Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel
Tanzania Beatrice Singano (kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa
uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA
NA GB 1 ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu
mbili tu Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda Hafla ya
uzinduzi huo umefanyika leo makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania
Isack Nchunda (kushoto) akiongea na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’
mpya ambapo itamuwezesha mteja wa
Airtel KUSMATIKA NA GB 1 ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu
mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu (kulia), ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel Tanzania Beatrice Singano, Hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo makao
makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda na Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano, wakionyesha bango lemye
aina mbalimbali za bando za huduma hiyo baada ya uzinduzi huo. Picha na Brian Peter
Airtel yaleta
‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ SMATIKA NA 1GB siku tatu kwa 2000 tu
f
- ‘SMATIKA NA 1GB Yatosha Intaneti inayokupa muda mrefu kwa gharama nafuu zaidi.
Airtel Tananzania Mtandao bora kwa Smartphone yako imewapatia wateja wake uhuru zaidi kwa kuwaletea bando mpya
za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ maalum kwa watumiaji wa huduma za intaneti.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Isack Nchuna wakati wa hafla ya kuzindua ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti,
alisema
“Airtel itaendelea kuleta huduma zenye ubora na ubunifu wa hali ya juu
ili kuendelea kuwa sambamba na mahitaji ya wateja katika huduma za
intaneti ambapo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa Airtel imejiwekea mikakati
endelevu mingi ili kukidhi uhitajika na wateja
wote”
“Tuaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya kutoa suluhisho la mawasiliano kupitia uzinduzi wa
‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ kwa kutoa huduma nafuu ya Intaneti
kwa watumiaji wote nchini huku tukiweka kipaumbele zaidi katika ubora
wa mtandao pamoja na kuwapatia wateja uhuru zaidi” aliongeza Nchunda.
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’
ni
zawadi ya awali kabisa tunayowapatia watumiaji wa Airtel katika msimu
huu wa sikukuu, tunaamini kuwa ndani ya msimu huu wa sikukuu wateja
wanauhitaji mkubwa sana wa intaneti katika kukamilisha
shamrasharna
wakiwa wanawasiliana na ndugu, jamaa na marafiki wakati
wote!”
Akifafanua zaidi Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano alisema Bando za
‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote wa airtel kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote.
“Mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kujipatia
MB 40, vilevlie mteja ataweza KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu” alieleza Bi Singano.
“kujiunga na ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ unatakiwa kupiga *149*99# kisha chagua 5
Yatosha Intanet vilevile unaweza kujiunga kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kisha chagua Yatosha Intanet”.
Airtel
Tanzania imekuwa katika programu ya uboreshaji wa miundombinu ya
mawasiliano yake ili kukamilisha lengo
lake la kutoa mawasiliano bora na yenye uhakika kwa kutumia teknolojia
ya kisasa ya U900. Tayari Airtel imezindua maboresho ya mtandao wake
kwa kutumia teknolojia hiyo ya U-900 kwenye mikoa ya Arusha, Dar es
salaam, Dodoma, Morogoro na Mwanza huku ikiendelea
kuwahakikishia wateja wake mawasiliano bora hasa katika maeneo ya nje
na ndani ya majengo marefu au yenye uhitaji zaidi.
0 comments:
Post a Comment