A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, October 13, 2022

SWISSPORT YAKABIDHI MSAADA WA ULTRASOUND CCBRT

   IMG_7289

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi akipokea kifaa tiba - mashine ya Ultrasound kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin katika hafka iliyofanyika leo Hospitalini hapo Jijini Dar es Salaam

 

WhatsApp%20Image%202022-10-13%20at%203.39.47%20PM

Muonekano wa kifaa tiba 'Ultrasound


IMG_7271

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi (kulia), akizungumza wakati wa hafla ya  makabidhiano  ya kifaa tiba cha Ultrasound kilichotolewa na Swissport kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto  chenye thamani ya shilingi Milioni 68.

IMG_7259
Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi kifaa tiba cha Ultrasound kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya mama ma mtoto katika Hospitali ya CCBRT leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi


KATIKA kuhakikisha sekta ya afya inazidi kukua na jamii ya watanzania  inakuwa na afya bora kampuni ya Swissport Tanzania PLC  imeendelea kuwa karibu na jamii na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Sama Suluhu Hassan kwa kutoa msaada wa kifaa tiba ‘Ultrasound’ chenye thamani ya shilingi milioni 68 katika taasisi ya CCBRT.



Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania PLC Mrisho Yassin amesema mchango huo umeelekezwa kuwasaidia akina Mama wajawazito.

‘’Tunatambua kuna changamoto ya vifaa tiba na sisi kama kampuni tumeliona hili na kuona kutoa mchango huu, kwa taarifa tuliyopewa kifaa hiki kitasaidia sana kutokana na uhiitaji wa mashine hii hapa CCBRT ili kusadia jamii ya watanzania  akina Mama wajawazito.’’ Amesema.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi ameishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia kifaa tiba hicho cha Ultrasound kitakachoongeza nguvu ya kuwahudumia akina Mama wajawazito wengi zaidi na kwa ufasaha.



‘’Sisi kama CCBRT asilimia 87 ya wagonjwa wanaokuja hapa ni aidha wanapata huduma za bure kabisa au wanachangia….Tunahitaji kushikwa mkono katika maeneo makuu matatu ya huduma za kibingwa na bobezi za afya, mafunzo kwa wafanyakazi na watoa huduma na eneo la vifaa na vifaa tiba na tunawashukuru Swissport na tuendeleze uhusiano huu.’’ Amesema.



Amesema, tangu kuanza kutolewa kwa huduma katika kitengo cha Mama na Mtoto mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu wamewahuduma akina Mama wapatao 225.



‘’CCBRT tunatoa shukrani zetu za dhati kwa SwissPort kwa kututembelea na kutoa kifaa hiki  kwa umoja huu iko siku ambayo tutaona kila mwanamke anayepata ujauzito anajifungua salama na kwa furaha….Tunashukuru sana kwa msaada wenu na ushirikiano wenye kwenye huduma hizi za kuokoa maisha ya watu.’’ Amesema.



Aidha amesema, mwezi Julai mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu alizindua rasmi kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto ambacho kimepewa jina la ‘CCBRT- Samia Suluhu Hassan Maternity Wing’ kutokana na juhudi binafsi na Serikali anayoiongoza katika kupigania afya za akina Mama wajawazito na watoto wachanga pamoja na maboresho makubwa ya sekta ya afya nchini kote.



‘’Lengo la kuanzishwa kwa kitengo hiki ni cha uzazi ni kutaka kuwahakikishia akina Mama wote uzazi salama, kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi sambamba na kuzuia ulemavu….kitengo hiki kimedhamiria kuwahudumia akina Mama wajawazito wenye ulemavu, wenye historia hatarishi za uzazi, akina Mama wenye historia ya fistula na mabinti wanaopata mimba katika umri mdogo.’’ Amesema.

Share:

Monday, October 10, 2022

Benki ya Absa kutoa huduma bora zaidi zinazokidhi mahitaji ya wateja

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Melvin Saprapasen (wa tano kushoto), Meneja wa Absa Tawi la Ohio, Ally Janja (kushoto kwake), wafanyakazi wa Absa pamoja na Wateja wakigonganisha glasi kutakiana afya njema na mafanikio katika moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Katika maadhimisho hayo viongozi wa ngazi za juu wa benki hiyo walitembelea matawi ya Absa nchini kote ili kuzungumza na wafanyakazi na pia Wateja wao ili kuweza kuona namna bora ya kuwahudumia na kushughulikia mahitaji yao.
Meneja wa Kitengo cha Bima wa Benki ya Absa Tanzania, Sandeep Chavda (kushoto), akimpa zawadi mmoja wa Wateja wa Absa Tawi la Dar City, huku Meneja wa tawi Hilo, Winford Mwang'onda akiangalia, katika hafla ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo, Dar es Salaam hivi karibuni.
Wafanyakazi wa Benki ya Absa Tawi la Alpha House pamoja na Wateja wao wakitakiana afya njema na mafanikio katika hafla iliyoandaliwa na tawi hilo kwa wateja wao, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Slipway, Veronica Okio (kulia), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wake katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Pugu, Heri Sijaona (kushoto), akizungumza na wateja wa benki hiyo tawini hapo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, katika
hafla ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Zanzibar, Rabia Abood (katikati), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wake, Jabir Alfarsy katika hafla kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi hilo visiwani humo hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa wateja Maalum katika tawi hi
lo, Salim Salum.
Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, John Beja (katikati, mwenye tai nyekundu) Mkurugenzi wa Fedha wa Absa Tanzania, Obedi Laiser (nyuma ya Beja), wakiselebuka pamoja na wafanyakazi na wateja wa Tawi la Absa Mikocheni, kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita
Mmoja wa watumishi waliofanyakazi kwa muda mrefu katika Benki ya Absa Tawi la Tanga, Mwanajumaa Darweshi (wa pili kulia), akionesha cheti cha shukurani muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Absa Tanzania, Ndabu Lilian Swere (kushoto), katika hafla iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi hilo, mjini Tanga juma lililopita. Wa pili kushoto ni Meneja wa tawi hilo, Gloria Mallya.
Share:

Sunday, October 9, 2022

Benki ya DCB yang'ara ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (katikati) akikata keki huku wafanyakazi na wateja wa Benki ya tawi la Victoria wakishangilia, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.

Benki ya Biashara ya DCB imeendelea kung'ara wakati ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu huku ikianisha baadhi ya mafanikio iliyopata tangu ilipoanzishwa Mwaka 2000.
  • Benki ya kwanza kufuzu kutoka benki ya kijamii kwenda Benki ya Biashara.
  • Benki ya kwanza Tanzania kusajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
  • Benki inayoongozwa na watanzania kuanzia Bodi ya Wakurugenzi hadi Menejimenti.
  • Benki imewanyanyua wajasiriamali wanawake zaidi ya 400,000 kupitia mikopo ya vikundi.
  • Benki inatoa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja.
  • Benki ina Wateja kuanzia wajasiriamali wadogo, wafanyabiashara wa kati na wakubwa, wateja binafsi, waajiriwa, mashirika na makampuni.
  • Benki ipo sambamba na waajiriwa na inatoa mikopo yenye riba nafuu.
  • Benki ipo sambamba na wazazi kuwawezesha watoto elimu hadi chuo kikuu kupitia akaunti ya Skonga na mkopo wa ada.
  • Benki inatoa mikopo ya nyumba yenye masharti nafuu.
  • Fanya miamala na malipo mahali popote kupitia DCB Pesa, DCB Wakala, Visa, Master Card QR, DCB Malipo na Internet Banking.
  • Kufanya miamala nje ya nchi kupitia International money transfer na Western Union.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa pili kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa mmoja wa Wateja wa Tawi la DCB Victoria, Halima Iddi, katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo tawini hapo, jijini Dar es Salaam wiki hii. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya DCB, Nelson Swai (katikati), akikabidhi msaada wa viti, mashine ya kuchapia (printa) na mifuniko ya tairi za gari vilivyotolewa na DCB kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Magomeni, Mrakibu wa Polisi Edward Masunga, ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kituoni hapo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Beki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki katika moja ya shamrashamra wakiwapokea Wateja wao wajasiriamali wa mikopo ya vikundi waliofika katika hafla ya kuwapongeza katika makao makuu ya benki hiyo, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza na wajasiriamali ambao kutoka vituo mbalimbali ambao ni wanufaika wa mikopo ya vikundi inayotokewa na DCB. Katika hafla hiyo DCB ilivitambua vituo bora na kukabidhi vyeti vya shukurani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa baadhi ya wajasiriamali ambao kituo chao kufanya vizuri kwenye mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo. Hii ilikuwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, jijini Dar es Salaam wiki hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa baadhi ya wajasiriamali ambao kituo chao kufanya vizuri kwenye mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo. Hii ilikuwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, jijini Dar es Salaam wiki hii.
Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAJIVUNIA KUSHEREHEKEA HUDUMA BORA

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Janemary Rutahoile ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga, Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki hiyo Jema Msuya na kushoto ni Meneja wa TCB Tawi la Mlimani City Happy Ernest.Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Anna Philemoni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga. Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy ErnestAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga pamoja na wateja wa wa benki hiyoAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki Deodarus Nkeyera ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga na Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy Ernest.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki hiyo.

Tanzania Commercial Bank (TCB)  imewahakikishia wateja wake kuwa inabuni mipango madhubuti ya kuzindua bidhaa mpya zinazoendana na mahitaji ya watumiaji wa huduma za kibenki kote nchini.

Akizungumza na wateja wake waalikwa wakati wa wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commercial Bank lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi,  alisema  wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa huduma bora na yenye kumdhamini mteja.

"Thamani yetu kuu iko katika uhakika kwamba tunamjali  na kuvutiwa na mteja, tunataka kuwahakikishia wateja wetu wapendwa kuwa tumejitolea kufanya uzoefu wako wa kibenki kuwa wa kufurahisha zaidi," alisema.

 

Anna Philemon, mteja wa Tanzania Commercial Bank alisema Benki ya TCB imeweka huduma zake na bidhaa ziko mikononi mwa mteja, na hivyo kuwasaidia wateja kufanya miamala kwa njia rahisi zaidi.

 

Anna alitoa wito kwa Watanzania kutoka nyanja mbalimbali kujiunga na Tanzania Commercial Bank na kufurahia baadhi ya huduma bora na bidhaa za kipekee zinazotolewa na benki hiyo.

Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAPIGA JEKI WAKULIMA WA ZAO LA MWANI UNGUJA

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi  (kushoto), akikabidhi   msaada wa kisima cha maji kwa Mbunge wa Jimbo la Paje Unguja  Mh Sudi Hassan kwa niaba ya wamama wa Jimbo hilo wanaojishughulisha na Kilimo cha mwani kwaajili ya kustawisha Kilimo cha zao hilo  hafla ya makabidhiano hayo yefanyika unguja mwishoni mwa wiki wengine pichani ni baadhi ya wamama waliopatiwa msaada huo


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wakulima wa zao la mwani kutoka jimbo la paje Unguja


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi  akifurahi pamoja na viongozi mbalimbali na wamama wakulima wa zao la mwani  Unguja mara baada yakukabidhi msaada wa kisima kwaajili ya kustawisha Kilimo cha zao hilo  hafla ya makabidhiano hayo yefanyika unguja.

Share:

Thursday, October 6, 2022

Benki ya Absa yakabidhi msaada wa vifaa vya usafi Hospitali ya KCMC ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (wa nne kulia) akikabidhi vifaa vya kuhifadhia takataka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC, Prof. Gileard Masenga, vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya Absa, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro Leo.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Moshi, Pendo Abdallah akizungumza katika Kanisa la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC, katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kuhifadhia takataka vilivyotolewa na benki hiyo, ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, hospitalini hapo, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga akizungumza katika Kanisa la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini ya KCMC wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya kuhifadhia takataka vilivyotolewa na Absa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, hospitali hapo, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga, baadhi ya wafanyakazi wa Absa na watumishi wa Hospitali ya KCMC, wakipiga picha ya kumbukumbu katika hafla ambayo, Absa ilikabidhi msaada wa vifaa vya kuhifadhia takataka ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo mjini Moshi, Kilimanjaro Leo.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive