A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, September 30, 2019

KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA ENERGY YAMKABIDHI RC MAKONDA HUNDI YA SHILINGI MILIONI 40 KWAAJILI YA KAMPENI YA UPASUAJI MOYO KWA WATOTO 20 KUTOKA FAMILIA DUNI


Kampeni ya Matibabu ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto 10 kutoka familia duni kila mwezi kwa Muda wa Miezi 6 iliyoanzisha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda imeendelea kuleta matokeo chanya na kuokoa Maisha ya Watoto ambapo leo September 30 Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy imemkabidhi Mkuu huyo wa Mkoa hundi ya shilingi Milioni 40 ikiwa ni sehemu ya Kuunga mkono kampeni hiyo.

Akipokea hundi hiyo RC Makonda amesema kiasi hicho cha fedha kitasaidia kuokoa maisha ya takribani watoto 20 kutoka familia Duni ambao wamelazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakisumbuliwa na tatizo la moyo lakini wameshindwa kupata matibabu kutokana na kushindwa kumudu gharama.


RC Makonda ameeleza kuwa alikutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Puma kwenye Hafla ya Ugeni wa Maraisi wa Nchi za SADC iliyofanyika Ikulu na katika hafla hiyo mkurugenzi huyo alijisogeza kwa RC Makonda kwa lengo la kujitambulisha ambapo Mkuu wa Mkoa alitumia nafasi hiyo kumuelezea Changamoto ya uwepo wa Watoto zaidi ya 500 wenye tatizo la moyo na mkurugenzi huyo alipokea kwa mikono miwili ombi hilo na hatimae leo amekabidhi hundi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Puma Energy Bw. Dominic Dhanah amesema kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za RC Makonda katika masuala mbalimbali yanayolenga kutatua kero za Wananchi wasiojiweza.
Hayo yote yamejiri wakati wa Hafla ya kufunga mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi zaidi ya 20,000 kutoka shule 9 za mkoa wa Dar es salaam yaliyotolewa na Taasisi ya AMEND na kudhaminiwa na Kampuni ya Puma Energy ambapo RC Makonda amewataka Madereva kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu za Usalama Barabarani ili kuepusha ajali kwa watembea kwa miguu.
Share:

Sunday, September 29, 2019

RC MAKONDA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MACHINJIO MAPYA YA VINGUNGUTI, ATOA MAAGIZO MATATU MAZITO MANISPAA YA ILALAMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti ikiwa ni mkakati wake wa kufuatilia bila kusubiri kuletewa taarifa ofisini ambapo amewapongeza Shirika la Nyumba la Taifa NHC kwa kufanya Kazi Usiku na Mchana kwa lengo la kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya Miezi mitatu kama ilivyo Matarajio ya Rais Dkt. John Magufuli.

Katika ziara hiyo RC Makonda amemuelekeza Mstahiki Meya wa Ilala Bw. Omary Kumbilamoto kuja na Mpango wa kuhakikisha miundombinu ya Reli inaunganishwa kwenye machinjio hayo ili Treni iweze kutumika kupokea wanyama na kusafirisha nyama ndani na Nje ya Nchi.

Aidha RC Makonda amemuelekeza Meya huyo kuhakikisha ujenzi wa Barabara ya Vingunguti unaanza Mara moja huku akiitaka Manispaa ya Ilala kufikiria uwezekano wa kulipa fidia kwa wakazi wanaozunguka machinjio hiyo ili kwa miaka ijayo machinjio iweze kupanuliwa na kuwa kubwa zaidi.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kuwa tayari mchakato wa kuagiza mashine mbili za kisasa za Kuchinja na kuchakata nyama umekamilika ambapo Mashine itakuwa na uwezo wa  kuchinja, kusafisha na kuchakata Wanyama 2,000 kwa siku moja.

Katika hatua nyingine RC Makonda amefanya ziara ya kustukiza kwenye Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa la Kisutu na kumuagiza Mkandarasi wa ujenzi wa Soko hilo kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika na kukabidhiwa kabla ya mwezi May Mwakani.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kutoridhishwa kasi ya ujenzi wa soko hilo ambalo limekuwa likisuasua mara kwa Mara huku wataalamu wakitoa taarifa za wongo kuwa ujenzi unaenda vizuri.

Share:

Friday, September 27, 2019

BOLLORE TRANSPORT AND LOGISTICS TANZANIA PARTICIPATING IN THE 4TH EDITION OF MARATHON DAY TO BENEFIT SOS CHILDRENS VILLAGESOn Thursday, September 26,  2019, 200 employees from Tanzaniaare taking part in the the 4th edition of the Marathon Day. This internal sporting event was created by Cyrille Bolloré, CEO of the Bolloré Group, to raise every funds for charity organisations every year.

Since 2016, Marathon Day has brought together employees from all Bolloré Group subsidiariesaround the world on the same day at the same time. This year, 200employees will be completing the 5-kilometre run in Dar es Salaam . For each registration, three euros are donated to a charity organisation. The Group, which supports young people through its sponsorship programs, has decided this year to support SOS Childrens Villages International, as it did last year in 2018.

For over 60 years, SOS Childrens Villages has supported children whose family situations have forced them to be housed elsewhere. It allows siblings to grow up together in a family-like environment, supported by an educational and effective long-lasting relationship in link with a family educator (the "SOS mother"). Beyond its mission to host children, it also develops programmes to promote access to education, professional training and healthcare. Furthermore, it works to strengthen family ties and prevent abandonment.

Closer to us here at Mabibo we pride ourselves in the change we are able to bring to the communities that surround us; in this regard we will be working closely with Mabibo Secondary School on the following actions in the months ahead:

1.       Donating 40 tables and office chairs to the school for use in the Administrative block (staff rooms);
2.       Creating a full-functional computer lab which will allow Mabibo Secondary Schools to offer computer studies and set itself apart while giving students the much needed introduction into today’s world of technology; and
3.       Constructing a state of the art buo-gas toilets for use by the students to improve hygiene conditions of the school as well as reducing expenses on the school as the bio-gas produced from the tudent’s waste can ne used to make cooking gas, electricity and even manure for use in garden.

BOLLORE TRANSPORT AND LOGISTICS TANZANIA.

Founded in 1968 Bollore Transport and Logistics Tanzania prides itself in employing more than 300 staff 99% of whom are local Tanzanias.


BOLLORE GROUP.

Founded in 1822, the Bolloré Group is one of the 500 largest companies in the world, with more than 81,000 employees in 127 countries, on five continents. Thanks to a diversification strategy based on innovation and on international development, it now holds strong positions in all its activities around three business lines: Transportation and Logistics, Communication, Electricity Storage and Systems.

Press contact:

KULWA, Busegi
Phone +255682 851 367
E-mailBusegi.Kulwa@bollore.com


Share:

LSF Projects assisted over 5 million needy-poor to access justice

Mr. Eugen Mawele (left)—a paralegal from Chemba district (Dodoma) receiving paralegals-re-fresher course certificate from LSF Chief Executive Officer, Lulu Ng’wanakilala, during legal aid stakeholders’ conference held in Dodoma and organized by LSF.  (Correspondent).   

More than 5 million poor Tanzanians have received legal aid services and helped out of legal and related problems through a national-wide paralegal projects implemented by legal aid organizations with funding from the Legal Services Facility (LSF).
This was revealed in Dodoma recently during a stakeholders meeting of legal aid providers involved in the implementation of LSF-financed paralegal and legal aid projects across the country—mainland and Zanzibar. The meeting which attracted representatives from 200 legal aid organization funded by LSF, sought to provide space for the stakeholders to discuss successes stories registered in the implementation of the project and put in place workable strategies for improvement of legal aid services delivery and assist millions of needy- poor to access justice.
Speaking to reporters on the sidelines of the meeting, LSF Chief Executive Officer, Lulu Ng’wanakilala said “In general, we have made great strides in the implementation of this project...we have reached more than 5 million people with various legal problems since the  project incepted in 2011. All these people have received legal aid services through paralegals from legal aid providers funded by LSF in the country.”
So far, LSF has recruited over 3,000 paralegals, who work mainly in rural areas, where the majority of people do not have access to legal aid services and experience various legal and related problems, especially women. Some of the problems facing many people include those related to inheritance, land, child custody, early pregnancy and many others, according to an official statement issued by LSF.
According to the LSF CEO, the meeting, besides other things, focused on enabling legal providers to evaluate the objectives of the project and find out what they have achieved or not and chart out strategies to widen the scope of legal aid services delivery and enable needy-poor Tanzanians to access justice. “Legal aid services has greatly expanded and helped many people to access justice across the country. For instance, last year more than 3 million people were reached and received legal aid services, whereby 76,000 cases were filed and 60 per cent of them were resolved.”
Mr Marius Isavika, Project Manager from KASADEFO (Simiyu Region), one of the organisations implementing LSF-financed project, said his organisation had resolved many land disputes and solved other problems facing people living in rural areas through paralegals in various wards in Simiyu Region.
“We focus more on women and poor people living in the rural areas, taking into account that it is only 7 per cent of Simiyu residents, who live in urban areas. The rest live in rural settings. So, we, KASADEFO, see the LSF project as a big help to poor people (with legal and problems) in Simuyu Region.”
For her part, Ms Veronica Olomi, Communication Officer of KWIECO (Kilimanjaro) said through about its 170 paralegals, the organization assisted many people out of various legal problems, “but we still have a big challenge because paralegals we have serve in fewer wards compared to the number of people in need of legal aid services. This means legal aid services are still inaccessible to many people.”
“However, as an organisation we continue raising public awareness especially in wards without paralegals to enable them to utilise available systems - ward tribunals, local government, social development officers and various organs – so that they may get their rights.”
The meeting focused also on building capacity, addressing various challenges in various parts of the country and set priorities in the implementation of projects to bring about development and get the anticipated results, which are equal rights to all for the development of the people and the country in general, according to Ms Scholastica Jullu, LSF Project Director.
“The meeting provided, among other things, an opportunity to LSF to highlight its strategic plan, which aims at improving legal aid services, including increasing access to legal aid services in urban areas because urban challenges differ from rural challenges and LSF has been implementing its projects especially in rural areas,” reads part of a statement from LSF.
Share:

Benki ya NBC yaendelea kuipiga jeki sekta ya madini

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimsikiliza  Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Geita, Martin Nkanda wakati wa maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Katikati ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira. NBC ni mmoja ya wadhamini wa maonesho hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Geita, Martin Nkanda katika Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini. Katikati ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Geita, Martin Nkanda wakati akiwasili katika hafla ya Ufunguzi wa Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita hivi karibuni. Wapili kulia ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira. NBC inadhamini maonyesho hayo.

Waziri Mkuu, Kassim Majakiwa (kushoto), akisalimiana na Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira, akipokwenda kufungua rasmi maonesho hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert (kulia) akisalimiana na Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira wakati akitembelea banda la benki hiyo katika  Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Katikati ni Meneja Uendeshaji Tawi, Thadei Tibalinda.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kulia), akisalimiana na Ofisa Huduma kwa Wateja, Aggrey Kanani wakati akitembelea banda la Benki hiyo wakati wa Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Katikati ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira.
Share:

Wednesday, September 25, 2019

Benki Ya DCB Yazidi Kung’ara


Benki ya Biashara ya DCB imetangaza kumaliza kampeni ya bidhaa yake ya akaunti ya muda maalumu inayojulikana kama ‘DCB Lamba Kwanza’ kwa mafanikio makubwa huku ikivuka malengo yake iliyojiwekea ya shilingi Bilion 15 na kuongeza amana kwa shilingi Bilioni 18.5 ambayo ni zaidi ya asilimia 123.

Kampeni ya DCB Lamba Kwanza iliyozinduliwa Mei 29 mwaka huu na kudumu kwa muda wa miezi mitatu huku ikiwa na lengo la kukusanya amana za kiasi cha shilingi Bilioni 15, iliwawezesha wateja wa benki hiyo  kuwekeza na kupata riba ya hadi asilimia 14 ya amana wanayowekeza  ambapo mteja alianza kupokea riba yake ya mwezi  papo hapo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko alisema ‘tunatoa shukurani zetu za dhati kwa wateja wetu kwa kuweza kuipokea bidhaa hii na kuweza kunufaika nayo kwani wamenufaika sana, kila mwezi umekua mwezi wa faida. Mteja anafurahia riba yake inayolipwa mwanzo wa mwezi kila mwezi, malipo ya riba ni rafiki mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu (3) mpaka miaka miwili (2). Ni jambo la fahari kuona Benki ya kitanzania inatoa fursa kwa Watanzania na kuwawezesha kuboresha maisha na uchumi’.

Alisema DCB Lamba Kwanza imepokewa kwa mikono miwili na wateja wetu na kufanikiwa kuvuka malengo kwa kukusanya amana ya zaidi ya shs bilioni 18.5 ambapo awali Benki ilikusudia kuuza kiasi cha shs bilioni 15.

 “Kwa namna ya kipekee ningependa kwanza kabisa kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kila bidhaa tunayoiingiza sokoni na kutuwezesha kuvuka malengo hii inaonyesha ni jinsi gani DCB inavyo aminika kwenye soko.

“Benki ya DCB tupo imara na tumejidhatiti katika kubuni na kuingiza bidhaa zitakazokidhi kiu ya mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja wetu,”

Kwa sasa benki imeendelea kufanya maboresho katika baadhi ya huduma zake ikiwa ni pamoja na kupunguza riba na kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 15 kwa mikopo ya ujenzi na ununuaji wa nyumba za makazi kwa wateja wetu wote hususan wafanyabiashara na waajiriwa. Hii imefanya benki yetu kuongoza kutoa mikopo mingi zaidi ya ujenzi wa nyumba na ununuaji wa nyumba Tanzania. (kwa takwimu za Tanzania Mortage Refinance-taasisi iliyo chini ya benki kuu). Tunatoa wito kwa wajasiriamali wote na wafanyakazi wenye lengo la kununua au kujenga nyumba kuwahi fursa hii.

Vilevile benki inatoa huduma za kidigitali kupitia DCB DIGITAL inayomuwezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi, DCB sokoni inayomsaidia mkulima,wenye viwanda vya kilimo  pamoja na wafanya biashara wa kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Vile vile tuna akaunti na huduma nyingi zinazotoa fursa kwa watanzania kuweka akiba lakini pia kupata faida ya fedha zao.

Kampeni hii ni muendelezo wa mafanikio yanayofanywa na Benki ya DCB kwani Benki hii imeendelea kupata faida, na kufikia kipindi cha nusu ya kwanza ya  mwaka huu imeweza kupata faida ya sh. bilioni 1.2 ikiwakilisha ongezeko la asilimia 118% kutoka faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2018. Utendaji wa benki umeimarika,huku ufanisi katika nyanja zote muhimu ukiongezeka kwa kiwango cha kuridhisha ukichagizwa na kukua kwa biashara na ukusanyaji wa mikopo chechefu. Vile vile benki imeendelea kuvunja rekodi  katika malengo kama  ilivyotokea  hivi karibuni ilipotangaza kuvuka malengo katika zoezi la uuzwaji wa hisa zake kwa  kuuza hisa milioni 36.6, ikiwa ni zaidi ya malengo ya awali  ya kuuza hisa milioni 33.9 na  kufanikiwa kukusanya sh. Bilioni 9.7 sawa na asilimia 108.99 ya matarajio ya awali ya kukusanya shilingi Bilioni 8.9.

“Tunafurahi kuwaambia kuwa lengo letu limetimia, kampeni imeisha lakini bidhaa ya DCB Lamba Kwanza itaendelea, hivyo wale wateja ambao bado hawajafungua akaunti hii bado ipo na wanaweza kuwahi katika matawi yetu kuanza kuwekeza na ‘KULAMBA’ riba.

Ikumbukwe Kuwa

Benki ya Biashara ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama Benki ya Jumuiya ya Wananchi “community bank” na Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kufuatia kilio cha wakazi wengi wa Jiji kutokuwa na njia rahisi ya kupata mitaji midogo midogo ya biashara.

Benki ya DCB imekuwa ni benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa mwaka 2008, na imeweza kukuza mtandao wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la Dodoma, na inatarajia kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.

Uboreshaji huduma na mahusiano ya wateja umekuwa ndio kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na za muda mrefu hasa kutoka kwa wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali yaliyoendelea kuwekeza na benki ya DCB. 

Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 195,611 Agasti 2019 na hivyo kuchangia ongezeko kubwa la miamala ya kibenki. 

Benki ya DCB imefungua mtandao wa mawakala na huduma za kijiditali hadi kufikia 1000 nchi nzima. 
Share:

Benki ya NBC yasaini makubaliano na Jeshi la Polisi ya ulinzi katika matawi yake nchini

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberat Sabas (wa pili kushoto) na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas wakibalishana hati za makubaliano ya ulinzi wa askari wa jeshi hilo katika matawi yote NBC nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Jana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Gustavus Babile, Mkuu wa kitengo cha Sheria wa NBC, Doxa Mbapila na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Alelio Lowassa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberat Sabas (kushoto) na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas wakisaini hati za makubaliano ya ulinzi wa askari wa jeshi hilo katika matawi yote ya NBC nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Jana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Gustavus Babile, Mkuu wa kitengo cha Sheria wa NBC, Doxa Mbapila na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Alelio Lowassa.
Share:

Monday, September 23, 2019

NBC yazindua mkopo wa bima

Waziri wa Ujenzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele (kushoto), akizungumza na MKurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto), mara baada ya mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori  Tanzania (TATOA), ambako benki hiyo ilizindua rasmi huduma yake mpya ya mkopo wa bima.  Wanaoangalia ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo.


BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua mkopo wa bima ikiwalenga zaidi wafanyabiashara walio katika sekta ya uchukuzi.

Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru alisema mkopo huo unapatikana kwa kuanzia kiasi cha shilingi milioni 1 mpaka milioni 300.

Alisema mkopo wa bima wa NBC ni kwa ajili ya bima za biashara zote zikiwemo biashara za magari, bidhaa zilizo safarini, majanga ya moto, ujambazi, hatari zote za barabarani na ajali kwa wafanyakazi.

“Mtu yoyote mwenye mahitaji ya bima akiwa na rasilimali zozote kama vile nyumba ana sifa ya kupata mkopo huu bila kuwa na dhamana yoyote.

“Utalipia miezi miwili ya bima yako NBC na sisi tutalipia miezi 10 inayobaki kwa wakala wa kwa niaba yako, nawe utailipa benki kila mwezi kidogo kidogo. Mkopo huu una riba ndogo kabisa kuliko mikopo yote inayotolewa na benki”, aliongeza Bwana Ndunguru.

Pamoja na hayo mkurugenzi huyo alisema, uamuzi wa kuanzisha huduma inayowalenga wafanyabiashara imetokana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano katika kuondoa kero zikizokuwa zikiizorotesha sekta ya uchukuzi.

“NBC imeongeza kutoa mikopo zaidi katika sekta ya usafirishaji, mkopo wa bima kutoka NBC unakuwezesha kuendelea kuikinga biashara yako dhidi ya hasara au matatizo mengine yoyote hata kama huna fedha taslimu za kulipia bima”, alisema.

Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Ujenzi,  Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwele alipongea NBC katika juhudi inazofanya katika kuinua  sekta ya biashara ndogo na za Kati.
Akitoa mfano Waziri Kamwele alisema ni hivi karibu Benki ya NBC ilisaini makubaliano na Shirika la Posta Tanzania ambapo benki itaweka ofisi katika kila palipo na tawi la Shirika hilo popote nchini.
Share:

Sunday, September 15, 2019

NBC yaendelea kusaidia ujenzi wa shule na ofisi za walimu nchini

Meneja wa Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (wa nne kushoto), akishikana mikono na Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan wakati akimkabidhi msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika shuleni hapo Visiwani Zanzibar jana.
Meneja wa Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (wa nne kulia) akikabidhi msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 8 kwa Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika shuleni hapo, Zanzibar jana.
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (katikati, mwenye suti nyeusi) akikabidhi baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwemo mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 8 kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Maandalizi ya Kisimkazi vilivyotolewa na NBC mjini Zanzibar jana. Wa nne kushoto ni Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan (wa pili kushoto), akizungumza kabla hajapokea msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kutoka benki ya NBC kwa ajili ya kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi katika hafla iliyofanyika visiwani Zanzibar jana. Wa nne kulia ni Meneja wa NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso.
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kwa ajili ya kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi vilivyotolewa na benki hiyo visiwani Zanzibar jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan.
Share:

Thursday, September 12, 2019

Benki ya NBC yasaidia ujenzi wa kituo cha polisi Lindi

Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda (katikati aliyevaa suti), akikabidhi msaada wa mabati 135 pamoja na  mifuko 30 ya simenti vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga kusaidia  ujenzi wa kituo cha polisi cha Rondo Mnara ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika tawi la NBC mkoani Lindi.
Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda (katikati aliyevaa suti), akikabidhi msaada wa mabati 135 pamoja na  mifuko 30 ya simenti vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga kusaidia  ujenzi wa kituo cha polisi cha Rondo Mnara ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika tawi la NBC mkoani Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, akishikana mikono na Meneja wa Tawi la NBC Mkoa wa Lindi, Iovin  (kulia) wakati akipokea  msaada wa mabati 135 pamoja na  mifuko ya simenti 30 yenye thamani ya shilingi milioni 4 vilivyotolewa na NBC kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi cha Rondo Mnara ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za beni hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Tawi la NBC mkoani Lindi. Kushoto ni  Mwakilishi wa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi, Inspekta Benard Simpemba.
Share:

Tuesday, September 10, 2019

Benki ya NBC yaendelea kusogeza huduma karibu na wateja

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega (kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya huku Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya akiangalia katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Arusha hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro (wa pili kushoto), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Linley Kapya wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na benki ya NBC jijini Arusha juzi. Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya (wa pili kushoto) akishikana mikono  na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Arusha hivi karibuni. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro na Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Linley Kapya (katikati) akizungumza na baadhi ya wateja katika hafla waliyowaandalia jijini Arusha hivi karibuni kwa lengo la kufahamiana na kupata mrejesho wa huduma wanazopewa na benki hiyo.
Share:

Wednesday, September 4, 2019

Taasisi ya SAP kupitia program ya INITIATIVE CODE WEEKS imeanza kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu

Mkurugenzi Ushirika na Uwajibikaji wa Jamii EMEA na Mkuu wa wiki ya Code Afrika, Claire Gillissen (kulia), akizungumza na Walimu kutoka shule mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kutoa  mafunzo ya Programming  kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima  yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na  na jamii nzima. uzinduzi huo umefanyika  leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa SAP, Liam Ryan, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kutoa  mafunzo ya Programming  kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima  yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na  na jamii. Uzinduzi huo umefanyika  leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kutoa  mafunzo ya Programming  kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima  yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na  na jamii. Uzinduzi huo umefanyika  leo jijini Dar es Salaam.

Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa akizungumza katika haflahiyo.


Kutokana na umuhimu wa teknolojia katika elimu na jamii  kiujumla kuongezeka,Kutokana na umuhimu wa teknolojia katika elimu na jamii  kiujumla kuongezeka,Taasisi ya SAP kupitia program ya INITIATIVE CODE WEEKS imeanza kutoa mafunzo  ya  Programming kwa walimu  kutoka Tanzania na Afrika nzima kwa lengo la kuwafikia wanafunzi wengi na kutengeneza msingi mzuri wa teknolojia kwa kizazi cha baadae.


Akizungumza  leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa SAP, Liam Ryan amesema kuwa SAP ikishirikiana na taasisi mbalimbali wamemekusudia kwa dhati kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya mia tano kutoka Tanzania na zaidi ya walimu elfu tano kutoka Afrika wakiwa na lengo la kuwafikia wanafunzi na watoto zaidi ya milioni moja na nusu Afrika nzima.

Kwa upande wake Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari amesema kuwa wanakusudia kuwafundisha walimu programu iitwayo scratch ambayo itatoa hamasa  na hamu ya wanafunzi kupenda kujifunza teknolojia ambpo amewataka walimu walioko kwenye mafunzo hayo wapende na  wajitume kujifunza  kuhusu programu hiyo na  teknolojia kwa ujumla ili waweze kuwafundisha wanafunzi kikamilifu.

Akizungumza mmoja wa walimu  katika mafunzo hayo,Mussa  Awadhi kutoka shule ya sekondari Benjaminj Mkapa, amesema kuwa programu  ya scratch inamuwezesha mwanafunzi kuelewa kwa urahisi masuala ya teknolojia kwani imetengenezwa kwa mfumo wa picha  (katuni)na ni rahisi kujifunzia. imeanza kutoa mafunzo  ya  Programming kwa walimu  kutoka Tanzania na Afrika nzima kwa lengo la kuwafikia wanafunzi wengi na kutengeneza msingi mzuri wa teknolojia kwa kizazi cha baadae.


Akizungumza  leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa SAP, Liam Ryan amesema kuwa SAP ikishirikiana na taasisi mbalimbali wamemekusudia kwa dhati kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya mia tano kutoka Tanzania na zaidi ya walimu elfu tano kutoka Afrika wakiwa na lengo la kuwafikia wanafunzi na watoto zaidi ya milioni moja na nusu Afrika nzima.

Kwa upande wake Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari amesema kuwa wanakusudia kuwafundisha walimu programu iitwayo scratch ambayo itatoa hamasa  na hamu ya wanafunzi kupenda kujifunza teknolojia ambpo amewataka walimu walioko kwenye mafunzo hayo wapende na  wajitume kujifunza  kuhusu programu hiyo na  teknolojia kwa ujumla ili waweze kuwafundisha wanafunzi kikamilifu.

Akizungumza mmoja wa walimu  katika mafunzo hayo,Mussa  Awadhi kutoka shule ya sekondari Benjaminj Mkapa, amesema kuwa programu  ya scratch inamuwezesha mwanafunzi kuelewa kwa urahisi masuala ya teknolojia kwani imetengenezwa kwa mfumo wa picha  (katuni)na ni rahisi kujifunzia.

Share:

BENKI YA KCB TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA 2019/20

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (kushoto), akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 kwa Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia, kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. Wanaoshuhudia, (watatu kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, (Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo Bi. Christine Manyeye na Mwanasheria Mkuu waBenki ya KCB, Bi. Anthonia Kilama hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (wa tatu kushoto), Pamoja na Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia, wakionyesha hundi ya shilingi milioni 500 iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. Benki ya KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. (watatu kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga,  wengine ni viongozi kutoka TFF na KCB.

Benki ya KCB Tanzania imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara  kwa msimu wa 2019/2020. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi  za Kitanzania 420,000,000 kabla ya kodi, ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario na Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Benki ya KCB Tanzania ilidhamini ligi hiyo kwa mara ya kwanza msimu wa 2017/18 kwa thamani ya shilingi za Kitanzania 325,000,000 na kuongeza udhamini kwa msimu wa 2018/19 kufikia shilingi za Kitanzania 420,000,000. Mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa udhamini wa misimu iliyopita ndiyo yameivutia Benki ya KCB Tanzania kuendeleza udhamini huo kwa kiasi cha shilingi za Kitanzania 420,000,000 kupelekea jumla ya udhamini ndani misimu mitatu kuwa shilingi za Kitanzania 1.165bn.

Hafla ya kutia saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, Katibu Mkuu TFF, Nd. Kidao Wilfred, Mwenyekiti wa bodi ya Ligi Kuu, Nd. Steven Mnguto na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura, Pamoja na Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba pamoja na dhamira ya benki hiyo kurudisha kwa jamii, udhamini huo pia ni fursa kubwa kwa Benki ya KCB kuwekeza kwenye sekta yenye kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kukuza ajira na vipaji vya vijana wa Kitanzania.

Zaidi ya kutengeneza ajira kwenye soka, Benki hiyo imewekeza kwenye programu ya KCB 2jiajiri ambayo hadi sasa imetoa mafunzo ya uweledi wa biashara kwa wanawake 256 na vijana 100 kuanzia mwezi Oktoba. “Matarajio ya benki yetu ni kuona Watanzania wengi zaidi wanapata ajira kupitia sekta mbali mbali tunazozigusa.” Alisema Nd. Kimario.

“Sisi Benki ya KCB, mbali na biashara tunatimiza  wajibu wetu katika jamii inayotuzunguka kwa kuiunga mkono serikali yetu kupinga umasikini nchini. Hivyo pia tunasaidia jamii hitaji kupitia sekta za: elimu, afya, mazingira, wajasiriamali, watoto waishio katika mazingira magumu.” Aliongeza Nd. Kimario.

Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia aliishukuru Benki ya KCB Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Tanzania Bara jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2019/20.  Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive