Washiriki wa Matembezi ya Wiki ya AZAKI wakiwa wameshika mabango yenye jumbe mbalimbali zinazohusu Asasi za Kiraia ikiwa ni siku ya kwanza ya Wiki ya Asasi za Kiraia iliyozinduliwa leo Jijini Dodoma. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Askari wa Kikosi cha JKT Makutupora wakiongoza Matembezi katika uzinduzi wa Wiki ya Asasi za kiraia (AZAKI) matembezi ambayo yalianzia kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Dodoma saa tatu asubuhi. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Meneja Miradi wa FCS Francis Uhadi (katikati) akia na Ms Rachel Chagoja (kushoto) MkurugenziMtendaji wa Shirika la HakiRasilimali - Mtandao wa Asasi za Kiraia unaofanyakazi za kimkakati katika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi, wakiwa wameshika Bango lenye ujumbe usemao (Azaki zinachangia kuboresha Afya) wakati wa matembezi hayo Jijini Dodoma. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Baadhi ya Maafisa FCS wakishiriki matembezi maalum kuelekea kwenye uzinduzi rasmi wa Wiki ya Azaki iliyozinduliwa rasmi leo na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai Jijini Dodoma. (wa kwaza kulia) ni Ayoub Masaki Meneja wa Fedha na uendeshaji wa FCS, (kua kwake) ni Karin Rupia Afasa wa FCS Uhamasishaji Rasilimali. (wa tatu kulia) ni Justice Rutenge mshauri wa Tathimini, na (wa pili kushoto) ni Afisa Mwandamizi wa Fedha wa FCS Maria Chang'a. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (katikati) akiwa na wadau wa Maendeleo Balozi wa Canada Nchini Tanzania Hellen Fytche (kulia) (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Matembezi yakiwasili kwenye viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwaajili ya kuendelea na shughuli za uzinduzi uliofanywa na Mhe. Job Ndugai Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, DODOMA | Wananchi mbalimbali wa Jiji la Dodoma wamejitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) ambapo mgeni rasmi amekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (MB).
Maadhimisho hayo ya Wiki moja yaliyobeba Kaulimbiu ya 'AZAKI NA MAENDELEO' yalianza kwa matembezi maalum yaliyoanzia katika Shule ya Sekondari ya Dodoma na kuelekea katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete ambapo ndipo kulipofanyika Shughuli za ufunguzi.
Aidha katika matembezi hayo yaliyofana sana washiriki walibeba mabango mbalimbali yenye jumbe tofauti za shuguli zinazofanywa na Mashirika ya Asasi za Kiraia ambazo zimekuwa na mchango mkubwa kwa Jamii ya watanzania na Taifa kwa ujumla.
Baadhi ya washiriki wa Matembezi hayo wamesema kuwa wameshiriki kwenye wiki ya Azaki mwaka huu kwaajili ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili waweze kufahamu shughuli zao ambazo kimsingi zimejikita katika kuwasaidia kupaza sauti zao na kuibua changamoto katika jamii ili Serikali iweze kuzifanyiakazi, na kwamba wao kama Azaki wanaona kuwa ushiriki wao kwenye Wiki ya Azaki utawapa fursa ya kuendelea kukuza mashirikiano baina yao.
Wiki ya AZAKI ni jukwaa pekee nchini linaloleta kwa Pamoja wadau wakuu wa maendeleo ikiwemo Serikali, Sekta binafsi na Asasi za Kiraia Pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu ustawi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla ambayo imezinduliwa rasmi leo) Octoba 23 na kufungwa tarehe 28, 2021
0 comments:
Post a Comment