A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, November 30, 2021

NIC Yaingia Makubaliano Ya Mkataba Wa Udhamini Wa UDSM Marathon

 
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule (kushoto) na Mkurugenzi UDSM Marathon Dk.Lulu Kaaya wakibadilishana hati za Makubaliano kwa ajili ya UDSM marathon.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule (kushoto) na Mkurugenzi UDSM Marathon Dk.Lulu Kaaya wakionesha hati za makubaliano mara baada ya kuzisaini.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule (kushoto) na Mkurugenzi UDSM Marathon Dk.Lulu Kaaya wakisaini Makubaliano ya NIC kudhamini mbio.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa NIC Yassaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini Makubaliano ya Udhamini UDSM marathon.
  • Dk.Jakaya Kikwete mgeni rasmi wa mbio
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam | RAIS Mstaafu wa awamu ya Nne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi wa UDSM Marathon zitazofanyika Desemba 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mbio hizo zimeingiwa na Makubaliano wa Mkataba wa Udhamibi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) na UDSM Marathon ambapo NIC imekuwa mdau mhimu kwa Chuo Kikuu kikongwe katika kwenda bega kwa bega.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja (NIC) Yessaya Mwakifulefule amesema wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika sekta ya michezo kwa lengo la kukuza vipaji kwa watanzania na pia katika kujenga afya ya kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza.

Amesema wana kila sababu ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa maana wamekuwa wadau wakubwa kwao katika biashara pia ndio Chuo Kikongwe nchini na kina mchango mkubwa kwa watendaji wa shirika kwa kusoma chuo hicho.

"Ni mara yetu ya kwanza kuipiga jeki UDSM Marathon na haitakuwa mara ya mwisho kufanya hivyo, tutaendelea kushirikiana kama ambavyo wamekuwa wadau wakubwa kwetu kwa muda mrefu tangu shirika lilivyoanzishwa". Amesema Bw.Mwakifulefule.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa UDSM Marathon Lulu Kaaya amesema katika mbio hizo wanatarajia kuwepo k mgeni rasmi Dkt.Jakaya Kikwete pia atashiriki kukimbia Kilomita 5.

Amesema mbio hizo zitakuwa na ruti kubwa tatu ambazo ni ruti ya Kilomita 21.ruti ya kilomita 10 na ruti pamoja na kilomita 5.

'Lengo kuu la mbio hizi ni kwa ajili ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kuboresha maisha ya wanachuo. Kwasasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo katika ujenzi wa kituo cha wanafunzi (Student Center) inayojengwa kwenye Campus ya Mwalimu Nyerere Mlimani Jijini Dar es Salaam ambacho ni mahususi kwa kutoa mazingir mazuri ya mapumziko kwa wanafunzi". Amesema
Share:

EPUKENI VITENDO VYA RUSHWA NA WIZI WA DAWA

 
  

Na. WAMJW – Dar es Salaam | Wafamasia nchini wametakiwa kusimamia miiko na maadili ya taaluma yao katika vituo vyao vya kazi na kuepuka vitendo viovu ikiwemo wizi wa dawa na ulaji rushwa.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Brig. Jen. Dkt. Gabriel Sauli Mhidize, alipo muwakilishai, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel Katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Fundi Dawa Sanifu na Fundi Dawa Wasaidizi (TAPHATA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mhidize kupitia ujumbe wa Naibu waziri wa Afya amesema, mkutano huo wa wana taaluma wote wa famasia wanatakuwa kuyafanyia kazi yote watakayo jifunza.

Naamini mtaenda kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za nchi katika kufikia lengo la utoaji wa huduma bora za Afya nchini” amesema Dkt. Mhidize

Kwa upande wake Msajili Baraza la Famasi, Elizabeth Shekalaghe ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya iweke miongozo itakayotoa maelekezo kwenye sekta zote (binafsi na Serikali) kuwa na Wataalamu sahihi wa dawa katika ngazi za zahanati, vituo vya Afya na Hospitalini.

Bi.Shekalaghe amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza Ajira kwa kada za wafamasia na zitasaidia kuboresha utoaji sahihi wa huduma bora za Afya nchini.

Tukiwa tunaenda kwenye uchumi wa viwanda kwa kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, tunaomba viwanda vilivyopo nchini kuajili Wataalamu sahihi ili kuboresha uzalishaji wa dawa” amesema Shekalaghe.

Aidha, Bi.Shekalaghe ameiomba Wizara ya Afya kupitia taasisi zake kupitia upya viwango vya madaraja ya ufaulu wa kujiunga na vyuo vinavyotoa kozi ya Fundi Dawa Sanifu na Fundi Dawa Wasaidizi ili kupata Wataalamu sahihi na wenye uwezo wa kutoa huduma.

Mkutano huo utadumu kwa siku mbili kuanzia 29-30 mwezi wa 11, 2021 na umewashirikisha Wana taaluma wa ufamasia kutoka Tanzania Bara
Share:

RC MAKALLA AIPA MAMBO MATANO TMDA KUDHIBITI WIZI WA DAWA NA DAWA BANDIA

 
  • Awataka Kudhibiti Wizi wa Dawa za Serikali na kutokomeza Dawa Bandia.
  • Asisitiza kufanyika kwa ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kudhibiti wezi wa dawa Na dawa bandia.
  •  Ataka "vishoka" ambao ni wakaguzi feki kukomeshwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameielekeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA kupatia ufumbuzi tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali na kutoa onyo kwa Maduka yanayonunua dawa za Wizi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Mafunzo ya siku tano kwa Wakaguzi wa Dawa wa Manispaa za Mkoa huo yaliyolenga kuwajengea uelewa wa maadili ya kazi na utambuzi wa dawa Bandia ili kuongeza ufanisi kwa faida ya watumiaji wa dawa.
Aidha RC Makalla amewataka Wakaguzi wa Dawa kuzingatia Weledi na maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo Kutokana na unyeji wa kazi hiyo ambayo inabeba dhamana ya Maisha na uhai wa Wananchi.

Hata hivyo RC Makalla ametaka Mamlaka hiyo Kudhibiti tatizo la Vishoka Wanaofanya ziara za ukaguzi kwenye Maduka huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa Maduka ya dawa.

Pamoja na hayo RC Makalla ameitaka Mamlaka hiyo kuweka utaratibu wa kufanya ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kubaini wababaishaji na kutaka uwepo wa watoa huduma Wenye sifa na Vigezo.
Share:

MNUFAIKA WA TASAF RUNDUGAI ASOMESHA MTOTO CHUO CHA USAFIRISHAJI (NIT)

 
Mwanaasha Mtei ambaye ni mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika kijiji cha Rundugai Wilayani Hai kujionea manufaa waliojipatia wanufaika wa mradi huo leo mkoani Kilimanjaro.
Mwanaasha Mtei ambaye ni mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wake wakati waandishi wa habari walipotembelea katika kijiji cha Rundugai Wilayani Hai kujionea manufaa waliojipatia wanufaika wa mradi huo leo mkoani Kilimanjaro.
Haya ni mabaji ya nyumba yake ya udongo iliyoezuliwa na upepo na kuanguka kisha baadaye akaanza kujenga nyumba nyingine mpya kwa matofali ya saruji kwa kuwezeshwa mtaji wa biashara ndi=ogondogo na TASAF.
Mtendaji wa kijiji cha Rundugai Kata ya Mnadani wliaya ya Hai Bw. Descory Mvungi akiwakaribisha waandishi wa habari na maofisa wa TASAF waliotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kuzungumza na wanufaika wa mradi huo wa kaya maskini kulia ni Charles Boniface Kodema Mwenyekiti wa kijiji cha Rundugai.
Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa TASAF waliotembelea katika kijiji hicho wakipata taarifa ya mradi huo kutoka kwa mtendaji wa kijiji Bw. Descory Mvungi.

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro | Mwanaasha Mtei ambaye ni mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) aliyekuwa anakula mlo mmoja kwa siku baada ya kutelekezwa na mume wake akiwa na watoto sita ameondokana na hali ya utegemezi na kuweza kumsomesha mtoto wake wa kiume Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.

Akizungumza Kijiji kwake Rundugai Masana Hai Mkoani Kilimanjaro Mwanaasha amesema, TASAF ilimuwezesha fedha ambazo amezitumia kuanzisha biashara inayomuwezesha kuendesha maisha yake huku akiwahudumia watoto wake.

Akifafanua amesema baada ya maisha kuwa magumu mume wake alimkimbia akiwa na ujauzito ambapo kupitia fedha hizo alianzisha miradi ya ufugaji kuku na mbuzi na kufanya biashara ndogondogo, ambapo kupitia mbuzi ameweza kulipa ada ya mtoto wake Shilingi 800,000 ikiwa ni kwa muhula wa kwanza.

Kabla ya mradi huu mimi na watoto wangu tulikuwa hatuna hata nguo za kuvaa, nikitaka kutoka ni lazima nikaazime nguo na nikirudi nizirudishe, lakini kupitia fedha za TASAF sasa nina nguo katika kabati langu,” amesema Mwanaasha.

Lakini Mwanaasha sasa amekumbana na janga lingine, nyumba yake aliyokuwa ameijenga kupitia uwezeshaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii imekumbwa na upepo mkali na kuanguka, sasa ujenzi wa nyumba nyingi upo katika hatua ya renta na amekwamia hapo kutokana na kutumia fedha zote kwa ajili ya kulipa ada ya mtoto.

Ombi lake kwa mradi huo na wadau wengine ni kumwezesha aweze kumalizia nyumba hiyo ili ahame katika nyumba ya hifadhi anayoishi sasa.

Akizungumzia Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hai Dionis Muyinga amesema wametenga zaidi ya Milioni 140 kuwezesha kaya maskini.

Akifafanua amesema baadhi ya kaya ambazo zimewezeshwa zimeshajikwamua na umaskini kwa kujenga nyumba, kuanzisha miradi ya biashara na mifugo inayowaingizia vipato.
Share:
 
Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani (wa pili kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya wa Taasisi ya Vijana ya Sisi ni Tanzania baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika Manispaa ya Singida mwishoni mwa wiki.
Viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho.

Na Dotto Mwaibale, Singida | VIJANA Nchini wametakiwa kujivunia miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika kwani ndio umeliletea Taifa maendeleo tuliyo nayo.

Hayo yamesemwa na Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani wakati akizungumza na viongozi wa mkoa na wilaya wa Taasisi ya Vijana ya Sisi ni Tanzania katika kikao kilichofanyika Manispaa ya Singida mwishoni mwa wiki.

"Sisi vijana tunapaswa kutambua kazi kubwa ya waasisi wa Taifa letu kwa pande zote za Muungano wa Jamhuri,Wazee wetu kama Julius Nyerere, Abeid Karume na Bibi Titi Mohammed walivyopigania Uhuru kwa nguvu zote na kutuunganisha ambapo hadi sasa tunafurahia matunda ya juhudi zao" alisema Ndahani.

Alisema wajibu wa vijana ni kuendelea kuulinda Uhuru wetu, kudumisha amani, upendo , mshikamano ,umoja na kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa lenye nguvu na uwezo wa kiuchumi.

Ndahani alisema tunapoadhimisha Miaka 60 ya Uhuru yapo mafanikio makubwa katika Nyanja za kiuchumi, kisasa,kiutamaduni na kijamii hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwashukuru viongozi wa awamu zote Sita katika kuliletea Taifa mafanikio makubwa ndani ya miaka 60.

Alisema vijana wengi wamepata elimu ya msingi, sekondari, vyuo vikuu na vya kati kwa sababu Serikali imeongeza idadi ya shule na vyuo ukilinganisha kipindi cha kabla ya uhuru, hivyo ni lazima vijana wajivunie Miaka 60 ya Uhuru.

Kwa upande wao vijana hao wameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapatia fursa za kiuchumi na mafunzo kupitia Programu ya uanagenzi inatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wamesema wataendelea kuiunga mkono Serikali ili kutekeleza ilani ilitolewa Kwa Wananchi Kwa miaka mitano.
Share:

COCA-COLA YAZINDUA KAMPENI YA 'MAAJABU HALISI' KWA MARA YA KWANZA NCHINI TANZANIA

 
Meneja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto) akizungumzia juu ya uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Akifuatilia kwa makini kulia ni Meneja Mkuu wa Shughuli za Biashara wa Kampuni ya Coca-Cola, Hellen Masumba. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Mkurugenzi wa Masuala ya Umma na Mawasiliano wa Coca-Cola Kwanza Tanzania, Salum Nassor, akizungumzia juu ya uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Mtangazaji wa kituo cha luninga cha Clouds TV, Shadee Weris akiwa amepozi kwa furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz (kulia) akiwa amepozi kwa furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Flava, Rosa Ree (kulia) pamoja na wa ‘kudensi’ Angel Nyigu wakiburudisha kwa mbwembwe wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Meneja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kulia) pamoja na Meneja wa Masoko ya Biashara wa Coca-Cola Kwanza Tanzania, Wahda Mbaraka (kushoto) katika picha ya furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM, B Dozen (kulia) akiwa amepozi pamoja na watangazaji wenzake, kutoka kushoto ni Kevoo wa kipindi cha Skonga cha EATV na Idris wa Kitaa wa kipindi cha mashamsham cha Wasafi FM, wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.

Kampuni ya Coca-Cola Tanzania imezindua kampeni mpya inayojulikana kama ‘Maajabu Halisi’, ambayo inamkaribisha kila mtu kusherehekea nyakati tofauti muhimu na za kusisimua kama binadamu.

Kampeni hii inaipa uhai ahadi ya kampuni – ambayo ni kuunganisha na kuwainua watu kila siku – kitu ambacho kinaendana na hali tunayoiishi kwa sasa duniani. Miezi 18 iliyopita ilikuwa na mafunzo mengi: miongoni mwake ni kwamba tunaweza kufurahia kwa pamoja nyakati muhimu tofuati miongoni mwetu pale tunapoungana na kushirikiana katika hali tusiyoitarajia na kutuinua kila siku kwa namna ya kipekee. Lakini pia inatambua changamoto wanazokumbana nazo kizazi cha sasa kutafuta namna bora ya kuishi maisha halisi badala ya kidigitali ambayo kwa asilimia kubwa kimeyazoea.

Tunapozindua kampeni hii ya ‘Maajabu Halisi’ Tanzania, dhumuni letu kuu ni kuwashirikisha na kusherehekea kwa Pamoja nyakati muhimu na za kusisimua kwenye Maisha yetu tofauti ya kila siku na watumiaji wa bidhaa zetu nchini kote ili kuwainua na kuwaunganisha,” alisema Unguu Sulay, Mkurugenzi Mtendaji, Coca-Cola Kwanza Tanzania.

Kwa zaidi ya miaka 100, dhima ya Coca-Cola imekuwa ni kusambaza matumaini ambapo kampeni ya ‘Maajabu Halisi’ imekuja kuendeleza ahadi hiyo. Tunaamini kwamba falsafa yake itaendana na watu wote duniani: kwamba wote tunaweza kuwa na nyakati za muhimu na za kusisimua katika Maisha yetu halisi iwapo tutajumuika na kushirikiana kwa Pamoja. Kupitia kampeni hii tutaunganisha na kusherehekea utofauti wa Maisha ya watumiaji wa bidhaa zetu nchini Tanzania kwa kushirikiana na wasanii na wahamasishaji tofauti, kwa lengo la kuwainua na kuwaunganisha watu kwenye nyakati halisi na za kusisimua,” aliongezea Sulay.

Maajabu Halisi’ imekuwa kampeni ya kwanza kuzinduliwa na Coca-Cola duniani kote tangu mwaka 2016 ambapo imezinduliwa Pamoja na utambulisho mpya wa Coca-Cola, vilevile na mtazamo mpya kwenye chapa ya Coca-Cola ambayo itahusisha shughuli zote za kimasoko za Coca-Cola. Ikiwa imehamasishwa na kifungashio maarufu cha Coca-Cola, mwonekano wa ‘Kumbato’ ni matokeo ya mabadiliko madogo kwenye chapa iliyozoeleka ambayo yanatoa tafsiri ya kufurahia na kusherehekea nyakati tofauti muhimu na za kusisimua katika shughuli zote za kimawasiliano za Coca-Cola.

Kampeni hii pia itakuwa imebeba kampeni nyingine inayojulikana kama ‘One Coke Away From Each Other,’ ambayo imetengenezwa kwa ajili ya na, jamii inayohitaji kitu tofauti zaidi tofauti na kile ambacho inakitegemea kutoka Coca-Cola. Katika kutengeneza kampeni hii, kampuni imeshirikiana na wasanii, wabunifu, na wahamasishaji wengine tofauti.

Coca-Cola inashirikiana na wasanii, na wahamasishaji mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ili kuipeleka dhana ya ‘Maajabu Halisi’ katika Maisha halisi kupitia chapa yenye muonekano wa ‘kumbato.’ Kupitia utofauti na ubunifu wao, wataweza kuzifanya nyakati za muhimu na kusisimua za kila siku kuwa kwenye uhalisia ambazo ni jumuishi na kuleta umoja, lakini pia zitajipambanua na kuzingatia utofauti.

‘Maajabu Halisi’ si maneno tu ya kawaida au kampeni ya mara moja: ni falsafa na Imani ya muda mrefu ya kampuni ambayo itaziendesha na kuziongoza shughuli za masoko na mawasiliano katika nyote zote za kibiashara za Coca-Cola.

Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote. Hii itajumuisha kwenye maduka, majumba ya sinema, na maduka makubwa ya manunuzi, kukiwa na ofa kabambe kwa ajili ya wateja.

Haya yote yatafikia kilele kwa shamrashamra kadha wa kadha kama vile msafara wa Coca-Cola wa Christmas, kuwepo kwa miti ya Christmas sehemu tofauti za wazi Pamoja na kuzipeleka nyakati za kipekee na kusisimua kwa wasafiri katika mabasi ya umma na kwa wale watakaosafiri kwa treni ili kuwa na wapendwa wao maeneo tofauti ya nchi wakati wa msimu wa sikukuu.

Kupitia kampeni ya ‘Maajabu Halisi,’ lengo kubwa ni kuwashirikisha watu kwa namna ya kipekee kabisa kupitia matukio tofauti ambayo yatawaacha wakiwa na kumbukumbu nzuri katika Maisha yao. Wateja wetu Tanzania kote watajionea na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kusisimua kupitia bidhaa tofauti za Coca-Cola zenye chapa yenye mwonekano unaofanana na ‘kumbato’ kipindi chote cha kampeni.

Kuendelea kuwaunganisha watumiaji wa bidahaa zetu na kampeni, tumejipanga kwa shughuli zikiwemo, matukio ya kushtukiza kutoka kwa wasanii na watu maarufu tunaoshirikiana nao ambao watajumuika na wateja katika matukio tofauti miongoni mwa mengi tukayokuwa tukiyafanya,” alisema Kabula Nshimo, Meneja Mwandamizi wa Coca-Cola Tanzania.
Share:

DC IKUNGI AOMBA KUMUOMBEA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi Yahaya Njiku (katikati) akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro, kuashiria uzinduzi wa Album ya Kwaya ya Malezi ya Vijana Usharika wa Emanueli Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Singida juzi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi Yahaya Njiku (katikati) akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro, katika uzinduzi wa Album hiyo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi Yahaya Njiku (kushoto) akiwa kwenye hafla hiyo.
Vijana Gospel Choir wakitoa burudani wakati wa uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale, Singida | MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Jerry Muro ametoa maombi ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kuliongoza Taifa kwa utulivu na amani.

Hayo yalisemwa juzi kwa niaba yake na Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung'unyi Yahaya Njiku katika hafla ya uzinduzi wa Album ya Kwaya ya Malezi ya Vijana Usharika wa Emanueli Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati.

DC Muro alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo lakini kutokana na majukumu mengine aliwakilishwa na Afisa Mtendaji huyu Yahaya Njiku.

"Ndugu zangu niwaombe na kuwasihi wote tuliopo katika hafla hii tuendelee kumuombea Rais wetu Samia Suluhu Hassan aendelee kuliongoza Taifa letu kwa amani na utulivu" alisema Njiku.

Pia Njiku aliwaomba waumini waliokuwepo kwenye hafla hiyo kuiombea Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake kwa jinsi ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo na kuhimiza umoja wa kitaifa na kukuza diplomasia na nchi zingine.

Njiku aliwapongeza vijana wa kanisa hilo kwa namna walivyo wa moja kwa kueneza neno la mungu kupitia uimbaji.

Alitumia nafasi hiyo kumshukuru Askofu Msaidizi wa Kanisa hilo, Katibu Mkuu wa Dayosisi, Mchungaji wa Usharika na viongozi wa usharika hui kwa ujumla katika kushiriki kwao hadi kukamilisha album hiyo.

Uzinduzi huo ulifanyika juzi Jumapili katika Kanisa la KKKT ( Msalaba mrefu) Singida mjini ambapo Vijana Gospel Choir walizindua album yao inayoitwa 'Wewe ni Mshindi'
Share:

MSTAHIKI MEYA JIJI LA ARUSHA MGENI RASMI KONGAMANO LA FURSA SEKTA YA MUZIKI

 
Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maximillian Iranghe.
Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel.
Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha Dkt. Christina Ngereza.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara Dkt.Noelia Myonga.
Mdau wa maendeleo hapa nchini Dkt.John Lucian anatarajiwa kuwepo kwenye kongamano hilo.
Wasanii kutoka Cultural Arts Center Makumira University ni miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani kwenye kongamano hilo.
Wasanii kutoka Cultural Arts Center Makumira University ni miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani kwenye kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale, Arusha | MSTAHIKI Meya wa jiji la Arusha Maximillian Iranghe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Fursa katika Sekta ya Muziki na Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru ambayo yameandaliwa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha kwa kushirikiana na Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO).

Kongamano hilo litakuwa la siku tatu na kufanyika katika makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha kuanzia Desemba 7, 2021 hadi Desemba 9, 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwa wanamuziki wataimba nyimbo mbalimbali za zamani na za sasa uliotumika katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru ambao ulichangia kuhamasisha maendeleo.

Alisema Mstahiki Meya amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo ambalo baadhi ya watu maarufu kutoka ndani na nje ya jiji la Arusha wamealikwa.

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha Dkt. Christina Ngereza alisema wameandaa kongamano hilo ili kutoa elimu na fursa mbalimbali zilizopo katika urithi wa muziki wa Tanzania ambao umebadilika sana katika miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.

Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard alitaja fursa zitakazo patikana siku hiyo kuwa ni kutolewa Bima ya Afya NHIF kwa gharama nafuu kwa ajili ya vipimo na matibabu kwa wanamuziki ambavyo vitatolewa kwenye Hospitali za Serikali na za binafsi.

Alisema kutakuwa na fursa lukuki kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na fursa za kibenki na nyingine nyingi.

Richard alisema Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na COSOTA watakuwepo kutoa elimu na usajili wa wanamuziki.

Joel alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali wa muziki kufika kwenye kongamano hilo na kuwa huduma ya chakula na vinywaji itapatika kwa gharama nafuu.

Wadau wengine walioalikwa kwenye kongamano hilo ni pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara Dkt.Noelia Myonga na mdau wa maendeleo hapa nchini Dkt.John Lucian.
Share:

I&M BANK LAUNCHES A NEW RELOCATED BRANCH IN ARUSHA

 
The Arusha Regional Commissioner, John Mongella unveils the new I&M Bank relocated branch in Arusha yesterday. Behind him, is the Bank Chief Executive officer, Mr. Baseer Mohammed and the Retail Banking Manager, Ms. Lilian Mtali. The branch will provide a range of services including the Select Banking for affluent clients.
The Arusha Regional Commissioner, John Mongella speaks during unveiling of the newly relocated branch in Arusha yesterday. The branch will provide a range of services including the Select Banking for affluent clients expecting to boost business operations in the region.
The Arusha Regional Commissioner, John Mongella in a jovial mood with I&M Bank CEO, Mr. Baseer Mohammed and the Retail Banking Manager, Ms. Lilian Mtali during unveiling of the newly relocated branch in Arusha yesterday.
  • Customers to enjoy convenience with a range of customized services including select Banking for affluent clients
Arusha. 30th November, 2021 - I&M Bank customers in Arusha will now enjoy convenience through the new relocated branch with state-of-the-art features including the Select Banking lounge for the affluent clients.

The branch was launched by the Arusha Regional Commissioner, John Mongella witnessed by different leaders and stakeholders on Tuesday 30th November 2021 at the new premises.

Speaking during the opening ceremony, the Bank Chief Executive Officer, Baseer Mohammed said the move aimed at ensuring easy accessibility of bank’s services to the customers in the region.

This initiative aimed at bringing convenience to our customers since the new branch is in city center offering easy accessibility. This branch has state-of-the-art features including the Select Banking Lounge that will serve the affluent clients, modern facilities, and safe deposit lockers, bureau de change etc. this is all to ensure that our customers are enjoying the banking experience while visiting our newly relocated branch” he said.

The bank has so far opened 8 branches located in Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, and Arusha and would be expanding to more strategic locations. The bank has been a pioneer in driving the digital strategy agenda in the country with introduction of unique products like WhatsApp Banking, Kamilisha (Digital Lending) and Multicurrency VISA prepaid Cards.

There has been an increase of total assets of the bank by 11.2% on year-on-year basis recording TZS. 567 billion by end of October 2021. During the year the Net advances increased by 12.3% and Customer deposits by 19% so far. The Bank has been consistently delivering profit over the years.

The branch is now situated at Goliondoi Street, Sunda Plaza from Jakaranda Street, Falcon Building where it was located before. The new strategic location is expected to speed up business operations in the region.

The Regional Commissioner commended the move by the bank arguing that it will boost economic activities among residents and foreigners who are mostly tourists.

Banking services are very essential in national economic growth; this initiative is a clear sign that the sector is stable and continues to grow every day. Having this modern branch here will speed up business movements, tourism activities and most importantly revenue collection,” he said.

The RC also appreciated the bank for introducing Select Banking Service for affluent client saying that it will boost business operations given the nature of the region that is full of business activities like tourism and mining.

We have also launched a bureau de change that will be available for long hours to allow Arusha residents and tourists to get the service anytime. Also, we our Safe Deposit Lockers service will help customer to safely keep their valuables and documents,” marked Lilian Mtali, the bank’s Retail banking Manager.

About I&M Bank Tanzania Limited

I&M Bank Tanzania is part of the I&M Group PLC, one of the fast growing commercial bank, offering a full range of Corporate, Business, Premium and Personal banking services.

Established in 1974, I&M Bank is wholly owned by I&M Group PLC which is listed on the Nairobi Stock Exchange and has a growing regional presence currently extending to Mauritius, Rwanda, Tanzania and Uganda. The Group lists CDC, which is a leading European Development Financial Institutions amongst its main shareholders. I&M prides itself on its strong values and key strengths of innovative service and strong customer relationships. I&M Group aspires to be Eastern Africa’s Leading Financial Partner of Growththrough offering innovative and market driven banking solutions for its target segments.

For more information visit www.imbank.co.tz

I&M Bank Media Contact

Anitha Pallangyo
Manager, Marketing and Communications
+ 255 689791060
Share:

MAMILIONI YA WATU WAISHIO VIJIJINI WANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA SBL KWENYE MAJI SAFI NA SALAMA

 
Upatikanaji wa maji umekuwa mwiba kwa baadhi ya maeneo ya nchi, ambapo watu hupita siku kadhaa bila kuyapata huku wengine wakikabiliwa na mgao. Halikadhalika, Serikali imeshatoa hali ya tahadhari kwa watumiaji huku Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) ikiwaomba watumiaji kuhifadhi maji kila yanapotoka. Hii ni kutokana na upungufu wa kina cha maji katika maeneo ya Ruvu Juu na Mto Wami, changamoto inayosababishwa na ukosefu wa mvua.

Hata hivyo, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso amewahakikishia Watanzania kuwa ofisi yake inachukua kila hatua ili kukabiliana na hali hiyo. Aidha, Waziri alisema wamekuwa wakifanya mageuzi makubwa ya kitaasisi, kifedha na kiufundi ili kupata huduma ya maji iliyo endelevu. Alisema, 'hadi sasa kuna wakala wa usambazaji maji vijijini wapatao 2,115 unaojumuisha wahasibu 1,362 na wataalam 1,611 katika maeneo ya vijijini’.

Wakati hayo yote yakiendelea, kampuni pendwa ya bia, Serengeti Breweries Limited (SBL) iko mstari wa mbele kuwekeza katika miradi ya maji safi na salama kwa mamilioni ya wakazi wa vijijini nchini Tanzania. Miradi hii ya maji imepewa jina, Water of Life, wenye lengo la kuchochea jumuiya yenye maendeleo endelevu. Mpango huu umeanishwa kwenye mkakati wake wa maendeleo wa muda mrefu unaoitwa Society 2030; Spirit of Progress.

Tangu mwaka 2010, SBL imetumia zaidi ya TZS 1.1bn/- kuchimba visima 18 nchini kote, jambo ambalo limechangia kupunguza uhaba wa maji nchini. SBL pia imeshirikiana na mashirika mengine kwenye ujenzi wa miradi hiyo ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata maji safi na salama katika baadhi ya maeneo yenye uhitaji zaidi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya SBL, John Wanyancha alisema kuwa SBL inachukulia maji kuwa jambo muhimu sana kwenye ustawi wa jamii, na ndiyo maana inashirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendeleo kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama nchini.

Mwaka huu SBL ilizindua mradi wa maji wenye thamani ya Tsh milioni 220 katika kijiji cha Machochwe wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwenye jitihada zake za kupeleka maji safi na salama vijijini. Mradi huu na uwezo wa kuhudumia watu zaidi ya 12,000. Mradi huu pia unajumuisha kisima na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nguvu ya jua na tanki la maji linaloweza kutoa lita 7,500 za maji kwa saa.

Vilevile SBL imewekeza kwenye mikoa mingine ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwapatia wanufaika zaidi ya milioni moja maji safi na salama. "SBL imeweka sera ya makusudi kusaidia ustawi wa jamii yetu Maji ikiwa ni mojawapo la maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeainisha katika malengo yake ya kutoa msaada wa kijamii", alisema Wanyancha. Alifafanua pia vipaumbele vingine vya kampuni kama utoaji wa stadi za maisha, utunzaji wa mazingira na elimu juu ya athari ya unywaji pombe kupita kiasi.

Zaidi ya hayo, miradhi hii ya maji pia imelenga kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji wa nafaka zao kama vile mahindi, mtama na shayiri ambazo ni malighafi muhimu sana katika utengenezaji wa bia. Mfano, mwaka 2020 pekee, SBL ilipata tani 17,000 za nafaka hizi ndani ya nchi, sawa na asilimia 70 ya mahitaji ya mwaka ya malighafi ya SBL kutoka kwa mtandao wa wakulima 400. Kufikia 2025, SBL imelenga kuongeza upatikanaji wa malighafi hadi asilimia 85. SBL pia inasaidia wakulima kwa kuwapa mbegu bure, kuwapa huduma za kiufundi za shambani na kuwaunganisha na taasisi za kifedha.

Ni jambo lisilopingika kwamba SBL imeweka hatua madhubuti za kusaidia maendeleo ya jamii kama kwenye uwekezaji wa maji safi na salama hususani nyakati hizi za uhitaji mkubwa wa maji nchini. Na kwa wakazi wa vijijini uwekezaji huu umeleta faraja ukizingatia ya kuwa bado kuna baadhi ya maeneo upatikanaji wa maji umekuwa mgumu sana na vyanzo vyake kutokuwa salama kwa afya zao.
Share:

ABSA FINANCIER OF CONSUMER CHOICE AWARDS AFRICA

 
Deputy Minister for Minerals, Prof. Shukrani Elisha Manya (left), presents a certificate of appreciation to Absa Bank Tanzania Citizenship Manager, Hellen Siria, in recognition of the financial transnational's support in the Consumer Choice Awards Africa 2021, during the prize-giving episode in Dar es Salaam on Sunday. Absa has featured as the classic event's main sponsor for the two consecutive years now.
Absa Bank Tanzania Head of Treasury Execution, Nicholous Mkisi (left), presents a trophy to winner of the Most Preferred Beauty and Health Product Dealers in Tanzania category to NN General Supplies Public Relations Officer, Nosim Lefara, during the 2021 version of Consumer Choice Awards Africa prize-giving episode in Dar es Salaam on Sunday. Absa has been the lead financier of the iconic showcase for two years consecutively. From right are Tanzanian actress, musician, model and entrepreneur Hamisa Mobetto, and NN General CEO, Selina Lerafa.
Absa Bank Tanzania Head of Enterprise Operation and Service Delivery, Mabula Elias (left), presents a trophy of the Most Preferred Soft Drink Manufacturer of The Year to Hill Group Sales and Marketing Manager, Raymond Mchani during the 2021 version of Consumer Choice Awards Africa prize-giving episode in Dar es Salaam on Sunday. Absa has been the lead financier of the iconic showcase for two years consecutively. Looking on is Hill Water Marketing Officer, Calvin Flex.
Absa Bank Tanzania Head of Sales and Workplace, John Maganga (left), presents the Most Preferred Detergent Manufacturer of the Year award to Azania Group Head of Business, Joel Kaiser, during the 2021 version of Consumer Choice Awards Africa during the prize-giving episode in Dar es Salaam on Sunday. Right is Azania Legal and Compliance Manager, Mahdi Mvungi.
Absa Bank Tanzania Governance and Control Manager, Adolf Massawe (left), presents the Most Alcoholic Drink Manufacturer of the Year Award to TBL Group Commercial Director, Timea Chogo, during the 2021 version of Consumer Choice Awards Africa prize-giving episode in Dar es Salaam on Sunday. Looking on is TBL Group Trade Marketing, Doreen Tamureebire.
Innocent Mungy, a Board Member for Consumer Choice Awards Africa 2021, presents the Most Advanced Digital Banking Services in Southern Africa award to Absa Tanzania Citizenship Manager, Hellen Siria (centre), during the 2021 version of Consumer Choice Awards Africa prize-giving episode in Dar es Salaam on Sunday. Looking on is Absa Bank Head of Enterprise Operation and Service Delivery, Mabula Elias.
Absa Bank Tanzania Head of Sales and Workplace, John Maganga (left), presents the Most Preferred Food Product Manufacturing Company of the Year award to Asas Dairies Marketing Manager, Jimmy Kiwelu, during the 2021 version of Consumer Choice Awards Africa prize-giving episode in Dar es Salaam on Sunday.

Share:

Monday, November 29, 2021

TANZANIA YAPATA FURSA YA KUSAFIRISHA PARACHICHI KWENDA INDIA

 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo (wa katikati upande wa kulia) leo ameongoza timu ya wizara katika mazungumzo ya awali kuhusu rasimu ya makubaliano (MoU) kati ya Tanzania na India kuhusu fursa ya kuuza mazao ya jamii ya mikunde kama vile mbaazi kwenye soko la India.

Ujumbe kutoka India uliongozwa na Bw. Anupam Mishra Joint Secretary, Department of Consumer Affairs, na Bw. Sunil Kumar Singh, Additional Managing Director, National Agricultural Cooperative Marketing Federation of India Ltd. (NAFED), Ministry of Consumer Affairs, Food and Public Distribution. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano, ofisi ndogo za wizara ya kilimo, kilimo4, jijini Dodoma, leo tarehe 29 Novemba, 2021
 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo(wa katikati upande wa kulia)leo ameongoza timu ya wizara katika mazungumzo ya awali kuhusu rasimu ya makubaliano(MoU) kati ya Tanzania na India kuhusu fursa ya kuuza mazao ya jamii ya mikunde kama vile mbaazi kwenye soko la India. Ujumbe kutoka India uliongozwa na Bw. Anupam Mishra Joint Secretary, Department of Consumer Affairs, na Bw. Sunil Kumar Singh, Additional Managing Director, National Agricultural Cooperative Marketing Federation of India Ltd.(NAFED), Ministry of Consumer Affairs, Food and Public Distribution. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano, ofisi ndogo za wizara ya kilimo, kilimo4, jijini Dodoma, leo tarehe 29 Novemba, 2021.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive