A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Tuesday, October 8, 2019

Wafanyakazi wa benki ya NBC watoa elimu ya kifedha na stadi za maisha kwa wanafunzi jijini Dar

Meneja Mahusiano Msaidizi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa kuhusu elimu ya fedha, ujasiriamali na stadi za maisha wakati yeye na wafanyakazi wenzake walipotembelea shule hiyo na kutoa elimu ikiwa ni sehemu ya majukumu ya kujitolea katika kuisaidia jamii. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Dar es Salaam, hivi karibuni.
Meneja Mahusiano  wa Benki ya  NBC, Toivo Mapunda (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa kuhusu elimu ya fedha, ujasiriamali na stadi za maisha wakati yeye na wafanyakazi wenzake walipotembelea shuleni hapo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Mmoja wa maofisa wa benki ya NBC, Isaya Komba (kulia), akitoa elimu ya masuala ya kifedha, ujasiriamali na stadi za maisha kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa  ikiwa ni sehemu ya majukumu ya kujitolea katika kuisaidia jamii yanayofanywa na wafanyakazi wa NBC sehemu mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo cha Makampuni wa Benki ya NBC, Elibariki Ndossi (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa kuhusu elimu ya kifedha, ujasiriamali na stadi za maisha wakati yeye na wafanyakazi wenzake walipotembelea shule hiyo na kutoa elimu ikiwa ni sehemu ya majukumu ya kujitolea katika kuisaidia jamii. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo, Dar es Salaam, hivi karibuni.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa akiuliza swali katika hafla hiyo.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa wakiwa katika mkutano huo ambapo wafanyakazi wa benki ya NBC walikwenda shuleni hapo na kutoa elimu ya masuala ya kifedha na ujasiriamali ikiwa ni sehemu ya majukumu yao katika kusaidia jamii.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive