A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, October 31, 2019

NBC kuendelea kuwapiga jeki wanawake wajasiriamali nchini

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kushoto), kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni   Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akizungumza na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Chiku Chambuso (kushoto), pamoja na mwenzake, Lena Mwakisale katika banda la benki hiyo wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lena Mwakisale pamoja mwenzake Isdory Maumba (kushoto), alipokutana nao wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akihutubia wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo Benki ya NBC  ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kulia), akishikana mikono na Kaimu Mwenyekiti Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.

NA Mwandishi Wetu, Dar

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wanawake nchini kuondoa hofu ya kutembelea na kuzungumza na wataalamu wa masuala ya fedha na biashara katika matawi ya benki hiyo ili kufahamu huduma zao na jinsi wanavyoweza kupata huduma za kifedha zitakazoweza kuinua biashara na maisha yao.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Kwanza la Wafanyabiashara Wanawake wakubwa na wa kati jijini Dar es Salaam jana ambao benki hiyo ililidhamini, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Benjamin Nkaka, alisema ni vyema kwa wafanyabishara hao wanawake kuzoea kufanya kazi na benki kwani ni njia rahisi na pekee itakayoweza kustawisha biashara zao.

“Kuna hofu imejengeka kwa wengi kuja benki. Hofu hiyo iondoke. Njooni benki muweze kufahamu ni nini tunakitoa katika kusapoti wajasiriamali hasa wanawake,” alisema Nkaka.

Alisema miongoni mwa majukumu ya benki hiyo ni kusaidia katika kukuza uchumi hasa wa wanawake wajasiriamali, na kuongeza:

“Kwa zaidi ya miaka 50 ya huduma za benki hii nchini, tunafahamu kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili  wajasiriamali wanawake ni elimu ya mikopo. Sisi tunatoa elimu hiyo pamoja na ushauri kwa wateja wetu wafanyabiashara kadri biashara yao inavyoendelea na kuwaunganisha na mnyororo wa thamani.

“NBC pia huwakutanisha wateja na wadau mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA) na taasisi nyingine. Katika harakati zetu za kuwasapoti wanawake, tumeanzisha Vikundi Akaunti ambazo hazina makato yoyote, huku pia tukishirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) kutoa mikopo yenye garantii ya hadi asilimia 80 kuwawezesha wanawake kuingia kwenye kilimo kwa nguvu.”

Mkutano huo ulihudhuriwa na takriban wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara 1,000 kutoka mikoa yote ya Tanzania huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.

Wanawake hao walikutanishwa kupitia mwavuli unaofahamika kama ‘Madirisha’ huku wadau mbalimbali wa maendeleo wakipata nafasi ya kuwaonyesha wanawake hao fursa mbalimbali zilizopo nchini katika kuboresha uchumi wao kama vikundi.

Kampuni ya GS1 iliandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) pamoja na taasisi ya PASS.

Share:

Tuesday, October 29, 2019

NBC YAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIDIGITALI

Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati  wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize akizungumza na baadhi ya wateja wao wa makampuni wa jijini Mwanza, walipokutana na kufanya mazungumzo nao wakiwafahamisha huduma mbalimbali zitolewazo na NBC na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma hizo na jinsi wanaweza kuwahudumia vizuri zaidi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo jijini humo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati  wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto), akiwasikiliza wateja wa benki hiyo Malesh Mathade (kulia), pamoja na Mitesh Metha, walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wa NBC jijini humo hivi karibuni. NBC katika kipindi cha mwezi wa huduma kwa wateja imefanya mikutano kama hiyo kwa wateja wake sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (katikati),akishikana mikono na Mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services,  Erick Hamissi, walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wa NBC jijini humo hivi karibuni.. Kulia ni Nelson Julius naye kutoka Marine Services.
Meneja wa Huduma kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Mary Opiyo (wa tatu kushoto), akishikana mikono na mteja wa benki hiyo, Mkurugenzi wa Bugando Medical Centre, Padre Engelbert Nyandwi, katika hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa makampuni ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja  jijini humo hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni maofisa uhusiano wateja wa benki hiyo, Abdallah Aruga na  Fainess Jeremiah.
Mkuu wa Kitengo cha wafanya biashara wa kati wa Benki ya NBC Moses Minja (kushoto), akishikana mikono na mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services, Erick Hamissi, walipokutana na wateja wao wa makampuni  mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wateja jijini humo  hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslimu na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa  NBC, Jimmy Myalize.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imeendelea kuongeza na kuimarisha huduma zake za kibenki kwa njia za kidigitali ili kuwawezesha wafanyabiashara na wateja wengine kufanya miamala mingi  ya kibenki mahali walipo imeelezwa jijini Mwanza hivi karibuni.

Akizungumza na wateja wa benki hiyo jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC, Meneja  Huduma katika  Kitengo cha Wateja wa Makampuni wa benki hiyo, Mary Opiyo alisema benki hiyo imerahisisha huduma zake nyingi kwenda  kidigitali ili kuwafanya wateja wao kupata muda zaidi wa kufanya biashara zao kuliko kupata huduma hizo katika matawi yao.

“Sasa mteja wetu anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake kwa njia ya mtandao wa intaneti akatuma pesa kwa wateja wake ambao pengine ingebidi awapelekee au waje pale, NBC itaendelea kuboresha na pia imo mbioni kuongeza huduma nyingine bora zaidi hususan malipo kwa njia ya mtandao ili kutengeneza fursa mbalimbali za kibiashara kwa wateja wetu”, aliongeza meneja huyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslimu na Miamala kwa wateja Wakubwa na wa Kati wa beni hiyo, Jimmy Myalize alisema mkutano huo una lengo la kuwashukuru wateja wao  kwa biashara wanayowapa na kuweza kuwaamini wakawa benki  waitumiayo  kwa ajili ya mambo yao ya kifedha.

Alisema pia katika kukutana kwao wameweza kuwafahamisha bidhaa zao mpya, benki ipo wapi na maendeleo ya benki kwa ujumla na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma za NBC na kama kuna maeneo wangependa yaboreshwe ili kuweza kuwahudumia vizuri zaidi.

“Pia tunawakutanisha wateja wetu ili kuweza kuongea biashara na  kutengeneza  fursa za kibiashara kati yao jambo litakalosaidia wateja wetu kukua kibiashara kwani mteja anapokua na sisi kama benki tunakua”

Benki ya NBC huadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja mwezi wa Oktoba kila mwaka kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa misaada mbalimbali na kutoa elimu ya kifedha na ujasiriamali kwa makundi tofauti, kutembelea wateja wao mahali walipo na kufanya mikutano na wateja hao.

Share:

Monday, October 28, 2019

Benki ya DCB yadhamini Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania

Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jaffo, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), kwa kutambua udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Godfrey Mweli.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa, Joseph Kandege (kulia), akishiakana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa baara ya kupokea cheti cha shukurani kutoka kwa Waziri wa Tamisemi, kutoka na udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akimfahamisha Angel Lomwai kuhusu faida ya akaunti maalumu ya mpango wa elimu ya ‘DCB Skonga’ iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Ofisa Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Dalila Issa (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu  akaunti maalumu ya masuala ya elimu ya DCB Skonga iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania  kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini.
Baadhi ya wahudhuriaji katika  hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini wakifuatilia matukio mbalimbali ya utoaji tuzo hizo.

BENKI ya Biashara ya DCB itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano  katika kuleta maendeleo ya elimu nchini huku ikileta bidhaa na huduma maalumu za kielimu zinazolenga kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora kwa mustakabali wa maendeleo yao binafsi na kwa taifa.

Akizungumza katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri  na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambazo DCB ilidhamini, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa  alisema DCB inatambua juhudi kubwa inayofanywa na Rais John Joseph Pombe Magufuli katika kuboresha na kuinua kiwango cha elimu nchini, juhudi zilizoanza kujionyesha mwanzo kabisa pale alipoondoa ada za shule kuanzia elimu ya msingi hadi Sekondari.

“Kwa kutambua umuhimu wa elimu Benki ya DCB hivi karibuni tulizindua akaunti maalumu iitwayo ‘DCB Skonga’ ikilenga kumsaidia mteja wetu kuweka akiba kidogo kidogo huku tukimpa uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufikia chuo kikuu.

“Kumekuwa na changamoto kubwa sana katika jamii inayotuzunguka pindi mzazi/mlezi anaetegemewa na familia anapopoteza maisha au kupatwa na ulemavu wa kudumu, kwani watoto wengi wanashindwa kuendelea na masomo hii imetengeneza hofu kwenye familia nyingi. Kutokana na changamoto hizo, DCB tulianzisha bidhaa hii maalum ya mpango wa elimu inayomuwezesha mtoto kusoma hadi kumaliza elimu ya chuo kikuu bila ya shida yoyote”, aliongeza mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo alisema akaunti hiyo inampa fursa mteja kuchagua muda wa kuweka akiba kuanzia mwaka 1 hadi 17 na endapo atapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kabla ya muda kwisha, mtegemezi hurudishiwa  kiasi cha fedha alichoweka kuanzia mwanzo wa mpango na vilevile mtoto atalipiwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba.

Kuhusu maendeleo ya benki Bwana Ndalahwa alisema DCB imeweka kipaumbele katika kusaidia jamii hususani kwenye utoaji wa elimu na mitaji midogo midogo kwa wananchi wa kipato cha chini ambapo hadi mwishoni mwa Disemba 2018 imeweza kutoa mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 160 kwa wafanyabiashara wadogo wa vikundi ikiwemo shilingi bilioni 16 zilizotolewa kwa mfuko wa wanawake na vijana wa halmashauri za Jiji la Dar es Salaam kupitia njia ya ukopeshaji wa vikundi vidogo.

“Mikopo hii yenye masharti na riba nafuu imeleta chachu katika kuendeleza jamii kwani imewasaidia wazazi kufanya biashara na kusomesha watoto wao. Benki imetoa mikopo kwa zaidi ya watanzania 38,000 ambao wananufaika na huduma hizi. DCB pia ndio benki ya kwanza kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali na kupitia mikopo hii wafanyakazi hawa wameweza kuimarisha maisha yao”, alisema.   

Pamoja na mikopo hiyo alisema DCB pia imeendelea kutoa mikopo ya nyumba za bei nafuu kwa watanzania ambao maeneo yao hayajapimwa na wanaamini kupitia mikopo hii pia wazazi wameweza kujenga nyumba zao na kusomesha watoto, yote hiyo ikiwa ni katika kuunga mkono serikali  ya awamu ya tano ya kuhakikisha watanzania wanaishi maisha bora.

“Benki ya DCB itaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa elimu katika mambo yenye kuleta maendeleo ya sekta za elimu nchini na tungependa kutoa pongezi zetu kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri katika mitihani ya taifa kwani washahili walisema ‘Mcheza kwao hutunzwa’ na leo tunawatunza”, alisema.

Share:

Friday, October 25, 2019

Benki ya NBC yasaidia ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu jijini Mbeya

Naibu waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa (wa tatu kulia) akipokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo (wa pili kushoto), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake, iliyotolewa na NBC kwa ajili ua ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu katika Jiji la Mbeya. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Mbeya jana.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais MenejimentI ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa (katikati), akizungumza wakati akipokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kutoka kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo (wa pili kushoto), wakati wa halfa ya makabidhiano msaada huo, uliotolewa na benki ya NBC kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu katika Jiji la Mbeya. Hafla hiyo ilifanyika jijini humo jana.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kutoka Benki ya NBC kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu katika Jiji la Mbeya. Hafla hiyo ilifanyika Mbeya jana. Kulia ni Meneja wa NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo na kushoto ni Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashikindi.
Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi akizugumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kutoka Benki ya NBC kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu jijini humo. Katikati ni Naibu waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa na kulia ni Meneja wa NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo.
Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa (kulia kwake), iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya afya na elimu jijini Mbeya. 
Naibu waziri Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa (katikati), Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi (kushoto kwa naibu waziri), wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya hafla hiyo jijini Mbeya jana.

Share:

Thursday, October 24, 2019

WAKANDARASI WALIOLETA "JANJAJANJA" MIRADI YA UJENZI DAR WAKAMATWA NA POLISI KWA AGIZO LA RC MAKONDA


Wakandarasi wa Kampuni za CHICCO Engineering na Nyanza Road Work leo wamekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam kwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae ameagiza kukamatwa kwa wakandarasi hao kwa kosa la Kushindwa kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Mto Ng'ombe na Barabara ya Kivule kwa wakati na kuleta usumbufu Mkubwa kwa wananchi ukiwemo wa Mafuriko, Nyumba Kubomoka, Uharibifu wa Mali, Ajali na Magari kuharibika huku wakandarasi hao wakila Maisha mitaani. 

Kwa mujibu wa RC Makonda Mkandarasi wa  Kampuni ya CHICCO amekamatwa kwa kushindwa kuanza Mradi wa ujenzi wa Mto Ng'ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ambapo licha ya Kusaini Mkataba Mkandarasi huyo hajaanza kazi kwa zaidi ya Miezi minne na hadi sasa amelipwa zaidi ya Shilingi Bilioni 4.8 huku wananchi wakiteseka na kero ya Mafuriko.

RC Makonda amesema jambo hilo ni uzembe na hujuma inayoweza kuchonganisha Wananchi na Serikali yao ambayo tayari imetoa fedha za ujenzi wa Mto huo ili kuwaondolea kero lakini Mkandarasi amekuwa akisuasua kuanza kazi.

Kwa upande wa Kampuni ya Nyanza RC Makonda ameagizwa kukamatwa kwa Mkandarasi huyo kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kivule na Daraja licha ya Kupokea fedha zaidi ya Shilingi Milioni 800 jambo linalopelekea wakazi wa Kivule kuteseka na kero ya ubovu wa Barabara na wakati mwingine kusababisha Ajali na Kuharibika kwa Vyombo vya usafiri.

Kwa Maelekezo ya RC Makonda Wakandarasi hao waliokamatwa watakuwa Wakilala Polisi Central na asubuhi watatokea polisi kwenda kufanya kazi ya Ujenzi hadi hapo atakapojiridhisha kuwa kazi inaenda vizuri huku akieleza kuwa zoezi hilo la ukamataji litakuwa endelevu kwa Wakandarasi wote wanaokwamisha miradi ya serikali.

Share:

Barclays Bank continues to invest in Tanzania’s key growth sectors as the bank transitions into Absa

Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed addresses participants during the bank’s Corporate Clients Economic Forum held in Dar es Salaam on Wednesday.
Barclays Bank Tanzania (BBT) Board Chairman, Simon Mponji (left), shakes hands with Absa Group Deputy Chief Executive Officer, Peter Matlare, as the bank’s Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed looks on,  during the Barclay’s corporate clients economic  forum held  in Dar es Salaam on Wednesday.
Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (right), chats with Barclays Kenya Head of Corporate & Investment Banking, James Agin (left), while Engen Petroleum (T) Ltd Chief Executive Officer, Paul Muhato looks on, during Barclays’s corporate clients economic forum held in Dar es Salaam on Wednesday.
Absa Group Deputy Chief Executive Officer, Peter Matlare (left), greets Chief Executive Officer of UAP Old Mutual Insurance Tanzania Limited Stephen Lokonyo,   during Barclays Bank Tanzania’s corporate clients economic forum held in Dar es Salaam on Wednesday. Looking on is BBT Corporate Banking Director, Brian Kalero.  
Barclays Bank Tanzania  Managing Director, Abdi Mohamed (left), chats with corporate executives  during the bank’s corporate clients economic forum held in Dar es Salaam on Wednesday. Engrossed in the conversation from his left is BBT Corporate Banking Director, Brian Kalero, Chief Executive Officer of Kagera Sugar Limited, Ashwin Rana and Barclays Kenya Head of Corporate & Investment Banking, James Agin 
Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left), talks to Barclays Kenya Head of Corporate & Investment Banking, James Agin (right) and Kagera Sugar  Chief Executive Officer, Ashwin Rana, during Barclays corporate clients economic forum held in Dar es Salaam on Wednesday.
Share:

Wednesday, October 23, 2019

SELCOM NA PUMA YAZINDUA BOMBA WEEKEND


Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Selcom Baguma Ambarei (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari akitoa mfano wa kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha kwa kutumia kadi hiyo, kutoka (kulia) ni mfanya kazi wa Puma, Khamis Ali, Mkurugenzi wa Puma, Dominic Dhanah, na Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj.
Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha kwa kutumia kadi hiyo (kulia), ni Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Dominic Dhanah.
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma, Dominic Dhanah (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kulipia mafuta kwa kutunia Mastercard kwa wamiliki magari wanaotumia vituo vya mafuta ya Puma kwa ushirikiano Makampuni hayo ambapo mteja atarudishiwa asilimia 5 ya fedha kwa kutumia kadi hiyo kulia kwa Dominic ni Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Sameer Hirj.

PUMA ENERGY, SELCOM NA MASTERCARD WAUNGANA KUHAMASISHA MALIPO YA KIELEKTRONIKI.

Dar es salaam, Tanzania; Puma Energy, Selcom Paytech LTD na Mastercard kwa wamezindua kampeni ya pamoja iitwayo #BombaWeekend ambayo inaangalia kurejeshea wateja hadi 5% ya pesa watakayotumia watakapojaza mafuta katika vituo vya Puma Energy endapo watalipia kupitia Mastercard QR.

Kampeni hiyo itaendeshwa kwa wiki 11, kila Ijumaa hadi Jumapili kuanzia saa 10 hadi 12 jioni kupitia mtandao wa Puma wenye vituo 52 nchi nzima. Pamoja na dhumuni la kuzawadia watumiaji wa huduma hiyo, Bomba Weekends ina dhamira ya kuchangia katika juhudi za serikali za kurasimisha malipo na kuhamasisha uchumi wa malipo ya kieletroniki ili kufikia malengo ujumuishaji wa kifedha wa nchini Tanzania.

Mchakato mzima wa kurudishia pesa wakati wa Bomba Weekends unaendeshwa kupitia huduma ya zawadi kwa wateja ya Qwikrewards iliyoundwa na Selcom Paytech LTD mahususi kwa watumiaji wa Mastercard QR. Qwikrewards inamuwezesha mtu yeyote kukusanya pointi au kupata pesa taslim kupitia akaunti iliyounganishwa na namba yake ya simu kila afanyapo malipo kutumia Mastercard QR. Watumiaji Qwikrewards wanaweza kukomboa pointi walizokusanya kwa kupiga *150*15* na kuzitumia katika maeneo zaidi ya 30,000 nchini ambapo Mastercard QR inakubalika kama njia ya malipo. Aidha Mastercard QR imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake nchini mwaka 2018 hadi sasa kupelekea kukubalika na watoa huduma mbali mbali zaidi ya 30,000 kuwa na uwezo wa kupokea malipo kutoka mitandao yote 7 ya simu na benki 15 nchini.

Akiongea na wanahabari katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Nd. Dominic Dhanah alisema, "Bomba Weekends inahamasisha wateja we kulipia  mafuta katika vituo yetu kutumia njia rahisi, haraka na salama zaidi na kunufaika papo hapo kupitia Qwikrewards kutoka Puma. Ushirikiano huu unadhahiri kwamba Puma ni kiongozi wa katika sekta ya mafuta inapofikia kujiunga na suluhisho bunifu za malipo ambazo hurahisisha malipo kwa wateja wetu na kutuwezesha kutoa huduma bora zaidi katika vitu vyetu."

Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Paytech LTD, Nd. Sameer Hirji, alionyesha matumaini makubwa kuelekea uchumi wa malipo ya kielektroniki akisisitiza kuwa ni lazima taasisi ambazo zinaongoza mchakato huo kuongeza thamani kwa wateja ili kuwapa hamasa zaidi kutumia malipo ya elektroniki."Kupitia Bomba Weekends tukishirikaina Puma Energy pamoja na Mastercard QR tumedhamiria kuwazawadia wateja watakaolipa kielektroniki katika matumizi yao ya kila siku, mafuta yakiwa sehemu kubwa ya matumizi hayo. Tunaamini kwamba tunavyozidi kurahisisha na kuimarisha upatikanaji na upokeaji wa malipo ya kieletroniki ndivyo tutazidi kuwajengea Watanzania imani ya kutoka nyumbani bila pesa taslim. Tukiwa na Qwikreward na maeneo zaidi ya 30,000 ambapo Mastercard QR inakubali kitaifa tunaamini tunaongoza mabadiliko kuelekea malipo ya kielektroniki na malengo ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Biashara wa Mastercard Ukanda wa Afrika Mashariki, Nd. Adam Jones alisema,”Mastercard itaendelea kutoa huduma shirikishi za malipo ambazo zitasaidia kusukuma jamii kuelekea malipo ya kieletroniki. Njia sahihi ya kufikia malengo haya ni kuendelea kuvumbua mifumo thabiti ya kidijitali kwa kushirikiana na mashirika kama Selcom na  Puma Energy. Tuna uhakika kampeni hii itawahakikishia wateja malipo rahisi, salama na ya uhakika katika kila kituo cha Puma, lakini pia kuchangia juhudi ya nchi kuelekea malipo ya kidijitali.”
Share:

Tuesday, October 22, 2019

BENKI YA KCB TANZANIA YAWANOA VIJANA

Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , vijana na ajira, Anthony Mavunde (wapili kushoto), akimkabidhi ruzuku ya gari aina ya kirikuu kwa Janeth Kipangula, mfanya biashara wa vifaa vya ujenzi wakati wa ambaye ni mmoja wa wanawake 256 ambao walipokea mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kupitia programu ya 2jiajiri. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa KCB Foundation, Bi. Jane Mwangi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario(kulia) hafla hiyo imefanyika hivi karibini Dar es Salaam
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , vijana na ajira, Anthony Mavunde (kushoto), akimkabidhi ruzuku ya komputa na vifaa vingine nya ofisini kwa Bi. Halima Haji Sasya, ambaye ni mmoja wa wanawake 256 ambao walipokea mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kupitia programu ya 2jiajiri. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa KCB Foundation, Bi. Jane Mwangi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario(wa pili kushito).
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , vijana na ajira, Anthony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya KCB 2jiajiri Youth Scholarship kwa wanafunzi wa Veta yaliyodhaminiwa na Benki ya Biashara ya KCB hafla ya uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya KCB, Cosmas Kimario, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya KCB 2jiajiri Youth Scholarship kwa vijana inayoendeshwa na VETA na kudhaminiwa na Benki ya KCB katika hafla ya uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.Share:

Benki ya DCB yashinda tuzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kushoto), akikabidhi tuzo ya  mshindi wa tatu katika kitengo cha makampuni bora ya mwaka katika eneo la uwekezaji katika sekta za  kibenki  kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wa Benki ya Biashara ya DCB, Regina Mduma wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanachama wa DSE jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  Wengine pichani kutoka kushoto ni;  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es salaam, Moremi Marwa,  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama na Ofisa katika kitengo cha Sheria wa DCB, Grace Ringo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akishikana mikono  Mkurugenzi wa Kitengo Cha Sheria was Benki ya DCB, Regina Mduma, baada ya kumkabidhi iliyoshinda benki hiyo ya  mshindi wa tatu katika kitengo cha makampuni bora ya mwaka katika eneo la uwekezaji katika sekta za  kibenki  wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wanachama wa DSE jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Ofisa katika kitengo cha Sheria wa DCB, Grace Ringo.
Mkurugenzi katika Kitengo cha Sheria wa Benki ya DCB, Regina Mduma (kulia), na Ofisa wa Kitengo hicho Grace Ringo wakionesha tuzo hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha
Share:

Friday, October 18, 2019

BENKI YA KCB YASAFIRISHA WAFANYABIASHARA KWENDA CHINA.

Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja
wa wafanya biashara wa vipodozi Irene Moshi, wakati wa kuwakabidhi tiketi
wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa
bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda
kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es
Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya
Biashara ya KCB, Christine Manyenye .
 Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja
wa wafanya biashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba,
wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi
china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na
walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo
makao makuu ya KCB Dar es Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye .
Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB,
Christine Manyenye (kulia) akizungumza wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa
benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa
mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda
kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam
Wengine pichani (watatu kushoto), Mkuu wa Kitengo cha wateja wadago na kati
Abdul Juma, Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule pamoja na
Mfanya biashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba.

 Benki ya KCB Tanzania Taarifa kwa Umma Tarehe 15.10.2019 Benki ya KCB Tanzania kupitia KCB Biashara Club yapeleka wafanyabiashara 10 kwenda nchini China kwa lengo la kukutana na wazalishaji halisi wa bidhaa mbalimbali ili kujifunza na kutafuta namna bora ya kuweza kuboresha biashara zao. 

Wafanyabiashara hao watakaa nchini China kwa siku 10 na kupata fursa ya kutembelea miji miwili mikubwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Mahusiano na Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye alisema wameanza kuwapeleka China wafanyabiashara hao ambao ni wateja wa benki hiyo ili wakakutane na wazalishaji halisi na si walanguzi au madalali ambao uwauzia bidhaa kwa bei ya juu. Alisema kwa muda mrefu wafanyabiashara nchini ambao wanakwenda China wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo za lugha na kuuziwa vitu bei za juu hivyo kupitia safari hizo wanazoziandaa mambo hayo hayatajitokeza. 

“Tatizo kubwa ambalo wafanyabiashara walikuwa wanakutana nalo ni kuuziwa vitu kwa bei ya juu na walanguzi au madalali sasa kupitia safari hii tutawakutanisha na wale wazalishaji halisi ambao wanaviwanda ambapo watapata fursa ya kutembelea viwanda vyao kisha kutoa oda za kutengenezewa bidhaa zao. Lakini pia kuna tatizo la lugha kule, kupitia safari hii tuliyoiratibu sisi KCB Benki tutawapatia wakalimani ambao watatembea nao kila mahali ili kurahisisha mawasiliano yao na wazalishaji hao,” alisema.

Naye Meneja Uhusiano wa Wateja Wadogo na wa Kati wa benki hiyo, Moses Kisaka alisema wanamatumaini kwamba siku hizo 10 wafanyabiashara hao wataweza kuzunguka na kukutana na wazalishaji pamoja na kutumia fursa hizo kufanya manunuzi ya bidhaa zao. Alisema wafanyabishara hao watakutana na wazalishaji halisi watakaowauzia vitu kwa bei ya chini kuliko ilivyokuwa awali walipokuwa wakienda wenyewe na kukutana na walanguzi waliokuwa wanawauzia vitu kwa bei ya juu. “Tunafanya hivi kwa lengo la kuwasaidia wapunguze gharama za kupata bidhaa, tunaamini safari hizi zitakuwa ni muendelezo na tunatumaini mwakani kuwapeleka wafanyabiashara wengi zaidi,” alisema.

 Aidha alisema benki hiyo imeanzisha kitengo cha KCB Biashara Club kwa lengo la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara mbalimbali na kuzungumza juu ya changamoto na fursa za kibiashara wanazokutana nazo. Kwa upande wake Mwakilishi wa wafanyabiashara wanaoenda China, Saada Sipemba alisema safari hiyo itawasaidia kupata fursa ya kuona maonyesho makubwa yanayofanywa na wenye viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo vyombo vya ndani pamoja na mashine. “Pia itatuwezesha kwenda kujifunza na kukutana na wazalishaji wenyewe bila kupitia kwa madalali wowote hivyo itatusaidia kununua bidhaa kwa bei nafuu na kuja kuziuza nchini kwa bei nafuu pia,” alisema Sipemba.
Share:

Wednesday, October 16, 2019

RC MAKONDA AMTAKA MKANDARASI WA KAMPUNI YA MISTECO KUKABIDHI JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITAL YA MWANANYAMALA KABLA YA DISEMBA 30Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 16 ametembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Gorofa tano la Mama na Mtoto Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala na kumtaka Mkandarasi wa jengo hilo Kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo hilo kabla ya Disemba 30 mwaka huu.


RC Makonda amesema ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona hilo changamoto hiyo na kuamua kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.

Aidha RC Makonda amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari.


Pamoja na hayo RC Makonda amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.
Share:

Benki ya NBC yatoaelimu ya bima ikiadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja

Ofisa wa Bima wa Benki ya NBC, Catherine Ngowi (kulia) akitoa elimu ya masuala ya bima n aina mbalimbali ya huduma za  bima zitolewazo na  NBC kwa ammoja wa wateja wa benki hiyo,  Miryam Mjema ikiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Bima wa benki hiyo, Benjamin Nkaka na ofisa mwingine wa NBC,  Batuli Kassim.

Ofisa wa Bima wa benki ya NBC, Emarynziana Mtega (kulia), akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kujiwekea bima na aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na NBC kwa mmoja wa wateja  wa benki hiyo kutoka Kampuni ya Mogas Tanzania Ltd, Grayson Kazeni kiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa benki hiyo mjini Dar es Salaam hivi karibuni.

Maofisa wa benki ya NBC, wakizungumza na wateja wakati wakitoa elimu kuhusu masuala ya bima kwa wateja ikiwa ni moja ya matukio ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo. Wafanyakazi hao walitoa elimu ya bima ikiwa ni pamoja na bidhaa mbalimbali za bima zitolewazo na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC.

NA Mwandishi wetu;

BENKI ya NBC imeendelea kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja kwa kufanya matukio sehemu mbalimbali nchini na hapo jijini Dar es Salaam ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa bima na pia ikiwaleleza wateja aina mbalimbali ya huduma za bima zitolewazo na benki hiyo.

Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema watanzania wanapaswa kuwa utamaduni wa kujiwekea bima wao pamoja na watoto wao dhidi ya matukio na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza wakati wowote.

Akitoa mfano wa bima hizo ni bima ya elimu ya Educare itolewayo na inayomuwezesha mzazi kuweka akiba kidogokidogo kwa ajili ya elimu ya mtoto wake pindi yatokeapo majanga yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.

“Tumekwishakuwa na huduma hii, tunachotaka sasa ni kwa wateja kuweza kuielewa vivuri, na ndio maana tumendaa hafla kama hii ili kuwafahamisha wateja wetu na wananchi kwa ujumla huduma ya bima ya elimu ya NBC inavyoweza kumkomboa mteja,” alisema.

Alisema kwa kupitia huduma hii mteja humwekea akiba mtoto wake kidogokidogo kwa kiasi atakachopanga kwa mkataba wa muda kuanzia miaka saba hadi 18 ili kugharamia elimu ya mtoto wake.

“Bima hii ya elimu ni mpango ambao mzazi huweka akiba kila mwezi hivyo kuleta faraja moyoni kwamba endapo chochote kitatokea iwe ulemavu wa kudumu ama kifo kabla ya muda huo basi bima itagharamia elimu ya mtoto wako.


“Kiwango cha chini ni miaka saba hadi 18 na kiwango cha chini cha kuwekeza katika mpango huu kwa mwezi  ni shs 7,500/- hakuna kiwango cha mwisho cha juu. Uwekezeji katika elimu ya mtoto ni jambo pekee katika kuhakikisha malengo ya kielimu ya mtoto yanatimia ,” aliongeza Bwana Nkaka.

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive