A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, December 20, 2020

Tanga Cement yashinda ushindi wa jumla tuzo za NBAA kwa Mwaka 2019

 03

Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo kutoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mthibiti Fedha wa kampuni ya Tanga Cement Emmanuel Nkonyoka.
02%2B%25282%2529
Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela (kulia) pamoja na timy ya wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement PLC wakifurahia tuzo ya ushindi wa Jumla ya uwasilishaji Bora wa Taarifa ya Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika tuzo hizo.
01
Kamishna wa Fedha anaesimamia sekta za maendeleo katoka Wizara ya Fedha Dk. Charles Mwamaja (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya ushindi wa kwanza wa kipengele cha Wazalishaji Bora katika tuzo za Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Mahesabu za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) ya mwaka 2019 kwa Mkuu wa divisheni ya Fedha wa Kampuni ya Tanga Cement PLC, Isaac Lupokela, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Wahasibu kutoka kampuni ya Tanga Cement.

KAMPUNI ya saruji, Tanga Cement Plc, imeibuka kidedea katika tuzo za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) yam waka 2019/2020 kwa mara ya tano mfululizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mhasibu Mkuu wa Tanga Cement Plc, Issaac Lupokela, alisema kuwa kampuni hiyo imeibuka na ushindi wa Jumla katika tuzo hizo kwenye kipengele cha watumiaji wa mahesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa (IFRS) kwa miaka mitano mfululizo. Mshindi mwingine katika kipengele cha viwango vya kimataifa vya utunzaji fedha katika Sekta ya Umma ni TRA

Aidha, Tanga Cement waliibuka kidedea tena kwa kutangazwa kuwa washindi wa kwanza katika wazalishaji viwandani katika uwasilishaji bora wa taarifa za mahesabu za Boodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Washindi wengine ni kampuni ya bia, TBL PLC na Kiwanda cha Sigara, TCC.

“Huu ushindi nimejisikia furaha sana na kama vile waswahili tunavyosema ngoja ngoja huumiza tumbo ilikuwa kila saa niangalie vitabu vyangu kama mahesabu yamekaa vizuri kwa sababu nilikuwa nina wasiwasi. Ushindi nimeupokea kwa furaha sana kubwa huu ushindi ni wa mara ya tano mfululizokwenye Idara ya Uzalishaji na Ushindi wa Jumla kwa Kampuni zinazotumia Kanuni za Kimataifa za Uaandaaji Mahesabu “International Financial Report Standards (IFRS) imedhihirisha vitu tunavyofanya kwa ubora wa hali ya juu Tanga Cement Plc,” alisema Lupokela.

Akizungumzia siri ya kuibuka na ushindi kwa miaka mitano mfululizo, Lupokela alisema kuwa “Kila siku Tanga Cement Plc inataka iwe bora zaidi ya jana ambapo wameweka viwango vya juu sana. Kampuni yetu inaangalia mbali katika uendeshaji wake.”

Lupokela anasema kila mara huwa anasoma sana kuhakikisha kila mifumo ya uhasibu inapobadilika na kuja mipya hujaribu kuendana nayo kwa mujibu wa kanuni za kimataifa kitu kinachosaidiankatika maboresho.

Mhasibu huyo wa Tanga Cement Plc ameipongeza Bodi ya NBAA kwa kubuni tuzo hizo zinazosaidia kuongeza ubora katika utunzaji wa hesabu kwenye taasisi za Umma na Binafsi.

“Kila mtu anapoandaa mahesabu anajua kwamba kuna shindano liko nyuma kwa hiyo mashindano haya yanatupa motisha sana wa kuyafanya kwa ubora Zaidi. Lakini kitaaluma kubwa wahasibu ndio wanahakikisha coporate zinafanya kazi. Mahesabu yakiandaliwa vizuri yanasaidia hao wanayoyatumia kutumia kwa kufanya maamuzi yaliyo mazuri sana,” alisema.

Kwenye kipengele cha Benki Bora; Benki ya CRDB PLC ilkiibuka kidedea huku ikifuatiwa na NMB PLC na ABSA. Pia kwenye kipengele cha Benki Ndogo; DCB iliibuka mshindi huku ikifuatiwa na KCB Bank Tanzania, na City Bank Tanzania.

Katika kipengele cha Biashara na Usamabazaji; Vodacom Tanzania iliibuka mshindi huku ikifiuatiwa ba Swissport Tanzania na CMC Automobile. Mbali na hilo lakini pia TRA, iliibuka mshindi kwenye kipengele cha Taasisi za Umma na kufuatiwa na TASAC pamoja na TBC. Aidha, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Taasisi nyingine zilizoibuka washindi ni TAAWASA, DAWASA, IRUWASA, EWURA, TCAA, KYERWA District Council, Msksmbsko Town Council, Ilsls Municipsl, Mzumbe University, Sokoine University, Institute of Social Work, Catholic University of Health Science Life, Ministry of Finance & Planing, Account General Deptment, Drug Control & Enforcement Authority.

Taasisi nyingine za umma zilizoibuka kidedea katika kipengele cha watumiaji wa utunzaji fedha kwa viwango vya kimataifa (IFRS) kwa sekta ya Umma ni TANESCO na AICC. Kwenye kipengele cha Sekta ya Bima; mshindi ni Tanzania Re-insurance Compny Limited na kufuatiwa na Sanlam Life Insurance. Kwenye kipengele cha Mamlaka zinazohudumia Maji (Regulatory Authorizes) nalo liliibuka mshindi Ufanyaji

Bw. Maneno: “NBAA ilibuni shindano kuhakikisha watumiaji wanatumia viwango hivyo. Imekuwa kawaida kwa mashirika ya Umma na Taasisi binafsi kuleta mahesabu yao NBAA ambapo tumeweka viwango tunavyotumia katika mtandao. Viwango vina vinavyozingatiwa ni pamoja na lazima mshindi afikie pointi 75. ”

Mwaka huu washiriki walifikia 61 ambapo waligawanywa katika makundi 13; Benki Kubwa, Benki Ndogo, Mashirika ya Uzalishaji (Manufacturers), Mashirika yanayofanya biashara ya Usambazaji (Trading & Distribution), Wakala wa Serikali (Government Agencies), Wanaotumia Hesabu za Umma, Wanaotumia Mahesabu kwa kutumia viwango vya Kimataifa (IFRS), Makampuni ya Bima, Makampuni Usambazaji Maji, Serikali za Mitaa, Vyuo, Tawala za Mikoa (Local Government), Wizara na Idara za Serikali, Taasisi zisizotengeneza faida (NGOs), Makampuni madogo ya Ukaguzi.

“Hesabu lazima ziwe za mwaka 2019 (Januari -Desemba 2019), Taarifa za hesabu lazima ziwe zimefuata katika viwango vya kimataifa, Kampuni lazi iwe imesajiliwa Tanzania, Lazima kampuni ama Taasisi ya Serikali iwe imefuata viwango vya kimataifa vya utayarishaji na ukaguzi iwe imetumian mkaguzi aliyesajiliwa na NBAA, Iwe imepata hati safi ya ukaguzi,” alisema.

Awamu nyingine; Kampuni/Taasisi ya Umma imetimiza sharia za kuundwa kwake kwa kuangalia sharia zilizoundwa na Bunge ama sharia za makampuni (Company’s Act), Wakurugenzi wake wameonesha taarifa za hesabu vizuri, Wamefwata kanuni kwa walioorodheshwa kwenye soko la hisa, Zimefwata kanuni bora kwa mujibu wa kanuni za Soko la Mitaji (CMSA), Namna gani wameonesha viwango vya mahesabu.

Bw, Maneno, ametoa rai kwa kampuni na taasisi za umma ambazo hazikushiriki kushiriki kwani ukishiriki wa mashindano haya ya tuzo hakuna adhabu lakini iwapo utatoa taarifa ambazo hazikufuata viwango tunakuadhibu.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive