A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, July 27, 2017

Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni kuliamsha Dude Bonn, Ujerumani Siku ya Ijumaa 28 Julai 2017 Saa 2.00 Usiku


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU -Ughaibuni au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" yenye makao yake nchini Ujerumani inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho la wazi la Orient-Afrika litakalo fanyika mjini Bonn,Ujrumani siku ya Ijumaa 28.Julai 2017 saa 2.00 Usiku (20.00 hrs).

Bendi hiyo inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja inadumu katika medani ya muziki kwa miaka 24 na kufanikiwa kuteka mashabiki wa kimataifa, pamoja na kuachia nyimbo na CD kadha.


Bendi hiyo imejizolea umaarufu katika majukwaa ya kimataifa kwa mdundo wa  Extraordinary "Bongo Dansi"  unaowatia kiwewe mashabiki barani ulaya.Usikose kujumuika nao kupitia:

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive