A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Sunday, October 31, 2021

Absa Group Appoints Saviour Chibiya as Group Executive: Absa Regional Operations

 
Absa Group today announced the appointment of Saviour Chibiya as Group Executive: Absa Regional Operations (ARO). Saviour will be responsible, together with RBB and CIB for the Group’s ARO businesses and for the Group’s strategy, collaboration and relationships with its key stakeholders across those businesses.

Saviour will be a member of the Group Executive Committee and will thus provide input in terms of the Group’s strategy overall and in particular the strategic choices for Absa’s growth in the ARO banks and will support and enable the Managing Directors in the countries in their strategic delivery. He will report directly to the Group Chief Executive.

Saviour joined the Group in 2010 as Managing Director and CEO of Barclays Bank Zambia Plc, after nearly two decades at Citibank. In 2017, he joined the ARO leadership team as Regional Managing Director, assuming increasingly pan-African regional responsibilities.

Saviour is a seasoned banker with deep institutional knowledge of the Group, as well extensive and diversified banking experience, at both country and regional level across the continent,” said Jason Quinn, interim Chief Executive for Absa Group.

We are proud that this appointment is drawn from within our leadership structures. Saviour’s experience will contribute immensely to the strength and diversity of our executive leadership team and we are excited about the perspectives that he will bring,” Jason added.

Saviour is a Fellow of the Zambia Institute of Banking and Financial Services and holds an Economics degree from the University of Zambia.

Our strong franchise across ARO is critical to the future growth of Absa Group. In most of the countries in which we operate, we are among the top financial services providers and we have strengthened this position through innovative product and service offerings catering to both our local customers and global clients,” said Saviour.

I am excited to be embarking on this journey, and look forward to collaborating with colleagues, customers, regulators and the communities in which we operate to bring Africa’s possibilities to life,” he added.
Share:

Friday, October 29, 2021

ASASI ZA KIRAIA NI CHACHU KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU - WAZIRI GWAJIMA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Dkt Doroth Gwajima akizungumza na wadau wa Asasi za kiraia alipohudhuria sherehe ya utoaji wa tuzo mbalimbali kwa wadau wa Asasi za kiraia (KIRAIA) Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. Jingu, akizungumza na wadau hao Katika hafla hiyo iliyofanyika Octoba 28,2021.

Na: Mwandishi Wetu Dodoma | Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Dkt Doroth Gwajima amesema Serikali inazitambua Asasi zote za Kiraia kwa kazi nzuri zinazofanya kwa ajili ya manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Mhe. Gwajima ameyasema hayo wakati akitoa tuzo mbalimbali kwa baadhi ya Asasi za Kiraia zilizofanya vizuri zaidi katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa wiki ya AZAKI.

Mhe. Dkt Gwajima alisema Asasi zote zinafanya vizuri lakini Tuzo hizo zimetolewa kwa wale walionesha ubunifu na kujitolea zaidi katika utendaji kazi zao katika kuhakikisha wananchi wanafaidika na miradi wanayoiendesha katika Mashirika yao.

"Tunapoikuza jamii yetu ya Kitanzania tunamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza maono yake kwenyeTaifa hili na nipende kumshukuru kwa maono yake amekuwa akihamasisha tuzidi kuimarisha ushirikiano na Asasi za Kiraia" amesema Dkt. Gwajima.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. Jingu ameipongeza AZAKI kwa midahalo iliyofanyika katika wiki yote ambayo ina lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao na kufanya tathmini ya kuboresha katika utekelezaji wa majukumu hayo.

"Nyie kama Wadau wa Maendeleo mkaoneshe kweli kuwa nyie ni wadau kwa kulenga kuleta matokeo zaidi na kubuni namna ya kupata Rasilimali kwa ajili ya kuendeleza shughuli zenu" amesema Dkt. Jingu.

Amesema Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa Asasi zote za Kiraia ikiwemo utoaji ya miongozo mbalimbali na kuwahimiza waendelee kufanya kazi kwa bidi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni zilizopo.

Naye Rais wa Asasi za kiraia Dkt. Stigmata Tenga ameishukuru Serikali kwa kuthamini mchango wa AZAKI na kuwapa nafasi katika kuchangia maendeleo ya Taifa kupitia miradi mbalimbali inatotekelezwa na Asasi hizo katika maeneo tofauti nchini.

"Wizara imekua ikionesha kutusikiliza na kukaribisha mawazo yetu hivyo kututia moyo zaidi kuendelea kufanya kazi” amesema.

PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA UTOAZI WA TUZO ULIOFANYWA NA MHE. WAZIRI DOROTH GWAJIMA
Share:

Thursday, October 28, 2021

WAZIRI UMMY MWALIMU AFUNGA RASMI WIKI YA ASASI ZA KIRAIA JIJINI DODOMA

  

Na: Hughes Dugilo, DODOMA | Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu ameshiriki hafra ya kuhitimisha Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) Jijini Dodoma.

Katika hotuba yake mbele ya Wadau wa Serikali na Mashirika ya Asasi za Kiraia nchini ameahidi kutoa ushirikiano kwa mshirika hayo na kuyasihi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa ni moja ya mchango mkubwa wa maendeleo ya nchi.

Kwa kutambua mchango wa Azaki natoa wito kwenu kuendelea kushirikiana na Serikali kuendelea kuihudumia jamii ambayo Asasi hizi mmekuwa mkifanya kazi nizuri kwa kuifikia jamii hasa wananchi walioko vijijini kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji na halmashauri" Amesema Mhe. Ummy
Aidha ametoa wito kwa Sekta Binafsi kuwekeza kwenye mashirika ya Asasi za Kiraia ili kuchangia ukuaji wa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla na kwamba kwa kufanya hivyo kutaisaidia Sekta Binafsi kutimiza malengo yao ya huduma za jamii kwani asasi hizo zimekuwa zikifanyakazi na jamii hizo kwenye maeneo yao.

Pia amezitaka Asasi za Kiraia kuongeza nguvu katika suala zima la kutoa elimu kwa wananchi na kuwajengea uwezo ili wananchi hao waweze kujisimamia katika shughuli zao za kimaendeleo na kiuchumi huku akiwataka kuwasaidia madiwani kwenye halmashauri kwa kuwajengea uwezo kwenye masuala mbalimbali yakiwemo usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo.

Napenda kuwapongeza sana kwa elimu mnayotoa kwa wananchi kwa kuwajengea uwezo, lakini naomba muende mbali zaidi kuyafikia mabaraza ya madiwani kwenye halmauri zetu ili nao wajengewe uwezo wa kusimamia halmashauri kwenye matumizi ya fedha na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo” Ameongeza Mhe. Ummy.

 
Awali akitoa Salamu na kuelezea shughuli mbalimbali zilizofanywa na Asasi ya Kiraia kwenye Wiki ya Azaki, mratibu wa Wiki ya Azaki na Mshauri wa Foundation for Civil Society (FCS) Justice Rutenge ameeleza kazi zilizofanywa katika wiki ya Azaki ikiwa ni pamoja na mijadala mbalimbali iliyowakutanisha wadau wa Asasi za Kiraia, Wabunge, Makundi Maaalum na wananchi ambapo kwa pamoja waliweza kushirikiana katika mazungumzo na mijadala iliyolenga kujadili masuala yanayohusu ustawi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Waziri Wiki ya Azaki mwaka huu imeweza kuzikutanisha Asasi zaidiya 300 ambao kwapamoja waliweza kukutana hapa Dodoma kuanzia siku ya ufunguzi na baadae kushiriki kwenye mijadala mbalimbali iliyowawezesha kutoa mawazo yao juu ya masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla" Amesema Justice.

Wiki ya AZAKI ni jukwaa pekee nchini lililowaleta kwa pamoja wadau wakuu wa maendeleo ikiwemo Serikali, Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia, pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu ustawi wa nchi na maendeleo ya Taifa ambapo yalizinduliwa rasmi leo Octoba 23 na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb), na kufungwa rasmi leo Octoba 28, 2021
Share:

Wednesday, October 27, 2021

ANNE MAKINDA: ASASI ZA KIRAIA ZIHAMASISHE WANANCHI KUSHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI

 
Kamisaa wa Sensa Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda akizungumza Akizungumza katika mkutano wa wadau wa Asasi za Kiraia kwenye Wiki ya AZAKI kuhamasisha wadau hao kuwafikia wananchi kuwapa elimu ya Sensa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga akifuatilia jambo sambamba na Mgeni rasmi Kamisaa wa Sensa Spika wa Bunge Mstaafu Mama Anne Makinda kwenye Mkutano huo uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM | ASASI za kiraia nchini(AZAKI)zimetakiwa kushirikiana na Serikali kuhamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika kufanyika Agosti 2022.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa Asasi za Kiraia kwenye Wiki ya AZAKI inayoendelea Jijini Dodoma, Kamisaa we Sensa Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda ameeleza kuwa umuhimu wa sensa unagusa kila nyanja hivyo ni wajibu kwa kila mtanzania kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.

"Sensa ni muhimu na inafanyika kila baada ya miaka kumi, ninyi watu wa AZAKI ni wadau namba moja, tunatakiwa kutoka kwenye uchumi wa kati tuendelee zàidi tufanane na wenzetu," ameeleza.

Amesema kuwa Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012 hivyo Sensa itakayofanyika itakuwa ni sensa ya sita kufanyika nchini tangu kupatikana kwa Uhuru na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Amesema kuwa kabla ya kupatikana kwa Uhuru zimewahi kufanyika Sensa nyingine tatu.

"Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini, kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla, watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum, kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo," amefafanua Makinda.
Kamisaa wa Sensa Spika wa Bunge mstaafu Anne Makinda akitoka na kiwasalimia wadau na washiriki wa mkutano huo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

Kwa umuhimu huo, Mama Makinda ameeleza upekee wa Sensa hiyo kuwa utazingatia taarifa za idadi ya watu katika husaidia mamlaka za wilaya kutekeleza mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.

"Taarifa za sensa zitawezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira, msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia, takwimu hizi zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa," amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga akizungumza mara baada ya kumalizika alipokuwa akimkaribisha Mgeni rasmi Kamisaa wa Sensa Spika wa Bunge Mstaafu Mama Anne Makinda kwenye Mkutano huo uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mtakwimu Mwandamizi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) David Mwaipopo ametumia fursa hiyo kuwaeleza wana AZAKI kuwa sensa ya mwaka 2022 kama zilivyo sensa zilizopita itatumia aina mbili kuu za Madodoso ambazo ni dodoso refu litakalotumika kuhoji asilimia 30 ya maeneo yote ya kuhesabia watu na Dodoso fupi litakalotumika kuhoji kwenye asilimia 70 ya maeneo yote ya kuhesabia watu.

Aidha ameyataja Madodoso mengine kuwa ni la Taasisi ambalo ni mahsusi kwa ajili ya wasafiri, waliolala hotelini, nyumba za wageni, na waliolazwa hospitalini, na Dodoso la wasio na Makazi maalum ambalo ni mahsusi kwa watu wote wanaolala maeneo yasiyo rasmi, kwenye baraza za majengo mbalimbali, kwenye madaraja na maeneo mengine.

"Utekelezaji wa sensa ya watu na makazi hufanyika katika awamu kuu tatu kuu ambazo ni kipindi kabla ya kuhesabu watu, wakati wa kuhesabu watu na kipindi baada ya kuhesabu watu," amesisitiza.

Licha ya hayo Mtakwimu huyo Mwandamizi amefafanua maswali yatakayoulizwa wakati wa sensa ya watu na Makazi huku akieleza kuwa moduli kumi na nne zitatumika kukusanya taarifa za watu na makazi yao kwa nchi nzima.

"Maswali hayo ni tarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, maswali yanayohusu ulemavu, tarifa za Elimu, maswali ya uhamaji, pamoja na taarifa za Watanzania wanaoishi nje ya nchi, mengine ni maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa, kama vile, vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva, pamoja na shughuli za kiuchumi na umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA," amesema.

Ameongeza kuwa maswali mengine yatakayoulizwa kipindi cha sensa kuwa ni tarifa za uzazi na vifo vilivyotokea ndani ya kaya, vifo vitokanavyo na uzazia, hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali, maswali ya kilimo na mifugo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii.

"Tunaomba AZAKI mshiriki kikamilifu kuelimisha jamii tufikie malengo,sisi kama Ofisi ya Takwimu tumejipanga vizuri kwa kutumia rasilimali chache zilizopo ili kukamilisha kwa wakati shughuli zote za maandalizi ikiwamo kazi ya utengaji wa maeneo ya kuhesabia watu katika ngazi ya kitongoji na mtaa ambayo ndiyo msingi wa kufanikisha sensa kwa ubora," ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga, amesema kuwa wao kama Asasi za Kiraia wamejipanga vyema kuhakikisha wanashirikiana na Serikari katika kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kutokana na mashirika ya Asasi za Kiraia kuwa karibu na wananchi kuanzia ngazi ya mashina, kata, vijiji na wilaya kupitia miradi mbalimbali wanayoisimamia kwenye maeneo hayo.

Tumefurahi kupata hiyo hamasa ambayo imetolewa vizuri sana na wataalamu na hasa sasa hivi Taifa letu linachangamoto ya kutoaminiana hasa kwenye mambo ya msingi kwahiyo sisi kama Asasi za Kiraia ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba tunatoa elimu sahihi ya wananchi kueliwa umuhimu wa zoezi hili la sensa ya Kitaifa lakini pia elimu ya wananchi kushiriki zoezi hili muhimu la Sensa ya Kitaifa
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-WAZALENDO Zitto Kabwe akipiga makofi akimpongeza Mama Anne Makinda mara baada ya kumaliza kuhutubia Mkutano huo.

Aidha ameeleza namna ambavyo wao kama Asasi za kiraia watakavyoshiriki kuifikia jamii na kuihamasha kushiriki kikamilifu zoezi hilo na kusema kuwa Asasi nyingi zipo vijijini hivyo ni rahisi wao kuifikia jamii husika kwakuwa wao ni miongoni mwa wananchi wanaoshiriki nao kwenye miradi mbalimbali ya huduma za kijamii na maendeleo.

Tunasema mbuzi kafia kwa muuza supu’ majukumu kama haya sisi ndio tuna uwezo mkubwa wa kuyasukuma na ndio nguvu yetu sisi kama Asasi ule ukaribu na wananchi na tunaamini kwenye hili taarifa sahihi zitafika kwa wananchi” Amesema Ameongeza Kiwanga.
Share:

BENKI YA ABSA KUENDELEZA USHIRIKA NA MAKAMPUNI YANAYOIBUKA YENYE UBUNIFU

 
Mkuu wa Huduma kwa Wateja na Digitali wa Benki ya Absa, Samuel Mkuyu (wa pili kulia), akichangia mada wakati wa warsha kuhusu uboreshaji wa huduma kwa wateja kwa kutumia njia za ubunifu wa kidigitali iliyoandaliwana kampuni ya teknolojia ya Hindsight Ventures kwa kushirikiana na Absa, jijini Dar esSalaam leo. Wanaongalia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa echo Tanzania, Aashiq Shariff, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kwa Njia ya Simu za Mkononi wa Tigo, Faith Pella na Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi wa Kampuni ya Hindsight, Ajay Ramasubramaniam.
Mkuu wa Huduma kwa Wateja na Digitali wa Benki ya Absa, Samuel Mkuyu (mbele), pamoja na washikiri wengine katika warsha kuhusu uboreshaji wa huduma kwa wateja kwa kutumia njia za ubunifu wa kidigitali iliyoandaliwana kampuni ya teknolojia ya Hindsight Ventures kwa kushirikiana na Absa, jijini Dar esSalaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu na Mwanzilishi wa Kampuni ya Hindsight Venture, Ajay Ramasubramaniam akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Hindsight Venture wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania wakipozi mbele ya wapiga picha mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki katika warsha hiyo wakisikiliza mada mbalimbali kutoka kwa watoa mada katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Seedspace katika Jengo la Tanzanite Tower jijini Dar es Salaam leo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam | BENKI ya Absa Tanzania imesisitiza dhamira yake katika kujenga ushirika na makapuni yanayoibuka yenye ubunifu nchini katika kuanzisha miradi ya kibiashara ambayo itakuwa na faida kwa pande zote mbili, ofisa wa ngazi ya juu wa benki hiyo ya kimataifa amesema leo mjini Dar es Salaam katika warsha iliyoandaliwa kuzipa nafasi kampuni zinazoibuka kuonesha miradi yao ya kibiashara.

Warsha hiyo, iliyokuwa na kauli mbiu ya Uboreshaji wa Huduma kwa Wateja kwa njia ya Kidijitali na Ubunifu, iljikita katika kubainisha namna gani mabadiliko ya kidijitali yanaweza kusambazwa kwenye sekta mbalimbali nchini sambamba na uboreshaji wa huduma kwa wateja unaoendana na mabadiliko hayo.

Lengo letu ni kutafuta njia mbalimbali ambazo tunaweza kuzitumia ili kujenga ushirika na kampuni za ubunifu zinazoibuka, katika kubuni bidhaa mbalimbali na kuziweka sokoni ili zizalishe kibiashara,” alisema Samuel Mkuyu, Mkuu wa Huduma kwa Wateja na Dijitali, akiongeza kuwa benki hiyo imekuwa kwa muda mrefu inazitafuta kampuni zinazoibuka.

Alisema kuwa kutokana na jinsi kampuni zilizoshiriki kwenye warsha hiyo zilivyowasilisha taarifa za miradi mbalimbali ya biashara waliyobuni, benki hiyo itachambua shughuli za kampuni hizo kwa lengo la kubaini fursa na mawazo ambayo yanaweza kugeuzwa bidhaa na huduma kwa njia ya ubia na benki hiyo.

Lengo letu si tu kuzimwagia fedha kampuni hizo zinazoibuka na zinazoendesha miradi ya ubunifu ya kibiashara, msingi wa ubia ambao tunalenga kuujenga ni kugeuza mawazo ya kampuni hizo kuwa miradi ya kibiashara inayozaa faida ambapo sote tutanufaika,” alisema Mkuyu, na kutoa mfano wa programu iliyozinduliwa hivi karibuni na benki hiyo inayomuwezesha mteja kupanga miadi mtandaoni (Virtual Branch Engagement Solution), kwamba ni ushirika kati ya Absa na kampuni ya FastHub.

Mkuyu alisema kuwa Absa ina nia thabiti ya kuweka kipaumbele katika miradi ya ubunifu wa kidijitali yenye uwezo wa kuzalisha masuluhisho endelevu ya kidijitali, huku thamani ya mteja ikiwekwa mbele tofauti na miradi mingine ambapo haigusi Mtindo wa Maisha wa mteja. Msimamo huu wa benki, alisema, unadhihirishwa na kutambuliwa kwake hivi karibuni kwa benki hiyo kushinda Tuzo ya Taasisi bora ya Fedha kwenye matumizi ya Tehama wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), uliofanyika jijini Arusha.

Lengo kuu la warsha hiyo, ambayo iliendana na mjadala ulioshirikisha watoa mada wabobezi kutoka kampuni mbalimbali, ilikuwa ni kujadili changamoto zinazokabili harakati za kuboresha huduma kwa wateja katika sekta mbalimbali na namna gani ubunifu wa kidijitali unaweza ukatatua mapungufu katika mikakati hiyo.

Akiongea katika warsha hiyo, Msimamizi wa Hindsight Ventures Tanzania, Paul Mandele, alitoa mchango wake kuhusiana na namna warsha hiyo ilivyokuja muda muafaka, ikizingatiwa kuwa warsha kama hizo ni muhimu kwa kuwa zinatoa fursa za kutatua changamoto ambazo zinafanya kampuni changa zishindwe kuboresha huduma kwa wateja kuendana na mabadiliko ya kidijitali kwa kasi ambayo wadau wa sekta wanategemea.

Mandele aliongeza kuwa changamoto hizo kama hazitatatuliwa kwa sasa, zitafanya kampuni nyingi zinazoibuka kushindwa kutekeleza miradi yake kama ambavyo imebainishwa kwenye dira zao ikizingatiwa kuwa wengi wa waanzilishi wa kampuni hizo ni wajasiriamali waliotoka vyuoni karibuni na wasiokuwa na mitaji, elimu stahili ya biashara, takwimu chache na kutokuwa na stadi maalum za biashara.

Kampuni nyingi zinazoibuka mara nyingi huwa zinakosa washirika wa kufanya nao kazi, jambo ambalo linazifanya zijiendeshe kwa kujitegemea zenyewe bila ya kuwa na kampuni kongwe kama mfano wa karibu wa kuigwa," Alisema Mandele.
Share:

Tuesday, October 26, 2021

ABSA COMMITS TO PARTNER WITH INNOVATIVE START-UPS

 
Absa Bank Tanzania Head of Customer Experience and Digital Banking, Samuel Mkuyu (second right), makes a presentation on enhanced customer experience with digital innovation during a one-day forum organised by Hindsight Ventures in partnership with Absa Bank in Dar es Salaam today. Looking on (from right) is Echo Tanzania Managing Director, Aashiq Shariff, Tigo Head of Mobile Financial Services, Faith Pella and Hindsight Ventures Founder & CEO, Ajay Ramasubramaniam.

Absa Bank Tanzania is committed to creating partnerships with tech start-ups in the country in order to create business ventures on a win-win situation, an official of the multinational financial institutions said today in Dar es Salaam during a clinic organized for start-ups to showcase projects and learn.

The event, dubbed thought leadership Event, Enhanced Customer Experience with Digital and Innovation, focused on how digital transformation can be rolled out hand-in hand with customer experience,it was co-organised by the bank and Hindsight Venture, a technological innovation and solutions firm.

“Our aim is to explore options through which we can partner with start-ups and co-create and co-commercialize products, said Samuel Mkuyu, Head of Customer Experience and Digital Banking at Absa, adding that the financial conglomerate had long initiated the process of identifying potential start-up partners.

He said that from the presentations that were made by the participating start-ups on their projects, they will analyse the presentations with a view to exploring potential opportunities and ideas for commercialization that can be turned into partnership between the bank and the start-ups.

“Our aim is not just to dish out money to the start-ups, the basis for our cooperation is that we turn the ideas into joint projects, in which both parties benefit, said Mkuyu, pointing to the recently- launched appointment arranging software, Virtual Branch Engagement Solution as a joint project with FastHub Solutions.

He said that the bank was committed to giving priority to digital innovation that creates sustainable solutions with the value to the customer being placed first as opposed to solutions that do not speak to Customers lifestyles. This is a stand that is testified to the recent award of the bank as “The Best Financial Institution in Using ICT” by the Ministry of Communication and Information Technology.

The core focus of the session was punctuated by a lively discussion led by panelists on burning challenges to customer experience across multiple industries and how the role of digital an innovation in addressing these gaps. The discussions shared a wide array of knowledge from multiple stakeholders on on the current global imperative to synchronize the drive to launch digital innovation with improvements in customer experience.

Speaking at the event, Hindsight Ventures Country Lead, Paul Mandele, shared the importance of the timing of the event and how such forums were necessary to bridge the gaps in the ecosystem and to drive digital innovation in Tanzania as per projected growth, which if not addressed now will see start-ups faced with challenges that hinder successful take-off of envisioned projects as most founders are fresh graduates with little capital, industry knowledge , limited data insights and necessary skill sets to bridge this gap.

Start-ups usually lack the right stakeholders to partner with that causes them to usually make it alone with no established business case models to learn from” said Mandele.
Share:

Monday, October 25, 2021

ASASI ZA KIRAIA ZAJADILI MCHANGO WAO KATIKA MAENDEO YA NCHI DODOMA

 
Mkurugenzi wa FCS Francis Kiwanga akichangia mada kuhusu Mchango wa AZAKI katika kuleta Maendeleo ya nchi wakati wa mkutano huo ulifanyika leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la WiLDAF na Mwenyekiti wa TANGO Anna Kulaya (kushoto) akiongoza mada kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe zaidi ya 600 Jijini Dodoma, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa FCS Francis Kiwanga, (anaefuata) ni Mkurugenzi wa HLRC Anna Henga, na (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa ANSAF Audax Lukonge.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) Anna Henga akizungumzia mchango wa Asasi za Kiraia katika kutoa msaada wa Kisheria kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa ANSAF Audax Rukonge akichangia mada katika Mkutano huo uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Na: Hughes Dugilo, DODOMA | Jamii imetakiwa kuendelea kuwa na imani na Mashirika ya Asasi za Kiraia nchini zinazofanyakazi kubwa ya kuchagiza maendeleo yao katika kuhakikisha wanapata huduma bora za kijamii na kukua kiuchumi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga alipokuwa akiwasilisha mada kwenye mkutano maalumu uliokuwa ukizungumzia mchango wa Asaasi za Kiraia katika Maendeleo ya nchi uliofanyika kwenye ukumbi wa mlimwa katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.

Katika Mkutano huo uliokuwa na wazungumzaji watatu akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) Anna Henga na Mkurugenzi Mtendaji wa ANSAF Audax Lukonge ulilenga kujadili Mchango wa AZAKI katika kuleta maendeleo ya nchi na kuudhuriwa na wajumbe zaidi ya 600, umetoa fursa kwa wajumbe hao kuweza kujadili kwa kina namna ya kuboresha na kuendeleza ushirikiano wao katika kuihudumia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii, usawa wa kijinsia, haki za Binaadamu na mazingira pamoja na kuihamasisha jamii katika kujiletea maendeleo baina yao na Taifa kwa ujumla.

Akijibu swali lililoulizwa na muongozaji wa mkutano huo Mkurugenzi wa Shirika la WiLDAF na Mwenyekiti wa TANGO Anna Kulaya kuhusu umuhimu wa AZAKI katika kuchangia na kukuza Maendeleo ya nchi, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga amesema kuwa eneo mojawapo ambalo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa ni kuhakikisha wanajenga imani kwa jamii na serikali kwa kuzitambua kazi mbalimbali wanazozifanya katika kuielimisha jamii na kuihamasisha kkuweza kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.

Amezitaka Asasi za kiraia ziendelee kujenga imani kwa jamii ambayo ndio nguzo yao kubwa nakwamba Asasi hizo ni daraja kati ya wananchi kuweza kupaza sauti zao kwa serikali ili iweze kutatua changamoto zao mablimbali zinazowakabili.

Eneo mojawapo ambalo tumefanikiwa zaidi ni hilo la kujenga imani na ndio maana unaona hata mwaka huu Serikali kwa kushirikiana na NaCoNGo wameweza kuendesha kongamano kubwa sana hata kuweza kumwita Mheshimiwa Rais ambae kwa maneno yake mwenyewe aliweza kutambua mchango wetu sisi kama AZAKI na kutupa hamasa zaidi ya nini tunaweza kuchangia zaidi ili kuweza kusongambele” Amesema kiwanga.

Ameongeza kuwa imani ipo kubwa kwa Serikali na kwa wananchi na hivyo kuwakumbusha wadau hao kuwa nguzo yao kubwa ipo kwa wananchi ambao kila siku wanajitahidi kuzipigania haki zao na huduma za kijamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) Anna Henga amesema kuwa Asasi za Kiraia zimeasaidia sana kuweza kuisaidia jamii kwenye masuala ya kisheria na kutolea mifano mbalimbali ya namna ambavyo kituo chao kimweza kuwasaidia wananchi waliopatwa na matatizo ya kisheria iliyowapelekea kukaa na kesi moja kwa miaka mingi bila kujua ni wapi wanaweza kwenda kupata msaada wa kisheria.

Mchango wa AZAKI katika utawala wa sheria ni mkubwa sana katika jamii yetu kwani hakuna mswada wowote unaenda Bungeni kabla ya kuupitia na kutoa mapendekezo yetu kama wadau hivyo tunaishukuru Serikali kwa kuutambua mchango wetu kwenye masula ya Kisheria” Amesema Anna.

Akichangia mada kwenye mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa ANSAF Audax Rukonge amezishauri Asasi za Kiraia kuendesha shughuli zao kwa uwazi na uwajibikaji ili kuendelea kujenga imani yao kwa Serikali na wananchi kwa ujumla nakwamba mchango wao ni mkubwa sana katika kuchangia uchumi wanchi.

kwa mfano sekta ya kilimo ni sekta muhimu sana katika kuleta maendeleo ya nchi na imekuwa ni muhimili muhimu wa uchumi, sekta hii imekuwa na wazalishaji wengi wadogo ambao hawajiwezi wakiwemo wanawake, hivyo AZAKI imesaidia sana kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi kupitia kilimo hususani pembejeo za kilimo kama mbolea” Ameongeza Rukonge

Ameongeza kuwa Asasi za Kiraia zisirudi nyuma katika kusaidia sekta ya kilimo nchini kwani ndio sekta pekee iliyoajiri wananchi wengi ambao maisha yao yametegemea kilimo kuweza kujipatia kipato na kukuza uchumi wao.

Wiki ya AZAKI inaadhimishwa Jijini Dodoma ambapo leo ni siku ya tatu tangu kuzinduliwa kwake na inatarajiwa kuhitimishwa Octoba 28 mwaka huu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima.
Share:

Saturday, October 23, 2021

UFUNGUZI WIKI YA AZAKI 2021 YAFANA JIJINI DODOMA

  
Washiriki wa Matembezi ya Wiki ya AZAKI wakiwa wameshika mabango yenye jumbe mbalimbali zinazohusu Asasi za Kiraia ikiwa ni siku ya kwanza ya Wiki ya Asasi za Kiraia iliyozinduliwa leo Jijini Dodoma. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Askari wa Kikosi cha JKT Makutupora wakiongoza Matembezi katika uzinduzi wa Wiki ya Asasi za kiraia (AZAKI) matembezi ambayo yalianzia kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Dodoma saa tatu asubuhi. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Meneja Miradi wa FCS Francis Uhadi (katikati) akia na Ms Rachel Chagoja (kushoto) MkurugenziMtendaji wa Shirika la HakiRasilimali - Mtandao wa Asasi za Kiraia unaofanyakazi za kimkakati katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi, wakiwa wameshika Bango lenye ujumbe usemao (Azaki zinachangia kuboresha Afya) wakati wa matembezi hayo Jijini Dodoma. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Baadhi ya Maafisa FCS wakishiriki matembezi maalum kuelekea kwenye uzinduzi rasmi wa Wiki ya Azaki iliyozinduliwa rasmi leo na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai Jijini Dodoma. (wa kwaza kulia) ni Ayoub Masaki Meneja wa Fedha na uendeshaji wa FCS, (kua kwake) ni Karin Rupia Afasa wa FCS Uhamasishaji Rasilimali. (wa tatu kulia) ni Justice Rutenge mshauri wa Tathimini, na (wa pili kushoto) ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa FCS Maria Chang'a. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (katikati) akiwa na wadau wa Maendeleo Balozi wa Canada Nchini Tanzania Hellen Fytche (kulia) (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Matembezi yakiwasili kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwaajili ya kuendelea na shughuli za uzinduzi uliofanywa na Mhe. Job Ndugai Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (PICHA NA HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DODOMA | Wananchi mbalimbali wa Jiji la Dodoma wamejitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) ambapo mgeni rasmi amekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (MB).

Maadhimisho hayo ya Wiki moja yaliyobeba Kaulimbiu ya 'AZAKI NA MAENDELEO' yalianza kwa matembezi maalum yaliyoanzia katika Shule ya Sekondari ya Dodoma na kuelekea katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete ambapo ndipo kulipofanyika Shughuli za ufunguzi.

Aidha katika matembezi hayo yaliyofana sana washiriki walibeba mabango mbalimbali yenye jumbe tofauti za shuguli zinazofanywa na Mashirika ya Asasi za Kiraia ambazo zimekuwa na mchango mkubwa kwa Jamii ya watanzania na Taifa kwa ujumla.

Baadhi ya washiriki wa Matembezi hayo wamesema kuwa wameshiriki kwenye wiki ya Azaki mwaka huu kwaajili ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili waweze kufahamu shughuli zao ambazo kimsingi zimejikita katika kuwasaidia kupaza sauti zao na kuibua changamoto katika jamii ili Serikali iweze kuzifanyiakazi, na kwamba wao kama Azaki wanaona kuwa ushiriki wao kwenye Wiki ya Azaki utawapa fursa ya kuendelea kukuza mashirikiano baina yao.

Wiki ya AZAKI ni jukwaa pekee nchini linaloleta kwa Pamoja wadau wakuu wa maendeleo ikiwemo Serikali, Sekta binafsi na Asasi za Kiraia Pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu ustawi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla ambayo imezinduliwa rasmi leo) Octoba 23 na kufungwa tarehe 28, 2021
Share:

Benki ya Absa Tanzania yatwaa tuzo ya Taasisi Bora ya Fedha katika Matumizi ya Tehama

 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainabu Chaula (kushoto) akikabidhi tuzo ya Taasisi bora ya Fedha kwenye matumizi ya Tehama kwa Ofisa Mkuu Mwendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (katikati) pamoja na Ofisa Mkuu wa Tehama wa Absa, Emmanuel Mwinuka, wakati wa Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), jijini Arusha jana.
Ofisa Mkuu Mwendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (kushoto) na Ofisa Mkuu wa Tehama wa Absa, Emmanuel Mwinuka, wakionyesha tuzo ya Taasisi Bora ya Fedha kwenye matumizi ya Tehama mara baada ya kukabidhiwa wakati wa Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), uliofanyika jijini Arusha jana.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainabu Chaula (kulia), akibadilishana mawazo na Ofisa Mkuu Mwendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa Mkuu wa Tehama wa Absa, Emmanuel Mwinuka (kushoto), wakati wa Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), uliofanyika jijini Arusha jana. Mwingine ni mmoja wa waandaaji wa mkutano, Tumaini Magila.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive