A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, January 29, 2019

Benki ya DCB yatangaza faida ya shilingi bilioni 1.9 katika mwaka 2018 Januari 29, 2019

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya  Biashara ya  DCB, Zacharia Kapama (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza benki hiyo kupata faida ya kablsa ya kodi ya Shilingi Bilioni 1.9 kwa  mwaka 2018.Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani, Deogratius Thadei.

Benki ya DCB yatangaza faida ya shilingi bilioni 1.9 katika mwaka 2018
Januari 29, 2019
Benki yabiasharaya DCBimefanikiwakupatafaidaya shilingibilioni 1.9katikamwaka 2018 huku ikiipiku hasara ya shilingi bilioni 6.9 iliyopatikana mwaka 2017 ambayo inawakilisha ongezeko la asilimia 463.
Benki imefanya juhudi za makusudi kuhakikisha inatoka kwenye hasara iliyopata mwaka 2017 na kurudi kwenye faida. Baadhi ya hatua zilizochukuliwa nikupitia na kuboresha ufanisi wa mfumo wa uendeshaji biashara ambapo gharama za uendeshaji zimeshuka huku huduma mpya za kidigitali zimeanzishwa, huduma hizi zimevutia wateja wengi zaidi kufungua akaunti za amana. Juhudizilizopelekea upatikanaji wa faida mwaka 2018;

1.      Mapato halisi ya ribakuimarika kutokanana utoaji mikopo katika sekta mbalimbali na kuchangia ongezeko la mikopo ghafi kutoka shilingi bilioni 88.6 mwaka 2017 hadi bilioni 90.6 mwaka 2018. Mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 65 imetolewa mwaka 2018 ambapo kati yake, shilingi bilioni 21 ni mikopo ya wajasiriamali wadogo.

2.      Kuboresha ufanisi katika mfumo wa uendeshaji biashara kupitia mfumo wa kidijitali hukumkazo ukiwekwa katika kuongeza amana za gharama nafuu kupitia bidhaa za amana za kidijiti na usimamizi wa mizania wenye ufanisi.Gharama za amana zimeshuka kutoka shilingi bilioni 9.8mwaka 2017 kufikia shilingi bilioni 6.8 mwaka 2018.

3.      Kuongeza kasi ya ukusanyaji madeni yatokanayo na mikopo chechefu na hivyo kupunguza tengo la mikopo chechefu kutoka shilingi bilioni 4.5 hadi shilingi milioni 263
4.      Kuongeza mkazo katika ufanisi wa utendaji na kuchangia upunguaji wa gharama za uendeshaji kutoka bilioni 21.2 mwaka 2017 kufikia shilingi bilioni 16.9 mwaka 2018

Uboreshaji huduma na mahusiano ya wateja umekuwa ndio kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na za muda mrefu hasa kutoka kwa wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali yaliyoendelea kuwekeza na benki ya DCB.
Huduma za kidigitalizimekuwa chachu ya kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji na gharama za riba. Hizi ni mathalaniakaunti ya kidijiti (DCB Digital Account), DCB Kibubu Digital Account, DCB FDR Digital account. Account hizi zinamuwezesha mteja kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki, Kutunza pesa na kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 175,204 mwaka 2018 na hivyo kuchangia ongezeko kubwa la miamala ya kibenki ambapo mapato yasiyo ya riba kuimarika katika mwaka 2018.
Benki ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama Benki ya Jumuiya ya Wananchi “community bank” na Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kufuatia kilio cha wakazi wengi wa Jiji kutokuwa na njia rahisi ya kupata mitaji midogo midogo ya biashara. Benki ya DCB imekuwa ni benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa mwaka 2008, na imeweza kukuza mtandao wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la Dodoma, na inatarajia kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.
Share:

Friday, January 25, 2019

KAMPUNI YA ALAF YAZINDUA KITUO CHA KISASA CHA MAUZO MWENGE JIJINI DSM

Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Daniel Chongolo (wa pili  kushoto), akikata utepe kuzindua  rasmi kituo cha mauzo  cha Kampuni ya Mabati ya ALAF  kilichopo Mwenge,  jijini Dar es Salaam leo.  Wanaoangalia kutoka kushoto ni, Ofisa Masoko, Theresia Mmasy, Meneja Mkuu, Dipti Mohanty na Maneja Masoko, Isamba Kasaka. 
Mkuu wa Wilaya ya Kiondoni, Daniel Chongolo akitoa hotuba ya uzinduzi wa kituo hicho leo.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Daniel Chongolo (katikat), Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stella Msofe (kulia), Meneja Mkuu wa Kampuni ya mabati ya ALAF, Dipti Mohanty (wa pili kushoto), na Meneja Masoko wa ALAF, Sophia Assey (kushoto), wakiwa katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Daniel Chongolo (katikati), Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stella Msofe (watatu kushoto) pamoja na Meneja Mkuu wa Kampuni ya mabati ya ALAF, Dipti Mohanty  wakiwa katika picha ya pamoja na daadhi ya wafanya kazi wa ALAF wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia), akiondoka baada ya tukio la uzinduzi wa kituo hicho cha mauzo. Kulia kwake ni Meneja Mkuu wa ALAF, Dipti Mohanty   pamoja na wafanya kazi wengine.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive