A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, January 31, 2018

WANANCHI WATAKIWA KUNAWA MIKONO ILI KUEPUKA MAGONJWA YA MILIPUKO

Afisa Afya Wilaya kinondoni John Kijumbe akizungumza na waandishi wa habari leo katika hafla yakufunga mradi wa magonjwa ya kuambukiza kwa kunawa mikono (kutoka kushoto) ni Mratibu wa Mradi huo Rose Temu, Mganga Mkuu  wa Kituo cha Afya Magomeni Omari Mwanga, na  ni Afisa Elimu Sayansikimu na Afya Manispaa ya Kinondoni Martha Kussaga. hafla hiyo imefanyika kashule ya Msingi Kigogo
Afisa Elimu Sayansikimu na Afya Manispaa ya Kinondoni Martha Kussaga. (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo katika hafla yakufunga mradi wa magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kunawa mikono, (kutoka kushoto) ni Mratibu wa Mradi huo Rose Temu, Mganga Mkuu  wa Kituo cha Afya Magomeni Omari Mwanga, na Afisa Afya Wilaya kinondoni John Kijumbe, hafla hiyo imefanyika kashule ya Msingi Kigogo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kigogo wakiwa katika hafla hiyo..... PICHA NA BRIAN PETER

Wananchi wametakiwa kunawa mikono wakati wote kabla ya kula ili kuepuka magonjwa ya milipuko yatokanayo na maradhi kutokunawa mikono. 

Akizungumza na waandishi wa habari Leo katika hafla ya kufunga Mradi  wa magonjwa wa kuambukiza kwa njia ya kunawa mikono jijini Dar es Salaam Afisa Afya Wilaya kinondoni JOHN KIJUMBE amesema walianzisha Mradi wa Kunawa mikono Uliofadhiliwa na shirika la  kimataifa kutoka Japan JICA,likishirikiana na kituo cha  Afya Magomeni ukiwa na lengo la kutoa elimu ya kujikinga na maradhi ya kuambukiza kwa Njia ya kunawa mikono .

Amesema Mardi huo ulianzishwa Julai na kuzinduliwa Septemba 25,2017  ambapo umekamili January 2018 ambapo ulilenga kutoa elimu ya kuanawa mikono mashuleni katika Wilaya ya Kinondoni ambapo waliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi pamoja na walimu na kubaini kuwa wananchi wanauelewa mdogo wa Kunawa mikono baada ya kutoka chooni,na kabla ya kula.

"Katika huu mradi tuliouanzisha chini ya shirika la kimataifa la Japan (JICA) likishirikiana na kituo cha Afya Magomeni tumeweza kutoa elimu kwa shule katika Wilaya ya Kinondoni  na kubaini kuwa wanafunzi wengi hawana elimu ya kunawa mikono jambo ambalo ni hatari kwa Afya zao na kusababisha magonjwa ya Milipuko "Amesema Kijumbe. 

Aidha amebainisha changamoto walizokumbana nazo ambapo amesema watu wanachukulia kunawa mikono siyo jambo  muhimu, pamoja na ukosefu wa vifaa vya kunawa mikono katika jamii na mashuleni pia, hivyo amesema mradi huo utakuwa ni endelevu kwa jamii ili kuweza kukuza elimu hiyo ya kunawa mikono. 

Pia amesema katika mradi huo wamepata mafanikio mbalimbali ambapo wameweza kufunga vifaa vya kunawia mikono kwa baadhi ya shule.

Kwa upande wake mratibu wa Mradi huo Rose Temu amesema Mradi huo utakuwa emdelevu na kutoa wito kwa watanzania kujenga mazoea ya kunawa mikono unapotoka chooni na  kabla ya kula ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive