A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, April 29, 2021

Hivi ndivyo TEHAMA inaweza kupunguza uzalishaji wa kaboni na kuifikishaAfrika katika uchumi wa kijani.

 Smarter%2BEnergy%2Bfor%2Ba%2BBetter%2BLife

(Johannesburg, 21 Aprili 2021) Kampuni ya teknolojia ya kimataifa, Huawei inaamini kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano au TEHAMA, ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni kwa asilimia 20 katika muongo mmoja ujao.

William Xu, ni Mkurugenzi wa Bodi na Rais wa Taasisi ya Utafiti wa Mikakati wa Huawei, hivi karibuni alisema uendelevu wa nishati ni changamoto kubwa ambayo itazikabili nchi zote kwa muongo mmoja ujao.

“Matumizi ya nishati ulimwenguni yanaongezeka kwa kiwango cha asilimia 1.7 kila mwaka. Hivi sasa asilimia 85 ya nishati hutokana mabaki ya mimea na wanyama wa kihistoria yaani ”fossils”. Uendelevu wa nishati hii ni changamoto kubwa inayotukabili sisi sote. Kwa kuwezesha sekta mbalimbali, teknolojia ya TEHAMA ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni kwa asilimia 20 katika muongo mmoja ujao." Xu alisema.

Aliongeza kuwa wakati nchi nyingi zimejikita kupunguza uzalishaji wa kaboni, mahitaji ya nishati mbadala yameongezeka, na hapa ndipo TEHAMA inapotoa fursa mpya katika uzalishaji, uhifadhi na matumizi ya umeme.

"Kwa matumizi ya nishati, lazima tupendekeze mifumo jumuishi ya nishati kwa majumbani na viwandani na kuunda jamii, vyuo na miji isiyozalisha kaboni.” alisema Xu.

Hivi karibuni, Huawei ilitangaza kuwa itazingatia ubunifu na teknolojia mpya kusaidia viwanda kupunguza matumizi yao ya nishati ili kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni.

Barani Afrika pia, nchi nyingi zinazidi kuhamia katika matumizi ya nishati mbadala ili kusonga mbele katika nishati endelevu kwa siku zijazo.

Pamoja na algorithm yake ya muunganisho wa gridi inayoendeshwa na utashi wa kutengenezwa (Artificial Intelligence), Huawei imetoa zaidi ya mifano ya gridi 200 ya umeme kwa nchi zaidi ya 30. Hii imesaidia mitambo ya umeme kuunganishwa na gridi kwa uimara huku ikipelekea kuwepo na chanzo bora cha umeme wa jua.

Katika umeme wa jua pekee, Afrika imepata maendeleo makubwa katika miaka ya hivi karibuni. Zaidi ya gridi 6,200 ambazo hujumuisha gridi kubwa kabisa, za biashara na viwanda pamoja na zile ndogo zimethibitishwa kuwepo barani humo.

Kwa kuongezea, mataifa mengine tisa ya Kiafrika, mbali na Afrika Kusini na Misri, yapo njiani kujiunga na 'Gigawatt Club', lebo isiyo rasmi kwa kundi la nchi zilizo na uwezo wa kuzalisha gigawatt moja ya umeme kutokana na jua.

Huang Su, Mkurugenzi wa Huawei katika Biashara ya Umeme Dijitali Kusini mwa Africa, alisema kwamba karibu nusu ya idadi ya watu wasio na uwezo wa kupata umeme duniani wanaishi kusini mwa jangwa la Sahara.

 

"Kwa hivyo kuna haja kubwa na ya dharura ya kuharakisha ukuaji wa nishati mbadala kote katika eneo hilo ili kuhakikisha nishati ya kutosha, nafuu na ya kuaminika kwa Waafrika wote na kwa nchi kupata faida ya uchumi wa kijani." anasema.

Huawei imetumia zaidi ya miaka 30 ya utaalam na uzoefu katika teknolojia ya kidijitali ili kufanya uzalishaji wa umeme wa jua na matumizi kuwa bora zaidi na ya kuaminika kwa gharama ndogo.

Share:

Sunday, April 25, 2021

Uongozi wa juu wa Benki ya DCB washuhudia mheshimiwa Rais Samia akihutubia bunge kwa mara ya kwanza mjini Dodoma wiki hii

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (mstari wa mbele, katikati) akiwa na baadhi ya wakuu wa taasisi za fedha wakisikiliza hotuba ya Mheshiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakati ajikihutubia bunge kwa mara ya kwanza mjini Dodoma wiki hii. Viongozi hao walialikwa na Spika wa Bunge, Mhe.Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Mama Samia Suluhu hassan (katikati) akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa taasisi za fedha ambapo Benki ya DCB iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Godfrey Ndalahwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Maharage Chande mara baada ya kulihutubia bunge kwa mara ya kwanza mjini Dodoma wiki hii.
Share:

Monday, April 19, 2021

Benki ya Absa yatoa msaada wa wheelchairs 20 kwa wanafunzi wenye ulemavu

  
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa (wa tatu kushoto), akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) kwa mtoto mwenye ulemavu, Briton Andrew vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Absa, Aron Luhanga na wengine kutoka kushoto ni Mshauri kutoka Taasisi ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles; mama wa mtoto, Stella Philipo na Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania Aron Luhanga (wa tatu kushoto), akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) Agnes Yohana, mama wa mwanafunzi mwenye ulemavu, Santieli Mduma (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa (katikati), akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) Steven Francis, baba wa mwanafunzi mwenye ulemavu, Flora Steven (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Ofisa Elimu Maalum Manispaa ya Morogoro, Daniel Maganga. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa, Bakari Msulwa (wa pili kushoto), akiwa na, kutoka kushoto; Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa, Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania Aron Luhanga, Ofisa Elimu Maalum Manispaa ya Morogoro, Daniel Maganga na Mshauri kutoka Taasisi ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles, wakipiga picha na wanafunzi watano wenye ulemavu baada ya kukabidhiwa msaada wa viti mwendo vilivyotolewa na Benki ya Absa mkoani Morogoro leo. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania Aron Luhanga (kulia) na Meneja wa Tawi la Absa Morogoro, Godfrey Chilewa wakikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) kwa mwanafunzi mwenye ulemavu, Hassan Moyo (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na benki hiyo katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).
Mshauri wa masuala ya walemavu kutoka Taasisi ya Ikupa Trust Fund, Peter Charles (wa pili kulia) akikabidhi moja ya viti mwendo 20 (wheelchairs) Halima Liana, mama wa mwanafunzi mwenye ulemavu, Hassan Moyo (aliyekaa), vilivyotolewa msaada na Benki ya Absa Tanzania katika hafla iliyofanyika mkoani Morogoro leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga, Ofisa Elimu Maalum Manispaa ya Morogoro, Daniel Maganga na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa (kushoto kabisa). Viti hivyo vina thamani ya shs milioni 10 vitakabidhiwa kwa shule za msingi tano zenye wanafunzi wenye ulemavu katika mikoa ya, Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3), na Zanzibar (5).

Benki ya Absa Tanzania imekabidhi vifaa vya usafiri 20 (wheelchairs) kwa wanafunzi walemavu waliopo shule za msingi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya na Zanzibar.

Vifaa hivi vina thamani ya Tsh milioni 10 na vitagawiwa kwa wanafunzi hao kuanzia mkoa wa Morogoro (5), Dodoma (5), Iringa (2), Mbeya (3) na Zanzibar (5).

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo mjini Morogoro jana, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga amesema “benki yetu inatambua umuhimu wa kuisaidia jamii katika kila nyanja na inasimama kidete kuhakikisha vijana wanafikia malengo yao kwa wakati na kwa kupata huduma stahili. Ndio maana leo tunashirikiana na shirika la Ikupa Trust Fund kwa kuwapatia wanafunzi hawa vifaa vya usafiri hivi ili waweze kufika shuleni kwa wakati na kuendelea na ratiba zao za masomo bila kukwamishwa”.

Bw. Aron alisisitiza kwamba Benki ya Absa ina lengo kuu la kuhakikisha vijana na watu katika jamii wananufaika zaidi kwa kufikia malengo yao ikiwa ndiyo moja ya nguzi kuu katika kuimarisha mchango wetu kwa jamii. Kwa kujali kwao ila pia kuzingatia vitu muhimu vya kuwasaidia vijana katika jamii kufikia malengo yao kwa upesi na kwa njia sahihi.

Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa alitoa wito kwa wazazi nchini kuwapekeka shuleni watoto wao wenye ulemavu ili kuweza kutambua vipaji vyao na kuviendeleaa.

Alisema kuzaliwa ama kupata ulemavu sio mwisho wa ndoto katika maisha kwani kuna walemavu wanaofanya vizuri katika njanja mbalimbali zikiwemo nafasi za uongozi serikalini, wanasiasa, wanamichezo na wataalamu mbalimbali.

"nachukua nafasi hii kuipongeza Benki ya Absa kwa kushirikiana na taasisi ya Ikupa Trust Fund na ni imani yangu tukio hili litaleta hamasa kwa taasisi na makampuni mengine kuiga Mfano wa Absa", alisema.

Kwa upande wake Meneja wa tawi la Absa mkoani Morogoro, Bw. Godfrey Chilewa pia amesema “kama benki tunazidi kuekeza nguvu katika jamii zinazotuzunguka huku tukishirikiana na wadau kama Ikupa Trust Fund na kwa kushikana mkono zaidi na uongozi mzima wa serikali yetu ili kuhakikisha tunaipa jamii huduma stahili na kufanikisha malengo ya watu pia”.

Mmoja wa wazazi wa wanafunzi waliokabidhiwa viti mwendo hivyo aliishukuru Benki ya Absa akisema kifaa hicho kitamrahisishia mtoto wake kwenda shuleni ukizingatia kuwa shule nyingi za msingi wilayani hapo ni za kutwa licha ya kuwa na vitengo maalumu vya wenye ulemavu.

"Naishukuru Absa, serikali na Ikupa, naona kama Absa imechukua jukumu la kuwa baba wa mtoto wangu kwani baba yake alishafariki, najua mtoto wangu anapoenda shule na ulemavu wake unapungua", alisema mama huyo.
Share:

HUAWEI YABORESHA UWEKEZAJI ILI KULINDA BIASHARA YAKE

  Eric%2BXuMwenyekiti wa kampuni ya Huawei Bw Eric Xu

Kampuni ya mawasiliano ya Huawei imebainisha mkakati wake wa kuboresha akaunti yake ya uwekezaji ili kukuza uthabiti na kukabiliana na hali ya mashaka katika biashara inayoletwa na mvutano wa kijiografia, kuibuka tena kwa virusi vya COVID-19 pamoja na kuzuiwa kufanya biashara Marekani.


Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw Eric Xu, wakati akiwasilisha hotuba kuu katika Mkutano  wa 18 wa Wachambuzi wa kidunia. Zaidi ya watu 400, ukijumuisha wachambuzi wa tasnia na wa kifedha, viongozi wa maoni na wawakilishi wa vyombo vya habari walishiriki katika mkutano huo wa siku 3 ulioanza liyoanza Aprili 12 hadi 14, kauli mbiu ikiwa "Ujenzi wa Ulimwengu Wa Maarifa na Uliounganishwa Kikamilifu."

“Uthibiti wa kibiashara ndio kanuni inayotuongoza. Tunataka kuongeza uimara wa biashara yetu yote, na tangu mwaka jana tumekuwa tukifanya kazi kuboresha uwekezaji letu tukiwa na lengo hili akilini.” alisema Eric Xu.

Ripoti ya mwaka 2020 ya Huawei inaonyesha mapato yaliotokana na mauzo ya kampuni hiyo mnamo 2020 yanafika CNY891.4 bilioni, ikiwa ni ukuaji wa asilimia 3.8 kulinganisha na mwaka uliopita, huku faida yake kamili ilifikia CNY64.6 bilioni, ambayo ukilinganisha na ripoti ya mwaka 2019 ni ukuaji wa asilimia 3.2.

Eric Xu alisema moja ya vipaumbele ni kuongeza zaidi uwezo wa uhandisi wa programu za Huawei. "Tunatafuta fursa mpya za kibiashara katika sekta ya programu. Tunapopata kitu kinachotufaa, tutaongeza uwekezaji ili kuongeza ushiriki wa huduma za program katika vyanzo vyetu vya mapato. "alisema Eric Xu.

Mwisho wa Novemba 2018, Huawei iliamua kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani bilioni 2 katika kuboresha uwezo wao wa uhandisi wa programu. Eric Xu alisema kampuni hiyo "inafurahishwa na matokeo hadi sasa".

Programu kwa ajili ya magari kujiendesha ni mojawapo ya malengo makuu ya uwekezaji ndani ya kampuni. Kulingana na Eric Xu, programu hiyo ipo mbioni kufikia hatua ambapo magari yatajiendesha yenyewe bila dereva kujishughulisha kwa namna yoyote ile.

"Pamoja na uwekezaji mkubwa, matumaini yetu ni kusukuma mwenendo huu mbele kwani program hizi zinawezesha ujumuishaji wa tasnia ya magari na ICT, ambayo nayo hutengeneza fursa za kimkakati za muda mrefu kwa Huawei. Mara baada ya ukamilifu wa program hiyo, kutakua na mabadiliko katika sekta zote zilizo karibu ambayo yataleta mabadiliko makubwa zaidi katika miaka 10 ijayo.” Alisema Mwenyekiti huyo.

Share:

BENKI YA EXIM YAPANIA KUNUFAISHA WATEJA WAKE HUDUMA ZA KIDIGITAL

Benki Ya Exim Yajizatiti na  'Mteja Kwanza' Utoaji Huduma Za Kidigitali.


Dar es Salaam: Aprili 18, 2021: Benki ya Exim imesisitiza kuhusu mkakati wake wa kuwekeza na kutanguliza zaidi maslahi ya wateja wake hususani katika mipango yake muhimu ikiwemo ile ya  uvumbuzi na utoaji wa huduma kwa wateja.


Akizungumza kuhusiana na mkakati huo jijini Dar es Salaam mwishoni nwa wiki, Ofisa Mtandaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu alisisitiza kuwa benki hiyo imejizatiti kuhakikisha kwamba wateja wake wananufaika zaidi na ukuaji wa technolojia katika utoaji wa huduma za kibenki.


"Lengo ni kuhakikisha kwamba benki ya Exim tunatumia vyema huu ukuaji wa kidigitali katika utoaji wa huduma za kibenki kwa wateja wetu…lengo ni kuona wanaridhishwa na huduma zetu na wanazifurahia. Tunaamini kwamba furaha na ukuaji wao ndio biashara yetu,'' alisema.


Aliongeza kuwa agenda ya uvumbuzi imebaki kuwa kipaumbele cha benki hiyo katika kuelekea kwenye lengo lake la msingi ambalo ni kuifanya benki hiyo kuwa ya kidigitali zaidi huku kipaumbele kikibaki kuwa ni 'mteja kwanza'.


Katika kabiliana na changamoto ya COVID 19 benki hiyo mapema mwaka jana ilizindua kampeni ya "Maliza Kirahisi Kidigitali' iliyodumu katika kipindi cha mwaka mmoja ikilenga kubadilisha tabia ya wateja na kuongeza kasi ya mabadiliko yanayoendelea ya nchi kutoka katika kutumia pesa taslimu kwenda malipo ya dijiti.


"Kampeni hiyo pia inakwenda sambamba na kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuhamasisha matumizi ya kidigitali katika kufanya miamala uchumi pamoja na  kuhakikisha wateja wetu wanahudumiwa bila kwenda kwenye matawi" aliongezea.


Ili kurahisisha zaidi miamala na kuifanya bora zaidi na rahisi kwa wateja, benki ina chaguzi kadhaa za huduma kupitia simu na kidigitali ambazo wateja wanaweza kuzitumia kupata huduma na kufanya miamala muda wowowte katika siku saba za wiki Katika kuhakikisha kwamba huduma za benki hiyo zinakuwa jumuishi, huduma ya USSD ndio ilihusika katika kuipamba kampeni hiyo.


''Kila mwingiliano na mteja ni nafasi kwetu kuwaelewa vizuri wateja wetu na namna ya kuwahudimia kulingana na mahitaji yao. Tunapoendelea kupanua huduma zetu, tunaweza kuona jinsi kila huduma inatimiza mahitaji ya watumiaji. Ni suala la kuendelea kujifunza na uvumbuzi. ’


"Zaidi, kusikiliza kwa karibu maoni ya wateja hutusaidia kupata mrejesho unaotuwezesha kufanya maboresho na uvumbuzi ili kuimarisha huduma tunazowapatia. Lengo ni kufanya maisha yao yawe rahisi. Tunazingatia urahisi wa matumizi, na kufanya huduma zetu kuwa thabiti, salama, na haraka.'' alisema.

Share:

Sunday, April 18, 2021

NBC YAUNGA MKONO SERIKALI SEKTA YA ELIMU YATOA MSAA VIFAA VYA ELIMU KIBITI

  nbc%2B1

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu (watatukushoto) akipokea msaada wa madawati  viti pamoja na meza 500 kwa ajili ya shule za wilaya hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa Benki ya NBC Bw Elibariki Masuke(wa pili kulia) msaada huo ukilenga kuboresha sekta ya elimu  Wengine pichani ni Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe (kushoto),Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bi Neema Singo (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kibiti Bw Abduljabir Marombwa hafla hiyo imefanyika hivi karibuni wilayani kibiti.nbc%2B3

Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke akizungumza na wajasiriamali wanawake wilayani Kibiti wakati wa mafunzo ya kibiashara na ujasiriamali kwa  wanawake wajasiriamali 150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza mitaji yao na benki hiyo.
NBC%2B5
M
eneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC Bw Jonathan Bitababaje akitoa mafunzo kwa wajasiriamali hao.

Kibiti, Pwani:  April 17, 2021: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa msaada wa madawati 250, viti viti pamoja na meza 250 wilayani Kibiti mkoni Pwani ikiwa ni sehemu ya Mpango wa kipekee wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ambao unaplenga kuchangia utoaji wa elimu bora nchini.

 

Zaidi, benki hiyo pia imetoa mafunzo ya kibiashara na ujasiriamali kwa  wanawake wajasiriamali 150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza mitaji yao.

 

Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya Hiyo Bw Gullamhussein Kifu . Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe pamoja na maafisa wengine wa wilaya hiyo akiwemo  Mkurugenzi Mtendaji.

 

Bwana Masuke alisema kuwa benki hiyo imejitolea kusaidia katika kuboresha ustawi wa jamii kupitia misaada ya kijamii ikiwemo elimu na kwamba wameguswa sana na suala la changamoto ya madawatikwenye baadhi ya maeneo hapa nchini sababu iliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo ili kuboresha  zaidi sekta hiyomuhimu.

 

"Ni furaha kwetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto kwenye sekta muhimu kama hii. Kupitia ushirikiano na ushawishi tunaoupata kutoka kwa Mbunge wa Kibiti na ofisi ya Mkuu wa wilaya tunaahidi kuendelea kushirikiana na jamii ya wana Kibiti huku pia tukifikiria namna kufungua tawi letu wilayani  Kibiti kufuatia fursa mbalimbali tunazoziona ikiwemo kilimo na mradi wa kituo cha kupozea umeme wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere,’’ alisema.

 

Alishauri pia wanafunzi na walimu watakaonufaika na msaada huo kutunza madawati na meza hizo ili viweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kusaidia walengwa wengi zaidi.

 

Kuhusu mafunzo kwa wajasiriamali wanawake  Bwana Masuke alisema kuwa miongoni mwa sababu zinazokwamisha utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wengi ni pamoja na wao kuendesha biashara zao bila kuzingatia misingi ya kifedha ikiwemo kutunza kumbukumbu za mahesabu ikiwemo mapato na matumizi.

 

Kwa mujibu wa Bw Masuke ni kutokana na uwepo wa changamoto hiyo ndio sababu benki hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi nyingine ikiwemo TanTrade, SIDO, VETA na washauri binafsi kuelimisha wajasiriamali kuhusu namna bora ya kusimamia na kuendesha biashara zao ili kuwajengea uwezo kabla ya kuwapatia mikopo.

 

"Tumekuwa tukishirikiana na washirika wengine kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kwenye maeneo kama usimamizi wa hesabu, utunzaji wa vitabu na uongozi, ili tuwaweke vizuri kwa ufikiaji rahisi wa mikopo", Masuke alisema.

 

Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa kutoa msaada kwa wakati haswa unaohitajika, aliiomba benki hiyo ifungue tawi lake wilayani humo mapema iwezeknavyo ili iweze kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara husani wadogo.

 

"Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika baadhi ya shule zetu…tunashukuru sana NBC tunaomba muendelee kusaidia kwenye maeneo mengine pia ikiwemo sekta ya afya ." Alisema.

 

Akizungumzia mafunzo kwa wajasiriamali wanawake wilayani humo Bw Kifu alitoa wito kwa washiriki kuhakikisha wanayatumia vyema kwa kuwa yanalenga kuwasaidia katika upatikanaji wa mikopo sambamba na kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kwa faida

 

“Kibiti ni wilaya  changa inayohitaji watu wake ili kuendelea. Kabla hatujapokea wawekezaji kutoka nje ni lazima tuanze sisi wenyewe humu ndani. Kupitia mafunzo haya tunakwenda kupata wajasiriamali na wafanyabaishara wenye weledi wa kutosha kutambua fursa zilizopo na kuzitumia,’’ alisema.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Bw Twaha Mpembenwe aliiomba benki hiyo iendelee kuwekeza zaidi wilayani humo kwa kufungua tawi lake sambamba na kuwasaidia wajasiriamali na wakulima hususani wa zao la ufuta pamoja na vijana ambao kwasasa wanakibiliwa na changamoto ya huduma za kifedhaikiwemo mikopo na elimu ya biashara na kilimo cha kisasa.

Share:

Thursday, April 15, 2021

TADB na NBC kuwawezesha maelfu ya wakulima kupata mikopo nafuu

 _E1A1886Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Elvis Ndunguru  (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini mikataba kwaajili kuingia makubaliano yakufanya kazi pamoja na Benki ya Taifa ya Biashara NBC yenyelengo la  kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo katika minyororo ya thamani ya kilimo wengine pichani kulia ni  maofisa wa Benki ya TADB._E1A1889Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC ElvisNdunguru (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  hafla yakuingia makubaliano  yakufanya kazi pamoja na Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB yenyelengo la  kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo katika minyororo ya thamani ya kilimo kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB, Derick Lugemala.

_E1A1922

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC ElvisNdunguru wapili (kushoto waliokaa) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB, Derick Lugemala wakitia saini Mkataba wa makubaliano wa kufanya kazi pamoja kwaajili ya kuwawezesha wakulima wadogo katika minyororo ya dhamani ya kilimo wanaoshuhudia kulia ni Meneja wa Mfuko maalum wa dhamana kwa wakulima wadodo kutoka TADB  Asha Tarimo pamoja na Mkurugenzi wa sheria wa TADB Edson Rwechungura Picha na Brian Peterdownloaddownload
TADB na NBC kuwawezesha maelfu ya wakulima kupata mikopo nafuu

·         Zadhamiria kukuza mitaji na kuleta mageuzi katika kilimo, uvuvi na ufugaji

Dar es Salaam. Jumanne, 13 April, 2021. Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia katika makubaliano na benki ya biashara NBC kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo wadogo nchini kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuweza kukuza biashara zao na kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji.


Makubaliano haya, yaliyosainiwa leo katika makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam, yataiwezesha benki hiyo kutoa dhamana kwa wakulima watakaoenda kuomba mikopo NBC kufanya shughuli za kilimo, ufugaji pamoja na uvuvi kwa riba nafuu ya asilimia kumi na nne (14%) tu. Dhamana hii inaratibiwa na TADB chini ya mfuko maalum wa dhamana kwa wakulima wadogo nchini ‘SCGS’.  


“Kwa muda mrefu tumeona wakulima wetu nchini wakipata changamoto ya mitaji. Wengi wakilazimika kukopa kwa riba za kibiashara ambapo wengi wao wamekuwa wakipata changamoto ya kuhimili riba hizo kubwa. Hivyo, kama taasisi ya maendeleo ya kifedha, kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo, tumeona umuhimu wa kutoa mikopo hii nafuu kwa kushirikiana na NBC ili kuwawezesha wakulima wengi zaidi kupata mitaji,” alieleza Derick Lugemala, Mkurugenzi wa Fedha kutoka TADB.


Kwa upande wake, Elvis Ndunguru, Mkuu wa Biashara za Kibenki kutoka NBC, alisema kwamba mikopo hiyo watakayokuwa wanatoa kwa dhamana ya TADB itawawezesha kuwakopesha wakulima wadogo mikopo ya mtaji hadi kiwango cha shilingi 50 milioni kwa mkulima mmoja mmoja, shilingi 500 milioni kwa vikundi na vyama vya wakulima, na hadi shilingi 1 bilioni kwa kampuni ambazo miradi yake inawaunganisha na kuwanufaisha wakulima wadogo wengi.


Akieleza vigezo vya kupata mikopo hiyo, Ndunguru alisema:

“Ili kukidhi vigezo vya kupata mikopo hii, mkulima anahitajika kuwa amefanya biashara ya kilimo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu, awe na leseni ya biashara. Awe na kumbukumbu ya taarifa za kifedha. Mikopo hii inapatikana katika matawi yote ya arobaini na saba (47) ya NBC yaliyopo Tanzania bara na Zanzibar. Tunatoa rai kwa wakulima wote wadogo kuchangamkia fursa hii.”

 

Hapo awali, Lugemala alisema, lengo la mikopo hii yenye masharti nafuu ni kuchagiza benki za kibiashara na taasisi za kifedha kutoa mikopo zaidi kwa wakulima na kuwezesha ukuaji wa minyororo yote ya thamani yanayohusiana na kilimo, uvuvi na ufugaji nchini.


“Mpaka Desemba 2020, mfuko huu wa dhamana ulikwisha toa mikopo katika miradi ya kilimo, uvuvi na ufugaji yenye thamani ya shilingi bilioni 66 na kuwafikia wanufaikaji zaidi ya 9000 moja kwa moja na wasionufaika moja kwa moja 750,000. Baadhi ya miradi tuliyowezesha ni pamoja na kwenye korosho, mpunga, kahawa, miwa, mahindi, mihogo, pamba na ufugaji wa kuku,” alifafanua Lugemala.


Kutokana na taarifa kutoka TADB, mfuko huu wa dhamana ulianzishwa Februari 2018. Na katika kipindi cha miaka mitatu sasa, TADB imeshashirikiana na benki na taasisi za kifedha kama NMB, CRDB, Azania, Benki ya Posta (TPB), Stanbic, FINCA Microfinance, UCHUMI Commercial Bank, Tandahimba Community Bank (TACOBA), Mufindi Community Bank (MUCOBA) na NBC.


“TADB inaamini kwamba kupitia mtandao huu wa ushirikiano wa kimkakati, idadi kubwa ya wakulima wadogo watafikiwa na kuwezeshwa,” alisisitiza Lugemala.

xxxx Mwisho xxxx

Kuhusu TADB:

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ni benki ya umma yenye malengo ya kuongoza mikakati ya kujenga uwezo na mipango ya kuimarisha mnyororo wa thamani wa kilimo na kuunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuunda na kutekeleza sera za kilimo na mikopo ya vijijini. Mpaka Desemba 2020, TADB imekwisha nufaisha wakulima 1,788,202 na kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 300 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mikopo hii imewezesha kukua kwa minyororo ya thamani kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

 

Kuhusu NBC:

Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopatikana katika mikoa na maeneo mbalimbali nchini ikiwa na matawi 47 na mashine za ATM zaidi ya 180, pamoja na Mawaka zaidi ya 3,000. Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali kwa zaidi ya miaka 54 nchini . Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,100 nchi nzima.

 

Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 or email us NBC_Marketingdepartment@nbc.co.tz

Kwa taarifa zaidi:

Amani Nkurlu, Meneja Mahusiano na Masoko – TADB

Barua pepe: amani.nkurlu@tadb.co.tz                                                                                                                                Simu: +255 754 878 385 au +255 712 223 839

 

David Raymond, Meneja Mwandamizi-Chapa na Mawasiliano

National Bank of Commerce Limited (NBC)

Barua pepe: david.raymond@nbc.co.tz

Simu: +255 717 742832

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive