A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Saturday, July 20, 2024

MADEREVA BODABODA TANGA WASHUKURU JESHI LA POLISI KWA KUTOA ELIMU KUHUSU USALAMA BARABARANI.

Na Mwandishi Wetu,Tanga

KAMANDA wa Polisi , Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga ACP Bernard Zacharia amewataka madereva bodaboda katika Mkoa huo kuwa  mfano wa kuigwa na mabalozi wazuri wa kutii bila shuruti sheria za salama barabarani ili kuhakikisha wanakuwa salama wao na abiria zao.
Akizungumza na madereva bodaboda 204 waliohitimu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani wilayani Tanga ,Kamanda Zacharia amesisitiza Jeshi la  Polisi linawahimiza watii sheria bila shuruti huku akiwashukuru Ubalozi wa Uswiss na Amend kwa ushirikiano wao na Jeshi la polisi kwa kuwaangalia vijana kwa ukaribu na kuwapatia mafunzo hayo.

"Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani tunafahamu kuwa bodaboda wamekua sehemu kubwa ya urahisishaji kwa abiria na mali zao,hivyo mafunzo waliyoyapata madereva bodaboda hao wa Wilaya ya Tanga na maeneo mengine ya mkoa huo yatawasaidia wao na abiria wao kuwa salama.

Amesema kwa Wilaya ya Tanga madereva bodaboda maarufu maofisa usafirishaji 204 wamehitimu mafunzo ya msasa ya usalama barabarani na kusisitiza waliopatiwa mafunzo wahakikishie wanakuwa.mabalozi kwa madereva wengine.Pia amesema anafahamu Kuna madereva bodaboda wengi waliofikiwa na mafunzo hayo katika Mkoa wa Tanga.

"Tunatarajia bodaboda Mkoa wa Tanga mtakua mfano wa kuigwa na mtakuwa mabalozi wazuri.Jeshi la Polisi linawahimiza kutii sheria bila shuruti na tunawashukuru Ubalozi wa Uswiss na Amend kwa ushirikiano huu na Jeshi la polisi kwa kuwaangalia vijana kwa ukaribu huu."

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Amend Ramadhan Nyanza amesema wanaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na mashirika yasio ya kiserikali kuzifikia jamii. 

"Katika kipindi cha mwaka mmoja kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswiss nchini ,- Shirika la Amend kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumefanikiwa kutoa mafunzo kwa vijana zaidi ya 900 kwa mkoa wa na Tanga na Dodoma."
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive