Meneja
Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza wakati wa
uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mjini Kahama, Shinyanga jana.
Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa
kati. Katikati ni mmoja wa wateja, Salum Selemani na Joshua John (kulia), Ofisa
Masoko wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kutoka ofisi
ya Mwanza.
Meneja
Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza na baadhi ya
wafanyabiashara wa mjini Kahama, katika semina iliyoandaliwa kabla ya
uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC hiyo iliyoanzishwa kusaidia
mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Hafla ya uzinduzi
ilifanyika mjiini Kahama, Shinyanga jana.
Meneja
wa Kanda wa NBC, Daudi Mfalla (kulia), akizungumza wakati akizungumza katika
hafla ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC iliyoanzishwa
kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kushoto ni Mkuu
wa Kitengo cha Wafanyabiashara wadogo na wakati wa NBC, Evance Luhimbo.
Baadhi
ya wateja wa NBC mjini Kahama waliohudhuria uzinduzi wa B-Club ya benki hiyo,
wakijipiga picha ‘selfie’ pamoja na bango lenye picha inayoonyesha kilele cha
Mlima Kilimanjaro ikiwa ni baadhi ya shamrashara zilizopamba uzinduzi huo.
Wafanyakazi
wa NBC tawi la Kahama wakipozi kwa katika hafla hiyo.
Wasanii
wakionyesha umahiri wao kucheza ngoma ya kadete ya kabila la wasukuma katika
hafla ya uzinduzi wa B-Club mjini Kahama, Shinyanga jana.
0 comments:
Post a Comment