A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Saturday, December 23, 2017

Disko Toto, Fataki vyapigwa marufuku Dar katika siku ya mkesha wa kuukaribisha mwaka




Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku kufyatua fataki siku ya mkesha wa sikukuu ya  mwaka mpya hivyo wananchi  wametakiwa kukusanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers  vilivyopo  Kawe ndipo wataruhusiwa kufyatua milipuko hiyo.

Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema upigaji wa fataki hizo umekuwa ukifanyika kiholela na kusababisha baadhi ya wananchi kupata mshtuko unaosababisha  ugonjwa wa moyo

Mambosasa amesema jeshi hilo limebaini siku ya mkesha wanapofyatua fataki hizo   baadhi yao wanatumia mwanya huo kufanya uhalifu na kupora mali mbalimbali za wananchi.

Pia amesema  baadhi ya watu wanatumia  silaha za moto kusherehekea mwaka mpya jambo ambalo linaweza kusababisha vifo vya watu.

"Mwananchi yeyote haruhusiwi kupiga fataki eneo lolote isipokuwa kwenye viwanja hivyo wanapotakiwa  kukusanyika na kupiga milipuko hiyo kwa nusu saa tu ambapo ulinzi utaimarika siku ya mkesha wa mwaka mpya katika eneo hilo’’ amesema

Ametoa onyo kwa mwananchi atakayeenda tofauti na hayo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria hivyo anayeruhusiwa kulipua milipuko ni yule aliyepewa kibali maalumu na jeshi la polisi.

Pia jeshi la polisi hilo limeweka mikakati ya kiusalama kwa ujio wa maadhimisho ya sikukuu za Krismasi na mwaka mpya ili kuhakikisha amani na usalama vinatawala wakati wa sherehe hizo.

Amesema watashirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa pamoja na kikosi cha zimamoto na uokoaji,kampuni binafsi za ulinzi, vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuhakikisha wanathibiti matukio ya uhalifu.

Amesema watatumia kikosi maalumu cha FFU, magari ya washawasha, mbwa na farasi na askari wa usalama barabarani na makachero wamepewa maagizo maalumu ya kuchukua hatua kabla ya matukio ya kihalifu kujitokeza.

Mambosasa amesema zitatumika doria za miguu na pikipiki katika barabara zote muhimu hivyo wananchi washerehekee sikukuu hizo kwa ngazi ya familia katika mitaa kwa amani na utulivu.

Aidha kikosi cha polisi wanamaji kitafanya doria kwenye fukwe za bahari na maeneo ya jiji zima huku helikopta za polisi zikifanya doria kuhakikisha usalama unakuwepo

"Polisi watatoa ulinzi katika fukwe za baharini kwa kuweka vituo vya polisi vya muda vinavyohamishika ili kutoa msaada wa haraka pindi unapohitajika," amesema

Pia jeshi hilo limepiga marufuku disko toto katika kumbi mbalimbali kutokana na sifa za kumbi zilizopo kutokidhi viwango vya kiusalama kwa watoto
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive