A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Friday, January 27, 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 100 YA SARUJI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KATA YA GOWEKO

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Diwani wa kata ya Goweko Mhe. Shaban Katalambula iliyotolewa na TCB kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB, Bi Chichi Banda akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji iliyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya katika kata hiyo.
Wananchi wakishusha cement iliyotolewa na Tanzania Commercial bank kwaajili ya kumalizia ujenzi wa zahanati

TCB imeunga mkono jitihada zilizoanzishwa na wanakijiji wa kata hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Kwa muda mrefu wananchi wa kata ya Goweko wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za afya, hivyo kwa msaada toka benki ya TCB itawezesha kutatua changamoto hizo kwa wananchi hao.

Katika kuhakikisha kuwa Tanzania Commercial bank TCB inaendelea kuwakaribu zaidi na watanzania ambao ndio wateja wake wakubwa, Iimeunga mkono juhudi za Wananchi wa kata ya Goweko kwakukabidhi msaada wa mifuko 100 ya Saruji.

Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Benk ya TCB, Bi Chichi Banda alisema kuwa Tanzania Commercial Bank kama ilivyokawaida yake imeguswa na imefanya maana inaamini hawa wananchi ndio wateja wa benki.

leo tunakabidhi msaada wa mifuko 100 hapa kwaajili yakukamilisha ujenzi wa kituo cha afya lakini pia hatukuishia hapa tumekabidhi mifuko 100 mingine kwa Diwani wa Kata ya kiburugwa Mbagala Dar es salaam kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha polisi cha kata hiyo".

Pia tukatambua umuhimu wa sekta ya elimu nako tumeweza kutoa mifuko 150 ya saruji katika Shule ya Msingi Ikamba iliyoko wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwaajili yakufanya maboresho ya madarasa.

tunawapongeza sana wakazi wa hapa kwakuona kuwa swala la afya sio la serikali pekeyake hivyo sisi kama TCB tumeguswa sana tumeona tuje hapa kusaidiana na wananchi kwa hali na mali kwani nyinyi ni sehemu yetu na sisi ni sehemu yenu,"

Tanzania Commercial Bank ni benki pekee nchini yenye mtandao mpana wamatawi na mawakala nchi nzima hivyo niwasihi ndugu wananchi muitumie Benki ya TCB kwani inabidhaa bora na rafiki.
Share:

Thursday, January 26, 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA MIFUKO 150 YA CEMENT KUBORESHA MADARASA

 Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala Edward Mwoleka, (wa tatu kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilamba iliyopo Mbagala Charambe iliyotolewa na TCB kwa ajili ya kufanya maboresho ya madarasa ya shule hiyo. Kutoka kulia ni Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Gloria Mutta, Diwani wa Kata ya Charambe Twahil Shabani, pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga.

Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Mbagala, Edward Mwoleka, (wa tatu kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga, iliyotolewa na TCB kwa ajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule ya msingi Kilamba iliyopo Charambe. Kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Leah Masaba, Diwani wa Kata ya Charambe, Twahil Shabani pamoja na Mjumbe wa shule.

Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Gloria Mutta (wa tatu kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa mifuko 150 ya Cement, kwa Mtendaji kata ya Charambe, Theodora Malata iliyotolewa na TCB kwa ajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya Shule ya Msingi Kilamba iliyopo Charambe. 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilamba, Leah Masaba, akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mifuko 150 ya Cement iliyotolewa na TCB kwa ajili yakufanyia maboresho ya madarasa ya shule hiyo.

Mtendaji kaya ya Charambe, Theodora Malata akitoa shukrani kwa niaba ya shule ya Msingi Kilamba kwa uongozi wa TCB baada ya kupokea msaada wa mifuko 150 ya Cement iliyotolewa na TCB kwa ajili ya kufanyia maboresho ya madarasa ya shule hiyo iliyopo Charambe jijini Dar es Salaam.

Share:

Sunday, January 22, 2023

MATUKIO YA MAUAJI WILAYA YA MANYONI WANANCHI WAMLILIA RC SERUKAMBA AWASAIDIE

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Manyoni na Itigi katika kikao cha kusikiliza kero kilichofanyika juzi wilayani humo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

UTARATIBU wa ziara aliounzisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba kwenda kusikiliza kero za wananchi katika wilaya zote mkoani hapa zimekuwa na tija kubwa kwani zimeibua mambo mengi yakiwemo matukio ya mfululizo ya kuuawa kwa watu wilayani Manyoni.

Mauaji ya mfululizo ya watu ambao maiti zao zinaokotwa kila wiki maeneo tofauti ya Wilaya ya Manyoni yamewashtua wananchi wa wilaya hiyo ambao wamelazimika kupaza sauti kumweleza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, kumuomba aingilie kati na kuwasaidia kuliondoa jambo hilo.

Katika hali ya kushangaza,wananchi hao wamesema mauji ya watu ambayo yameibua hofu kubwa kwa jamii baadhi ya pikipiki zinazomilikiwa na askari polisi wa Manyoni kwa ajili kuendesha biashara zao ndizo zinatumika kwenye mauaji hayo.

Wananchi wa Manyoni walimweleza juzi hayo Mkuu wa Mkoa wa Singida,Serukamba ambaye alikwenda katika wilaya hiyo kusikiliza kero mbalimbali ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake zakusikiliza kero.

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa hapa Manyoni vifo vimekithiri sana kila wiki lazima tuokote maiti mahala fulani lakini sio kwamba wananchi wa Manyoni hawawafahamu wahalifu bali wanawafahamu," alisema Prisca Maleta.

Maleta ambaye wakati akizungumzia suala hilo mamia ya wananchi waliokuwa kwenye kikao hicho walikuwa wakimshangilia, alisema wananchi wanashindwa kutoa taarifa polisi kutaja wanaohusika na uhalifu huo kwasababu baadhi ya polisi sio waaminifu wanaficha siri za watoa taarifa.

"Tatizo linakuja kwa Jeshi la Polisi mimi kama Prisca ninapokwenda kutoa taarifa polisi kabla mtuhumiwa hajaenda kukamatwa wanampa taarifa kuwa fulani amekuja kukuripoti huku,vitengo hivi ndio vinasababisha vifo kuongezeka kwasababu kunakuwa na visa na visa," alisema.

Maleta alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa kuna baadhi ya askari ambao anawajua kwa sura na majina ambao wanamiliki pikipiki zao ambazo ndizo zinazoshiriki kwenye uhalifu wa mauji ya watu.

"Kuna baadhi ya askari kwa sura na majina ila siwezi kuwataja hapa ila ukihitaji nitakutajia wana pikipiki zao ambazo ndizo zinashiriki kwenye uhalifu," alisema.

Mwananchi mwingine Khalfan Zuberi Paloto alilalamikia jeshi hilo kitengo cha upelelezi kuwa mtu anapopeleka mashitaka kituoni na kufunguliwa jadala, badala ya kukutanishwa na askari mpelelezi wa kesi yake hupewa namba ya simu na kila ikipigwa muhusika husema yupo nje ya wilaya.

Mimi nilipeleka kesi ya wizi nikapewa namba ya simu ya mpelelezi nilipompigia akataka nimpe namba ya simu ya mshukiwa, alipigiwa simu akimuita kituoni lakini mshukiwa alipofika hakumkuta ayelimuita,” alisema.

Paloto alisema tatizo hilo limekuwa sugu kwenye idara ya upelelezi ya polisi wilayani humo, hali inayowafanya waamini huduma haziwezi kuwa na ubora unaotakiwa kutokana na unyeti wa idara hiyo.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Manyoni (OCD), Ahmad Makele akijibu madai hayo alikiri kuwepo kwa mauaji hayo ya mara kwa mara wilayani humo.

"Vifo vinavyotokea sio vya kisasi wala kuwania mali sababu mtu akiuawa vinachukuliwa viungo vya mwili wake kama vile sehemu za siri," alisema.

Makele alisema Jeshi la Polisi limeanza kuchukua hatua za kukabiliana na mauaji hayo na watu kadhaa wamekwisha kamatwa na misako zaidi bado inaendelea kufanyika ili kukomesha vitendo hivyo.

Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Serukamba amemwagiza Afisa wa Usalama wa Taifa wa Wilaya ya Manyoni (DSO), kuunda kamati itakayoshirikisha vyombo vyote vya usalama kuchunguza mauaji hayo.

Serukamba ambaye alionekana kuchukizwa na suala hilo alisema mkoa anaoungoza hawezi kukubali kuwa na askari wanaoshirikiana na wahalifu.

"Haiwezekani watu wanauawa kirahisi rahisi na serikali ipo, vinginevyo tumwambie IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini) awaondoe Manyoni, pia hatuwezi kuwazuia na polisi wanaoshirikiana na wahalifu, hatuwezi kuwafukuza kazi lakini tunaomba wapelekwe mikoa mingine hapa tunahitaji kuona polisi wema ambao wanalinda wananchi na mali zao," alisema.

Alisema Jeshi la Polisi linao uwezo wa kuwajua wahalifu,washirikina na wanaofukua makaburi hivyo wote wafahamike wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mlagaza, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkazi wa Manyoni Prisca Maleta.akitoa kero yake mbele ya mkuu wa mkoa.
Mkazi wa Manyoni Khalfani Zuberi akinyoosha kidole kuomba apewe nafasi ya kutoa kero zake.
Mkazi wa Manyoni Khalfan Zuberi akitoa kero zake.
Meneja wa Tanesco Wilaya ya Manyoni Mhandisi James Mushi akizungumza katikakikao hicho wakati akitoaufafanuzi kufuatia kero zilizokuwa zikiwasilishwa na wananchi.
Kero zikitolewa mbele ya mkuu wa mkoa.
Kikao cha kero kikiendelea.

Share:

Thursday, January 19, 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YASHIRIKI UZINDUZI UJENZI WA RELI YA KISASA KUTOKA TABORA HADI ISAKA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Phillip Mpango akisikiliza maelezo ya ushiriki wa benki ya Tanzania Commercial Bank TCB katika ujenzi wa Reli ya kisasa(SGR) kutoka kwa Mkurugenzi wa wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB),  Adolphina William wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga

Mkurugenzi wa wateja Wakubwa wa Tanzania Commercial Bank (TCB),  Adolphina William wakati (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa ujenzi wa reli ya SGR LOT 4 kati ya Tabora na Isaka, uliofanyika leo mjini Isaka, mkoani Shinyanga ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Phillip Mpango.


Tanzania Commercial Bank (TCB) Imeendelea kushiriki zoezi endelevu la ujenzi wa kipande cha nne cha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165.


TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka chenye urefu wa kilomita 165..


TCB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika sekta mbalimbali na kuhakikisha kuwa inatoa huduma stahiki kila kona ya Tanzania na kuhakikisha inaunga mkono kwa asilimia zote maendeleo ya nchi.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa  Tanzania Commercial Bank Adolphina William  wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya nne leo Mkoani Shinyanga.


Adolphina amesema, Tanzania Commercial Bank  ni Benki ya Wananchi na  wamejitoa na wameshiriki kwa hatua kubwa katika kuhakikisha shirika la Reli Tanzania (TRC) linafanikisha mradi wa SGR   kwa mafanikio makubwa.


“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC wanafanya kazi nzuri sana kuhakikisha wanaunganisha wananchi kwa njia ya usafiri wa reli hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio makubwa hapa nchini.


Adolphina ameeleza kuwa kwa Sasa Tanzania Commercial Bank ina matawi kila pembe ya Tanzania hivyo imejipanga vyema kutoa huduma kwa watanzania pamoja na wageni kutoka nje hivyo amewasihi watanzania ambao bado hawajafungua akaunti na benki ya TCB wakafungue akaunti ili kunufaika na huduma zinazopatikana katika Benki hiyo.

Share:

Tuesday, January 17, 2023

USAID KIZAZI HODARI TUMAINI JIPYA KWA JAMII ZA WAATHIRIKA WA UKIMWI

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima (wa pili kushoto) akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Deloitte Consulting, Zahra Nensi baada ya kuzindua mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu KKKT, Mhandisi Robert Kitundu. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima akibonyeza kitufe kuzindua mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini, Kate Somvongsiri akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na USAID.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Mradi wa Kizazi Hodari Kanda ya Kusini, Dorothy Matoyo baada ya kuzindua mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Deloitte Consulting, Zahra Nensi. Mradi huo unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Mkurugenzi Mkazi wa Deloitte Consulting Limited, Zahra Nensi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Mkurugenzi wa Mradi wa Kizazi Hodari, Dorothy Matoyo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Mkuu wa Kanisa la KKKT, Askofu Dk. Fredrick Shoo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaosaidia Serikali ya Tanzania katika kuboresha afya, ustawi na ulinzi wa watoto yatima na vijana wanaoishi kwenye jamii zilizoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi katika mikoa 12 nchini unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Baadhi ya Viongozi wa dini wakihudhuria wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.
Baadhi ya wahudhuriaji wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), jijini Dodoma leo. Mradi huo unaratibiwa na Taasisi za Deloitte na Kanisa la KKKT.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Jamii na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima ameagiza utekelezaji wa mradi wa Kizazi Hodari unaowalenga kuimarisha afya, ustawi na ulinzi kwa Watoto na vijana balehe wanaoishi katika mazingira hatarishi yenye Kasi kubwa ya maambukizi ya VVU.

Mradi wa Kizazi Hodari utatekelezwa kwa miaka mitano chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) na unawalenga watoto balehe wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 17.

Watekelezaji wa mradi huo ni Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Shirika la Deloitte na Shirika la kidini la KKKT

Taasisi ya Deloitte ikisimamia mikoa mitano ya Kanda ya Kusini ya; Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na Njombe huku Kanisa la KKKT likisimamia mikoa Saba ya Kanda ya Kaskazini ya; Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Singida na Dodoma.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa mradi huo, Dk Gwajima alisema mbali na mambo yaliyoainishwa katika mradi huo utakaotekelezwa kwenye mikoa 12 nchini, ni muhimu mradi huo ukajihusisha na utoaji wa elimu sahihi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Ni vema afua zifuatazo zikawekwa katika mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa Kizazi Hodari ni kutoa elimu sahihi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na kuendeleza programu za kuwaandaa wavulana kuwa wanaume bora wajao,” alisema.

Akielezea kuhusu mradi huo, Dk Gwajima alisema jumla ya watoto yatima na kaya 138,944 zitafikiwa na mradi huo ambao unalenga katika kuimarisha afya, ustawi na ulinzi kwa watoto na vijana balehe wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Deloitte, Zahra Nensi alisema mradi huo unalenga katika kuongeza wigo wa kuwatambua watoto wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na kuwaunganisha karika huduma za afya ili kufubaza VVU.

Kuongeza upatikanaji wa huduma za kuzuia maambukizi, kuzuia ukatili na huduma za mwitikio kwa watoto yatima na vijana,” alisema.

Pia alisema lengo jingine ni kukuza uchumi kwa ajili ya mabinti balehe na walezi wa watoto yatima na waishio mazingira hatarishi.

Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Kate Msomvongsiri amesema hadi mwisho wa mradi huo inategemewa utakuwa umeajiri na kuwapatia huduma mbalimbali walau kwa asilimia 90 ya watoto na vijana hao.

Alisema vijana hao ni hasa kutoka kwenye vituo vya afya vinavyohudumiwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR).
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive