A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Showing posts with label SPORTS. Show all posts
Showing posts with label SPORTS. Show all posts

Wednesday, December 27, 2023

BAYPORT YANOGESHA ROMBO MARATHON

Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko akikabidhi cheti cha shukurani kwa Meneja Rasilimali Watu wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport, Bi. Evalyn Hall (kulia), kutambua mchango wa kampuni hiyo kama mdhamini mkuu wa mbio za Rombo Marathon 2023 zilizotimua vumbi lake mjini Rombo mkoani Kilimanjaro jana. Kulia kwa Naibu waziri mkuu ni Waziri wa Elimu na Mbunge wa Rombo, Prof. Adolf Mkenda na kushoto kwake ni Waziri Biteko ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bwana Nurdin Babu.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport, Bwana Nderingo Materu (wa pili kushoto), Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo, Bwana Lugano Kasambala (kushoto kwake), pamoja na wakimbiaji wengine, wakishiriki mbio za Rombo Marathon mjini Rombo, Kilimanjaro jana. Mbio hizo zilizodhaminiwa na Bayport, zina lengo la kuhamasisha vivutio vya utalii mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bwana Nurdin Babu (kulia), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport, wakishiriki mbio za Rombo Marathon mjini Romb, Kilimanjaro jana. Mbio hizo zilizodhaminiwa na Bayport, zina lengo la kuhamasisha vivutio vya utalii mkoani humo.

Na mwandishi wetu, Rombo, Kilimanjaro

TAASISI ya Kifedha ya Bayport imenogesha na kufanikisha mbio za Rombo Marathon 2023 zilizofanyika mjini Rombo, Kilimanjaro jana, zikiwa na lengo la kuhamasisha vivutio vya utalii wilayani humo.

Ikiwa ni mwaka wa pili sasa Rombo Marathon imefanyika ikihudhuriwa na viongozi wa kiserikali, wageni, na watu mashuhuri huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dk. Doto Biteko.

Akizungumza wakati wa mbio hizo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bayport, Bwana Nderingo Materu alisema Bayport ilikubali kuwa mdhamini Rombo Marathon ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na muasisi wa mbio hizo, Waziri wa Elimu na Mbunge wa Rombo, Prof. Adolf Mkenda katika kukuza utalii pamoja na suala zima la uhifadhi wa mazingira.

Kama mnavyofahamu sisi Bayport tumekuwa namba moja katika suala la utunzaji wa mazingira kwa njia ya upandaji miti, leo hii tumeamua kudhamini Rombo Marathon na tutaendelea kuunga mkono juhudi zozote nchini zenye lengo la kukuza utalii na kuhifadhi mazingira."

Lakini pia kama inavyofahamika umuhimu wa kufanya mazoezi ya mwili kwa ajili ya ubora wa afya za wafanyakazi na familia zetu, tunaamini mbio hizi zitaleta hamasa pia kwa watanzania kutilia mkazo umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,” alisema Bwana Materu.
Katika hotuba yake, Naibu Waziri Mkuu, Mhe, Dk. Biteko alitoa pongezi kwa waandaaji na wadhamini wa mbio za Rombo Marathon akisema zimekuwa na mafanikio makubwa lakini kikubwa ikiwa ni kujifunza utamaduni wa wana Rombo pamoja ya vivutio vya utalii vinavyopatikana katika wilaya na mkoa huo.

Natoa pongezi nyingi kwa muasisi wa Rombo Marathon, Waziri wa Elimu na Mbunge wa Rombo, Prof. Mkenda, natoa pongezi kwa serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Rombo bila kuwasahau wadhamini wote waliojitolea rasilimali zao kufanikisha tukio hili."

Serikali chini ya Rais, Mhe, Dk. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuunga mkono juhudi yoyote inayofanywa yenye lengo la kuwaletea maendeleo watu wa Rombo na kwa watanzania kwa ujumla,” alisema Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu.

Naye Waziri wa Elimu, Mbunge wa Rombo na muasisi wa mbio hizo, Prof. Adolf Mkenda alitoa shukurani zake kwa Mhe. Naibu Waziri Mkuu, Dk. Biteko kwa kukubali kuwa mgeni rasmi pamoja na wadhamini wa mbio hizo Taasisi ya Kifedha ya Bayport kwa kufanikisha tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya watu wa Rombo na wananchi wa Kilimanjaro.

Namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu kwa kuungana na wana Rombo katika kushiriki tukio hili, natoa pia shukrani kwa wadhamini wote waliowezesha kufanya tukio hili kuwa lenye ubora ikiwemo Taasisi ya Bayport Financial Services,” alisema Prof. Mkenda.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bwana Nurdin Babu, alichukua nafasi hiyo kuwakaribisha wageni wote wanaotoka ndani na nje ya Tanzania kwenda kuangalia vivutio vya utalii mkoani humo akisema Kilimanjaro ipo salama na wapo tayari kuwapokea na kuwahudumia.
Mbio za Rombo Marathon zinazofanyika kwa mwaka wa pili sasa zimeshirikisha mbio za Km 21, Km 10 na mbio za kujifurahisa za kilomita 5.
Share:

Monday, May 8, 2023

Benki ya Absa kuendelea kudhamini Absa Dar City Marathon

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo walioshiriki mbio za Absa Dar City Marathon zilizofanyika Kwa udhamini mkuu wa benki hiyo jijini Dar es Salaam Jana. Wafanyakazi 200 wa Absa walishiriki katika mashindano hayo yaliyoshirikisha wakimbiaji zaidi ya 3000.
Mshindi wa Kwanza wa Mbio za Absa Dar City Marathon, , Augustino Sulle ( kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser mara baada ya kufanyika Kwa kinyang'anyiro hicho jijini Dar es Salaam Jana. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki hiyo, Aron Luhanga. Benki ya Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo ikitoa kiasi cha shs milioni 45 kufanikisha mashindano hayo.
Mshindi wa nne wa Mbio za Absa Dar City Marathon, Oscar Shananga ( kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga mara baada ya kufanyika Kwa kinyang'anyiro hicho jijini Dar es Salaam Jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Obedi Laiser. Benki ya Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo ikitoa kiasi cha shs milioni 45 kufanikisha mashindano hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (kushoto) pamoja na washiriki wengine wakipoza viungo muda mfupi baada ya kumalizika Kwa mbio za Absa Dar City Marathon zilizofanyika Kwa udhamini mkuu wa benki hiyo jijini Dar es Salaam Jana.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (kushoto), Meneja Mahusiano wa benki hiyo, Theresia Kahesa (katikati) pamoja na wakimbiaji wengine wakishiriki mbio za Kilomita 21 za Absa Dar City Marathon zilizofanyika jijini Dar es Salaam jana. Benki ya Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa mbio hizo ikitoa kiasi cha shs milioni 45 kufanikisha mashindano hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (katikati) akipozi kwa picha ya kumbukumbu na baadhi ya wakimbiaji baada ya kumalizika kwa mbio za Absa Dar City Marathon zilizofanyika Kwa udhamini mkuu wa benki hiyo jijini Dar es Salaam Jana.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (kushoto), akipokea cheti cha shukurani kutoka Kwa mmoja wa maofisa wa The Runners Club, Kwa kutambua mchango wa Absa kama mdhamini Mkuu wa mbio za mwaka huu.

BENKI ya Absa Tanzania imesema itaendelea kudhamini mbio za Absa Dar City Marathon ikiwa kama mdhanini mkuu kutokana na faida za mbio hizo kwa ustawi wa afya za watanzania.

Akizungumza wakati wa mbio hizo zilizotimua vumbi jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi Laiser alisema kama Absa wanaamini kukimbia kunaleta fursa nyingi katika maisha ikiwa ni pamoja na afya njema jambo muhimu katika ufanisi wa shughuli za uzalishaji mali.

Katika kukimbia tunajenga afya zetu, ili tuweze kufanya shughuli zetu, tuweze kuishi kwa muda mrefu, ni dhana mojawapo ambayo sisi Absa tunaiishi na ndio maana tukaungana na The Runners Club ili tuweze kuboresha maisha ya watanzania,” alisema Bwana Laiser.

Alisema Absa kama benki kongwe kuliko zote Tanzania ikitoa shughuli za kibenki tokea mwaka 1925 ni imani yao kwa kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo, Klabu ya The Runners mbio hizo zitaendelea kukua na kufikia viwango vya Kimataifa.

The Runners Club ni wabobezi katika marathon na sisi kama Absa ni wabobezi hasa inapokuja katika utoaji wa huduma bora za kibenki hivyo tunaamini kwa pamoja tunaweza kuifikisha marathon hii mbali zaidi,” alisema mkurugenzi huyo.

Katika mbio hizo Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Runners Club, alisema pamoja na mambo mengine mbio hizo zina malengo ya kutangaza vivutio vya utalii wa Jiji la Dar es Salaam na ndio sababu zilianzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo na kuzunguuka katika mitaa na barabara mbalimbali maarufu jijini humo.

Zaidi ya wanariadha 3000 kutoka mikoa mbalimbali nchini walipimana ubavu wakishindana katika mbio za km 21, 10 na 5 huku washindi walikabidhiwa zawadi ya za medali na pesa taslimu.
Share:

Tuesday, May 2, 2023

Benki ya Absa yatoa sh milioni 45 kudhamini Absa Dar City Marathon

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (wa pili kulia) akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza udhamini wao wa shs milioni 45 katika mbio za Absa Dar City Marathon zinazotarajiwa kutimua vumbi jijini humo mei 7 mwaka huu. Wengine kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Britam Insurance, Leoncia Makobo, Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya The Runners, Godfrey Mwangungulu, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni wa Bima ya Alliance Life Assurance, Jawa Masomo na na Katibu wa The Runners, Scola Kisanga.
Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya The Runners, waandaaji wa Dar City Marathon ,Godfrey Mwangungulu (wa pili kulia), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (kulia), Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya The Runners, Godfrey Mwangungulu, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni wa Bima ya Alliance Life Assurance, Jawa Masomo, Meneja Masoko wa Britam Insurance, Leoncia Makobo na Katibu wa The Runners, Scola Kisanga, wakionyesha fulana zitakazovaliwa siku ya mbio za Absa Dar City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Mei 6 jijini Dar es Salaam. Absa imetoa udhamini wa kiasi cha shs milioni 45. Hafla hiyo imefanyika jijini humo leo.

*'Ni kwa ajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza'*

WATANZANIA wameshauriwa kulinda afya zao Kwa kushiriki mbio na mazoezi ya viungo kwani afya ni mtaji muhimu katika shughuli za uzalishaji mali.

Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga wakati akizungumzia udhamini wa Absa katika mbio za kilomita 21 za Absa Dar City Marathon, zinazotarajiwa kutimua vumbi jijini humo jumapili wiki hii.

Bwana Aron alisema Benki ya Absa kwa kutambua kuwa afya ni mtaji mkubwa sana Kwa wafanyakazi, wateja na Kwa jamii ya watanzania na kuwa bila ya kuwa na afya njema shughuli za kiuchumi haziwezi kwenda kadri zinavyotakiwa benki yao imekubali kutoa udhamini wa mbio hizo wenye thamani ya shs milioni 45.

Kama Absa tunajisikia furaha sana kuungana na waandaaji wa Dar City Marathon tukiwa wadhamini wakuu wa mbio hizi tukitoa udhamini wa kiasi cha shs milioni 45 ambazo pia zikiwa na lengo la kuisaidia jamii kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza."

Natoa wito kwa watanzania, wateja wetu kujitokeza Kwa wingi kushiriki mbio hizi, mtu akiwa anafanya mazoezi akiwa anakimbia, anajenga afya na hapo hapo anapata utajiri wake."

Baada ya mbio hizi tutaungana na Runners Club kwenda katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ili kukabidhi vifaa vitakanyosaidia jamii wakiwemo watoto kupambana na magonjwa yasiyoambukiza”, alisema Bwana Aron.

Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Habari Klabu ya The Runners waandaaji wa mbio hizo, Godfrey Mwangungulu alitoa shukurani kwa Absa pamoja ma wadhanini wengine kwa kudhamini mbio hizo ambazo zaidi ya Watu 3000 watashiriki akisema pamoja mambo mengine zitasaidia kutangaza vivutio vya utalii vya Jiji la Dar es Salaam kwani zitapita katika mitaa mashuhuri ya jiji hilo.

Tunaungana na majiji mengine sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa sehemu ya historia kwenda kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii katika Jiji letu la Dar es Salaam, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mbio hizi kufanyika katikati ya jiji, natoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi kwa pamoja na mbio hizo pia kuna burudani mbalimbali zimeandaliwa zitakazofanyika katika ziwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam", alisema.

Mbio za Absa Dar City Marathon zitajumuisha mbio za kilomita 21, mbio za kilomita 10 na mbio za kujifurahisha za kilomita 5 ambazo zawadi mbalimbali zitatolewa zikiwemo pesa tasilimu kwa mshindi wa kwanza hadi wa 10 kwa wanawake na wanaume. 
Share:

Saturday, December 11, 2021

KP MOTORZ YANG’ARISHA FAMILIA MARATHON 2021 YAKABIDHI GARI KWA MSINDI WA KM 21 WANAWAKE

   
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kulia), akikabidhi funguo ya gari jipya aina ya Toyota Passo lenye thamani ya shs milioni 9.5 kwa mshindi wa kwanza wa KM 21 Wanawake wa mbio za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim, jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Meneja Mauzo kwa Makampuni wa KP Motorz, Protas Mbeya na Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa pili wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Jamila Abdallah, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa tatu wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Verah Mrema, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa nne wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Shameeza Mukhi, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Kuagiza na Kuuza Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe (kushoto), akikabidhi cheti kwa mshindi wa tano wa KM 21 Wanawake wa mashindano ya mbio za Familia Marathon 2021, Nimishal Ladha, wakati wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Familia Marathon, Francisca Alphonce.
Mshindi wa Mbio za KM 21 Wanawake za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim akijaribu kuwasha gari lake mara baada ya kukabidhiwa na wadhamini, Kampuni ya Magari ya KP Motorz mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dar es Salaam leo. Aisha atakuwa pia balozi wa KP Motorz kwa muda wa mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa Familia Marathon 2021, Francisca Alphonce (wa nne kushoto), akikabidhi tuzo kwa Mkuu wa Mauzo na Uendeshaji wa Kampuni ya Magari ya KP Motorz, Lucas Mwamfupe ya kutambua mchango wa udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za mwaka huu za Familia Marathon zilizotimua vumbi jijini Dar es Salaam leo zikifanyika eneo la Msasani Beach Club. KP Motorz ilitoa gari jipya aina ya Toyota Passo kwa mshindi wa pili wa KM 21 Wanawake.
Mshindi wa Mbio za KM 21 za Familia Marathon 2021, Aisha Ibrahim akipozi kwa picha mbele ya gari lake, Toyota Passo lililotplewa zawadi na Kampuni ya kuagiza na kuuza magari ya KP Motorsz mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Wednesday, December 8, 2021

FAMILIA MARATHON 2021 KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI DISEMBA 11

Mwenyekiti wa mbio za Familia Marathon 2021, Bi. Francisca Alphonce (wa tatu Kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Disemba 11, jumamosi. Wengine ni wawakilishi wa Kampuni zinazodhamini mbio hizo.
Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye (wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kutimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii. Usajili unaendelea kufanyika katika Tawi la KCB Mlimani City.
Ofisa Habari Familia Marathon (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Disemba 11, jumamosi. Mbio zitaanzia Msasani Beach Club kuanzia saa 12 asubuhi zikijumuisha mbio za 21km -half marathon, 10km- Corporate Run na 5km -Social Run.
Mkurugenzi Mtendaji was Kampuni ya magari ya KP Motors, Anita Kisima (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kutimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii. KP Motors itatoa zawadi ya gari aina ya Passo mpya kwa mshindi mwanamke kati ya washindi kumi atakayeshinda mbio za KM 21. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye na Ofisa Masoko wa UTT Amis, Rahim Mwanga.
Mkurugenzi Uendeshaji wa Planet Fitness, Ramadhani Mdula (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii.
Meneja wa Kampuni ya Rani Sanitary Pads, Mawi Zahor (kulia ), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii.
Waandaaji na wadhamini wa Familia Marathon 2021 wakionyesha kwa waandishi habari, Dar es Salaam leo, medani na baadhi ya zawadi watakazopewa washiriki wa mbio hizo zitakazofanyika kwa mtindo wa kutembea na kukimbia jijini humo jumamosi wiki hii. Mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na KCB Bank, KP Motors, UTT Amis, Premier Security, Optical Centre, Rani Sanitary Pads, Planet Fitness, Knight Support na Xpress Rent.
Share:

Thursday, December 2, 2021

SERENGETI LAGER YAWAKUTANISHA MASHABIKI WA MBEYA USO KWA USO NA TAIFA STARS

 
Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa tayari kwa ajili ya kujibu maswali ya mashabiki katika tukio la kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Taifa Stars’ lililofanyika jijini Mbeya ambapo mashabiki walikutana uso kwa uso na baadhi ya nyota wa timu ya taifa.
Mchezaji wa Taifa Stars Kibwana Shomari, akijibu moja ya swali kutoka kwa mashabiki wa soka wakati wa tukio lililowakutanisha wacheza wa timu hiyo ya taifa na washabiki wao lililofanyika jijini Mbeya chini ya kampeni ya Nje ya Dimba na Stars inayoendeshwa na bia ya Serengeti Lager.
Baadhi ya mashabiki wa Taifa Stars mkoani Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo ya taifa, muda mfupi baada ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na bia ya Serengeti Lager ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Taifa Stars’.

Bia ya Serengeti Lager leo imewakutanisha uso kwa uso baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars na mashabiki katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Mbeya ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars

Kampeni ya 'Nje ya Dimba na Stars' inalenga kuwapa nafasi mashabiki wa Taifa Stars kukutana na nyota wanaowapenda katika baa zao na pia watapata fursa ya kuwauliza maswali kuhusu maisha yao nje ya soka pamoja kupiga nao picha za ukumbusho. Kampeni hiyo ya nchi nzima itadumu kwa miezi mitatu.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, meneja masoko wa kanda za juu kusinini wa SBL Denis Tairo alisema bai ya Serengeti lager ikiwa kama shabiki mkuu wa Taifa Stars inajivunia kuwaletea mashabiki wa Taifa Stars mkoani Mbeya nyota inaowapenda na kuwapa nafasi kuzungumza nao na hivyo kuwafahamu kwa undani zaidi.

Shabiki mkuu na mdhamini wa timu yetu ya taifa, Taifa Stars Bia ya Serengeti Lager leo amewakutanisha mashabiki wa hapa Mbeya uso-kwa-uso na nyota ambao mara nyingi wamekuwa wakiwaona uwanjani. Hii ni fursa pekee ya mashabiki kujua maisha ya nota wao nje ya uwanjani,” alisema

Denis alisema kampeni hiyo ya nchi nzima itahusisha wachezaji wa Taifa Stars ambapo watatembelea mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha na kukutana na mashabiki wao kupitia matukio kama pati za mwisho wa mwezi ‘Nje ya Dimba na Stars’. Kwenye matukio kama hayo mashabiki wataweza pia kujishindia zawadi mbali mbali na ofa za bei yao pendwa ya Serengeti lager.

"Wachezaji watakuwa kwenye baa mbali mbali na wakati wateja wetu wa bia ya Serengeti Lager wakiendelea kuburudika na bia yao pendwa iliyotengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na isyoongezwa sukari, watapata nafasi ya kuwauliza maswali, kupiga picha na kupata sahihi zao,” alisema

Aliwataka mashabiki wa Stars kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya bia ya Serengeti Lager Pamoja na kusikiliza redio kwa ajili ya kujua linin a wapi nyota wa taifa Stars watakuwa.
Share:

Tuesday, November 30, 2021

MSTAHIKI MEYA JIJI LA ARUSHA MGENI RASMI KONGAMANO LA FURSA SEKTA YA MUZIKI

 
Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maximillian Iranghe.
Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel.
Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha Dkt. Christina Ngereza.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara Dkt.Noelia Myonga.
Mdau wa maendeleo hapa nchini Dkt.John Lucian anatarajiwa kuwepo kwenye kongamano hilo.
Wasanii kutoka Cultural Arts Center Makumira University ni miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani kwenye kongamano hilo.
Wasanii kutoka Cultural Arts Center Makumira University ni miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani kwenye kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale, Arusha | MSTAHIKI Meya wa jiji la Arusha Maximillian Iranghe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Fursa katika Sekta ya Muziki na Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru ambayo yameandaliwa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha kwa kushirikiana na Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO).

Kongamano hilo litakuwa la siku tatu na kufanyika katika makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha kuanzia Desemba 7, 2021 hadi Desemba 9, 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwa wanamuziki wataimba nyimbo mbalimbali za zamani na za sasa uliotumika katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru ambao ulichangia kuhamasisha maendeleo.

Alisema Mstahiki Meya amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo ambalo baadhi ya watu maarufu kutoka ndani na nje ya jiji la Arusha wamealikwa.

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha Dkt. Christina Ngereza alisema wameandaa kongamano hilo ili kutoa elimu na fursa mbalimbali zilizopo katika urithi wa muziki wa Tanzania ambao umebadilika sana katika miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.

Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard alitaja fursa zitakazo patikana siku hiyo kuwa ni kutolewa Bima ya Afya NHIF kwa gharama nafuu kwa ajili ya vipimo na matibabu kwa wanamuziki ambavyo vitatolewa kwenye Hospitali za Serikali na za binafsi.

Alisema kutakuwa na fursa lukuki kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na fursa za kibenki na nyingine nyingi.

Richard alisema Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na COSOTA watakuwepo kutoa elimu na usajili wa wanamuziki.

Joel alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali wa muziki kufika kwenye kongamano hilo na kuwa huduma ya chakula na vinywaji itapatika kwa gharama nafuu.

Wadau wengine walioalikwa kwenye kongamano hilo ni pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara Dkt.Noelia Myonga na mdau wa maendeleo hapa nchini Dkt.John Lucian.
Share:

Thursday, November 25, 2021

ABSA STARS AMONG RALLY OF IRINGA 2021 KEY MOVERS

 
Absa Bank Iringa Branch Manager, Sheillah Kajuna, flags-off to officially launch Rally of Iringa 2021 in Iringa recently. Absa was among key supporters facilitating the race. With her is the regions rally club patron and former Iringa DC, Richard Kasesera.
Absa Bank Iringa Branch Manager, Sheillah Kajuna (right) listens to a former Iringa District Commissioner, Richard Kasesela during the opening session of rally of Iringa 2021 in Iringa recently. Absa was among key supporters of the contest. On Kasesela's right are, Iringa rally club chairman, Amjad Khan, Kalenga legislator, Jackson Kiswaga and Iringa Regional Acting Fire and Rescue force Commander, Inspector, Peter Mziwanda.
Absa Bank Iringa Branch Manager, Shailla Kajuna (centre), greets Kalenga Constituency MP, Jackson Kiswaga, during the official flag-off of the Rally of Iringa 2021 in Iringa recently. Absa was among key supporters for the contest. Looking on is former Iringa DC and region's rally club patron, Richard Kasesera.
Iringa Rally Club Chairman, Amjad Khan (right), presents a certificate of appreciation to Absa Bank Iringa Branch Manager, Sheillah Kajuna, reciprocating the financial transnational's support in the Rally of Iringa 2021 contest which roamed in the region recently.
Absa Bank Iringa Branch Manager, Sheillah Kajuna (left), confers a medal for long-time rally participation to veteran driver, Depak Kotak, at the just-ended Rally of Iringa 2021, held in Iringa, which featured Absa among its key supporters.
One of the cars taking part in the Rally of iringa 2021 is daringly steered in a hair-raising manoeuvre.

Share:

Wednesday, October 7, 2020

BENKI YA CRDB YADHAMINI LIGI YA TAIFA YA MPIRA WA KIKAPU

Benki ya CRDB imetangaza udhamini wa shilingi milioni 200 kwa ligi ya mpira wa kikapu ya taifa 2020 itakayofanyika Dodoma katika viwanja vya Chinangali kuanzia tarehe 12 Novemba na kilele chake ni 21 Novemba, 2020. 

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa amesema benki hiyo imefikia makubaliano na Shirikisho la Taifa la Mpira wa Kikapu (TBF) ya udhamini wa ligi hiyo ya taifa ya mpira wa kikapu ambayo imepewa jina la “CRDB Bank Taifa Cup”.

Mwambapa alisema udhamini wa ligi hiyo ya taifa ya mpira wa kikapu ni muendelezo wa jitihada za Benki ya CRDB katika kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia michezo. Aliongezea kuwa Benki hiyo kupitia sera yake ya Uwezeshaji katika Jamii (CSI Policy) imekuwa ikiwekeza katika michezo ya vijana kwa kuamini kuwa inasidia kuongeza ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.


Akizungumzia kuhusu msukumo uliopelekea Benki hiyo kudhamini ligi hiyo ya taifa ya kikapu yenye kauli mbiu ya “Ni Zaidi ya Game, Ni Maisha”, Mwambapa alisema mchezo wa mpira wa kikapu umekuwa haupewi sana kipaumbele kulinganisha na michezo mingine, Hivyo kupelekea kiwakatisha tamaa vijana wengi ambao wamekuwa wakionyesha vipaji katika mchezo huo.

CRDB Bank Taifa Cup” inakuja kuleta hamasa si tu kwa vijana na wapenzi wa mpira wa kikapu bali kwa Watanzania wote kwa kuwaonyesha umuhimu wa kuwekeza katika michezo ya vijana na fursa zilizopo ikiwamo ajira,” alisema Mwambapa.

Mwambapa alisema mbali na zawadi zitakazokuwa zikitolewa kwa timu zitakazofanya vizuri katika “CRDB Bank Taifa Cup”, Benki ya CRDB pia imetenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya “Scholarship” kwa wachezaji watakaofanya vizuri.


Tutakuwa pia na zawadi kwa ajili ya wapenzi wa mpira wa kikapu katika kila hatua za mashindano. Niwaombe watanzania waanze kutufuatilia kupitia Azam TV na mitandao yetu ya kijamii kujua namna ya kushiriki,” aliongezea Mwambapa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Mike Mwita aliishukuru Benki ya CRDB kwa kudhamini ligi hiyo ya taifa ya mpira wa kikapu huku akisema udhamini huo utaongeza mapenzi ya mpira wa kikapu kwa vijana kama ilivyo kwa mpira wa miguu na michezo mingine.

Mwita alisema: "Tunafurahi sana kwa udhamini na ushiriki thabiti wa Benki ya CRDB katika jitihada hizi zinazolenga kukuzwa kwa mpira wa kikapu nchini. Sio tu kwamba udhamini wa Benki ya CRDB utaboresha kiwango cha ligi, lakini pia utavutia Watanzania wengi kufuatilia mchezo huu na kuhamasisha vijana wengi kushiriki."


Naye Msimamizi wa vipindi vya michezo Azam TV, Michael Maluwe amewataka Watanzania kuanza kufuatilia CRDB Bank Taifa Cup kupitia chaneli ya michezo ya Azam Sports 2, ambapo Benki hiyo imeanzisha kipindi maalum kuelekea mashindano hayo ya mpira wa kikapu. “Azam TV itaweka kambi Dodoma kuwaletea burudani Watanzania kuelekea mashindano haya, niwakaribishe Watanzania tujiunge na Azam TV ili kuwashangilia vijana wetu,” alisema Maluwe.

CRDB Bank Taifa Cup inatarajiwa kuhusisha timu 36 za mpira wa kikapu kwa upande wa wanaume na wanawake. Mashindano hayo pia yatatanguliwa na michuano ya timu za veteran zza Benki ya CRDB, Bunge, Pazi, Bahari na timu za walemevu. Pamoja na Benki ya CRDB kuwa mdhamini mkuu, CRDB Bank Taifa Cup pia imedhaminiwa na Azam TV, kampuni ya bima ya Sanlam na kampuni ya maji ya Cool Blue.


Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive