (NBAA) kwa mwaka 2017 kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Prof. Isaya Jairo.
Mkurugebzi wa Fedha wa DCB, Zacharia Kapamba (katikati) akionyesha tuzo ambayo benki hiyo imeshinda, muda mfupi baada ya kukabidhiwa na naibu waziri wa fedha. Pamoja naye ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo. 
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Utendaji cha DCB, Siriaki Kiriki, wakionyesha tuzo ambayo benki hiyo imeshinda katika kitengo cha benki ndogo ngodo na za kati katika tuzo za  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)
Share:

Wednesday, December 5, 2018

NBC WAJIBIKA PROGRAMME ON THE MOVE!

James Mwang’amba (right) NBC Wajibika Youth Employability Programme coordinator describes the advantages of Wajibika programme to students from St. Joseph’s University at the university’s premises in Dar es Salaam recently. NBC Wajibika Youth Employability Programme is a program that is designed to prepare the youth for the world of work be it employment or self-employment by providing them with the requisite skills. The NBC Wajibika Programme is available online for free.
Eliana Mwibari (right) a coordinator with the NBC Wajibika Youth Employability Programme coordinator sharing knowledge of the NBC Wajibika programme to students of St. Joseph’s University at the university’s campus in Dar es Salaam recently. NBC Wajibika Youth Employability Programme is a program that is designed to prepare the youth for the world of work be it employment or self-employment by providing them with the requisite skills. The NBC Wajibika Programme is available online for free.
Share:

Tuesday, December 4, 2018

Experts meet in Dar to discus food safety concerns in Africa

African food experts, researchers and stakeholders will meet in Dar es Salaam  today to discuss challenges and concerns related to food safety, food borne diseases and chart out strategies on the best ways to improve food safety, nutrition and security for millions of Africans.

The international meeting is part of the commemoration of the Africa Day for Food and Nutrition Security 2018, is organized under the main theme “Sustained Food Safety Action for Improved Nutrition and Health of Africans,” bringing together participants from various African countries and key international and national agencies, World Food Programme, UNICEF, World Health Organization, Food and Agriculture Organization of the United Nations, African Union Commission, NEPAD and Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA).

The main agenda of the meeting, expected to be graced officially by the Permanent Secretary in the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Women, is food safety concerns and their associated main outcome, food-borne diseases, according to an official statement issued by the organizing agency, TFDA.

“Food-borne disease imposes large direct and economic burdens worldwide…Africans are not exception to this…” noted TFDA statement.

Experts says food borne disease are a constraint to the development and flourishing of domestic and exports food sectors in African economies, noting that “will be difficult to attain sustainable development goals or to meet the Malabo Declaration unless food borne disease in Africa is brought under control.”

TFDA said participants to the meeting will broadly and critically issues around food safety concerns, saying that “as developments advance towards a free trade zone for the continent, food safety concerns will become of even greater concern.”

There will be presentations of strategic and technical papers on food safety status in Africa, covering the health and economic burden, the riskier foods and people most at risk, current and previous food safety initiatives in the continent.

“Strategic papers will also include issues related to considerations on the nexus between food safety, nutrition and health and proposals on strategic directions towards improved food safety and regulatory frameworks,” noted part of TFDA statement.
Dr. Kandida Shirima, Director of Food Safety at TFDA, presenting a paper on food
safety status in Africa at the Africa Day for Food and Nutrition Security—2018 conference being held in Dar es Salaam which discusses food safety concerns in Africa.
Participants to the Africa Day for Food and Nutrition Security—2018 conference following proceedings of the meeting being held in Dar es Salaam which will discuss food safety concerns in Africa.
Share:

Monday, December 3, 2018

NBC kufanya maboresho makubwa ya huduma na biadhaa zake


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akielezea mpango mkakati wa miaka mitano ya benki hiyo  wenye lengo la kuboresha kwa kiwango kikubwa huduma za benki hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,  Theobald Sabi (kushoto),  akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mpango mkakati wa miaka mitano wa benki  hiyo wenye lengo la kufanya maboresho makubwa kwenye huduma zake. Kushoto kwake ni jopo zima la wakurugenzi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,  Theobald Sabi (katikati),  akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mpango mkakati wa miaka mitano wa benki  hiyo wenye lengo la kufanya maboresho makubwa kwenye huduma zake. Walioketi ni baadhi ya wakurugenzi wa NBC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,  Theobald Sabi (wa pili kushoto mstari wa mbele), akipiga picha ya kumbukumbu na wakurugenzi wa NBC waliohudhuria mkutano huo jijini Dar es Salaam leo .


Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive