A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Friday, December 29, 2017

TANGA CEMENT YAIPIGA JEKI SEKONDARI YA NYAMATONGO MKOANI MWANZA

Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Cement, Lawrence Masha akishikana mikono na Mbunge wa zamani wa Geita, Dk. Fortunatus Masha kabla ya kukabidhi msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yanga Makaga (kulia), iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana ya Shule ya Sekondari Nyamatongo iliyo wilayani humo mkoani Mwanza juzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Cement, Lawrence Masha ( wa pili kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yanga Makaga, iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana ya Shule ya Sekondari Nyamatongo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yanga Makaga (kulia), akishikana mikono na Mbunge Mstaafu wa Geita, Dk Fortunatus Masha (kushoto), katika hafla ambayo Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Cement, Lawrence Masha (katikati), alikabidhi msaada wa mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shs milioni 10 kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana ya Shule ya Sekondari Nyamatongo iliyopo wilayani Sengerema, Mwanza hivi karibuni.
Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor (kushoto) akizungamza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa  mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shs milioni 10 kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Nyamatongo wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi.
Meneja Mauzo Taifa wa Kampuni ya Tanga Cement, Leslie Massawe (kushoto) akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa  mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shs milioni 10 kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Nyamatongo wilayani Sengeremea mkoani Mwanza juzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Tanga Cement, Lawrence Masha (kushoto) akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa  mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shs milioni 10 kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Nyamatongo wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Tanga Cement, Lawrence Masha (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Enock Ndekeja katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya shs milioni 10 kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Nyamatongo jijini Mwanza juzi. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema,Yanga Makaga. Halfa hiyo ilifanyika shuleni hapo, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza juzi.
Share:

Sunday, December 24, 2017

Rose Muhando awafungukia wanao msema kuhusu kujiunga na CCMMsanii wa muziki wa Injili nchini Tanzania, Rose Muhando ameamua kufunguka ya moyoni baada ya kupokea maoni mengi ya watu wakimponda kuhusu maamuzi yake ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

Rose Muhando amesema wanaomponda na kumkebehi anawachukulia ni watu wa kawaida kwani hawezi kujifunza kwa watu walioshindwa huku akidai ameshazoea kusemwa.

“Watu wengine hawaelewagi nini wanachoongea, wanaongea ili waonekane nao wanaongea. Mimi ni mtu ambaye ninayejitambua sawa eehhh!! mimi hata sijali, nimeshazoea kutukanwa kwahiyo hata sihangaikagi na maneno yao. Mimi ni funzi kwa walioshindwa na nimeondoka kwa walioshinda, walioshindwa wana maneno mengi kutokana na nilishaimba uoga wako ndio umasikini wako, Mimi siwezi kuishi kwa uoga kwenye nchi yangu kwani ni maamuzi yangu na sijavunja sheria ya nchi na ningeogopa zaidi kama ingekuwa ni dhambi.”amesema Rose Muhando kwenye mahojiano yake na E-Gospel ya Radio E-FM.

Mapema mwezi huu kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma, Rose Muhando alialikwa kutumbuiza kwenye mkutano huo na kabla ya kukaribishwa Jukwaani, Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema Rose na Kundi lake wamekuja na maombi mawili likiwemo la kujiunga CCM na kutumbuiza huku akisema kuwa vyote vimekubaliwa.

Awali Rose Muhando hakuwa kwenye upande wowote wa vyama vya kisiasa na amesema kujiunga CCM au Chama chochote ni maamuzi yake na sio dhambi wala kosa kisheria.
Share:

Mwanamke Amfungia Mumewe Ndani na Kisha Kumchoma Moto - MtwaraJeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamsaka mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zuhura Ismail (29) kwa tuhuma za kumuua mume wake baada ya kumfungia ndani na kisha kuichoma nyumba kwa petroli.

Taarifa hizo zimetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Lucas Mkondya, ambapo amesema kwamba chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, baada ya mwanamke huyo kugundua kuwa aliyekuwa mume wake anaishi na mke mwingine, na kuamua kumvizia nyumbani kwake kisha kuichoma moto na kusababisha kifo chake.

"Ni kweli Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linamsaka mwanamke mmoja ayefahamika kwa jina la Zuhura Ismail kwa tuhuma za kuichoma nyumba aliyokuwa anaishi mume wake na mwanamke mwingine, kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya Zuhura kugundua kuwa mumewe anaishi na mke mwingine, na kuamua kwenda kuchoma nyumba hiyo moto na kuwasababishia majeraha makubwa, ambapo mumewe alipelekwa hospitali lakini kutokana na majereha hayo makubwa alifariki dunia, lakini mwanamke aliyekuwa nae anaendelea vizuri", amesema Kamanda Mkondya.

Aidha Kamanda Mkondya amesema mara baada ya tukio hilo mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Zuhura Ismail alitoroka na kwenda kusikojulikana, na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka na pindi atakapopatikana watatoa taarifa.
Share:

Saturday, December 23, 2017

Disko Toto, Fataki vyapigwa marufuku Dar katika siku ya mkesha wa kuukaribisha mwaka
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku kufyatua fataki siku ya mkesha wa sikukuu ya  mwaka mpya hivyo wananchi  wametakiwa kukusanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers  vilivyopo  Kawe ndipo wataruhusiwa kufyatua milipuko hiyo.

Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema upigaji wa fataki hizo umekuwa ukifanyika kiholela na kusababisha baadhi ya wananchi kupata mshtuko unaosababisha  ugonjwa wa moyo

Mambosasa amesema jeshi hilo limebaini siku ya mkesha wanapofyatua fataki hizo   baadhi yao wanatumia mwanya huo kufanya uhalifu na kupora mali mbalimbali za wananchi.

Pia amesema  baadhi ya watu wanatumia  silaha za moto kusherehekea mwaka mpya jambo ambalo linaweza kusababisha vifo vya watu.

"Mwananchi yeyote haruhusiwi kupiga fataki eneo lolote isipokuwa kwenye viwanja hivyo wanapotakiwa  kukusanyika na kupiga milipuko hiyo kwa nusu saa tu ambapo ulinzi utaimarika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika eneo hilo’’ amesema

Ametoa onyo kwa mwananchi atakayeenda tofauti na hayo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria hivyo anayeruhusiwa kulipua milipuko ni yule aliyepewa kibali maalumu na jeshi la polisi.

Pia jeshi la polisi hilo limeweka mikakati ya kiusalama kwa ujio wa maadhimisho ya sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ili kuhakikisha amani na usalama vinatawala wakati wa sherehe hizo.

Amesema watashirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa pamoja na kikosi cha zimamoto na uokoaji,kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuhakikisha wanathibiti matukio ya uhalifu.

Amesema watatumia kikosi maalumu cha FFU, magari ya washawasha, mbwa na farasi na askari wa usalama barabarani na makachero wamepewa maagizo maalumu ya kuchukua hatua kabla ya matukio ya kihalifu kujitokeza.

Mambosasa amesema zitatumika doria za miguu na pikipiki katika barabara zote muhimu hivyo wananchi washerehekee sikukuu hizo kwa ngazi ya familia katika mitaa kwa amani na utulivu.

Aidha kikosi cha polisi wanamaji kitafanya doria kwenye fukwe za bahari na maeneo ya jiji zima huku helikopta za polisi zikifanya doria kuhakikisha usalama unakuwepo

"Polisi watatoa ulinzi katika fukwe za baharini kwa kuweka vituo vya polisi vya muda vinavyohamishika ili kutoa msaada wa haraka pindi unapohitajika," amesema

Pia jeshi hilo limepiga marufuku disko toto katika kumbi mbalimbali kutokana na sifa za kumbi zilizopo kutokidhi viwango vya kiusalama kwa watoto
Share:

Askari mwingine JWTZ aliyeshambuliwa DRC afariki Dunia


                                    PICHA. NA MAKTABA

ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu.

Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC.

Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku.

Katika taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala.

Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na serikali ya Tanzania kutokana na msiba huo.

Source: Global Publisher
Share:

Friday, December 22, 2017

Tigo Yaibua Mamilionea Saba Zaidi Katika Promosheni Murwa ya Tigo Pesa

live it love it
                                                           PRESS RELEASE
Tigo Yaibua Mamilionea Saba Zaidi Katika Promosheni Murwa ya Tigo Pesa
 • Wateja Wengine 28 Wajishindia Zawadi za TZS 500,000 Kila Mmoja.

Dar es Salaam, 22 Desemba, 2017- Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa imewaibua jumla ya mamilionea saba (7) wapya  katika droo ya wiki hii ya promosheni yake inayoendelea ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde’.

Washindi wengine 28 nao wamejinyakulia donge nono za kila siku za TZS 500,000 kila mmoja, na kufanya jumla ya wateja walipotakana hadi sasa kufikia 90.

Akitangaza washindi wa wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema kuwa pamoja na zawadi hizo za kila siku, wateja wa Tigo Pesa wana fursa kubwa ya kushinda zawadi kubwa za TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni ambapo washindi watajulikana usiku wa kuamkia mwaka mpya.
Kufikia sasa tumetoa until now we have given out Tzs 69 Million to 90 winners and we expect  to give out Tzs 51Million more to remaining 63 winners

‘Kufikia sasa tumtoa jumla ya TZS 69 milioni kwa washindi 90 na bado tuna zawadi za TZS 51 milioni zitakazotolewa kwa washindi wengine 63, ikiwa pamoja na mamilionea wapya tutakaowapata usiku  wa kuamkia mwaka mpya wa 2018. Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda, kwa hiyo nawaasa wateja wote wa Tigo wachangamkie fursa hii ya kutimiza ndoto zao za sikukuu na mwaka mpya’ alisema.

Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya  70,000 waliosambaa nchini kote.  

Kuhusu Tigo:

Tigo Tanzania ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya kidigitali nchini Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995.

Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali kwa kuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na huduma ya kwanza inayowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki.   
  
Tigo ni kampuni ya pili kwa ukuwa nchini na imekuwa kampuni ya simu inayokuwa kwa kasi zaidi nchini kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini

Tigo inajivunia jumla ya watumiaji milioni 10 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.  

Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani.
………………………………………………………………………………………………………

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na: 
Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano

Simu: +255 713 123431            Barua pepe: Woinde.shisael@tigo.co.tz
Share:

Thursday, December 21, 2017

ABB completes EPC business model change

ABB

ABB today announced actions across three divisions to complete the business model change for engineering, procurement and construction (EPC) as it ends its transition year 2017. These decisions are fully in line with ABB’s strategy to shift the center of gravity towards strengthened competitiveness, higher growth segments and lower risk.

In the Power Grids division, ABB has signed an agreement to form a joint venture with SNC-Lavalin for electrical substation EPC projects; SNC-Lavalin will have majority and controlling interest. The new entity will leverage ABB’s power technology leadership and SNC-Lavalin project expertise to capture opportunities for profitable growth. These actions complement the ongoing ”Power Up” program; as part of this program, ABB started to shift its focus towards solutions and service-based customer offerings.

In the Industrial Automation division, ABB has previously announced the oil & gas EPC joint venture with Arkad Engineering and Construction Ltd., a fully integrated EPC contractor for the energy sector based in Saudi Arabia; the closing of the transaction is now expected by December 31, 2017.

ABB’s current oil & gas EPC business will be transferred into the new JV company, in which, Arkad will have majority and controlling interest. The new JV company, Arkad-ABB S.p.A., will provide the full range of integrated EPC services for oil & gas plants. It will build on more than 50 years of experience in oil & gas EPC and the successful delivery of more than 300 projects globally.

In the Robotics and Motion division, ABB has decided to wind down its turnkey full train retrofit business, beyond meeting current contractual commitments. Robotics and Motion will continue its strong role as innovation partner for the rail industry.
 

ABB COMPLETES EPC BUSINESS MODEL CHANGE 2/2


“We are taking decisive actions to complete our EPC business model change as we end our transition year. These actions are in line with our strategy to shift our center of gravity towards strengthened competitiveness, higher growth segments and lower risk,” said ABB CFO Timo Ihamuotila “We will book the related charges in Q4 2017 and report the divisions starting in 2018 excluding these legacy businesses.”


The fourth quarter 2017 results of Power Grids and Robotics and Motion are each expected to be impacted by approximately $75 million on operational EBITA. The transfer of the turnkey oil & gas EPC business into the JV with Arkad is expected to result in a non-operational pre-tax charge to net income of approximately $75 million. 


ABB will report these businesses as a non-core operating unit within Corporate & Other. This unit is expected to retain and execute parts of the existing legacy backlog until the transition out of these businesses is complete. The new unit will report to ABB’s CFO Timo Ihamuotila effective January 1, 2018. Group and divisional proforma data for 2016 and 2017 year-to-date excluding the transferred activities will be made available December 21, 2017 on our website www.abb.com/investorrelations.


ABB (ABBN: SIX Swiss Ex) is a pioneering technology leader in electrification products, robotics and motion, industrial automation and power grids, serving customers in utilities, industry and transport & infrastructure globally. Continuing a history of innovation spanning more than 125-years, ABB today is writing the future of industrial digitalization and driving the Energy and Fourth Industrial Revolutions. ABB operates in more than 100 countries with about 136,000 employees. www.abb.com


Important notice about forward-looking information This press release includes forward-looking information and statements as well as other statements concerning the outlook for our business. These statements are based on current expectations, estimates and projections about the factors that may affect our future performance, including global economic conditions, the economic conditions of the regions and industries that are major markets for ABB Ltd. These expectations, estimates and projections are generally identifiable by statements containing words such as “expects,” “believes,” “estimates,” “targets,” “plans,” “is likely”, “intends” or similar expressions. However, there are many risks and uncertainties, many of which are beyond our control, that could cause our actual results to differ materially from the forward-looking information and statements made in this press release and which could affect our ability to achieve any or all of our stated targets. The important factors that could cause such differences include, among others, business risks associated with the volatile global economic environment and political conditions, costs associated with compliance activities, market acceptance of new products and services, changes in governmental regulations and currency exchange rates and such other factors as may be discussed from time to time in ABB Ltd’s filings with the U.S. Securities and Exchange Commission, including its Annual Reports on Form 20-F. Although ABB Ltd believes that its expectations reflected in any such forward-looking statement are based upon reasonable assumptions, it can give no assurance that those expectations will be achieved.

This is information that ABB Ltd is obliged to make public pursuant to the EU Market Abuse Regulation. The information was submitted for publication, through the agency of the contact persons set out below, at 6:45 am CET, on December 20, 2017
Share:

Sanlam General Insurance Empowers General Insurance Agents

Sanlam Chief Executive Officer, Mr. Manasseh Kawoloka.
Sanlam Chief Executive Officer, Mr. Manasseh Kawoloka. Introducing Sanlam General Insurance Management Team. On his right is Business Development Manager - Mr. Jabir Kigoda, on his left is Chief Finance Officer, Mr. Geofrey Masige, and Chief Operating Officer, Mr. Lester Chinyang’anya (gray suits)
Chief Executive Officer, Mr. Manasseh Kawoloka opening the event
Business Development Manager, Mr. Jabir Kigoda taking questions from agents.

Sanlam General Insurance Empowers General Insurance Agents

Sanlam General Insurance conducted a day long training session at Serena Hotel in Dar es Salaam. The event was attended by over 45 agents from different firms and regions.

The train focused on different areas such as Use of Modern Technology on Premium Payments and Collections the insuring public, Finance management, Market Developments and new regulations.

The Chief executive Officer, Mr Manasseh Kawoloka, who officially opened this event shared with gathering new developments and regulations that have been recently introduced in insurance industry. He emphasized the requirement that all agents should understand and comply with the regulatory changes introduced in the market. The new law requires the client to pay premium before or on the date of commencement of the insurance cover.

On the other hand, as part of improving service delivery on how Agents do business, Sanlam General has introduced a new system to their Agents that will assist to improve the work flow and business in general. The system will reduce manual transaction between the Agents, their Clients and Sanlam General especially on covernote issuance, premium payments and collections.

“Sanlam General believes that training Agents is part of doing business the right way and it is something that is enjoyed and like to do. Trainings on this nature offers opportunities to interact with agents more freely and in informal way”, said Business Development Manager Mr. Jabir Kigoda.

Agents were very excited and pleased with the training and they are looking forward for more opportunities for training in the year ahead 2018.Share:

Wednesday, December 20, 2017

Vijana wachangamkia fursa kupitia Program ya Wajibika ya Benki ya NBC

01
Mmoja ya waratibu wa programu ya  Wajibika ya Benki ya NBC, Michael Mwangoka (kushoto), akizungumza na baadhi ya vijana na wanafunzi katika viwanja Leaders, Dar es Salaam juzi kuhusu  Programu ya Wajibika yenye lengo la kuwaandaa vijana na wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.
02
Mmoja ya  waratibu wa programu ya  Wajibika ya Benki ya NBC, Debora Maboya (kulia), akizungumza na baadhi ya vijana katika viwanja Escape One, jijini Dar es Salaam kuhusu  Programu ya Wajibika yenye lengo la kuwaandaa vijana na wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.
03
Mmoja ya waratibu wa programu ya  Wajibika ya Benki ya NBC, Michael Mwangoka (kulia), akizungumza na baadhi ya vijana katika viwanja Leaders, Dar es Salaam kuhusu  Programu ya Wajibika. Program ya Wajibika ya NBC yenye lengo la kuwawezesha vijana wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi ilizinduliwa Julai 8 mwaka jana.
04
 Mmoja ya waratibu wa programu ya  Wajibika ya Benki ya NBC, Imani Sinkonde (kushoto), akitoa maelezo jinsi ya kujiunga kwa njia ya mtandao na program ya Wajibika ya Benki ya NBC kupitia tovuti ya benki hiyo kwa baadhi ya vijana katika viwanja vya Escape One, Dar es Salaam. Programu ya Wajibika ina lengo la kuwaandaa vijana na wahitimu wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kuingia katika soko la ajira rasmi na binafsi.
Share:

WATOTO YATIMA WAISHUKURU KAMPUNI YA QNET TANZANIA

Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi misaada mbalimbali ikiwepo vyakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo wengine pichani ni baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki (kulia) akikabidhi mashine ya  kusafishia  maji ya kunywa (water purifier) pamoja na mahitaji mengine ya kibinadamu  kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

QNET imetoa Msaada wa mashine ya kusafishia maji (water purifier) na vyakula kwa watoto yatima wa kituo cha Khayraat, Dar es salaam

Tarehe 20th Desemba, Dar es salaam – Moja kati ya taasisi inayokua kwa kasi sana Tanzania ya masoko ya mtandao QNET, leo imetoa msaada wa mashine yenye mfumo wa kusafisha maji ya Water purifier na chakula chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 kwa kituo cha watoto yatima cha Khayraat jijini Dar es salaam.

Msaada wa QNET ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo za kuwajibika katika jamii, ambazo zimeelekezwa katika kutoa msaada wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watoto 500 wenye uhitaji katika kituo cha kulelea watoto yatima na kuwapatia chakula kwaajili ya kuwawezesha kufurahia sikukuu za krimasi katika kipindi hiki cha sikukuu kama watoto wengine.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa QNET Tanzania Benjamin Mariki, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ina sera bora ya uwajibikaji kwa jamii ambayo inatafuta kutoa kwa jamii inayoihudumia.

“Katika kampuni ya QNET, tunaamini kuwa zaidi ya kusambaza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu kwa wateja wetu, tuna jukumu la kusaidia serikali na wadau wengine katika kutekeleza shughuli ambazo zina athari nzuri kwa jamii, hasa miongoni mwa wanajamii wenye uwezo mdogo,” alisema Mariki.

Mariki alisema kuwa msaada uliotolewa kwaajili ya kituo ni pamoja na ufungaji wa mashine ya kusafishia maji, kilo 100 za Mchele, kilo 100 za maharage, kilo 100 za unga, lita 60 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za sukari, kilo 100 za sabuni ya kufulia pamoja na biskuti, pipi na juisi.

Akipokea msaada huo, Mwasisi wa kituo cha Khayraat Orphans Centre, Bi Khadija Khussein aliishukuru kampuni ya QNET kwa kutoa msaada akisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiwango kikubwa watoto walioko kituoni.

“Tunashukuru kwa msaada huo tukiwa tunatambua kuwa mashine ya kusafishia maji ya water purifier itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwaajili ya watoto, hivyo kutoa uhakika wa afya kwa watoto kwa kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa maji kama vile typhoid na Kipindupindu wakati vyakula vitawapa watoto nafasi ya kufurahia sikukuu ya krimasi na mwaka mpya”. Alibainisha Bi KhusseinKuhusu QNET

Ni kampuni maarufu ya mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia, QNET inatoa aina mbalimbali za bidhaa za kuboresha maisha ambazo zinatolewa kupitia mfumo wake wa biashara ya mtandao (e-commerce) kwa wateja na wasambazaji katika zaidi ya nchi 100. Kampuni hii pia ina baadhi ya ofisi zake na Mawakala katika nchi 25 duniani kote, na zaidi ya watayarishaji 50, nje ya waendeshaji wa ndani ya nchi au mawakala katika nchi kadhaa.

QNET ni mwanachama wa Chama cha wauzaji wa moja kwa moja (Direct Selling Association) cha Malayasia, Singapore, Ufilipino na Indonesia. QNET pia ni sehemu ya Chama cha Chakula Bora cha Hong Kong (Hong Kong Health Food Association) na Chama cha viwanda vya Virutubisho vya afya cha Singapore (Health Supplements Industry Association) miongoni wa vingine.

QNET pia inafanya vizuri katika kudhamini michezo dunia kote, ikijumuisha mpira wa miguu (Mshirika wa moja kwa moja wa mauzo wa Klabu ya Manchester City), Mashindano ya Magari ya fomula One, badminton na zaidi, kufuatia imani thabiti ya kampuni ya QNET kwamba msukumo, ari na kufanya kazi kwa pamoja katika michezo kunaendana na ule wa QNET

Kwa maelezo zaidi kuhusu QNET, Tafadhali tembelea Wavuti ya QNET,  www.qnet.net
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive