A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, December 3, 2017

GMS SASA YAWAPELEKA WATEJA WAKE DISNEY HONG KONG

Kuelekea msimu wa sikukuu maduka ya GSM wanakuletea ofa maalum itakayowawezesha wateja wake kushinda safari ya kuelekea Disney, Hong Kong nchini China.
 
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza ameeleza kuwa mteja akifanya manunuzi yatakayofikia kiasi cha shilingi laki moja na nusu (150,000) ataingizwa katika droo maalum itakoyomuwezesha kushinda safari ya kuelekea Disney, Hong Kong China.
"Endapo mteja wetu atafanya manunuzi ya kuanzia laki na nusu atafanikiwa kuingia katika droo maalum ambapo mwanzo mwa mwezi January atangazwa mshindi ambaye atapata fursa ya kusafiri Disney, Hong Kong, China" Alisema Farida.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa GSM Foundation Fahad Ahmad amesema kuwa GSM wataendelea kutoa ofa kwa wateja wao kupitia maduka yao mbalimbali jijini Dar es Salaam huku akisisitiza bidhaa ni bora na gharama yake ni nafuu kulingana na maisha ya mtanzania wa kawaida.
Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza (kushoto),  akizungumza na wandishi wa habari katika hafa hiyo katikati ni Mkurugenzi wa GSM Foundation Fahad Ahmad (kulia), ni Meneja Mwendeshaji wa kampuni hiyo Yahya Zuhidi.
Meneja Mwendeshaji wa kampuni hiyo Yahya Zuhidi akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo
Picha zote na Brian Peter
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive