A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, April 19, 2023

DCB Elimu Mpango Mzima Na Mama Samia Yazidi Kupaa

Ofisa Elimu Manispaa ya Temeke, Abdul Buhety (kushoto), akipokea msaada wa madawati 30 Kwa niaba ya Shule ya Msingi Sandali kutoka Kwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Ruth Mpangalala yaliyotolewa na benki hiyo, ikiwa ni ni sehemu ya kampeni ya kisaidia elimu ya DCB Elimu Mpango Mzima na Mama Samia.
Msimamizi wa Huduma za Wateja na Masoko wa Benki ya DCB, Elizabeth Ntulu (kulia), na Ofisa Mahusiano wa Benki hiyo, Dalila ISSA (kushoto), wakikabhi sehemu ya madawati 30 yaliyotolewa na DCB kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Sandali kupitia kampeni Yao ya DCB Elimu Mpango Mzima na Mama Samia, shuleni hapo
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa Shule ya Msingi Sandali, Yohana Ndunguru (kushoto), akipokea msaada wa madawati 30 Kwa niaba ya shule hiyo kutoka Kwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Ruth Mpangalala.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Sandali wakimpa mkono wa shukurani Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya DCB, Ruth Mpangalala baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati.
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya DCB, Caroline Gabriel (kulia) katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 30 yaliyotolewa na DCB kwa Shule ya Msingi Sandali kupitia kampeni yao ya DCB Elimu Mpango Mzima na Mama Samia, shuleni hapo, Temeke, Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Msingi Sandali, Bakari Jaribu, akizungumza katika hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, Ruth Mpangalala, Ofisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, Abdul Buhety na Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule hiyo, Yohana Ndunguru.
Share:

Monday, April 17, 2023

TANZANIA COMMERCIA BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI UKUTA WA CHUO CHA TIBA MTWARA

 


Meneja wa Tanzania Commerical Bank Plc, Tawi la Newala Mkoa wa Mtwara Bw.Alex Minai (wapili Kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 100 ya Saruji kwa Mbunge wa jimbo la Newala Mhe. George Huruma Mkuchika iliyotolewa na Benki hiyo kwaajili ya kusaidia ujenzi wa ukuta wa chuo cha Uuguzi na Ukunga hii ni kampeni ya Benki ya TCB kuunga mkono juhudi za Serikali hususani Sekta ya Afya ili kuondoa changamoto zilizopo. Wengine pichani ni maofisa kutoka Chuoni hapo.
Share:

Friday, April 14, 2023

MAENDELEO BANK PLC YAJIVUNIA KUWEKA REKODI MPYA YA MAFANIKIO

 


2Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya akizungumza wanahabari pamoja na maofisa wa benki hiyo wakati akitangaza rekodi mpya ya mafanikio kuwa ni benki yenye faida kwa miaka nane mfululizo.hafla yakutangaza faida hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyi jijini Dar es Salaam.

1Baadhi ya maofisa wakiwa Maendeleo Bank wakifuatilia kwa umakini rekodi mpya ya mafanikio kuwa ni benki yenye faida kwa miaka nane mfululizo.hafla yakutangaza faida hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyi jijini Dar es Salaam.

Maendeleo Bank yaweka rekodi mpya ya mafanikio faida ya mwaka 2022 ni shilingi Bilioni 1.984 ambalo ni ongezeko la mara mbili Zaidi.

Akiungumza wakati akitangaza rekodi hiyo mpya Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya alieleza kuwa Maendeleo Bank Plc imeendelea kuwa benki yenye faida kwa miaka 8 mfululizo, kwa mujibu wa taarifa za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2022, ikiwa na mambo yafuatayo;


Ameeleza kuwa “Faida kabla ya kodi: TZS 1.984 bilioni, ukuaji wa mwaka 181%

Faida baada ya kodi: TZS 1.415 bilioni, ukuaji wa mwaka wa 141%

Jumla ya amapato: TZS 12. bilioni, ukuaji wa mwaka wa 5%

Amana: TZS 72.0 bilioni ukuaji wa 11%

Mikopo: TZS 61.0 bilioni ukuaji wa 5%


 Ukuaji mzuri wa faida hizi umechangiwa Zaidi na timu iliyojitolea na ikiwa na lengo la kuifanya benki kuwa moja wapo ya wadau muhimu wa sekta ya kifedha katika uchumi. Ningependa kuangazia baadhi ya vichochezi vya faida ambavyo ni pamoja na; ukuaji wa jumla ya mapato kwa asilimia 26 mwaka hadi mwaka kutoka TZS 14.23 bilioni hadi TZS 17.97 bilioni mwaka 2022.

Benki pia imeendelea kuonyesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi, huku uwiano wa gharama kwa mapato ikiongezeka hadi 58% kutoka 74% katika kipindi kama hicho mwaka jana,ukiwa na nia ya kufikia kiwango elekezi kutoka benki kuu cha 55% ifikapo juni 2023.

Amana za wateja ziliongezeka kwa 11% kutoka TZS 70 bilioni mwaka 2021 hadi TZS 77.8 bilioni mwaka 2022 wakati mikopo ilongezeka kwa asilimia 5 kutoka TZS 57.7 bilioni hadi hadi TZS 60.6 bilioni mwaka 2022.


Mbinu iliyotumika katika uhamasishaji na ukuaji wa amana kwa wateja ulichangiwa kwa kiasi kikubwa uboreshaji wahuduma na bidhaa bunifu ambazo benki imekuwa ikitoa. Kuongezeka kwa bidhaa za kidijitali kama vile huduma za kibenki kwa simu, huduma za uwakala ambapo Zaidi ya benki mawakala 1300 (maendeleo Bank Wakala) Zimechangia ukuaji huu unaoshuhudiwa leo hii.


Akihitimisha wakati akitoa matokeo ya mwaka mzima ya benki hiyo mkuu wakitengo cha biashara Emmanuel Mwaya alisema”ninajivunia sana na ninashukuru kwa mafanikio yetu kama timu, nab ado nina Imani kubwa kwa ya  utekelezaji wa mkakati wetu, kuongezeka kwa mahusiano ya wateja wetu, ari ya utendaji wa wafanyakazi, na uongozi thabiti tutadumisha kasi hii ya ukuaji wa biashara yetu kuu

Share:

Thursday, April 13, 2023

Absa Bank Tanzania Fetes its Dodoma Customers to Spice Ramadhan

Managing Director of Absa Bank Tanzania, Obedi Laiser (right), serves Iftar dish to some of the bank’s customers during an Iftar gala organized by Absa as a gesture of corporate care for its Dodoma customers in the Tanzania capital on Wednesday.
Absa Bank Tanzania Citizenship Manager, Hellen Siria (right), serves Iftar dish to Dodoma Region Kadhi, Sheikh Kisusu Mvumbi at an Iftar gala thrown by Absa to nourish its Dodoma customers in the city on Wednesday. On Sheikh Mvumbi right is Dodoma District Commissioner, Jabir Shekimweri.
Absa Bank Tanzania Dodoma Branch Manager, Innocent Mwamcha (right), serves Iftar meal to some of the banking potential customers during an iftar function especially set up by the bank as a gesture of kindness for its Dodoma customers in the city on Wednesday.
Absa Bank Tanzania Head of Retail Banking, Ndabu Lilian Swere (right), serves Iftar dish to some of the bank’s customers at a special iftar gala set up to fete its Dodoma customers in the city on Wednesday.
Absa Bank Tanzania Head of Business Banking, Melvin Saprapasen (right), serves Iftar dish to some of the financial giant’s customers during an iftar party set up by Absa as a gesture of care for its Dodoma customers in the city on Wednesday.
Dodoma District Commissioner, Jabir Shekimweri (left), addresses some Absa Bank customers and staff members during an Iftar function organized by the bank for its Dodoma customers to spice the Holy Month of Ramadhan in the city on Wednesday.
A cross- section of Absa Bank Dodoma customers enjoy their meal during an Iftar gala organized by the bank in the city on Wednesday.
Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

   

Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), wakiwaongoza wateja wa  pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kupata mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (kushoto), akiongozana pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  Sheikh Walid Alhad Omar na viongozi mbalimbali wa kidiniwa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na TCB kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium tower

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  Sheikh Walid Alhad Omar akitoa neno la shukrani kwa Mkurungenzi Mtendaji waTanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, kwakujali na kuona umuhimu wa mfungo wa Ramadani na kuandaa mlo wa futari kwaajili ya wateja wake wa Dar es Salaam.hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la milenium tower.Maofisa wa Tanzania Commercial Bank (TCB) pamoja na wateja wa benki hiyo wakishiriki mlo huo.

wafanya kazi wa TCB pamoja na wageni waalikwa wakiendelea kupata mlo 

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB,  Bi Chichi Banda (kushoto), akiwa kwenye picha ya pozi na Meneja Mawasiliano na Uhusiano  wa Benki hiyo Bi Gloria Mutta wakati wa hafla yakupata mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally
Share:

Sunday, April 2, 2023

TANZANIA COMMERCIA BANK YATOA MSAADA WA MADAWATI MKOANI TABORA


IMG-20230402-WA0001
Mkuu wa wilaya ya Nzega Mh Naitapwaki Tukai akizungumza wakati wa hafla yakupokea msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo
IMG-20230402-WA0000
Meneja wa Tanzania Commercia Bank Tawi la Nzega Shomari Shabani, (kushoto mwenyekoti jeusi), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Veronica Ng'waru kushoto kwake na Maofisa kutoka TCB pamoja na wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Benki ya TCB kukabidhi msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya kampeni Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo.

Tanzania Commercia Bank imetoa msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo katika kusaidia Serikali kuboresha ubora wa elimu hapa nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa benki ya TCB tawi la Nzega Bw. Shomari Shabani alisema msaada huo ni sehemu ya jitihada ambazo benki hiyo imekuwa ikifanya kusaidia jamii inayoizunguka.

Alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikijiweka mstari wa mbele kushirikiana na serikali kufanikisha mipango mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu, afya hapa nchini hatua inayopelekea kuwa ndio chachu ya maendeleo kwa sekta zote ikiwemo ya benki pia.

Mchango uliotolewa na Tanzania Commercia Bank wa kuchangia katika elimu unatokana na matumaini yetu kuwa bila kuwa na jamii iliyoelimika hata huduma za kibenki tunazozitoa zitadhoofika kutokana na ukweli kwamba biashara yetu hii inategemea sana mafanikio ya jamii inayotuzunguuka mafanikio ambayo tunaamini yataletwa na elimu,’’ alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa Wilaya ya Nzega Mh. Naitapwaki Tukai pamoja na kuishukuru Tanzania Commercia Bank kwa msaada huo alisema msaada huo umepatikana kwa wakati muafaka kwa kuwa shule hiyo ipo kwenye mkakati wa kutafuta madawati zaidi kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo.

Alisema shule hiyo sasa bado inakabiliwa na uhaba wa madawati zaidi na hivyo kutoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kuiga mfano kwa Tanzania.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive