A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Showing posts with label ENTERTAINMENT. Show all posts
Showing posts with label ENTERTAINMENT. Show all posts

Sunday, September 10, 2023

Tamasha la Airtel Wasafi Festival 2023 lawapagaisha wakazi wa Ruangwa

Rais wa WCB na Balozi wa Airtel Diamond Platnumz akifanya vitu vyake katika Tamasha la Airtel Wasafi Festival mjini Ruangwa, mkoani Lindi jana. Ili kunogesha tamasha aliingia kwa staili ya aina yake akivaa vazi la kizombi.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Lavalava akikonga nyoyo za maelfu ya wakazi wa Ruangwa na sehemu jirani wakati wa Tamasha la Airtel Wasafi Festival 2023 mjini Ruangwa, Lindi jana.
Msanii wa Bongo fleva, Rayvanny (kushoto), akiimba wakati wa Tamasha la Airtel Wasafi Festival mjini Ruangwa jana. Rayvanny aliingia na staili ya nyumba na familia ya kiafrika akiwa na mifugo mbalimbali.
Baadhi ya maelfu ya wakazi wa mjini wa Ruangwa na maeneo ya jirani wakishuhudia Tamasha la Airtel Wasafi Festival 2023 lililofanyika wilayani Ruangwa, mkoani Lindi jana.
Licha ya burudani ya nguvu kutoka katika steji ya Airtel Wasafi Festival 2023, wahudhuriaji hupata fursa ya kupata huduma mbalimbali kutoka Airtel kama kufanya miamala ya Airtel Money, kusajili laini kama inavyoonekana pichani.

LIKIWA katika onyesho lake la pili, baada ya Mtwara, Tamasha la Airtel Wasafi Festival linalodhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel limeendelea kuonesha kuwa ni moto wa kuotea mbali baada ya safari hii kuutikisa mji wa Ruangwa pamoja na viunga vyake baada ya kushuhudia wasanii wakali zaidi 21 wakilishambulia jukwaa kila mmoja kwa staili ya aina yake.

Wasanii hao wengi wao wakiwa ni kutoka crew ya Wasafi Classic Baby (WCB) walilishambulia jukwaa bila kuchoka wakiongozwa na Rais wa WCB na Balozi wa Airtel Diamond Platnumz ambaye yeye alivunja rekodi kwa kuingia na staili ‘Kizombi’ hivyo kufanya maelfu ya wakazi wa Ruangwa kushangilia kwa nguvu muda wote wakati mkali huyo akishusha ngoma zake zinazobamba katika chati kwa sasa na kupiga shoo ya nguvu akianza kwa kuchagiza akitaja jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye yeye ni mwenyeji wa Ruangwa na hivyo kuamsha kelele za shangwe kutoka kwa mashabiki wake.

Na kama hiyo haitoshi, mkali mwingine, Rayvvany huyu naye awali akitokea WCB, lakini sasa akimiliki lebo yake iitwayo ‘Next Level Music’ yeye aliamua kuibadilisha steji kuwa kama yupo kijijini baada ya kuweka jengo la nyumba yenye asili ya kiafrika huku akiwa na mifugo kadhaa, ikiwemo sungura na mbuzi lakini hayo yote ikiwa ni kutia chachandu Tamasha la Airtel Wasafi Festival ambalo mwaka huu limekuja kivingine.

Akizungumza, Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema, kama ilivyoahidiwa siku ya uzinduzi wa tamasha hili, ndicho kinachofanyika kwani Tamasha la Wasafi Festval 2023 chini ya udhamini wa Airtel halifanyiki kwa mtindo wa kimazoea.

Airtel Wasafi Festival 2023 ni moto wa kuotea mbali, sisi kama Airtel Tanzania tunataka watanzania wapate burudani ya uhakika hususani katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Lakini sio burudani tu kutoka crew nzima ya WCB na wasanii wengine bali kila panapofanyika matamasha haya, Airtel tumeendelea kutoa huduma za mtandao wetu bora ikiwa ni pamoja na kufungua maduka ya Airtel Money ili kuweza kusogeza huduma zetu karibu zaidi kwa wateja wetu na kwa watanzania kwa ujumla.

Airtel tunahamasisha watanzania wote wasikose fursa hii ya kuhudhuria kwa wingi katika matamasha haya yanayoendelea kwani Airtel Wasafi Festival 2023 ni zaidi ya burudani,” alisema Bwana Mmbando.

Mara baada ya onesho la Ruangwa tamasha litakalofuata la Airtel Wasafi Festival linatarajiwa kufanyika katika mji wa Songea mkoani Ruvuma, ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi wa Airtel, Diamond Platnumz atafungua Airtel Money Branch, kuhudumia wateja na kufanya shughuli nyingine za kijamii mkoani humo.

Mbali ya Rais huyo wa WCB, baadhi ya wasanii wengine wanafanya makamuzi katika Tamasha la Wasafi Festival la mwaka huu ni, Jux, Rayvan, Mbosso, Mr Blue, Darasa, Young Lunya, Lavalava, Zuchu, Chid Benz, Billnas, Mabantu, Linex, J Melody, Kusah, Weusi, Chege & Temba na wengine wengi.
Share:

Tuesday, October 24, 2017

Sherehe za Siku ya Wanafamilia wa Tanga Cement zafana


Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), wakiwavuta wenzao  ili kumpata mshindi  katika mchezo wa kuvuta kamba katika sherehe za Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo katika Uwanja wa Mkwawani mjini Tanga hivi karibuni.


Mtifuano wa kutafuta mshindi katika mchezo wa kuvuta kamba ukiendelea.


Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga wakishangilia baada ya kukabidhiwa keki maalumu ya kusherehekea siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.


Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Diana Malambugi (kushoto), akishikana mikono na mmoja wa wanafamilia wa Tanga Cement.


Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Diana Malambugi (kushoto), akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wafanyakazi na familia zao waliohudhuria sherehe hizo.


Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Mtanga Noor (kushoto), akizungumza na wafanyakazi na wanafamilia wa kampuni hiyo katika sherehe za Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo katika Uwanja wa Mkwawani mjini Tanga.


Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Diana Malambugi (kushoto), akizungumza na wafanyakazi na wanafamilia wa kampuni hiyo katika sherehe za Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo katika Uwanja wa Mkwawani mjini Tanga
Share:

Monday, August 21, 2017

Tigo, Clouds Wazindua Msimu wa ‘Tigo Fiesta 2017 – Tumekusoma’

Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.

Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta, Sebastian Maganga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.

Mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Wengine toka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga na Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga.


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tigo Fiesta 2017, Sebastian Maganga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 'Tumekusomaa' leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Meneja wa Masoko Tigo, William Mpinga na mwakilishi toka Basata, Mrisho Mrisho.
Share:

Thursday, July 27, 2017

Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni kuliamsha Dude Bonn, Ujerumani Siku ya Ijumaa 28 Julai 2017 Saa 2.00 Usiku


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU -Ughaibuni au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" yenye makao yake nchini Ujerumani inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho la wazi la Orient-Afrika litakalo fanyika mjini Bonn,Ujrumani siku ya Ijumaa 28.Julai 2017 saa 2.00 Usiku (20.00 hrs).

Bendi hiyo inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja inadumu katika medani ya muziki kwa miaka 24 na kufanikiwa kuteka mashabiki wa kimataifa, pamoja na kuachia nyimbo na CD kadha.


Bendi hiyo imejizolea umaarufu katika majukwaa ya kimataifa kwa mdundo wa  Extraordinary "Bongo Dansi"  unaowatia kiwewe mashabiki barani ulaya.



Usikose kujumuika nao kupitia:

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Labels

Blog Archive