Monday, August 31, 2020
Absa Bank TZ Pugu Branch launch in pictures
Thursday, August 27, 2020
Benki ya DCB yamtembelea Mama Mkapa na kumpa mkono wa pole
Wednesday, August 26, 2020
DAWASA WAZIDI KUSOGEZA HUDUMA YA MAJI KWENYE MAENEO YALIYOKUWA NA CHANGAMOTO UKOSEFU WA MAJI SAFI
NMB Yawakomboa Wananchi Mlimba
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero - Ismail Mlawa (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Mlimba Wilayani Kilombelo Mkoani Morogoro wakati wa hafla ya ufunguzi iliyofanyika jana. Kutoka kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Baraka, Ladislaus, Meneja wa tawi la NMB Mlimba - Omary Mtibiro, Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara - Salie Mlay, Meneja wa Kanda ya Mashariki - Dismas Prosper na Afisa Tarafa ya Mlimba - Emiliana Simanga.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, kwa niaba ya Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Salie Mlay alisema ujenzi wa tawi hilo Mlimba ni utekelezaji wa sera ya Benki hiyo ya kuwasogezea wanachi huduma za kibenki.
Mlay alisema kuwa, NMB imeendelea kuimarisha huduma mbalimbali na mpaka sasa wameshafungua jumla ya matawi 12 Mkoani Morogoro - lengo likiwa kuhakikisha jamii inapata huduma za kibenki zilizo bora na kwa ukaribu zaidi
Akizindua tawi hilo la NMB Mlimba, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero - Ismail Mlawa alisema, ujenzi huo ni sehemu ya ushahidi wa Serikali kumletea mwanachi maendeleo ili aweze kuondokana na changamoto zinazomzunguka na kuwataka wafanyabiashara kuitumia Benki hiyo kwaajili ya kufanya maendeleo.
Kwa niaba ya wafanyabiashara - Joyce Chaula ameishukuru Benki ya NMB kwa kuwasogezea huduma, kwani wanaamini watanufaika ikiwemo fedha zao kuwa salama na hata wao wenyewe kuweza kupata mikopo ili kukuza biashara.
Katika uzinduzi huo NMB imetoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni tano ikiwa ni mabati kwaajili ya uwezekaji wa shule ya Sekondari ya Kalengakelu iliyopo Tarafa ya Mlimba hii ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.
Tuesday, August 25, 2020
ZANTEL ORGANISES A GOLF TOURNAMENT AT LUGALO GOLF GROUNDS
Monday, August 24, 2020
Absa Earnings Decline as Economic Impact of COVID-19 Increases Impairment Charges
- Revenue increased 3% to R40.1 billion
- Operating costs fell 2% to R21.6 billion
- Cost-to-income ratio improved to 53.9% from 56.7%
- Pre-provision profit increased 9% to R18.5 billion
- Impairments increased four-fold to R14.7 billion
- Headline earnings declined 82% to R1.46 billion
- Return on equity declined to 2.6% from 16.4%
- Group CET 1 ratio of 11%, well above regulatory requirements
- Zero dividend declared
- Home loans registrations were down 31% while the market contracted by 39%
- Vehicle and asset financing decreased 19% in a market that shrunk by 42%
- Retail deposits grew 12%, in line with the market
- Solid net insurance premium growth of 9%
- Gross loans and advances grew by 7% to R530 billion
- Deposits grew by 10% to R373 billion
- Non-interest income grew by 6%
- Cost-to-income ratio improved to 57.7% from 58.4% in 2018
- Customer growth of 1% to 9.7 million
- Market share growth in retail deposits and retail loans and advances, including personal loans, new home loans and vehicle finance.
- Continued growth momentum in ARO with total income growing 15% (12% in constant currency) to R7.4 billion
- Solid income growth from Corporate Bank franchise up 9% (8% in constant currency) to R10.6 billion
- Strong growth momentum in the trade finance business in SA, with a CAGR of 19% in the last four years.
- Revenue grew by 14% (11% in constant currency)
- Pre-provision profits increased by 17% (14% in constant currency)
- Cost-to-income ratio improved to 57.8%
- While separating, ARO has grown its retail primary customer base in 2019 to 1.5 million customers.
Tuesday, August 18, 2020
RC KUNENGE AMTAKA MKANDARASI WA KAMPUNI YA NYANZA KUKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA KIVULE KABLA YA SEPTEMBER 30
ABSA TANZANIA LAUNCHES A NEW BRANCH IN DODOMA
Friday, August 14, 2020
ABSA TANZANIA KUENDELEA KUWA MSTARI WA MBELE KUSAIDIA JAMII
Thursday, August 13, 2020
NBC yasaidia ujenzi wa madarasa shule ya Kizimkazi mjini Unguja
Tuesday, August 11, 2020
Absa wins the Euromoney 2020 Excellence in Leadership in Africa award
WAZIRI KALEMANI AWAONYA WANAOAGIZA VIFAA VYA KUUNGANISHIA UMEME KUTOKA NJE
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani (kushoto), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa kiwanda cha Inhemeter kinachojishughulisha na kutengeneza vifaa vya kuunganishia mifumo ya umeme kutoka katika miundombinu mikubwa na kupeleka majumbani hafla hiyo imefanyika jana kiwandani hapo kinondoni Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akizungumza na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Inhemeter wakati akizindua kiwanda cha Inhemeter kinachojishughulisha na kutengeneza vifaa vya kuunganishia mifumo ya umeme kutoka katika miundombinu mikubwa na kupeleka majumbani yaani kwa wananchi hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mh Daniel Chongolo. Hafla hiyo imefanyika jana jjini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Inhemeter , Abraham Rajakili akizungumza wakati wa hafla hiyo
WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani amesema kuwa Serikali haitaruhusu tena uingizwaji wa vifaa mbalimbali vya kuunganishia umeme kutoka nje ya nchi kwa sababu tayari hapa nchini kuna viwanda vya kutosha vya kuzalisha vifaa hivyo.
Pia Dk. Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Wakala wa Umeme Vijiji (REA) na wakandarasi wanaochukua tenda za kusambaza umeme vijijini kuacha kuagiza vifaa nje ya nchi badala yake kuchukua vya ndani ili kuweza kupunguza gharama na kuokoa muda wa kupeleka umeme kwa wananchi.
Dk. Kalemani ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua kiwanda cha Inhemeter kinachojishughulisha na kutengeneza vifaa vya kuunganishia mifumo ya umeme kutoka katika miundombinu mikubwa na kupeleka majumbani yaani kwa wananchi.
Amesema hakuna kifaa chochote cha kuunganisha umeme kitakachotoka nje ya nchi kwa sasa na kuongeza kuwa manunuzi yote ya vifaa mbalimbali vya umeme ikiwamo nguzo na trasnfoma vinunuliwe hapa nchini.
"Umeme ni muhimu sana katika maendeleo na uchumi wa viwanda na kamwe uwezi kusema unataka kujenga uchumi wa viwanda alafu unategemea vifaa kutoka nje ya nchi hivyo Serikali itaendelea kusisitiza watu kununua vifaa vinavyotengenezwa hapa nchini na ujengwaji wa viwanda vya ndani," amesema
Aidha amesema hadi kufikia leo Julai 10, 2020 jumla ya vijiji 9512 vimeshasambaziwa umeme huku vijiji 2700 vilivyobakiwa vikiratajia kuanza kuwekewa umeme Agosti mwaka huu.
Dk. Kalemani amesema kuanzia Agosti 20 hadi Septemba 20 mwaka huu, Serikali itaanza kusambaza wakandarasi watakaofanya kazi ya kuvipelekea umeme vijiji na vitongoji vyote vilivyosalia kupata umeme hapa nchini.
Amesema takribani kiasi cha Sh. Bilioni 851 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo na kuongeza kuwa anakipongeza kiwanda cha Inhemeter kwa uzalishaji wa viunganishi zaidi ya 600,000 vya umeme kutoka miundombinu mikubwa kwenda kwa wananchi huku mahitaji ya nani ya vifaa hivyo yakiwa 300,000.
"Pamoja na kwamba mtazalisha vifaa vingi hakikisheni mnazingatia viwango na ubora unaokubalika ili viweze kuuzika hapa nchini na nje ya nchi," amesema Dk Kalemani.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda hicho, Abraham Rajakili amesema uwekezaji katika kiwanda hicho unathamani ya Shilingi Bilioni tano na kusisitiza kuwa bidhaa zina ubora na viwango vinavyokubalika.
Amesema kwa sasa wauwezo wa kuzalisha vifaa hivyo vya kuunganishia umeme vipatavyo Milioni 1.5 kwa mwaka na wanategemea kutoa ajira 120 katika kiwanda hicho huku aliongeza kusema kuwa idadi hiyo ya ajira itaongezeka kutokana na ongezeko la uzalishaji.
"Lengo letu si tu kuzalisha bidhaa hizi hapa Tanzania tu bali kuziuza nje ya nchi hivyo tunahitaji kupata ushirikiano kutoka kwa Serikali ili jambo hili liweze kutimia," amesema