Meneja Huduma Bora wa
NBC, Jane Dogani akiwawekea chakula baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo
wakati wa hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio
ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki ya NBC, Benjamin Nkaka akizungumza na watoto wa wateja wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi kuhusu umuhimu wa wazazi kuwafungulioa watoto wao akaunti ya Chanua na pia bima ya elimu ya educare ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao wakati wawapo hai ama wasipokuwepo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Malipo ya Ndani
wa NBC, Suzyo Gwebe Nyirenda akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja
wa benki hiyo katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu
ya matukio ya benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma Bora wa
NBC, Jane Dogani akikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wa wateja wa benki hiyo
katika hafla ambayo NBC iliwaandalia watoto hao ikiwa ni sehemu ya matukio ya
benki hiyo kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja. Hafla hiyo ilifanyika jijini
Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watoto
waliohudhuria katika hafla hiyo wakichorwa picha ikiwa ni sehemu ya shamra
shamra zilizokuwepo katika kuadhimisha moja ya matukio ya mwezi wa huduma kwa
wateja ambapo NBC iliandaa sherehe hiyo kwa watoto wa wateja wao.
Baadhi ya watoto
walihudhuria hafla hiyo wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwepo katika
siku hiyo ikiwa ni moja ya matukio ya NBC kuadhimisha mwezi wa huduma kwa
wateja.
Na Mwandishi wetu,
Na Mwandishi wetu,
BENKI
ya Taifa ya Biashara (NBC), imetoa wito kwa wazazi kote nchini kufungua akaunti
maalumu ya watoto ya Chanua pamoja na bima ya elimu ya Educare za benki hiyo
ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao pindi wawapo hai ama wasipokuwepo.
Wito
huo umetolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Wateja
Binafsi wa benki hiyo, Benjamin Nkaka katika hafla waliyoiandaa kwa ajili
ya watoto wa wateja wao ikiwa ni sehemu ya matukio ya kuadhimisha Mwezi wa
huduma kwa wateja wa NBC.
Mkurugenzi
huyo alisema akaunti ya watoto ya Chanua ya NBC pamoja na bima ya elimu ya
educare vitamuwezesha mzazi kuanza kuwekeza kidogodogo kwa ajili ya mtoto wake
hivyo kuondoa hofu ya watoto kupata elimu bora pindi mzazi
anapoondoka duniani.
“Akaunti
ya Chanua na bima ya Educare za NBC ni suluhisho la uhakika kwa elimu ya
watoto, wakati mzazi awapo duniani,asipokuwepo au atakapotapa ulemavu wa
kudumu, nawashauri wazazi kuwafungulia watoto wenu akaunti hii na kuanza
kuwekeza pamoja na bima ya educare zote kutoka NBC,” alisema.
Kuhusu
hafla hiyo Bwana Nkaka alisema NBC imekuwa na desturi ya kukutana na wateja wao
mara kwa mara ikiwa ni moja ya azma yao ya kusogeza huduma zao karibu na wateja
wao hivyo licha ya kuwaeleza watoto walioambata na wazazi wao bidhaa
mbalimbali zinazotolewa na benki hususan zinazowalenga watoto, lakini pia
watoto walishiriki burudani za aina mbalimbali jambo ambalo ni muhimu katika
malezi ya watoto.
“NBC
imekuwa ikibadilika siku hadi siku tukitumia njia mbalimbali katika kuwafikia
wateja wetu, licha ya kuwa na mtandao mpana wa matawi lakini pia tumeanzisha
NBC Kiganjani inayomuwezesha mteja kupata huduma mbalimbali za kibenki kwa
kupitia simu yake ya mkononi.
“Lakini
hii haitoshi NBC inao mtandao mkubwa wa mawakala wake wakitoa huduma mbalimbali
za kibenki nchini kote, lakini hivi karibuni tumeingia ushirika na Shirika la
Posta ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma zetu za kibenki katika ofisi
zote za shirika hilo mahali kote nchini,” aliongeza mkurugenzi hiuyo.
0 comments:
Post a Comment