A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, January 31, 2018

WANANCHI WATAKIWA KUNAWA MIKONO ILI KUEPUKA MAGONJWA YA MILIPUKO

Afisa Afya Wilaya kinondoni John Kijumbe akizungumza na waandishi wa habari leo katika hafla yakufunga mradi wa magonjwa ya kuambukiza kwa kunawa mikono (kutoka kushoto) ni Mratibu wa Mradi huo Rose Temu, Mganga Mkuu  wa Kituo cha Afya Magomeni Omari Mwanga, na  ni Afisa Elimu Sayansikimu na Afya Manispaa ya Kinondoni Martha Kussaga. hafla hiyo imefanyika kashule ya Msingi Kigogo
Afisa Elimu Sayansikimu na Afya Manispaa ya Kinondoni Martha Kussaga. (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo katika hafla yakufunga mradi wa magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kunawa mikono, (kutoka kushoto) ni Mratibu wa Mradi huo Rose Temu, Mganga Mkuu  wa Kituo cha Afya Magomeni Omari Mwanga, na Afisa Afya Wilaya kinondoni John Kijumbe, hafla hiyo imefanyika kashule ya Msingi Kigogo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kigogo wakiwa katika hafla hiyo..... PICHA NA BRIAN PETER

Wananchi wametakiwa kunawa mikono wakati wote kabla ya kula ili kuepuka magonjwa ya milipuko yatokanayo na maradhi kutokunawa mikono. 

Akizungumza na waandishi wa habari Leo katika hafla ya kufunga Mradi  wa magonjwa wa kuambukiza kwa njia ya kunawa mikono jijini Dar es Salaam Afisa Afya Wilaya kinondoni JOHN KIJUMBE amesema walianzisha Mradi wa Kunawa mikono Uliofadhiliwa na shirika la  kimataifa kutoka Japan JICA,likishirikiana na kituo cha  Afya Magomeni ukiwa na lengo la kutoa elimu ya kujikinga na maradhi ya kuambukiza kwa Njia ya kunawa mikono .

Amesema Mardi huo ulianzishwa Julai na kuzinduliwa Septemba 25,2017  ambapo umekamili January 2018 ambapo ulilenga kutoa elimu ya kuanawa mikono mashuleni katika Wilaya ya Kinondoni ambapo waliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi pamoja na walimu na kubaini kuwa wananchi wanauelewa mdogo wa Kunawa mikono baada ya kutoka chooni,na kabla ya kula.

"Katika huu mradi tuliouanzisha chini ya shirika la kimataifa la Japan (JICA) likishirikiana na kituo cha Afya Magomeni tumeweza kutoa elimu kwa shule katika Wilaya ya Kinondoni  na kubaini kuwa wanafunzi wengi hawana elimu ya kunawa mikono jambo ambalo ni hatari kwa Afya zao na kusababisha magonjwa ya Milipuko "Amesema Kijumbe. 

Aidha amebainisha changamoto walizokumbana nazo ambapo amesema watu wanachukulia kunawa mikono siyo jambo  muhimu, pamoja na ukosefu wa vifaa vya kunawa mikono katika jamii na mashuleni pia, hivyo amesema mradi huo utakuwa ni endelevu kwa jamii ili kuweza kukuza elimu hiyo ya kunawa mikono. 

Pia amesema katika mradi huo wamepata mafanikio mbalimbali ambapo wameweza kufunga vifaa vya kunawia mikono kwa baadhi ya shule.

Kwa upande wake mratibu wa Mradi huo Rose Temu amesema Mradi huo utakuwa emdelevu na kutoa wito kwa watanzania kujenga mazoea ya kunawa mikono unapotoka chooni na  kabla ya kula ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
Share:

Friday, January 26, 2018

HALOTEL YATOA MILIONI HAMSINI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Pham Dinh Quan (watatu kushoto), akikabidhi hundi ya shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu 402  zilizoko jijini hapa  katika hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi Mapinduzi jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi Mkuu  wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Pham Dinh Quan, , (kushoto),   akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi mbalimbali wa kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu alipokwenda kukabidhi hundi ya  shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu 402  zilizoko jijini hapa  katika hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi Mapinduzi jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano  wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Mhina Semwenda, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi mbalimbali wa kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu wakati kampuni hiyo ilipo kwenda kukabidhi hundi ya  shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania,Picha na Brian Peter


Dar es Salaam, Januari 22 2018…………… Katika kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa mchango wa fedha taslim Shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni moja ya utekelezaji wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali na ofisi hiyo katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402 kati ya hizo shule 295 ni za elimu ya awali/msingi na shule 107 ni za sekondari zilizoko mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mchango huo kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Halotel, Le Van Dai amesema mchango huo ni sehemu tu ya jitihada kubwa zinazofanywa na kampuni hiyo katika kusaidia na kuinua sekta ya elimu nchini ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha maendeleo ya nchi hasa kupitia sekta ya elimu ambayo ni muhimili wa maendeleo ya kila nchi duniani.

“Tunatambua kuwa, huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na waalimu ni moja ya msingi imara katika kukuza sekta ya elimu nchini, kwa kuzingatia hili tumeamua kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa mchango wetu wa kifedha ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa ofisi za waalimu ikiwa ni sambamba na kuboresha mazingira utendaji kazi kwa waalimu ya kazi na kurahishisha ufanisi wao katika kuwafunza wanafunzi ambao ni taifa la leo na kesho” alisema Dai.

“ Halotel tumekuwa mstari wa mbele tukishirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu kupitia teknolojia, kwa mfano tumekuwa tukitekeleza mradi wa kuunganisha shule zaidi ya 400 nchi nzima na huduma ya intaneti ni ya kipekee sana, tumeendelea kuhakikisha sisi kama kampuni tunausimamia na kuhakikisha unaleta mabadiliko na tija kwa elimu yetu.” Alisema.

“Katika kuhakikisha mradi huo wa intanenti unawanufaisha waalimu na wanafunzi katika kuboresha uelewa na ufaulu wa masomo yao, Halotel kwa ushirikiano na Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tumeunda jukwaa (Mfumo) wa kujisomea kupitia mtandao wenye masomo ya Sayansi na Hisababati kwa kufuata Mtaala uliokubaliwa na serikali, ambalo unawawezesha waalimu na wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza (I) mpaka cha nne (IV) nchini kote kusoma masomo hayo. Mfumo huu unaoitwa  Halostudy, na linapatikana kupitia tovuti

(http://www.halostudy.ac.tz/). Jukwaa hili ni Tofauti na majukwaa mengine yanayofanana, kwa maana maudhui yaliyotengenezwa yameunganishwa na vipengele vya multimedia kama vile video, sauti, na michoro katika maeneo maalum ambapo maudhui mengine ni vigumu kuelewa kutumia maandishi pekee:” Aliongeza Dai.


Kampuni ya simu za mikononi ya Halotel imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali na itaendelea kufanya hivyo katika kuboresha sekta ya mawasiliano nchini, pamoja na sekta nyingine ikiwa ni utekelezaji wa kuboresha maisha ya watanzania kupitia uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni hiyo nchini Tanzania.

Share:

MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC YAZINDUA BIDHAA KWA AJILI YA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kibenki kwa njia ya Mitandao wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), John Mhina  (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’  ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Luteganya na Meneja Masoko wa benki hiyo, Rahma Ngassa.   
Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko  wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa tatu kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’  ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa njia ya Mitandao, John Mhina na Meneja Masoko, Rahma Ngassa.    
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi tukio la uzinduzi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’  ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura jana katika ukumbi wa tawi la benki hiyo Barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
Share:

Wednesday, January 24, 2018

TPB kuijenga Tasisi ya Tanzania skauti association

Benki ya TPB yasaini mkataba wa mahusiano na taasisi ya Tanzania  skauti association lengo ikiwa ni kuweza kusaidiana katika kuijenga Taasisi hiyo ya skauti. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshindi amesema lengo la kusaidia kuijenga Tanzania skauti association na kusaidia kutengeneza data za kuwatambua wanachama wao waliopo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa kadi za kisasa kwa ajili ya wanachama wao 

Amesema katika kutengeneza mahusiano yao kutawasaidia kutoa elimu kwa Vijana  namna ya kuweka akiba kwa manufaa yao na kizazi kijacho pia. 

"Niwashukuru Sana Tanzania skauti association walivyokuja na wazo hili kwani kutasaidia kuelimisha na kutoa elimu kwa Vijana ya namna ya kuweka akiba kwani Vijana wengi hawajui njia za kuweka akiba yao ya mbeleni. "Alisema Mkurugenzi wa TPB

Aidha amesema wataweza kuwasaidia Tanzania skauti association kukusanya mapato yao kwani watakuwa tayari wamefahamu wanachama wao kutokana na ladies zitakazotolewa. 


Kwa upande wake kamishna Wa chama cha skauti Tanzania Abdulkarim Shah, meishukuru Benki ya TPB kwa kukubali kusiani mkataba wa mahusiano na kuweza kupata kadi zitakazotambulisha wanachama,ambapo amesema itasaidi kuwatambulisha na kufahamu wanachama wa skauti anapopatikana. 
Share:

Sunday, January 21, 2018

Wateja sita wa Benki ya NBC wajinyakulia Suzuki Carry ‘kirikuu’ kampeni ya Malengo

Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Kampeni, Mtenya Cheya na kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi hao ni Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
Meneja wa Amana za Wateja wa Benki ya NBC, Dorothea Mabonye (wa pili kushoto), akichezesha droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi hao ni Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.  Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid, Meneja Kampeni ya Malengo, Mtenya Cheya na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi.
Meneja Kampeni wa NBC, Mtenya Cheya (kushoto), akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi sita aliyejishindia zawadi ya Suzuki Carry maarufu ‘Kirikuu’ wakati wa droo kubwa ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (wa pili kulia ), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo ambapo NBC imetoa zawadi zawadi ya gari aina ya Suzuki Carry 'Kirikuu' kama inavyoonekana moja ya gari hilo (kushoto) likionyeshwa kwa waandishi wa habari wakati wa droo hiyo.

Na Mwandishi Wetu.

WATEJA sita wa Benki ya NBC wameibuka kidedea baada ya kila mmoja kujishindia gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama  ‘Kirikuu’ katika droo kubwa ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Kampeni hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu imeshuhudia wateja hao kutoka katika maeneo yaliyogawanywa katika kanda sita nchini  wakitangazwa washindi wa magari hayo yenye thamani ya shs millioni 30 kila moja jumla yakiwa na thamani ya shs milino 180.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi  alisema kampeni hiyo iliyovutia waterja wengi wapya kujiunga ilishuhudia washindi wengine 24 kupatikana katika droo mbili zilizofanyika katika miezi miwili ya nyuma ambapo kila mmoja alijishindia zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1.

“Kampeni hii  ya Akaunti ya Malengo ya NBC imekuwa na mafanikio makubwa kwani tumeshuhudia zaidi ya akaunti mpya 6000 ziikifunguliwa na wateja wetu wakihamasika kujiwekea akiba kwa malengo yao ya baadae”, alisema.

Alisema kampeni hiyo ilizinduliwa mwaka jana kipindi ambacho NBC ilikuwa ikiadhimisha miaka 50 ya huduma bora kwa wateja tokea kuanzishwa kwake.  

Katika droo hiyo zawadi hizo za Suzuki Carry sita  ‘kirikuu’ zilikwenda kwa Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini.

Hii ni mara ya tatu Benki ya NBC kuendesha kampeni ya akaunti ya Malengo mara hii ikitoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya shs milioni 204 ambapo mwaka 2016  wateja wawili Aldo Nsuha mkazi wa Tabata  Dar es Salaam na Lawrence Njozi kutoka Masasi mkoani Mtwara wakijishindia magari mapya aina ya Toyota Hilux double cabin.

Share:

Tuesday, January 16, 2018

WATEJA WA UMOJASWITC WAJIZOLEA MAMILIONI

Kampuni ya UmojaSwitch leo imechezaesha droo yake ya bahati nasibu ya Shinda na Umoja  kwa wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8 Januari mwaka huu   ambapo zaidi ya wateja 25 wameibuka washindi katika droo ya leo.

UmojaSwitch ilianzisha bahati nasibu  hiyo ya Shinda na Umoja   mwezi Desemba mwaka jana kwa lengo la kutoa hamasa kwa wateja wao kupitia kampeni yao ya kubadili kadi za UmojaSwitch kutoka kwenye mfumo wa zamani na kwenda kwenye  mfumo mpya wa ‘Microchip’

Katika makundi matatu yaliyo chezeshwa leo kundi la  kwanza limetoa washindi   25 waliojishindia  T-Shirt za UmojaSwitch,
Mzunguruko wa pili umetoa washindi wa tano wa Simu za Mkononi (Smart Phone),  mzunguruko wa tatu umepata  washindi  wawili wa fedha taslimu mara mbili ya fedha walizokuwa wanatoa kwenye Akaunt zao kupitia kadi za UmojaSwitch na Mzunguzuro wa nne umepata mshindi mmoja aliejishindia kiasi cha Shilingi Milioni Moja Taslimu.
   
Akiendesha Droo hiyo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Bi BeatriceEmmanuel  Chini ya  Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari Maggid amewapongeza washindi wa zawadi hizo na kudai kuwa  watafanya mawasiliano na Benki husika wanazotumia washindi wao ili kuweza kuwapatia zawadi zao muda mchache kuanzia leo.

Aidha Beaterice amewataka wateja ambao bado hawajabadilisha kadi zao za awali  kufika kwenye Benki husika ili kubadili kadi zao na kuwea kuingia katika bahati nasibu hiyo ya Shinda na UmojaSwitch kwenye droo inayofuata.

Kampuni ya UmojaSwitch inaunganisha mabenki zaidi ya 27 Tanzania kwa lengo la kushirikiana kutoa fedha kwa njia ya kilectronic ya ATMs
Afisa Masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel (kushoto) akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda na Umoja  kwa wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8 Januari mwaka huu   ambapo zaidi ya wateja 25 wameibuka washindi katika droo hiyo hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika katika ofizi zao jijini Dar es Salaam leo (kulia) ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari Maggid
Afisa Masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Share:

Monday, January 15, 2018

MWALIMU COMMERCIAL BANK YAANZA MWAKA NA AKAUNTI YA TUKUTANE JANUARIMkurugenzi Mkuu wa Benki ya Mwalimu Commercial Plc,  (MCB) Ronald Manongi (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la kuhamasisha moyo wa ujiwekea akiba kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Lutegenya na Meneja Mahusiano kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa mkombozi kwa wateja kuweza kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji muhimu yanayojitokeza  mwanzoni mwa mwaka.  
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi ya akaunti mpya ya ‘Tukutane Januari’ yenye lengo la kuhamasisha moyo wa kujiwekea akiba kwa wateja wake na kwa watanzania kwa ujumla. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja wa Tawi la Samora, Leticia Ndongole, Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Lutegenya na Meneja Mahusiano kwa Wateja, Charles Shadrack. Akaunti hii itakuwa mkombozi kwa wateja kuweza kujiwekea akiba itakayowawezesha kumudu mahitaji muhimu yanayojitokeza  mwanzoni mwa mwaka. 
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi tuki la uzinduzi wa akaunti mpya ya Tukutane Januari ya Benki ya Mwalimu Commercial Plc jijini Dar es Salaam leo. 

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC YAZINDUA BIDHAA KWA AJILI YA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA.

15 JANUARI 2018, Dar es Salaam – Mwalimu Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo Tukutane Januari Akaunti, ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla.

Akizungumzia Kuhusu akaunti hii mpya ya akiba ya ‘Tukutane Januari’, Mkurugenzi Mkuu wa MCB, Bwana Ronald Manongi alisema, mteja ataweza kujiwekea akiba kidogo kidogo wakati wowote katika kipindi chote cha hadi kufikia Januari. Akaunti hii ina riba ya kuvutia ambayo mteja wetu atalipwa kila robo ya mwaka.

Vilevile inamuwezesha mteja wetu kupata mkopo wa hadi asilimia 30 ya amana yake katika kipindi cha mwaka husika. Hivyo Mteja atakapoweka akiba zaidi atafaidika zaidi, na atakuwa na uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kulingana na akiba ya akaunti yake.

Akaunti hii ya akiba itamuwezesha mteja kujiondolea usumbufu wa kutatua mahitaji muhimu ya kipesa kipindi cha mwanzo wa mwaka husika ikiwa ni pamoja na ada za shule na vyuo na manunuzi mengine ya vifaa vya shule, pia kodi za nyumba hivyo kuondokana na dhana ya Januari kuwa ni mwezi mgumu.

Mkurugenzi huyo pia aliwaasa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba mara kwa mara kwani husaidia sana kutatua matatizo mengi yanayoikabili familia na jamii kwa ujumla. “Mara nyingi watu wamejikuta wakiingia katika madeni makubwa na fedheha pale wanaposhindwa kulipa madeni hayo”, alisema Ndugu Manongi. Akiendelea Ndg Manongi alisema “Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imebuni mkakati huu kuisaidia jamii kuazimia kupunguza na/ama kuondokana na fedheha, adha na madhara yanayotokana na kuwa na majukumu mazito mwezi huo wa kwanza wa mwaka”.

Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko aliongeza kwa kusema “Uzinduzi wa huduma hii mwanzoni mwa mwaka 2018 ni moja ya ishara kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa wateja wetu. Hivyo tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza kufaidi huduma na bidhaa zetu.
MWISHO.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa:
Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB).
Mlimani Tower - Mezzanine Floor, Sam Nujoma Road
P.O. Box 61002, Dar es Salaam
Telephone: 022-2772954/7 and +255 629 331 151
Email; info@mcb.co.tz
Share:

Wednesday, January 10, 2018

Stanbic Bank yaanza mwaka 2018 na akaunti ya HATUA,

Dar es Salaam, Sunday 07th January 2018. Stanbic Bank Tanzania imezindua akaunti mpya ijulikanayo kama HATUA, ambayo ni kwa ajili ya watoto yenye lengo la kuwasaidia wazazi kuwawekea akiba watoto wao huku wakiwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba.
Kwa kuanzishwa kwa aina hii mpya ya akaunti, Stanbic bank inaendelea kuwapatia wateja wake huduma mpya na bora za kibenki kila siku kuendana na mahitaji ya wateja an hali halisi ya soko.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, mkuu wa mauzo wa benki hiyo Shangwe Kisanji amesema kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuwapatia wateja wake huduma mpya kila mara na nyakati zote huduma hizo huendana na mahitaji ya wateja na mahitaji ya jumla ya soko la huduma za kibenki hapa nchini.
“Wakati wote tumekuwa tukiangalia njia mbalimbali za kuwahudumia vyema wateja wetu katika kutunza fedha zao ikiwemo kuwawekea watoto akiba kwa manufaa yao ya baadae na pia kuwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba wawapo wakubwa, utamaduni ambao ni muhimu sana kwa uchumi na maisha yao”
Ameeleza kuwa akaunti hiyo ya HATUA ni muendelezo mzuri wa kuwatoa watoto kwenye utamaduni wa kujiwekea akiba kwenye vibubu na badala yake kuanza utamaduni wa kujiwekea akiba kwa njia rasmi zaidi.
Amesema akaunti hiyo haina makato ya huduma na kiwango cha chini cha amana ni shilingi 20,000 tu. Amebainisha kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu ya kuiendesha  na inaruhusu kutolewa kwa fedha mara moja kwa robo ya mwaka ili kusaidia katika majukumu yanayowahusu watoto kama vile ada za shule, sare na kadhalika. Amesema pia akaunti hiyo hujipatia riba kulingana na amana iliyopo.
Note to Editors
Stanbic Bank Tanzania is part of the Standard Bank Group, Africa’s largest bank by assets. Stanbic Bank Tanzania provides the full spectrum of financial services. It’s Corporate and Investment Banking division serves a wide range of requirements for banking, finance, trading, investment, risk management and advisory services. Corporate and Investment Banking delivers this comprehensive range of products and services relating to: investment banking; global markets; and global transactional products and services.

Stanbic Bank’s corporate and investment banking expertise is focused on industry sectors that are most relevant to emerging markets. It has strong offerings in mining and metals; oil, gas and renewables; power and infrastructure; agribusiness; telecommunications and media; and financial institutions.

Stanbic Bank Tanzania’s personal and business banking unit offers banking and other financial services to individuals and small-to-medium enterprises. This unit serves the increasing need among Tanzania’s small business and individual customers for banking products that can meet their shifting expectations and growing wealth.

Picha  za matukio mbalimbali ya hafla ya uzinduzi wa akaunti mpya ya HATUA ya benki ya Stanbik jijini Dar es salaam. Akaunti hiyo mpya ni kwa ajili ya watoto na ina lengo la kuwasaidia wazazi na walezi katika mahitaji ya watoto kama vile ada za shule na pia kuwajengea watoto utamaduni mzuri wa kujiwekea akiba
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive