Maendeleo Bank yaweka rekodi mpya ya mafanikio faida ya mwaka 2022 ni shilingi Bilioni 1.984 ambalo ni ongezeko la mara mbili Zaidi.
Akiungumza wakati akitangaza rekodi hiyo mpya Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Biashara wa Maendeleo Bank, Emmanuel Mwaya alieleza kuwa Maendeleo Bank Plc imeendelea kuwa benki yenye faida kwa miaka 8 mfululizo, kwa mujibu wa taarifa za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2022, ikiwa na mambo yafuatayo;
Ameeleza kuwa “Faida kabla ya kodi: TZS 1.984 bilioni, ukuaji wa mwaka 181%
Faida baada ya kodi: TZS 1.415 bilioni, ukuaji wa mwaka wa 141%
Jumla ya amapato: TZS 12. bilioni, ukuaji wa mwaka wa 5%
Amana: TZS 72.0 bilioni ukuaji wa 11%
Mikopo: TZS 61.0 bilioni ukuaji wa 5%
Ukuaji mzuri wa faida hizi umechangiwa Zaidi na timu iliyojitolea na ikiwa na lengo la kuifanya benki kuwa moja wapo ya wadau muhimu wa sekta ya kifedha katika uchumi. Ningependa kuangazia baadhi ya vichochezi vya faida ambavyo ni pamoja na; ukuaji wa jumla ya mapato kwa asilimia 26 mwaka hadi mwaka kutoka TZS 14.23 bilioni hadi TZS 17.97 bilioni mwaka 2022.
Benki pia imeendelea kuonyesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi, huku uwiano wa gharama kwa mapato ikiongezeka hadi 58% kutoka 74% katika kipindi kama hicho mwaka jana,ukiwa na nia ya kufikia kiwango elekezi kutoka benki kuu cha 55% ifikapo juni 2023.
Amana za wateja ziliongezeka kwa 11% kutoka TZS 70 bilioni mwaka 2021 hadi TZS 77.8 bilioni mwaka 2022 wakati mikopo ilongezeka kwa asilimia 5 kutoka TZS 57.7 bilioni hadi hadi TZS 60.6 bilioni mwaka 2022.
Mbinu iliyotumika katika uhamasishaji na ukuaji wa amana kwa wateja ulichangiwa kwa kiasi kikubwa uboreshaji wahuduma na bidhaa bunifu ambazo benki imekuwa ikitoa. Kuongezeka kwa bidhaa za kidijitali kama vile huduma za kibenki kwa simu, huduma za uwakala ambapo Zaidi ya benki mawakala 1300 (maendeleo Bank Wakala) Zimechangia ukuaji huu unaoshuhudiwa leo hii.
Akihitimisha wakati akitoa matokeo ya mwaka mzima ya benki hiyo mkuu wakitengo cha biashara Emmanuel Mwaya alisema”ninajivunia sana na ninashukuru kwa mafanikio yetu kama timu, nab ado nina Imani kubwa kwa ya utekelezaji wa mkakati wetu, kuongezeka kwa mahusiano ya wateja wetu, ari ya utendaji wa wafanyakazi, na uongozi thabiti tutadumisha kasi hii ya ukuaji wa biashara yetu kuu
0 comments:
Post a Comment