A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, September 26, 2018

TAXIFY YAZINDUA HUDUMA ZAKE JIJINI DODOMA

IMG-20180925-WA0082
Huduma ya teknologia ya teksi inayoongoza Ulaya na Afrika ya Taxify leo imezinduliwa jijini Dodoma na mamia ya madereva teksi ambao wamesajiliwa na Taxify wameanza kutoa huduma kwa wananchi.

Huduma ya Taxify mjini Dodoma itatoa njia salama na ya bei nafuu kwa abiria kupata usafarishaji na usalama wa wateja umeongezeka kwa kutumia teknolojia ya “Share your ETA“ ambayo inampatia mteja fursa ya kutaarifu familia na marafiki safari yake na kuwahakikishia usalama wake.

Menjea Mkuu Tanzania Bw. Remmy Eseka amesema: "Baada ya kuzindua huduma yetu jijini Dar es Salaam na Mwanza, tunaendelea kupanua wigo wa huduma, na mji mkuu wa Dodoma ni mojawapo ya miji ya msingi katika soko letu. Tuna imani ya kwamba watanzania watanufaika na huduma zetu.”

Taxify imetua Dodoma na ofa mbalimbali ambazo zimelengwa kunufaisha madereva ambao wamejisajili na huduma yao. 

Kampuni imetoa mikopo ya simu za kisasa za kiganjani zitakazowawezesha madereva kujiunga na tukutmia teknologia hii katika kutoa huduma kwa wateja.

Katika hili madereva wamepatiwa fursa ya kulipia kwa awamu ya mwezi kwa mwezi kutokana na faida watakayopata kwenye biashara.

Aidha kampuni imeshirikiana na kampuni ya mafuta ya Total na kutoa punguzo la bei ya mafuta na bidhaa za Total kwa madereva wote ambao watajiunga na kadi ya Total.

"Tunafurahia kuwa wa kwanza kutoa huduma ya teknologia ya texsi mjini Dodoma na kuunganisha madereva mbalimbali na huduma yetu. Tuna uhakika teknologia yetu italeta urahisi na kupunguza ucheleshewaji  wa kutoa huduma katika jijini,”* alisema Shivachi Muleji, Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki.


Pia, kampuni imelenga kuwanufaisha madereva kwa kutoza ada ndogo ya kutumia teknologia yao kwa asilimia 15 tu,  ambayo ni zaidi ya nusu ya ada wa washindani wao nchini na kote duniani.

"Daima tunatafuta ushirikiano na fursa ambazo zitawezesha madereva kupata faida kubwa zaidi kwa kupunguza gharama za kufanya biashara. Tunaamini  kwamba  madereva watafurahia kazi yao na kutoa huduma bora kwa wasafirishaji.  Madereva tulionao wamefurahishwa na punguzo la gharama ya mafuta kwa kuwa punguzo ni la hapo papo kwenye pampu,"* alisema Remmy Eseka.

Kampuni ya taxify imeweka mipango ya kupanua wigo wa huduma katika Afrika Mashariki na inayomikakati ya kuleta huduma yao kwa madereva bajaji na pikipiki.
Share:

Thursday, September 13, 2018

TAASISI YA LEGAL SERVUCES FACILITY YAENDESHA SEMINA KWA WABUNGE JIJINI DODOMA


Meneja Mradi wa  Legal Services Facility LSF,  Ramadhan Masele (kushoto), akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba wakati wa kikao chakujadili namna watakavyoweza kushirikiana na serikali namna ya kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma na msaada wa kisheria kwa wananchi  hafla hiyo imefanyika jana  jijini Dodoma.
Meneja Mradi wa  Legal Services Facility LSF,  Ramadhan Masele, akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Wabunge Tanzania wameombwa kuunga mkono kazi za wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za msaada wa kisheria, ambao ni nguzo muhimu katika kuwasaidia mamilioni ya Watanzania kutoka katika vitendo vya kikatili, manyanyaso na udhalimu.
“Ni kweli kwamba wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za msaada wa kisheria wengine wamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaoteswa na kunyayaswa, lakini hawawezi kazi hii kwa ufanisi bila kusaidiwa au kuungwa mkono na watu kama vile wabunge,” Ramadhani Masele, Meneja wa Programu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria (LSF) wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya siku mbili kwa wabunge kuhusu wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za kisheria nchini, uliofanyika Dodoma jana.
LSF ni shirika lisilokuwa la kiserikali lilioanzishwa Mwaka 2011, linalofadhiliwa na Shirika la Kimataifa  la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID). LSF inatoa fedha kwa mashirika mbalimbali yanayotoa msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.
Lengo kuu la semina ya wabunge, ni kuwawezesha wabunge kujua masuala mbalimbali, ikiwemo namna wasaidizi wa kisheria wanavyotoa huduma zao, idadi ya wilaya wanazofanya kazi, na aina ya kesi wanazozishughulikia, msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria, kazi za LSF na ushiriki wake katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 17 ya Umoja wa Mataifana
Semina hii ya mafunzo inakuja wakati kuna ongezeko la matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu nchini, kama vile watu kuteswa, ukatili wa kijinsia, udhalilishaji wa kijinsia, kuwashambuliwa wanawake kwa kuwapiga, uporaji wa  ardhi na matukio mengine yanayofanana na hayo.
Kwa kupatia ufadhili kutoka LSF, wasaidizi wa kisheria na watoa msaada wa kisheria wameweza kuwasaidia wanawake, wanaume na wasichana maskini na makundi ya watu wengine wananyimwa haki zao, kupata huduma za kisheria kwa gharama nafuu au bila gharama yoyote na huduma bora za msaada wa kisheria na hivyo kupata haki zao, kwa mujibu wa meneja Mpango wa LSF.
“Lakini wasaidizi wa kisheria na watoa msaada wa kisheria wengine wangeweza kutoa huduma na kuwafikia watu wengi zaidi ambao haki zimeminywa au kuvunjwa kama wakiungwa mkono na wabunge,” aliongeza Masele, huku akisema kwamba  “wanawake na wanaume wanaoteswa, kudhalilishwa au kufanyiwa ukatili wa kijinsia, ambao haki zao za ardhi na mirathi zimevunjwa, wanaishi katika majimbo yanayoongozwa na wabunge wenyewe.”
Pamoja na mambo mengine, alisema semina ya mafunzo itawasaidia wabunge kufahamu masuala yanayohusu wasaidizi wa kisheria, jinsi wanavyofanya shughuli zao na jinsi gani wasaidizi wa kisheria wanavyoweza kushirikiana na wabunge kupanua wigo wa huduma za msaada wa kisheria.
“Lengo kuu kuwasaidia watanzania wengi wanaohitaji msaada wa kisheria na kupata haki zao zilizokiukwa. Ni muhimu kwa wabunge kuungana na wasaidizi wa kisheria kwa sababu wananchi wenye matatizo wanatoka katika majimbo yanayoongozwa na wabunge,” alisisitiza Masele.
Kwa mujibu wa maelezo ya LSF, semina hii itawawezesha wa bunge kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na wasaidizi wa kisheria, ambao kwa sasa wanafanya kazi katika wilaya 170 nchini, namna ya kuwasiliana nao, namna ya kupata huduma zao na kueneza taarifa za huduma zao majimboni kwao.
“Taarifa muhimu kama hizi zitarahisha kazi za wabunge na wasaidizi wa kisheria  katika kutatua matatizo/kero mbalimbali za wananchi katika majimbo yao—migogoro ya ardhi, ndoa na mimba za utotoni, mirathi, wanaume kutelekeza familia zao nk,” inasema sehemu ya taarifaya LSF.
Mada za kimkakati zilitolewa na wataalamu wa LSF kwenye semina iliyohudhuriwa na wabunge kutoka Kamati ya Kudumuya Bunge ya Katiba na Sheria na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Maendeleo ya Jamii.
Share:

Wednesday, September 12, 2018

KWA JAMBO HILI KCB BENKI MUNGU ANAWAONA

 Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh Felix Lyaniva akiongoza mamia ya wakazi wa m
Mbagala pamoja na wafanya kazi wa Benki ya KCB wakati wa hafla yakuazimisha siku ya usafi, hafla hiyo imefanyika maeneo ya viwanja vya Zakhem jijini Dar es Salaam jana.                       
Wafanya kazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa mbagala baada ya kukamilisha zoezi la kufanya Usafi.
02
Wafanya kazi wa Benki ya KCB wakishirikiana na wakazi wa Mbagala kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh Felix Lyaniva hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam jana.

Benki ya KCB Tanzania, Jumamosi ya tarehe 8 Septemba imefanya shughuli za usafi ikishirikiana na wakazi wa Mbagala katika eneo la Mbagala Zakhem ambapo benki hiyo imefungua tawi lake la 14 nchini hivi karibuni.

Clouds Media Group, Green WastePro Limited, kampuni ya kazoa na kuchakata taka pamoja na The Creative Company, kampuni kutengeneza matangazo ndiyo walikuwa washirika wakuu wa Benki ya KCB Tanzania katika zoezi hilo liliyopokelewa kipekee na wakazi wa Mbagala ambao pia walishiriki. Zoezi hilo la kufanya usafi pia lilipewa uzito kwa kuwepo kwa ofisi za uongozi za Wilaya ya Temeke ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Mazingira na Watendaji wa Kata na mitaa.

Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh. Felix Lyaniva ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, aliipongeza Benki ya KCB kwa juhudi na kufanikisha kuwaleta wadau mbali mbali pamoja na wananchi wa Mbagala kushiriki katika kufanya usafi. “Mlichokifanikisha leo si kidogo na ninawapongeza lakini pia iwe chachu ya kutaka kufanya zaidi katika jamii yenu, ni mfano  mzuri wa kuigwa hata na makampui mengine.” aliongeza Mh. Felix Lyaniva.

Afisa Mazingira wa Wilaya ya Temeke, Nd. Ally Hatibu aliwashukuru wakazi wa Mbagala kwa kuitikia wito wa Benki ya KCB. Alisema ni ishara njema inayoonyesha kwamba wakazi wa hao wanalipa kipaumbele swala la kutunza mazingira.”Ninawasihi kuendeleza kuukuza ushirikiano huu na kufanya shughuli endelevu za kutunza mazingira.” alisema.

Hafla hiyo pia ilitoa fursa pekee kwa mama ntilie wanaofanya shughuli zao katika maeneo yanayozunguka Tawi la Benki ya KCB Mbagala, kwa kutoa huduma ya chakula kwa washiriki zaidi ya 100 katika hafla hiyo. “Kutoa fursa hii kwa akina mama hawa ilikuwa na jambo la kusudi na tuliwafuata bayana na kuwaomba kushiriki. Tutaendeleza ushirikiano wa aina hii kwa wajasiriamali wote wanaolizunguka tawi letu hasa wakina mama.’’ Alisema Bi. Christine Manyeye, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Tanzania.

Kwa upande wake, Bi. Jamila Dilunga ambaye alikuwa muwakilishi wa mama ntilie waliohudhulia zoezi hilo, aliishukuru Benki ya KCB kwa fursa waliyotoa kwa wakina mama wa Mbagala.

 Alisisitiza kwamba hakuna sababu ya Mbagala Zakhem kuwa chafu hasa baada ya ujio wa Benki ya KCB inayojali mazingira na usafi wa eneo la biashara zao. Aidha, aliiomba Benki ya KCB kufanya swala la kuhamasisha usafi katika eneo hilo kuwa endelevu.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki. 

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro. 


Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
Share:

Tuesday, September 4, 2018

FROM DESPAIR TO TRIUMPH: A WIDOW’S JOURNEY TO HER RIGHTFUL INHERITANCE

Msegena displays the judgement on an inheritance case she had won and recovered her house and other properties left by her deceased husband. Geita paralegals helped her claim her inheritance rights.


Under the Constitution of Tanzania every person is entitled to owning property, a right extended equally to both men and women and governed by the provisions of the Land Act and the Village Land Act. One would therefore rightly assume that this is a straight-forward, clear-cut situation; well, not quite. Incidents of widows losing their inheritance rights after the demise of a husband remain a serious problem in many societies across the country.

In the north-western region of Geita, Ms. Msegena Jeremia lost her husband in 2015 leaving her with the sole responsibility to bring up six children. while still overwhelmed by the pain of losing her husband, members of her clan convened an inheritance distribution meeting, a gathering that would ultimately and without her consent impose the destiny of any valuable assets.

Customarily, the eldest male child is placed in charge of any assets left behind by a deceased father and in Msegena’s case Joshua, a stepson and the eldest of the six children became the overseer of the assets which included a house, money deposited in a bank account and a motorcycle. Joshua was instructed to immediately withdraw TShs.1.9 million from the bank account and after opening an account for each of his siblings deposit an agreed amount into each account. The house and motorcycle would be sold.

This was to be the beginning of what seemed like a series of problems for Msegena. To her utter surprise, Joshua deposited all the money in his bank account and when she confronted him about this breach she said he attacked her physically and threatened to chop her hands off. With relations between the two of them deteriorating her husband’s relatives came together and began forcing her out of her matrimonial home.

“Joshua went so far as to lock me out of the house forcing me to spend two nights outside with no regard for my safety whatsoever. On the third day I couldn’t take it anymore so I went into town to seek any help I could get,” said Msegena with tears welling in her eyes.

In town she knocked on every door she believed would open for her to lay down her tons of burdens – from local community leaders to the police and finally the court. One of her attempts at seeking relief through the court and reclaim the inheritance hit a dead end when Joshua, now loaded with cash, bribed the magistrate who went on to rule in his favor.

Not every member of her late husband’s family wasn’t touched by what she was going through and at this point her sister-in-law, Safi, who apparently knew of a Geita-based paralegal, Bernard Mosira decide to help Msegane by introducing her to Bernard for further assistance. The rescue came to Msegena through Bernard Mosira who took up the case and immediately established communication with her.

“I called Bernard and explained my problem. He advised me to return home and promised me that he would remain in touch with me and that he will pursue my case”, she said.

Upon setting foot home however, the village chairman convened a traditional meeting traditionally known as “Nzengo” to isolate and force her out of the village on the fabricated claim that she engaged in untoward practices and was hence unfit to be part of the village.

On hearing the startling news Bernard travelled to the village the next day and approached the local leaders to at least help Msegena to start settling down again and get on the path to being in full control of her life, while also pointing the leaders to the consequences of their actions.

Seeing an open call to empower Msegena, Bernard used this experience to educate her on relevant provisions of the law, her rights and her responsibilities.

Armed with a new understanding and ripe confidence, she reported the maltreatment Joshua put her through to the local police station and within days he was apprehended and appeared before the primary court.  The court ruled in her favour ordering the clan members and her late husband’s relatives to desist from selling the house as intended, and effectively declared her its legal owner and of the motorcycle.

“During the hearing, I spoke like someone who knew the law, and people, particularly the magistrate and police, were surprised and wondered where I got such knowledge. I surely didn’t look convincing to anyone” stated Msegana.

“we are delighted to know the importance of observing laws and we have gone as far as inviting Bernard and his team and they have come up here twice now to provide legal education during our regular village meetings”, added the elder.

Msegena’s story paints a vivid picture of how effective legal education can be, often drawing two sides that were once polarized closer and closer and ultimately helping them find common ground under the canopy of the law. It makes a strong case for the sensitization of women’s rights and also the banishing of unjust customs and traditions.

Msegena, now a legally-empowered and free woman leads an improved life raising poultry and growing crops on land spreading out at the back of her house. The motorbike she once had no hope of ever seeing again now ferries people between nearby villages earning her extra income and allowing her to provide for her family.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive