A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, January 21, 2018

Wateja sita wa Benki ya NBC wajinyakulia Suzuki Carry ‘kirikuu’ kampeni ya Malengo

Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Kampeni, Mtenya Cheya na kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi hao ni Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
Meneja wa Amana za Wateja wa Benki ya NBC, Dorothea Mabonye (wa pili kushoto), akichezesha droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi hao ni Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.  Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid, Meneja Kampeni ya Malengo, Mtenya Cheya na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi.
Meneja Kampeni wa NBC, Mtenya Cheya (kushoto), akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi sita aliyejishindia zawadi ya Suzuki Carry maarufu ‘Kirikuu’ wakati wa droo kubwa ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (wa pili kulia ), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo ambapo NBC imetoa zawadi zawadi ya gari aina ya Suzuki Carry 'Kirikuu' kama inavyoonekana moja ya gari hilo (kushoto) likionyeshwa kwa waandishi wa habari wakati wa droo hiyo.

Na Mwandishi Wetu.

WATEJA sita wa Benki ya NBC wameibuka kidedea baada ya kila mmoja kujishindia gari jipya aina ya Suzuki Carry maarufu kama  ‘Kirikuu’ katika droo kubwa ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Kampeni hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu imeshuhudia wateja hao kutoka katika maeneo yaliyogawanywa katika kanda sita nchini  wakitangazwa washindi wa magari hayo yenye thamani ya shs millioni 30 kila moja jumla yakiwa na thamani ya shs milino 180.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi  alisema kampeni hiyo iliyovutia waterja wengi wapya kujiunga ilishuhudia washindi wengine 24 kupatikana katika droo mbili zilizofanyika katika miezi miwili ya nyuma ambapo kila mmoja alijishindia zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1.

“Kampeni hii  ya Akaunti ya Malengo ya NBC imekuwa na mafanikio makubwa kwani tumeshuhudia zaidi ya akaunti mpya 6000 ziikifunguliwa na wateja wetu wakihamasika kujiwekea akiba kwa malengo yao ya baadae”, alisema.

Alisema kampeni hiyo ilizinduliwa mwaka jana kipindi ambacho NBC ilikuwa ikiadhimisha miaka 50 ya huduma bora kwa wateja tokea kuanzishwa kwake.  

Katika droo hiyo zawadi hizo za Suzuki Carry sita  ‘kirikuu’ zilikwenda kwa Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini.

Hii ni mara ya tatu Benki ya NBC kuendesha kampeni ya akaunti ya Malengo mara hii ikitoa zawadi zenye thamani ya zaidi ya shs milioni 204 ambapo mwaka 2016  wateja wawili Aldo Nsuha mkazi wa Tabata  Dar es Salaam na Lawrence Njozi kutoka Masasi mkoani Mtwara wakijishindia magari mapya aina ya Toyota Hilux double cabin.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive