A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Sunday, December 20, 2020

Tanga Cement yashinda ushindi wa jumla tuzo za NBAA kwa Mwaka 2019

 03

Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo kutoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mthibiti Fedha wa kampuni ya Tanga Cement Emmanuel Nkonyoka.
02%2B%25282%2529
Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela (kulia) pamoja na timy ya wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement PLC wakifurahia tuzo ya ushindi wa Jumla ya uwasilishaji Bora wa Taarifa ya Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika tuzo hizo.
01
Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo katoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement.

KAMPUNI ya saruji, Tanga Cement Plc, imeibuka kidedea katika tuzo za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) yam waka 2019/2020 kwa mara ya tano mfululizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mhasibu Mkuu wa Tanga Cement Plc, Issaac Lupokela, alisema kuwa kampuni hiyo imeibuka na ushindi wa Jumla katika tuzo hizo kwenye kipengele cha watumiaji wa mahesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa (IFRS) kwa miaka mitano mfululizo. Mshindi mwingine katika kipengele cha viwango vya kimataifa vya utunzaji fedha katika Sekta ya Umma ni TRA

Aidha, Tanga Cement waliibuka kidedea tena kwa kutangazwa kuwa washindi wa kwanza katika wazalishaji viwandani katika uwasilishaji bora wa taarifa za mahesabu za Boodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Washindi wengine ni kampuni ya bia, TBL PLC na Kiwanda cha Sigara, TCC.

“Huu ushindi nimejisikia furaha sana na kama vile waswahili tunavyosema ngoja ngoja huumiza tumbo ilikuwa kila saa niangalie vitabu vyangu kama mahesabu yamekaa vizuri kwa sababu nilikuwa nina wasiwasi. Ushindi nimeupokea kwa furaha sana kubwa huu ushindi ni wa mara ya tano mfululizokwenye Idara ya Uzalishaji na Ushindi wa Jumla kwa Kampuni zinazotumia Kanuni za Kimataifa za Uaandaaji Mahesabu “International Financial Report Standards (IFRS) imedhihirisha vitu tunavyofanya kwa ubora wa hali ya juu Tanga Cement Plc,” alisema Lupokela.

Akizungumzia siri ya kuibuka na ushindi kwa miaka mitano mfululizo, Lupokela alisema kuwa “Kila siku Tanga Cement Plc inataka iwe bora zaidi ya jana ambapo wameweka viwango vya juu sana. Kampuni yetu inaangalia mbali katika uendeshaji wake.”

Lupokela anasema kila mara huwa anasoma sana kuhakikisha kila mifumo ya uhasibu inapobadilika na kuja mipya hujaribu kuendana nayo kwa mujibu wa kanuni za kimataifa kitu kinachosaidiankatika maboresho.

Mhasibu huyo wa Tanga Cement Plc ameipongeza Bodi ya NBAA kwa kubuni tuzo hizo zinazosaidia kuongeza ubora katika utunzaji wa hesabu kwenye taasisi za Umma na Binafsi.

“Kila mtu anapoandaa mahesabu anajua kwamba kuna shindano liko nyuma kwa hiyo mashindano haya yanatupa motisha sana wa kuyafanya kwa ubora Zaidi. Lakini kitaaluma kubwa wahasibu ndio wanahakikisha coporate zinafanya kazi. Mahesabu yakiandaliwa vizuri yanasaidia hao wanayoyatumia kutumia kwa kufanya maamuzi yaliyo mazuri sana,” alisema.

Kwenye kipengele cha Benki Bora; Benki ya CRDB PLC ilkiibuka kidedea huku ikifuatiwa na NMB PLC na ABSA. Pia kwenye kipengele cha Benki Ndogo; DCB iliibuka mshindi huku ikifuatiwa na KCB Bank Tanzania, na City Bank Tanzania.

Katika kipengele cha Biashara na Usamabazaji; Vodacom Tanzania iliibuka mshindi huku ikifiuatiwa ba Swissport Tanzania na CMC Automobile. Mbali na hilo lakini pia TRA, iliibuka mshindi kwenye kipengele cha Taasisi za Umma na kufuatiwa na TASAC pamoja na TBC. Aidha, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Taasisi nyingine zilizoibuka washindi ni TAAWASA, DAWASA, IRUWASA, EWURA, TCAA, KYERWA District Council, Msksmbsko Town Council, Ilsls Municipsl, Mzumbe University, Sokoine University, Institute of Social Work, Catholic University of Health Science Life, Ministry of Finance & Planing, Account General Deptment, Drug Control & Enforcement Authority.

Taasisi nyingine za umma zilizoibuka kidedea katika kipengele cha watumiaji wa utunzaji fedha kwa viwango vya kimataifa (IFRS) kwa sekta ya Umma ni TANESCO na AICC. Kwenye kipengele cha Sekta ya Bima; mshindi ni Tanzania Re-insurance Compny Limited na kufuatiwa na Sanlam Life Insurance. Kwenye kipengele cha Mamlaka zinazohudumia Maji (Regulatory Authorizes) nalo liliibuka mshindi Ufanyaji

Bw. Maneno: “NBAA ilibuni shindano kuhakikisha watumiaji wanatumia viwango hivyo. Imekuwa kawaida kwa mashirika ya Umma na Taasisi binafsi kuleta mahesabu yao NBAA ambapo tumeweka viwango tunavyotumia katika mtandao. Viwango vina vinavyozingatiwa ni pamoja na lazima mshindi afikie pointi 75. ”

Mwaka huu washiriki walifikia 61 ambapo waligawanywa katika makundi 13; Benki Kubwa, Benki Ndogo, Mashirika ya Uzalishaji (Manufacturers), Mashirika yanayofanya biashara ya Usambazaji (Trading & Distribution), Wakala wa Serikali (Government Agencies), Wanaotumia Hesabu za Umma, Wanaotumia Mahesabu kwa kutumia viwango vya Kimataifa (IFRS), Makampuni ya Bima, Makampuni Usambazaji Maji, Serikali za Mitaa, Vyuo, Tawala za Mikoa (Local Government), Wizara na Idara za Serikali, Taasisi zisizotengeneza faida (NGOs), Makampuni madogo ya Ukaguzi.

“Hesabu lazima ziwe za mwaka 2019 (Januari -Desemba 2019), Taarifa za hesabu lazima ziwe zimefuata katika viwango vya kimataifa, Kampuni lazi iwe imesajiliwa Tanzania, Lazima kampuni ama Taasisi ya Serikali iwe imefuata viwango vya kimataifa vya utayarishaji na ukaguzi iwe imetumian mkaguzi aliyesajiliwa na NBAA, Iwe imepata hati safi ya ukaguzi,” alisema.

Awamu nyingine; Kampuni/Taasisi ya Umma imetimiza sharia za kuundwa kwake kwa kuangalia sharia zilizoundwa na Bunge ama sharia za makampuni (Company’s Act), Wakurugenzi wake wameonesha taarifa za hesabu vizuri, Wamefwata kanuni kwa walioorodheshwa kwenye soko la hisa, Zimefwata kanuni bora kwa mujibu wa kanuni za Soko la Mitaji (CMSA), Namna gani wameonesha viwango vya mahesabu.

Bw, Maneno, ametoa rai kwa kampuni na taasisi za umma ambazo hazikushiriki kushiriki kwani ukishiriki wa mashindano haya ya tuzo hakuna adhabu lakini iwapo utatoa taarifa ambazo hazikufuata viwango tunakuadhibu.
Share:

Saturday, December 19, 2020

AKIBA COMMERCIAL BENKI YAIPIGA JEKI TAASISIS YA FATA VICOBA ENDELEVU YADHAMINI MKUTANO WA MWAKA

 
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kushoto) akizungumza na wanachama wa Taasisi ya fata vicoba endelevu wakati wa halfa ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi hiyo ambapo mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam (wapili lishoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi futa vicoba endelevu Hanipha Tarimo, katibu wa Taasisi hiyo Rehema Sombi pamoja na Mtunza fedha Jefferson Makubo. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo
Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Innocent Ishengoma akizungumza na wanachama wa Taasisi ya fata vicoba endelevu wakati wa halfa ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi hiyo ambapo mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa ili watimize ndotozao kupitia benki ya ACB. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo
Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo ambae pia alikuwa Mgeni rasmi katika hafla ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi ya fata vicoba endelevu mkutano uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa ili waweze kutimiza ndotozao kupitia Benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi futa vicoba endelevu Hanipha Tarimo akitoa ufafanuzi kuhusu Taasisi hiyo wakati wa halfa ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa Taasisi hiyo ambapo mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya ACB kwa lengo la kukuza nakunufaisha wajasiliamali wadogo na wakubwa ili watimize ndotozao kupitia benki ya ACB. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa 361 uliyopo mwenge jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kinondoni kaya ya Mwananyamala Mulinga Samangwa, Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB),Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo, katibu wa Taasisi ya fata vicoba endelevu Rehema Sombi, pamoja na Mtunza fedha wa Taasisi hiyo Jefferson Makubo. Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mwanasheria Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Godfrey Songolo
Baadhi ya wanachama wa Taasisi ya fata vicoba endelevu na wateja wa Benki ya ACB wakiwa katika hafla ya Mkutano wao wa mwisho wa mwaka Uliodhaminiwa na Benki hiyo.
Picha ya Pamoja
Share:

KITILA MKUMBO AANZA KAZI ZAKUSAKA WA WEKEZAJI KWA SPEED YA 4G


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo (wa kwanza kutoka kushoto) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha KNAUF Gypsum Tanzania Ltd kilichopo mkoani Pwani, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ilse Boshoff (Aliyevaa nguo za Kitenge.)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji) Prof. Kitila Mkumbo akisalimiwa na baadhi ya Maafisa wa Halmashauri ya Ubungo alipofika kuangalia fursa za Uwekezaji katika Kituo kipya cha Mabasi Mbezi Luis.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akipata maelekezo ya Uzalishaji wa Unga katika Kiwanda cha Bakheresa Group kilichop Buguruni jijini Dar es Salaam.

KATIKA kuhakikisha Sekta ya Uwekezaji nchini inaendelea kukua kwa kasi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo ameendelea na uhamasishaji katika kutangaza vivutio vya Uwekezaji kwa kutembelea Miradi mbalimbali Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Prof. Kitila ametembea Kiwanda cha KNAUF Gypsum Tanzania Limited cha uzalishaji ‘Gypsum’ kilichopo mkoani Pwani ambacho kinazalisha bidhaa mbalimbali za ‘Gypsum Boards’, ‘Metal Profile’ na ‘Plaster Powder’ mahususi kwa ujenzi.

Akizungumza wakati wa ziara yake Kiwandani hapo, Prof. Kitila amepongeza uwekezaji huo kwa Uwekezaji hilo bora katika eneo hilo la mkoa wa Pwani, amesema Serikali inahitaji uwekezaji ambao unazalisha Ajira kwa Vijana na kuheshimu utu wa Watanzania. 

Prof. Kitila amepongeza Kiwanda hicho kukosa changamoto nyingi, pia ameeleza Serikali inahitaji kuwa na Uwekezaji ambao utaleta faida.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ilse Boshoff amesema wamevutiwa kuwekeza Tanzania kutokana na jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, hivyo wao kuona fursa ya Uwekezaji.

Pia ametembelea Kiwanda cha Bakheresa Group ambacho kinazalisha Unga kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam, Prof. Kitila amesema Serikali ina maono ya kuvutia, kuchochea Uwekezaji ili kusukuma Uchumi. 

“Bakheresa ni Mwekezaji mkubwa hapa nchini, sisi tumekubali kwa hilo tunaona ametoa ajira kwa Watu wapatao 4500 ambao ni wengi. Pia ni Mwekezaji anayetumia Malighafi za hapa ndani Kwa hiyo ni Mwekezaji muhimu kwa Wakulima”, amesema Prof. Kitila.

Amesema kuna uhitaji mkubwa wa mazoa ya Kilimo hivyo ni budi kwa Wakulima wa ndani kuhakikisha wanakuzi Kilomo cha ndani ili kuwa na Malighafi za kutosha kwa Wawekezaji, pia amesisitiza kuwa na ushirika kwa Wakulima hao ili kufikia lengo la uzalishaji wa Malighafi hizo.

Katika Kituo cha Kipya cha Mabasi kilichopo Mbezi Luis, Prof Kitila amefika kuangalia fursa za Uwekezaji kwa Wawekezaji wa ndani na wa nje, ameagiza Kituo cha Uwekezaji TIC kufanya uchambuzi wa kutosha kuhusu fursa zinazopatikana.
Share:

ZANTEL YAWAWEZESHA WATEJA KUMILIKI SIMU ZA SMARTA KWA URAHISI KUPITIA MALIPO KIDOGO KIDOGO

 

Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Haba na Haba Hununua Smarta’ iliyofanyika jana. Kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kununua simu aina ya Smarta kwa kulipa kidogo kidogo kuanzia Shilingi elfu moja kupitia akaunti ya Ezypesa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga.
Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga akionesha namna ya kufanya malipo kidogo kidogo kupitia akaunti ya Ezypesa ili kununua simu aina ya Smarta wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ijulikanayo kama ‘Haba na Haba Hununua Smarta’. Kushoto ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa.

Na Mwandishi Wetu | Zanzibar | Kwa kulipa kidogo kidogo kuanzia Shiling elfu moja, wateja wa Zantel wanaweza kununua simu aina ya Smarta ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni kuwawezesha watu wengi zaidi kunufaika na huduma za kidigitali.

Huduma hiyo imezinduliwa chini ya kampeni ijulikanayo kama ‘Haba na Haba Hununua Smarta’ itawawezesha wateja wa Zantel kutunza fedha kidogo kidogo kuanzia shilingi elfu moja (1,000/-) kwenye akaunti za Ezypesa na pale mteja anapofikisha kiwango cha 39,999/- ataweza kukitumia kununua simu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Mussa alisema kama kampuni ya kidigitali imeona kuna haja ya kuja na suluhisho litakalowawezesha wateja kumiliki simu janja bila kuathiri bajeti au matumizi muhimu kwa kulipa kidogo kidogo.

Tunatambua kwamba siyo watu wote wana uwezo wa kununua simu kwa kulipa pesa taslimu (Cash) na ndiyo maana tumekuja na huduma hii ili kuwawezesha wateja kulipa kidogo kidogo na kuwapunguzia mzigo wa kulipa kwa mara moja,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Bidhaa na Bei wa Zantel, Aneth Muga alisema mbali na kutunza pesa kwa njia ya Ezypesa, kupitia huduma hii wateja wanaweza kuchangiana kwa kumuingizia kiasi cha fedha kwenye akaunti yake ya Ezypesa ili kumuwezesha mmoja wao kumiliki simu janja aina ya Smarta.

Azma yetu ni kuhakikisha kila mtu anafikiwa na huduma za kidigitali na anufaike na fursa zake ikiwamo kujumuika na ndugu jamaa na marafiki lakini pia kufanya shughuli za uchumi.Kupitia huduma hii tumerahisisha zaidi upatikanaji wa simu janja bila kujali kipato cha mteja wetu,” alisema Muga.

Ili kupata huduma hii mteja wa Zantek atatakiwa kupiga *149*15# kisha 0 na kufuata maelekezo.Wateja watakaofanikiwa kufikisha kiwango wataweza kununua simu za Smarta kupitia maduka ya Zantel yaliyopo nchi nzima.

Simu za Smarta ni simu za bei nafuu zaidi sokoni hivi sasa zenye uwezo wa 4G na zinakuja na application mbalimbali ikiwamo YouTube, Google, Facebook na WhatsApp zinazomuwezesha mtumiaji kufurahia huduma mbalimbali za kidigitali.

Kuhusu Zantel:

Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.

Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).

Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.
Share:

Friday, December 18, 2020

BENKI YA CRDB YAWAPA ZAWADI ZA KUFUNGA MWAKA WANAFUNZI WA VYUONI

  
Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Abel Lasway (katikati) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa kampeni ya JIPE 5 na Scholar ambayo inaendeshwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo hapa nchini. Kulia ni Meneja wa Udhamini na Matukio wa Benki ya CRDB, Lilian Kanora na kushoto ni Evance Mkao ambae ni Meneja Uhusiano Upande wa Mauzo katika benki hiyo.
Sehemu ya laptop (kompyuta pakato) na smart phone (simu janja) ambazo zitatolewa kwa washindi wa kampeni ya JIPE 5 na Scholar ambayo inaendeshwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo hapa nchini.

Benki ya CRDB imetoa zawadi kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya kampeni ya JIPE 5 ambayo ilizinduliwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa na malengo ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba kuelekea mwisho wa mwaka. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja Mwandamizi wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Abel Lasway amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 mwezi huu, benki tayari imeshatoa jumla ya zawadi zinazofikia Shilingi Milioni 20. Zawadi hizo zimetolewa kwa wateja zaidi ya 4,000 huku akaunti zaidi ya 74,000 zikiwa zimekwisha funguliwa.

Tunawashukuru sana Watanzania kwa kuipokea vyema kampeni ya Jipe Tano ambapo mafanikio yaliyopatikana sio tu ni kwa faida ya Benki ya CRDB bali yanaonyesha ni kwa jinsi gani Benki ya CRDB imeweza kuwajumuisha Watanzania wengi katika mfumo rasmi wa huduma za fedha,” alisema Lasway.

Meneja huyo mwandamizi alisema katika kampeni hiyo ya Jipe Tano makundi mbalimbali ya wateja yameweza kuzawadiwa ambapo kwa mwezi huu wa Disemba Benki inawazawadia ada za shule wazazi wanaofungua akaunti ya watoto za Junior Jumbo. Jumla ya Shilingi Milioni 30 zimeandaliwa kwa ajili ya kutolewa kama zawadi ya ada kwa akaunti za watoto za Junior Jumbo zitakazofunguliwa mwezi Disemba.

“Benki ya CRDB tunajinasibu kwa kauli mbiu yetu ya “Ulipo Tupo” ambayo haiishii tu kufikisha huduma mahali ambapo wateja wetu wapo bali inalenga kuhakikisha Benki inakua pamoja na mteja katika hatua zote za maisha yake,” aliongezea Lasway.

Sambamba na zawadi hizo kwa akaunti za akiba na watoto, alisema Benki ya CRDB pia ililenga kundi la wanafunzi wa vyuo ambavyo vimefunguliwa hivi karibuni ambapo timu ya mauzo ya Benki iliweka kambi katika vyuo mbalimbali nchini ili kutoa elimu ya masuala ya fedha pamoja na kutoa huduma za kufungua akaunti kwa wanafunzi.

Nimefurahi kuona tumeweza kufanikiwa kuwaingiza katika mfumo rasmi wa fedha wanafunzi wengi na tukaona pamoja na kuwapa huduma hizi tuweze kuwazawadia vitu ambavyo vitarahisha maisha yao wawapo chuoni,” alisema Lasway huku akiongeza kuwa kupitia kampeni hiyo ya wanafunzi ya JIPE 5 na Scholar, jumla ya wanafunzi 100 kutoka vyuo mbalimbali nchini watazawadiwa laptop (kompyuta pakato) na smart phone (simu janja).

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa laptop (kompyuta pakato), Jackline Masayanyika mwanafunzi kutoka chuo cha Mtakatifu Agustino kilichopo jijini Mwanza, amesema kuwa zawadi hiyo itakua msaada mkubwa katika masomo yake ukizingatia uwepo wa fursa nyingi za masomo zinazopatikana mtandaoni.
Share:

TIC YAPOKEA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI UTURUKI

 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea Ugeni wa wafanyabiashra/wawekezaji kutoka Nchini Uturuki na umejumuisha Makampuni matano. Ugeni huo ukiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof. Elizabeth Kiondo ugeni huo umefika chini ili kukutana na wadau mbalimbali wanaohusika na kuwezesha uwekezaji nchini. 

Vilevile imebainika kwamba ugeni huo umefika nchini kutokana na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji yanayosimamiwa na Kituo cha Uwekezaji kwa wawekezaji Tanzania TIC ambapo muwekezaji anaweza kupatiwa ardhi, usajili wa kampuni, vibali na ushauri wa kimazingira. 

Akizungumza na vyombo vya habari, Mhe.Prof. Kiondo ameeleza kwamba ujgeni huo unawakilisha sekta za kilimo na zana za kilimo, viwanda vya nguo, viwanda vya kutengeneza pampas za watoto na watu wazima, vifaa tiba na dawa na viwanda vya kuunganisha vifaa vya kilimo. 

Pamoja na mambo mengine, ugeni huo umefika ili kueleza nia yao ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. Wawakilishi wa Taasisi zenye jukumu la kusaidia wawekezaji, wameeleza kwamba maeneo wanayokusudia kuwekeza ni miongoni mwa kipaumbele cha Serikali. 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Taasisi ambayo inahamasisha na kuvutia uwekezaji nchini, imetumia fursa hiyo kuelezea maeneo ambayo nchi inakaribisha wawekezaji hususan eneo la kuongeza thamani bidhaa za kilimo, uvuvi, madini, ufugaji, vifaa tiba, na katika eneo la utalii. 

Naye mmoja ya wageni hao akizungumza na waandiahi wa habari ameeleza kwamba wamekuja Tanzania kwa kuwa wameshafanya uchunguzi na kubaini kuwa Tanzania inakwenda na kasi ya Uchumi wa viwanda hivyo wamefanya maamuzi ya kuweka kiwanda cha kutengeneza pampas na vifaa tiba ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, katika sekta ya uchumi wa Viwanda. . 

Tayari tuna wawekezaji nchini kutoka Uturuki ambao wamewekeza kwenye sekta ya viwanda, elimu, ujenzi, kilimo na madini. 

Mkutano huo pia umehudhuriwa na wawakilishi kutoka TPSF, EPZA, SIDO, TCCIA na TNBC ambapo taasisi zote zimeonesha utayari wa kushirikiana na kampuni hizo katika kufanilisha uwekezaji wao hapa nchini.
Share:

PROF. KITILA ATINGA TIC, ATAKA TAARIFA ZA UWEKEZAJI KILA BAADA YA MIEZI MITATU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akisikiliza jambo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Ardhi anayehudumia Wawekezaji katika Kituo cha Uwekezaji (TIC,) Kituo cha Huduma za Mahala za Pamoja (One Stop Centre).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo (watatu kulia waliosimama) akitoa maelekezo kwa Maafisa mbalimbali wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), katika Kituo cha Huduma za Mahala za Pamoja (One Stop Centre).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA anayehudumia Wawekezaji katika Kituo cha Uwekezaji (TIC,) Kituo cha Huduma za Mahala za Pamoja (One Stop Centre).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Viongozi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC,) alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika ofisi hizo.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji,) Prof. Kitila Mkumbo rasmi ameanza kazi kwa kutembelea Ofisi za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) zilizopo jijini Dar es Salaam, kuangalia utendeji kazi wa Kituo hicho na kuhakikisha uhamasishaji Uwekezaji kutoka nje na ndani ya nchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Prof. Kitila amesema amefika TIC kuwapa muelekeo wa Serikali ya awamu ya tano kuhusu Uwekezaji, pia kusisitiza kubadili mifumo ya utendaji, Mitazamo ili kuvutia Wawekezaji.

Wawekezaji wa ndani wasisahaulike lazima wachukue nafasi yao, namna moja ya kusukuma Uchumi wetu ni kuvutia Uwekezaji wa ndani na nje.” ameeleza Prof. Kitila.

Prof. Kitila amesisitiza TIC kuhakikisha Wawekezaji kutoka nje ya nchi wanakamilishiwa taratibu za uwekezaji ndani ya siku 14, amesema jambo hilo linawezekana na tayari wamejipanga kukamilisha suala hilo, pia amewapa hamasa TIC kuhakikisha wanajulikana, kujitangaza kuhusu majukumu yao.

Tunataka TIC ijitangaze Kimataifa, fursa za Uwekezaji Tanzania na namna ya kuwekeza kwa Wawekezaji wa Wakubwa duniani kupitia Majarida ya Kimataifa na Vyombo vya Kimataifa”, amesema Prof. Kitila.

Pia Prof. Kitila ameagiza kuripotiwa maendeleo ya Uwekezaji nchini Tanzania kila baada ya miezi mitatu, kutoa taarifa ya idadi ya Wawekezaji, maeneo ya Uwekezaji, kiasi cha mitaji ya Wawekezaji, ajira zinazozishwa, pia kuwa na mahusiano na Taasisi za Serikali. 

Katika ziara hiyo Kituoni hapo, Prof. Kitila ametembelea Kituo cha Huduma za Mahala za Pamoja (One Stop Centre) katika idara zake mbalimbali za Uhamiaji, Ardhi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Shirika la Viwango (TBS).

Share:

Thursday, December 17, 2020

SGA SECURITY WINS TOP SECURITY AWARD AT THE TANZANIA CONSUMER CHOICE AWARDS CEREMONY IN DAR ES SALAAM

 
SGA Security Managing Director, Eric Sambu (second left) displays the award that his company received after being announced overall winner of the Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020 at the Tanzania Consumer Choice Awards ceremony held in Dar es Salaam over the weekend.
SGA Security Managing Director, Eric Sambu (seated second right) in a group photo with the award that the company won after it was announced overall winner of the Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020 at the Tanzania Consumer Choice Awards ceremony held in Dar es Salaam over the weekend.

SGA Security has made another first by being declared the overall winner of the Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020 at the Tanzania Consumer Choice Awards ceremony Dar es Salaam over the weekend.

SGA Security had been shortlisted with seven other security companies in a competitive survey that consumers were required to vote online. The competition ran for one month from 5th November 2020.

After the announcement, SGA Security officers were overwhelmed with joy as they took to the podium to accompany their Managing Director, Mr Eric Sambu, who received the award.

In his appreciation speech, Mr Sambu explained that SGA was celebrating its 50th anniversary this year, and was the first security company to be registered in Tanzania, as Group 4 Security (T) Ltd. They have remained on top since and currently employs over 6,000 Tanzanians.

We dedicate this award to our customers for having faith and confidence in our service. This motivates us to work extra hard to give them value for money”, Mr Sambu said.

He also saluted his staff for giving the company competitive advantage. “There are about 2,000 private security companies in Tanzania. What differentiates us is how we deliver the service to our customers. This award is a clear demonstration that we know what the customers want, and we know how to deliver it. Our employees remain our focus to ensure that they always exceed customer expectation”, he added.

On her part, SGA Marketing Manager – Faustina Shoo – expressed joy after receiving the award during a very challenging year caused by Covid-19 pandemic. “At SGA we remained forthright and customer focused. Together, we are stronger amidst the pandemic. We thank the customers and the public for their trust”, she said.

SGA Security provides guarding services, alarm response service, cash services, electronic security solutions, courier services amongst others. The company is the only ISO18788 certified (Security Operations Management System). It also has ISO 9001: 2015 and ISO 45000:2018 (Occupation Health and Safety) amongst other accolades.

Mr Sambu explained that he values the close working relationship with police force, especially in training, pre-employment vetting, investigation, response and operations.

He urged other companies to adhere to good standards of service by emulating this and called on them to take care of their employees by paying good salaries and on time so that they are motivated to work. “Investing in people is a good investment. Continuous training as required by police is key to success”, he added.

While stating the future plans for SGA, Mr Sambu said they will continue to invest in people, technology and innovation to give value for money to its customers and continue to create value to the society.

He said they look forward to retaining the trophy next year as he thanked the organisers of the Consumer Choice Awards for the approach used, for having customers vote for who they prefer, adding that this is the most legitimate award in the region. It will bring positive change in service delivery.
Share:

Wednesday, December 16, 2020

BENKI YA CRDB YAENDELEA KUIBUKA KINARA KATIKA TUZO ZA MABENKI NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), akikabidhiwa tuzo ya benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi kwenye hafla ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika tarehe 13 Desemba 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akiwashukuru wateja kwa kuichagua Benki ya CRDB kuwa benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi kwenye hafla ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika tarehe 13 Desemba 2020.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania (kushoto), Sanjay Rughani kwenye hafla ya tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika tarehe 13 Desemba 2020.

Benki ya CRDB imeibuka na tuzo ya benki ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi (Most Preferred Domestic Bank of the Year) kwenye tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards 2020 zilizofanyika Jumapili, 13 Desemba 2020. Tuzo hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu Benki ya CRDB ilipoibuka kinara kwenye tuzo zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kama Taasisi ya Fedha iliyoongoza kwa kuwasilisha Taarifa ya Fedha bora kwa mwaka 2018/2019 kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Tuzo za Tanzania Consumer Choice Awards ni tuzo zinazotolewa kila mwaka zikilenga kutambua ubora wa biashara mbalimbali kutokana na kura zinazopigwa na wateja wake. Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abudlmajid Nsekela amewashukuru wateja na Watanzania kwa ujumla kwa kuichagua Benki ya CRDB kama benki yenye asili ya ndani ya nchi inayopendwa zaidi (Most Preferred Domestic Bank of the Year).

Ushindi huu ni ishara tosha kuwa wateja wetu na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Benki yao ya CRDB na hivyo hii kwetu sisi ni deni ambalo tunapaswa kuwalipa kwa imani hii kubwa waliyotupa. Ahadi yetu ni kuendelea kutoa huduma bora zinazoendana na mahitaji ya wateja ambayo yamekua yakibadilika kila uchao” alisema Nsekela.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye tuzo hizo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe ameitaka sekta binafsi kuwa mstari wa mbele katika kusukuma mbele gurudumu la uchumi wa nchi kwa kuwa sasa hivi wameshaelewa maono na mtazamo wa Serikali ya Awamu ya Tano katika masuala ya uchumi.

Wito wangu kwa wafanya biashara ni kuhakikisha wanazalisha bidhaa na huduma ambazo zitakidhi mahitaji ya soko la ndani lakini pia kuweza kushindana katika masoko ya nje na naamini uwezo huo tuko nao na sisi kama serikali tutaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya wafanyabiashara", Alisema Naibu Waziri Kigahe
Share:

Monday, December 14, 2020

Absa Tanzania Yashinda Tuzo Ya Benki Bora Ya Kimataifa nchini Tanzania

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe Exaud Silaoneka Kigahe (wa pili kulia) akikabidhi cheti cha shukrani kwa kutambua mchango wa Benki ya Absa Tanzania kama mdhamini mkuu wa tuzo za kila mwaka za walaji (Tanzania Consumer Choice Awards), kwa Ofisa Fedha Mkuu wa benki hiyo, Obedi Laiser katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Lavine International Agency, Albert Makoye na Mwanzilishi wa tuzo hizo, Diana Laiser.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (katikati) akikabidhi tuzo ya kampuni bora ya vinywaji laini nchini kwa Meneja Mkuu wa Kundi la Mampuni ya Vinywaji ya Sayona, Nitin Menon na Meneja Mkuu wa Uzalishaji, Shahid Choudhary wakati wa hafla ya Tuzo bora za mwaka za Walaji (Tanzania Consumer Choice Awards), iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (katikati) akikabidhi tuzo ya kampuni bora ya bima nchini kwa Meneja Mkuu Msaidizi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, Abdul Rauf Suleiman wakati wa hafla ya Tuzo bora za mwaka za Walaji (Tanzania Consumer Choice Awards), iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Marco Yambi. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (wa pili kulia) akikabidhi tuzo ya kampuni bora ya mafuta na gesi nchini kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil, Frank Nyabundege wakati wa hafla ya utoaji tuzo bora za walaji za kila mwaka (Tanzania Consumer Choice Awards), iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Maofisa wa kampuni hiyo. Benki ya Absa ni mdhamini mkuu wa tuzo hizo. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Exaud Silaoneka Kigahe (wa tatu kulia) akikabidhi tuzo ya Benki Bora ya Kimataifa ya Mwaka nchini kwa Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo bora za walaji za kila mwaka (Tanzania Consumer Choice Awards) iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo. Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizo ikitoa jumla ya shs milioni 20 kuzidhamini.
Share:

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Apongeza Uwezeshaji Unaofanywa Na Benki Ya CRDB Kwa Wanawake

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mahusiano Tawi la Oysterbay, Witness Kileo kuhusu uwezeshaji unaofanywa na Benki yetu kwa Wanawake kupitia CRDB Malkia wakati wa Mkutano Mkuu wa Pili na Madirisha uliofanyika jumamosi hii katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini kupitia huduma ya CRDB Malkia. Mheshimiwa Pinda ametoa pongezi hizo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Pili wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake la MADIRISHA uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) ambapo Benki ya CRDB ilikuwa ni mdhamini mkuu. 

Nimefurahishwa kusikia hapa tayari mmeshafanya uwezeshaji wa zaidi ya shilingi bilioni 600 kwa wanawake wajasiriamali kupitia CRDB Malkia. Uwezeshaji huu unaleta chachu ya wanawake wengi zaidi kushiriki katika shughuli za Maendeleo katika taifa letu. Hongereni sana,” alitoa pongezi Mheshimiwa Pinda.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Pili na Madirisha uliofanyika jumamosi hii katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Pinda aliipongeza Benki hiyo pia kwa ushiriki wake katika makangamano na semina mbalimbali za uwezeshaji akisema kwa kufanya hivyo kunasaidia kufikisha elimu ya ujasirimali na masuala ya fedha kwa wanawake zaidi. Tafiti zinaonyesha ni asilimia 60 tu ya Wanawake ndio waliofikiwa na huduma za kifedha huku wengi wao wakiwa nyuma katika shughuli za ujasiriamali kutokana na kukosa elimu.

Leo hii mmetoa elimu nzuri sana juu ya fursa za uwezeshaji zinazotolewa na Benki hii. Niwapongeze lakini niwasihi mfikishe elimu hii kwa wanawake wengi zaidi mjini na vijijini,” aliongezea Mheshimiwa Pinda. 

Akizungumzia kuhusiana na huduma za uwezeshaji kwa Wanawake zinazotolewa na Benki ya CRDB, Mheshimiwa Pinda alipongeza hatua ya Benki hiyo kupunguza riba ya mikopo inayotolewa kwa wanawake wajasiriamali kutoka asilimia 24 hadi asilimia 14.

.. Kupungua huku kwa riba na masharti mengine yaambatanayo kunatoa fursa kwa Wanawake wengi zaidi kunufaika na CRDB Malkia,” alisema Mheshimiwa Pinda huku akiwahamasisha Wanawake wote kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hizo zinazotolewa na Benki yao ya CRDB.


Akiwasilisha mada katika mkutano huo, Meneja Uwezeshaji Wanawake Benki ya CRDB, Rehema Shambwe alisema huduma ya CRDB Malkia imelenga katika kumtambua, kumpa nafasi na kumuwezesha mwanamke wa Kitanzania kufikia malengo yake kupitia mikopo ya biashara na ujasiriamali, kujiwekea akiba kwa akaunti ya Malkia na mafunzo ya uendeshaji biashara. 

“Mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi June mwaka huu, Benki yetu tayari ilikuwa imekwisha toa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 600 kwa wanawake zaidi ya elfu 55,” alisema Rehema huku akibainisha kuwa zaidi ya wanawake 30,000 tayari wameshajiunga na akaunti ya Malkia. 

Rehema alisema pamoja na mafanikio ambayo Benki ya CRDB imeyapata katika kumuwezesha mwanamke, bado idadi ndogo ya wanawake wamekuwa wakijitokeza kupata huduma kutokana na changamoto ya riba, masharti magumu ya dhamana na kukosa uelewa wa huduma za kifedha.


Tukiwa Benki ya kizalendo inayothamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu, tukasema ni vyema tukatafuta suluhisho la changamoto hizi ili kuweza kumsaidia mwanamke kufankisha malengo yake zaidi,” alisisitiza Rehema. 

CRDB Malkia sasa hivi inawawezesha wanawake kupata mikopo kwa riba ndogo ya asilimia 14 kulinganisha na asilimia 24 iliyokuwa ikitozwa mwanzo huku masharti ya upatikanaji wa mikopo yakirahisishwa kwa kiasi kikubwa. 

Kupungua kwa riba kuna maana wanawake sasa wanaweza kukopa zaidi na kwa gharama nafuu kulinganisha na mwanzo hivyo kusaidia kufanikisha malengo yao kwa uharaka zaidi,” alisema Rehema.  

Rehema alibainisha kuwa kupitia CRDB Malkia, Benki ya CRDB pia imeanzisha huduma ya Malkia Rafiki katika mitandao wake wa matawi ambao watakuwa wanawasidia wanawake kupata huduma stahili kwa uharaka na elimu juu ya huduma hizo ili kuwawezesha kufikia lengo.


Naye Muanzilishi na Mwenyekiti wa Jukwaa la MADIRISHA, Fatma Kange aliishukuru Benki ya CRDB kwa udhamini iliyoutoa kufanikisha Mkutano Mkuu huo ambao kwa mara ya kwanza umeweza kuhudhuriwa na wanawake zaidi 1,000.

.. Wanawake sasa tumepata Benki kimbilio na sehemu ya kuelezea mahitaji yetu. Tuishukuru Benki ya CRDB kwa kutushika mkono na kwa kutuheshimisha Wanawake kupitia CRDB Malkia,” alisema Fatma Kange huku Akitoa rai kwa Wanawake wote kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki hiyo.

Share:

Saturday, December 12, 2020

Wafanyakazi Wa Benki Ya Absa Wajitolea Kusaidia Watoto


Mkuu wa Huduma za Kibiashara wa Benki ya Absa Tanzania, Pius Makalle akikabidhi baadhi ya vitu walivyotoa msaada kwa Meneja wa Mahabusu ya Watoto Upanga, Darius Damas (wa tano kushoto), kituoni hapo, Upanga, Dar es Salaam Jana. Katika hafla hiyo wafanyakazi hao walikabidhi vifaa vya umeme wa sola, jokofu, vyakula na misaada mingine ya kibinadamu vyenye thamani ya zaidi ya shs milioni 6.7.
Meneja Rasilimali watu wa Benki ya Absa Tanzania, Anna Chacha, akikabidhi baadhi ya vitu walivyotoa msaada kwa Meneja wa Mahabusu ya Watoto Upanga, Darius Damas (wa tano kushoto), kituoni hapo jijini Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo wafanyakazi hao walikabidhi vifaa vya umeme wa sola, jokofu, vyakula, na misaada mingine ya kibinadamu vyenye thamani ya shs milioni 6.7.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania wakibeba misaada mbalimbali wakati wakiwasili katika mahabusu ya watoto Upanga jijini Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo wafanyakazi hao walikabidhi vifaa vya umeme wa sola, jokofu, vyakula, na misaada mingine ya kibinadamu vyenye thamani ya shs milioni 6.7.
Share:

Monday, December 7, 2020

STAMICO YAPATA TUZO YA MFANYABIASHARA MSHIRIKA BORA, NCHINI INDONESIA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt.Venance Mwasse akiwa katikati akiwa ameshika tuzo ya Mfanyabiashara na Shirika Bora katika sekta ya madini zilizotolewa na Ubalozi wa Indonesia nchini ,jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Indonesia nchini akiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kutoa tuzo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya Balozi wa Indonesia akiwa baadhi ya walitunukiwa vyeti na Tuzo katika sekta ya madini katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kuchanja mbuga kimataifa baada ya kupata tuzo ya mfanyabiashara mshirika bora katika sekta ya madini kutoka nchi ya Indonesia kwa mwaka 2020. 

Tuzo hiyo imetolewa na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Prof. Ratlan Pardede katika hafla ya kutambua na kuthamini mchango wa wafanyabiashara washirika wa nchi ya Indonesia iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa Indonesia zilizopo jijini Dar es salaam.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse ameushukuru ubalozi wa Indonesia kwa kutambua mchango wa shirika katika uwekezaji kwenye sekta ya madini na kusema kuwa tuzo hiyo ni chachu ya kimaendeleo na ishara ya mabadiliko ya STAMICO katika kujiendesha kibiashara na kujitanua kimataifa.

Dkt.Mwasse alisema STAMICO imekuwa na ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu baina yake na Shirika la Madini la Indonesia lijulikanalo kama PT.Timah, ushirikiano huo umepelekea kusaini hati ya makubaliano katika kuendeleza sekta ya madini kupitia miradi mbalimbali hususani ya madini ya bati yaliyopo wilayani Kyerwa.

Ushirikiano huo umefungua milango ya wataalamu wa madini kutoka Shirika hilo la madini kuja nchini kujionea maeneo ya uwekezaji na kufanikiwa kuchukua sampuli za madini ya bati na dhahabu na kuyapeleka katika maabara ya madini iliyo chini ya wakala wa jiolojia na utafiti GST jijini Dodoma ili kuweza kujiridhisha zaidi.

Katika kuendeleza ushirikiano huo Balozi wa Indonesia Prof. Dkt. Ratlan Pardede ameishukuru STAMICO kwa hatua ya kusaini hati ya makubaliano na kutoa ushirikiano mkubwa wa kitaalamu kwa wawekezaji waliokuja nchini na kuwapeleka katika maeneo mbalimbali ya miradi.

Aidha, ameipongeza STAMICO chini ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake Dkt. Mwasse kwa jitihada zake za dhati za kuendeleza mawasiliano na taasisi ya PT.Timah licha ya kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa Covid19 ambao ulitikisa dunia. 

Alisema hii ni dhamira ya dhati inayodhihirisha nia ya Shirika hilo katika kuwavutia wawekezaji kwenye sekta ya madini. 

Alisema STAMICO imetunukiwa tuzo hiyo miongoni wa taasisi nne zikiwemo ambazo zimetoa mchango na ushirikano mkubwa kwa wawekezaji kutoka nchini Indonesia.

“Tuzo hii kwa STAMICO ni ishara kuwa Shirika limeanza kufungua milango ya kuwasaidia wachimbaji wadogo, kwa kuwaunganisha wawekezaji na wachimbaji wadogo ili kuweza kuboresha shughuli na kuinua sekta ya uchimbaji mdogo ambayo kwa muda mrefu imeonekana ni sekta duni.” alisema.

Aidha, aliahidi kuendelea kufanya kazi na STAMICO bega kwa bega ili kuboresha sekta ya madini nchini na kutoa mwaliko kwa wataalamu wa STAMICO kutembelea taasisi za madini zilizopo nchini indonesia ili kupata uzoefu utakaoleta chachu ya mabadiliko katika sekta hiyo.

Akizungumzia malengo ya baadaye Dk. Mwasse ameongeza kuwa bado kuna mikakati mingi inayoiunganisha STAMICO na nchi ya Indonesia ikiwemo biashara ya madini ya bati inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

“Kuna mpango wa kufanya ziara ya wataalamu katika taasisi ya PT.Timah iliyopo nchini Indonesia kufuatia mwaliko walioupata tangu mwanzoni mwa mwaka huu kwenda kujionea na kujifunza kwa vitendo namna Indonesia inavyofanya kazi katika sekta ya madini.

“Pia tutaimarisha mradi wa madini ya bati ili kuboresha soko la madini hayo litakalochochea kukua kwa uchimbaji wa madini ya bati na kubora hali ya Maisha ya wachimbaji wadogo,” alisema.

Aidha, Alisema imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dk. John Magufuli za kuboresha na kuendeleza uwekezaji nchini kwa kuhakikisha wawekezaji wanapewa ushirikiano na kupata taarifa zinazohusika
Share:

Tanga Cement yashinda ushindi wa jumla tuzo za NBAA kwa Mwaka 2019

Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo kutoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mthibiti Fedha wa kampuni ya Tanga Cement Emmanuel Nkonyoka.
Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela (kulia) pamoja na timy ya wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement PLC wakifurahia tuzo ya ushindi wa Jumla ya uwasilishaji Bora wa Taarifa ya Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika tuzo hizo.
Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo katoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive