A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


 • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

  CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

 • TIB slashes losses, bad loans up!

  TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

 • MALINZI blesses TFF elections

  THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

 • Barrick, government talks next week

  BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, November 30, 2023

MKAZI WA KINONDONI MANYANYA AJISHINDIA PIKIPIKI KUPITIA DROO YA Y9 MICROFINANCE

 

Meneja Masoko wa Taasisis ya Kifedha ya Y9 microfinance Bi Sophia Mang’enya (kulia), akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya nane Bw.Anold Jacob ambae aliibuka mshindi  wakati wakuchezesha droo hiyo wiki iliyopita ikiwa nimuendelezo wa Taasisi hiyo kutoa zawadi kila wiki kwa wateja wake wa Pakua APP ya Y9 na ukope na ulipe kwa wakati ili kuingia kwenye droo na ushine zawadi ya simu janja na pikipiki. hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika nyumbani kwa kina  Anold kinondoni manyanya jijini Dar es Salaam. Na baada ya wiki mbili itachezeshwa droo kubwa ambapo mshindi atajinyakulia Gari mpya kabisa Toyota Ist.

Meneja Masoko wa Taasisi ya Kifedha ya Y9 microfinance Bi Sophia Mang’enya (kulia), akizungumza wakati wa hafla yakukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya saba Anold Jacob ambae aliibuka mshindi  wakati wakuchezesha droo hiyo wiki iliyopita ikiwa nimuendelezo wa Taasisi hiyo kutoa zawadi kila wiki kwa wateja wake wa Pakua APP ya Y9 na ukope na ulipe kwa wakati ili kuingia kwenye droo na ushinde zawadi ya simu janja na pikipiki hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika nyumbani kwa kina  Anold kinondoni manyanya jijini Dar es Salaam na baada ya wiki mbili itachezeshwa droo kubwa ambapo mshindi atajinyakulia Gari mpya Toyota Ist.

Mshindi wa pikipiki wa wa Pakua APP ya Y9 Microfinance ushinde Bw. Anold Jacob akionesha ufunguo wa pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Masoko wa Taasisis ya Kifedha ya Y9 microfinance Bi Sophia Mangenya wakati wa hafla yakukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya nane . Na baada ya wiki mbili itachezeshwa droo kubwa ambapo mshindi atajinyakulia Gari mpya Toyota Ist.

Mshindi wa pikipiki wa wa Pakua APP ya Y9 Microfinance ushinde Bw. Anold Jacob akionesha plate namba na kadi ya pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Masoko wa Taasisis ya Kifedha ya Y9 microfinance Bi Sophia Mangenya wakati wa hafla yakukabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya nane . Na baada ya wiki mbili itachezeshwa droo kubwa ambapo mshindi atajinyakulia Gari mpya Toyota Ist
Share:

Wednesday, November 29, 2023

Sabasaba Moshingi, kuipeleka DCB kwenye kilele cha mafanikio

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya Biashara ya DCB, Bwana Sabasaba Moshingi (katikati), akizunguza mara baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Bi. Zawadia Nanyaro (kushoto kwake), kumtambulisha rasmi jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa Benki, Bi. Regina Mduma, Mkurugenzi wa Biashara, Bi. Lilian Mtali na Ofisa Fedha Mkuu, Bwana Deusdedit Mulindwa.

Benki ya Biashara ya DCB, moja kati ya benki kongwe inayoongoza katika mabenki yenye ukubwa wa kati, imemtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wake mpya katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Akizungumza, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro alimtambulisha Bwana Sabasaba Moshingi, kuchukua nafasi hiyo adhimu ya kushika usukukani wa kuongoza benki hiyo akisema, licha ya mchakato kuchukua muda mrefu lakini kama benki pamoja na wanahisa wake wanayo furaha kwa kumtapata mtu anayekidhi vigezo walivyohitaji.

Benki yetu, wateja wetu pamoja na wanahisa wake walihitaji mtu sahihi atakayesukuma mbele vyema gurudumu la maendeleo la DCB, kwa weledi, umakini na uhakika zaidi, atakayeweza kuitoa DCB mahali ilipo na kuipeleka mbele zaidi kimafanikio, na baada ya kupitia hatua na taratibu kadhaa Bodi na Menejimenti ya DCB zina kila sababu ya kutembea vifua mbele kwa kumpata mtu sahihi ambaye kutokana na ukongwe wake katika tasnia za kibenki na taasisi za fedha tuna imani matarajio yetu yametimia."

Bwana Moshingi ni Mtaalamu mbobevu katika masuala ya benki kwa zaidi ya miaka 12, Bwana. Moshingi, analeta pamoja naye hazina kubwa ya uzoefu katika tasnia za kibenki za Kitaifa na Kimataifa akiwa na rekodi thabiti katika Uendeshaji wa Benki, Biashara za Fedha, Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi, Masuala ya Mikopo na mengineyo."

Bwana Moshingi ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara katika Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amethibitishwa na Taasisi ya Mabenki Tanzania na kabla ya uteuzi wake wa sasa, Bw. Moshingi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB akishika pia nafasi mbalimbali za uongozi katika benki za, Standard Chartered, Stanbic na KCB."

Ni matumaini ya benki yetu, wateja wetu na wanahisa wetu kuwa ujio wa Bwana Moshingi umekuja kwa wakati sahihi na kutokana na historia iliyotukuka ya mafanikio aliyoyapata katika taasisi alizowahi kufanya kazi, tunaiona benki yetu ikizidi kupanda kila siku kuelekea katika kilele cha mafanikio”, alisema Bi Zawadia.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya benki, Bi Zawadia alisema DCB inazidi kupiga hatua siku hadi siku ikizidi kuendeleza jukumu mama la kuanzishwa kwake tokea miaka 21 iliyopita likiwa ni kutoa huduma bora za kifedha ikijikita zaidi katika kusaidia miradi endelevu ya kupunguza umasikini na kuendeleza jamii kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu kwa wateja.

Alisema Benki ya DCB kwa miaka 21 imepiga hatua mbalimbali za kimaendeleo ikikuza mtaji wake kutoka kiasi cha shs Bilioni 1.7 ilipoanzishwa hadi kufikia kiasi cha shs Bilioni 27.5 kwa sasa, maendeleo hayo yalichangia mabadiliko mbalimbali katika benki ikiwa ni pamoja na kutoka kuwa Benki ya Kijamii hadi kuwa Benki kamili ya Biashara.

Benki yetu imeendelea kunyanyua wajasiriamali wengi wadogo kiuchumi ambao hawakuwa na namna ya kupata mitaji huku DCB ikiwa mstari wa mbele katika kutoa mikopo ikiwemo mikopo ya vikundi kwa wajasiriamali wadogo, mikopo ya biashara kwa wafanyabiashara wa kati na wakubwa."

Benki yetu imeendelea kupata faida mwaka hadi mwaka, kwa mwaka jana benki ilipata faida baada ya kodi ya shs 747 milioni, faida iliyochangiwa na mapato yasiyotokana riba ya shs 10.3 bilioni ambayo ni mafanikio ya asilimia 111 ya malengo tuliyojiwekea kwa mwaka 2022, huku mapato yatokanayo na riba yakifika shs 28.6 bilioni ikiwa ni asilimia 86 ya malengo tuliyojiwekea."

Akizungumza zaidi Bi Zawadia alisema “mali za benki zimekuwa hadi kufikia shs 227 bilioni hadi kufikia Septemba mwaka huu, kutoka shs 132 bilioni kwa mwaka 2018. Tukijivunia ukuaji huu ulioitoa benki yetu kutoka kwenye kundi la benki ndogo za biashara hadi kufikia benki za ukubwa wa kati nchini. Haya ni mafanikio makubwa ambayo ni matumaini yetu Mkurugenzi Mtendaji wetu mpya Bwana Sabasaba Moshingi ataendelea kushika usukani wa DCB kwa ustadi mkubwa kwa ukuaji zaidi wa benki yetu."

Benki ya DCB itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wananchi wengi zaidi wa maeneo ambayo hakuna matawi ya benki wanafikia na huduma za kifedha, ikienda sambamba na vipaumbele vya benki yetu kuhakikisha huduma zetu bora za kibenki zinapatikana nchi nzima na hii inatikana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika huduma zetu za kibenki kwa njia za kidigitali, hususan DCB Wakala na DCB Kidigitali inayowawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kibenki mahali walipo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti."

Huduma mbalimbali za kibenki zinapatikana kwa njia ya kidigitali mfano DCB Pesa ambayo mteja anaweza kufanya malipo na manunuzi kama vile, kuweka akiba au kutoa pesa, kulipa bili ya maji au umeme, kulipia ving’amuzi na pia kufanya malipo malipo ya serikali."

Aidha Mwenyekiti huyo wa Bodi alitaja baadhi ya huduma na akaunti zinazoendesha na benki hiyo kama kaunti ya elimu ya DCB Skonga, Wahi Akaunti kwa wenye mahitaji ya kutimiza malengo kwa njia ya kuwekeza kidogo kidogo, Akaunti za Mshahara & mikopo ya nusu mshahara, akaunti ya Wastaafu, Mikopo ya Nyumba, Lamba Kwanza na nyinginezo nyingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo, Bwana Sabasaba Moshingi alitoa shukurani zake kwa Bodi ya Wakurugenzi na Wanahisa wa benki hiyo kwa kuwa na imani naye akiahidi kutumia uzoefu wake wa miaka 21 alioupata katika kutumikia taasisi mbalimbali za fedha kuiinua DCB kutoka mahali ilipo na kuipeleka mbali zaidi.

Alisema anajua matarajio ya wateja wa DCB, wanahisa wao, Bodi, wafanyakazi, wateja pamoja na wadau, ni matumaini yake kuwa kwa kutumia uzoefu alionao pamoja na ushirikiano wa wadau wote wataweza kutimiza matarajio makuu ikiwa ni kutoa huduma bora za kifedha zinazolingana na mahitaji ya wateja na kutoa huduma bora zenye kiwango cha kimataifa.

Nikiwa na uzoefu wa miaka mingi katika maeneo ya biashara za kifedha, mikopo na wateja binafsi, ni matumaini yangu kuwa kwa pamoja tutaendeleleza azma hii kwa kutoa suluhu nyingi zaidi za mitaji kwa wafanyabiasha wadogo na wakati na pia kuliangalia kwa jicho la pembeni uboreshaji wa huduma za kifedha kwa njia za kidigitali ili zilingane na mahitaji ya watanzania lakini pia ziwe na ubora wa kimataifa."

Nina imani kwa ushirikiano wa pamoja hakuna kitakachoshindikana, maendeleo niliyoyapata katika taasisi nilikotoka, yanawezekana na hapa pia, tukae tayari kwa biashara."

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi na Waandishi wa Habari, Kwa kuwa leo sio siku yangu, ni siku ya Mwenyekiti wetu, ni siku tu ya kutambulishwa kwangu, ningeomba niishie hapa ili panapo majaliwa ya Mungu basi tutawaita tena ili tuweze kuzungumza pamoja kuhusu maendeleo ya benki yetu ukizingatia kuwa wengi kati yenu tunafahamiana vizuri tokea huko nyuma”, alisema Bwana Moshingi.
Share:

Saturday, November 25, 2023

SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI, MAGONJWA YA NGONO NA HOMA YA INI

 

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalim akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi, magonjwa ya ngono na homa ya ini uliozinduliwa leo.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani Nchini Tanzania, Bw. Sagoe Moses akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi magonjwa ya ngono na homa ya ini uliozinduliwa leo na Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalim ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Mratibu Mwandamizi Ofisi ya Uratibu wa PEPFAR Ubalozi wa Marekani Nchini Dk. Hiltruda Chrisant Temba akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi, magonjwa ya ngono na homa ya ini uliozinduliwa Leo na Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalim ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalim pamoja na viongozi mbalimbali wakiserikali na wadau wa sekta ya afya wakikata utepe kuashiria Uzinduzi rasmi wa mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi, magonjwa ya ngono na homa ya ini uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Serikali imedhamiria kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto pamoja na kuzuia maambukizi mapya ya ukimwi kwa kundi la vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24 kutokana na takwimu kuonyesha kuwa kundi hilo la vijana ndilo linaloathirika zaidi na maambukizi hayo.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa Taifa wa kudhibiti ukimwi, magonjwa ya ngono na Homa ya ini jijini Dar es salaam Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema licha ya hatua kubwa ambayo serikali na wadau wa masuala ya afya iliyopigwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi ikiwemo kupungua kwa maambukizi lakini bado makundi hayo yanahitaji nguvu zaidi katika kuyasaidia dhidi ya ugonjwa huo.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amebainisha kuwa bado kuna ongezeko kubwa la maambukizi ya magonjwa ya ngono na Homa ya Ini nchini hivyo serikali inakuja na mpango mkakati wa wa kuhakikisha kutokomeza maambukizi hayo.

Waziri ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita imeboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya taifa hadi msingi kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu zaidi na maeneo yao

“Serikali kupitia Wizara ya Afya wadau wa sekta na wataalamu wengine tayari wamefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na bunge na semina zimefanyika kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kuhusu umuhimu wa bima za Afya kwa wote”.

“Kwa sasa nchi yetu iko mbali katika utoaji wa huduma, kuna vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa, huduma nyingi za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini lakini pia huduma za Afya zimesogezwa sana kwa wananchi hivyo kama serikali tuko tayari kutekeleza na kuhakikisha kuwa tunaendelea kuboresha huduma za afya kote nchini”.

Nayo baadhi ya mashirika ya kimataifa ambayo ni Shirika la La afya la Kimataifa WHO pamoja na Shirika la misaada la Marekani UNAIDS yaliyohudhuria uzinduzi huo kupitia kwa wawakilishi wao wamesifu juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muuungano waTanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi na kusema wataendelea kuunga mkono juhudi hizo
Share:

Friday, November 24, 2023

MTEJA WA Y9 MICROFINANCE AJISHINDIA PIKIPIKI KWA MKOPO WA BUKU MBILI

 

_L5A2403

Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya Kifedha Y9 Microfinance Fredrick Mtui (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya saba kwa njia ya simu Anorld Jacob na Jekapo ambaye amejishindia simu janja wote ni wakazi wa Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa Y9 kutoa zawadi kila wiki Kwa wateja wake. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani ni Meneja Masoko ya Taasisi hiyo Bi. Sophia Mang'enya pamoja na mshindi wa pikipiki Wa droo ya sita Bw Baraka Bazarae (kushoto).

_L5A2489Meneja Masoko ya taasisi Bi Sophia Mang'enya akimkabidhi zawadi ya pikipiki mmoja kati ya washindi wa droo ya sita Baraka Bazarae katika hafla ya uchezeshwaji wa droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

_L5A2481Mshindi wa pikipiki Droo ya sita ya Y9 Microfinance Baraka Bazarae Katikati akizungumza wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya saba iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance Fredrick Mtui (kulia) na Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi (kushoto).

_L5A2495Meneja Masoko ya Taasisi ya Kifedha ya Y9 Microfinance Bi Sophia Mang'enya (kulia), akimkabidhi zawadi ya pikipiki kwa mshindi wa droo ya sita Baraka Bazarae ambae aliibuka kidedea wakati wakuchezesha droo ya sita wiki iliyopita makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa yakuchezesha droo kwaajili ya kutafuta washindi wa droo ya Saba. Kushoto ni Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi (kushoto).Washindi wa Droo ya saba ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Anorld Jacob na mshindi wa simu Jekapo wote wakiwa ni wakazi wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Mkurugenzi wa mauzo na usambazaji taasisi ya kifedha Y9 microfinance Fredrick Mtui ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.

Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ilikuwa ni kuhakikisha kuwa kila mteja wa Y9 microfinance anapata nafasi ya kushiriki na kushinda katika droo inayochezeshwa kila wiki.

Alitoa wito kwa watanzania kujiunga na Y9 microfinance ili kupata huduma za kifedha kwa urahisi pia kujiweka katika nafasi nzuri za ushindi.

Alieleza kuwa sasa tunakwenda ukingoni Kwenye uchezeshaji wa droo hizi tuliahid Kwa watanzania kuwa tutatoa pikipiki 8 na simu 8 hivyo hadii sasa washindi Saba wa pikipiki na wasimu janja wameshapatikana.

Aliongezea kwa kusema "Hadi sasa tumeshatoa zawadi ya pikipiki sita na simu sita na mshindi wa Saba pikipiki na simu wameshapatikana hivyo tumesalia na droo Moja yakutoa zawadi ya pikipiki na simu ili kumamilisha Ile ahadi tuliyotoa".

Mtui amewakumbusha watanzania kuwa "sasa tunakwenda mwisho wakuchezesha droo zetu hivyo niwasihi nduguzangu wakati wako ni sasa tumia App ya Y9 Microfinance ili upate mkopo Kwa njia rahisi pia kujishindia zawadi mbalimbali".

"Baada ya droo yetu ya nane kukamilika tutakwenda kuchezesha droo kubwa ambapo mchindi ataondoka na ndinga mpya kabisa Toyota Ist hii sio ya kukosa endelea kupakuwa app yetu kopa na ushinde".

Alieleza namna ya kushiriki ni rahisi hakikisha umepakua app ya Y9 microfinance kisha kujisajili na kuanza kukopa na moja kwa moja utaingia kwenye droo hii baada ya marejesho.

Kwa upande wake Mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Salim Buguvi ameeleza "kama bodi ya michezo ya kubahatisha nchini tumeridhishwa na namna ya uchezeshwaji wa droo hii na uhalali katika upatikanaji wa washindi”.
Share:

Thursday, November 23, 2023

Airtel, itel washirikiana kuzindua simu janja mpya na ya kisasa aina ya A70

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania, Bwana Jackson Mmbando, akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu mpya aina ya Itel A70 AWESOME ya kampuni Itel kwa ushirikiano na Airtel katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania, Bwana Jackson Mmbando (kushoto) Meneja Bidhaa wa Kampuni ya Itel, Bwana Thomas Wang (wa pili kulia), pamoja na wengine kutoka kampuni hizo, wakipozi wa picha ya 'selfie' katika hafla ya uzinduzi wa simu mpya aina ya Itel A70 AWESOME ya kampuni Itel kwa ushirikiano na Airtel katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

• Wateja wa Airtel kuunganishwa na GB 75 kwa miezi kumi na 12 wakinunua simu ya Airtel katika maduka ya Airtel na itel popote nchini
• Ni toleo maalum kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel leo kwa pamoja wameshirikiana wamezindua simu mpya ya itel A70 iliyoambatanishwa na ofa ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha BURE cha GB 75 ambacho kinadumu kwa muda wa miezi kumi na mbili.

Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya kisasa kabisa yenye ofa kabambe, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema “Tunajivunia ushirikiano wa Airtel na itel kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A70".

Wenzetu wa itel wanalenga kuhudumia wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuu, hivyo basi Airtel ikiwa moja ya makampuni yanayotoa huduma za smartphone za kisasa na uhakika, tukaona tuwafikishie ofa hii kabambe watanzania wote ili kuwawezesha kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wetu ulio bora na ulioenea kote nchini na simu ya itel.

Simu ya A70 itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini ikiwa na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 75GB kwa muda wa miezi kumi na mbili.

Kwa upande wake, Meneja wa Chapa wa itel kutoka itel Mobile Bw, Thomas Wang, alisema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A70 ambayo ni Smartphone ambayo ni toleo la kisasa na inapatikana kwa bei nafuu kabisa Tanzania nzima.

Simu ya A70 ni nyepesi sana na inatoa suluhisho bora kwa watumiaji wa huduma za kidigitali kwa uhakika na haraka kabisa itapatikana kwa gharama nafuu,

Aliongeza kuwa simu ya itel A70 ina uwezo wa 128GG ROM + 8GB RAM, 6,6” na ukubwa wa kioo wa 13MP super HDR CAM. Hivi vyote kwa pamoja vinampa mtumiaji kufarahi matumizi ya simu hii pamoja na kumpa Uhuru wa mawasiliano.

‘Sababu kubwa ya ushirikiano baina ya Airtel na itel ni kuwapa Watanzania kuwa na uwezo wa kutumia smartphone za kisasa zenye ubunifu wa hali ya juu kwa gharama nafuu pamoja na kufurahi kifurushi cha intaneti cha 75GB kutoka Airtel kwa mwaka mzima.
Share:

Friday, November 17, 2023

Shirika la USAID laipongeza serikali ya Tanzania mafanikio katika miradi ya elimu na afya nchini

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bwana Craig Hart (kushoto), akikabidhi mipira kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Njia Panda, Bi. Tatu Mohamedi (kulia), wakati wawakilishi wa USAID, Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR) pamoja na mashirika yanayosimamia miradi inayotoa huduma kwa wagonjwa wa VVU inayofadhiliwa na mfuko huo, wakitembelea shule hiyo kuangalia maendeleo ya miradi ya USAID Kizazi Hodari Kusini, inayotekelezwa na Shirika la Deloitte shuleni hapo, Iringa, jana. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Mradi wa Kizazi Hodari, Bi. Dorothy Matoyo, Mkurugenzi Msaidizi wa USAID kitengo cha afya nchini, Bi. Anna Hofmann na Kaimu Ofisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Iringa, Samweli Mtovagakye. Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa PEPFAR.
Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kusini, Bi. Dorothy Matoyo, akitoa maelezo kuhusu mafanikio ya mradi huo unaoendeshwa na Shirika la Deloitte, wakati wawakilishi wa USAID, PEPFAR, pamoja na mashirika yanayosimamia miradi inayotoa huduma kwa wagonjwa wa VVU inayofadhiliwa na PEPFAR, wakitembelea shule ya msingi Njia Panda, kuangalia maendeleo ya afua mbili za wanafunzi wasichana ya Dreams na wavulana ya ‘coaching boys into men' (CBIM) shuleni hapo, Iringa, jana.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Bwana Craig Hart (katikati), akiangalia michoro inayotumika kufundishia afua za Dreams na CBIM kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Njia Panda shuleni hapo jana. Afua hizo zinahusu elimu ya uzazi, maambukizi ya VVU, tabia njema na stadi za maisha ikiwemo elimu ya kifedha. Miradi hiyo imechangia ufaulu wa shule hiyo kwa mwaka 2022, darasa la saba ufaulu ukiwa ni 97% huku darasa la nne ukiwa ni 93%.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Bwana Craig Hart, akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Njia Panda mjini Iringa, alipokwenda pamoja na ujumbe wake kukagua miradi ya USAID Kizazi Hodari Kusini inayofadhiliwa na Mfuko wa PEPFAR.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Bwana Craig Hart (kulia), akiagana na Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kusini, Bi. Dorothy Matoyo (wa pili kushoto), mara baada ya kutembelea Shule ya Msingi Njia Panda kuangalia maendeleo ya inayosimamiwa Shirika la Deloitte kupitia mradi wa Kizazi Hodari Kusini, chini ya ufadhili wa Mfuko wa PEPFAR.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), Bwana Craig Hart (katikati), pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa USAID kitengo cha afya nchini, Bi. Anna Hofmann (wa pili kushoto), wakipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya mabinti wanaohudumiwa na mradi wa EpiC unaosimamiwa na Shirika la FHI360 kwa ufadhili wa Mfuko wa PEPFAR, wakati wawakilishi wa USAID na PEPFAR nchini wakifanya ziara mkoani Iringa kuangalia maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na mfuko huo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa PEPFAR. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa USAID.
Mkurugenzi wa Shirika la FHI360, Bwana Bernard Ogwang, linalosimamia mradi wa EpiC, akitoa maelezo kuhusu mafanikio ya mradi huyo katika kutoa huduma kwa wenye VVU.
Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Bwana Craig Hart (katikati kulia), akiangalia ubunifu wa kazi za mikono za mmoja wa mabinti wenye VVU wanaohudumiwa na mradi wa EpiC chini ya usimamizi wa Shirika la FHI360 mjini Iringa wakati wa ziara ya wawakilishi wa USAID, PEPFAR, mashirika yanayosimamia miradi ya USAID pamoja na waandishi wa habari kuangalia maendeleo ya miradi hiyo mkoani humo.

Na Zuhura Rashidi, Iringa

SHIRIKA la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), limeipongeza Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, chini ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa zinazofanyika katika kuboresha maendeleo ya miradi ya afya na elimu nchini.

Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID, Bwana Craig Hatz, katika Shule ya Msingi Njia Panda Mkoani Iringa wakati akihitimisha ziara ya siku tatu ya wawakilishi wa shirika hilo na wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR), pamoja na mashirika yanayosimamia utekelezaji wa miradi ya ukimwi inayofadhiliwa na PEPFAR.

Akihitimisha ziara hiyo ambayo pamoja na mambo mengine ilienda pamoja na maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa PEPFAR, Bwana Hart alisema jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na USAID, PEPFAR, zimechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya miradi yote inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia USAID kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita.

Serikali ya Marekani kwa zaidi ya miaka 20 imewekeza zaidi ya USD Bilioni 6 nchini Tanzania, kuhakikisha tunashirikiana pamoja na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi, wazazi na familia kukabiliana na HIV/AIDS."

Dola bilioni 6 inaweza kuonekana nyingi, Mwaka 2000 hadi 2019 umri wa kuishi kwa mtanzania uliongezeka kwa miaka 15, ikimaanisha sasa watanzania wote wameongeza umri wao wa kuishi kwa miaka 15 zaidi, wadau wote hawa wameungana kwa ajili yako, mpo katika mazingiza bora, mnapata elimu pamoja na elimu bora ya afya, muhimu sana kwa Tanzania ya kesho, maisha yako na maisha yetu ya baadae”, alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kusini, Bi. Dorothy Matoyo alisema wao kama Deloitte wanayo furaha kupata uwezo wa kuchangia katika maendeleo ya kizazi chenye furaha na kinachojiamini na ndipo jina lao lilipotokea.

Kizazi tunachokiangalia sasa tunatumaini baada ya miaka 10 ama 20 ijayo kitakuwa kizazi salama chenye kujiamini, chenye upendo, kujua jinsi ya kujilinda na VVU, unyanyapaa na ukatili wa kijinsia."

Deloitte kupitia mradi wa Kizazi Hodari Kanda ya Kusini, ni wajibu wetu kuhakikisha tunawasaidia watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu katika kuwaunganisha katika vituo watakavyoweza kupata usaidizi”, alisema Bi Dorothy.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Njia Panda, Bi. Tatu Mohamedi alisema alisema shuleni hapo chini ya uratibu wa Mradi wa Kizazi Hodari Kusini, wanajishughulisha na afua mbili za ‘Dreams’ kwa wanafunzi wa kike na ‘Coaching Boys Into Men’ (CBIM) ambapo jumla ya watoto wa kike 235 na wa kiume 204 wamenufaika na mpango wa mafunzo katika afua zote mbali.

Afua hizi zinalenga kuwasadia watoto kujitambua, kujithamini na kujiheshimu hivyo watoto hawa wamepata mafunzo kuhusu ugonjwa wa ukimwi, afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia na kuondokana na unyanyapaa kwa wale wenye virusi."

Miradi hii imeleta mafanikio makubwa hata kwa wanafunzi wetu kitaaluma, kupitia USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kusini wamesaidia vifaa vya shule kama madaftari na kalamu kwa watoto wa kike 235 kwa lengo la kuwasaidia watoto hao kufanya vizuri katika mitihani yao”, alisema mwalimu huyo.

Mkurugenzi wa Shirika la FHI360, Bwana Bernard Ogwang alisema shirika lao linalosimamia mradi wa EpiC kwa ufadhili wa USAID na PEPFAR, limechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya vijana wa kike na wa kiume wanaoishi katika mazingira hatarishi ya kupata Virusi vya ukimwi.

Katika mikoa 11 tunayohudumia, tuna idadi ya vijana wa kike na wa kiume 225 wanaopata huduma kamili ya kinga na tiba ya VVU, lakini pia vijana hawa hujishughulisha katika shughuli za kiuchumi ili waweze kuboresha maisha yao”, alisema.

Baadhi ya mabinti wenye VVU wanaopata huduma kupitia mradi wa EpiC wakitoa ushuhuda ni jinsi gani miradi ya Mfuko wa PEPFAR imeboresha maisha yao mara baada ya kugundua hali zao na kujiunga katika vituo vya huduma na tiba walisema moja ya changamoto zinazochangia kutojitokeza kwa watu wengi kupima virusi vya ukimwi ni unyanyapaa unaotokana na imani, mila potofu na kukosa elimu sahihi juu ya ugonjwa wa ukimwi.
Share:

Thursday, November 16, 2023

ROTARY TANZANIA KUENDESHA KAMBI YA MATIBABU BURE KWA WAKAZI WAA BUNJU.

 

Rais wa Rotary Club upande wa Oystarbay jijini Dar es Salaam Abdulrahman Hussein (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitangaza fursa ya kutoa huduma ya afya na matibabu bure kwa wakazi wa Bunju ikiwa ni muendelezo wa Rotary kusaidia jamii hasa katika sekta ya afya hii imekuwa ni utaratibu wa Rotary kujitolea kuhakikisha wanasaidia watu ambao wanamatatizo mbalimbali ya kiafya na kukosa uwezo wakujitibu. Hafla hiyo hiyo imefanyika leo masaki jijini humo wengime pichani ni Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Diamond Carvalho pampja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi Mehreen Khatri.


Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Diamond Carvalho (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitangaza fursa ya kutoa huduma ya afya na matibabu bure kwa wakazi wa Bunju ikiwa ni muendelezo wa Rotary kusaidia jamii hasa katika sekta ya afya hii imekuwa ni utaratibu wa Rotary kujitolea kuhakikisha wanasaidia watu ambao wanamatatizo mbalimbali ya kiafya na kukosa uwezo wakujitibu. Hafla hiyo hiyo imefanyika leo masaki jijini humo wengine pichani ni Rais wa Rotary Club upande wa Oystarbay jijini Dar es Salaam Abdulrahman Hussein pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi Mehreen Khatri.


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Bi Mehreen Khatri(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wakitangaza fursa ya kutoa huduma ya afya na matibabu bure kwa wakazi wa Bunju ikiwa ni muendelezo wa Rotary kusaidia jamii hasa katika sekta ya afya hii imekuwa ni utaratibu wa Rotary kujitolea kuhakikisha wanasaidia watu ambao wanamatatizo mbalimbali ya kiafya na kukosa uwezo wakujitibu. Hafla hiyo hiyo imefanyika leo masaki jijini humo wengime pichani ni Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Diamond Carvalho pamoja na Rais wa Rotary Club upande wa Oystarbay jijini Dar es Salaam Abdulrahman HusseinMamia ya wakazi wa Bunju na maeneo ya Jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi Novemba 18 2023 katika viwanja vya shule ya msingi bunju kupima afya zao katika kambi maalum ya afya itakayoendeshwa na Rotary Tanzania.


Rotary ikishirikiana na wadau mbalimbali wa afya na wafadhili, wataendesha huduma hiyo siku nzima ya Jumamosi Novemba 18, ili kuwawezesha wakazi wengi wa Bunju, maeneo ya Jirani na Dar es Salaam kwa ujumla kupata mud awa Kwenda kupima afya zao na kupata ushauri wa kitaalamu bure bila malipo yoyote.


Hayo yameelezwa na Diamond Carvalho, Mwenyekiti wa Rotary Tanzania wakati akizungumza na waandishi wa habari masaki jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea kuhusu maandalizi ya kambi hiyo ya siku moja itakayofanyika Bunju jijini Dar es Salaam.


Inakadiriwa kuwa kuna wanafunzi 3500 na watu wazima 1500 watakaoshiriki, na kila mmoja wao atapata huduma muhimu kama vile vipimo, na elimu ya afya na kinga, uchunguzi wa macho, uchunguzi wa saratani mbali mbali, ukaguzi wa meno, elimu ya hedhi salama, na fursa ya kupata chanjo, dawa na rufaa za wataalamu kama itahitajika.


Kwa moyo wa kujitolea, madaktari takribani 100 wakiwemo madaktari wa kawaida 50 na wataalamu wengine 50 wa meno, Macho, Ngozi, Watoto, na huduma nyingine wameahidi kutoa msaada wao kwa kutoa huduma hizi muhimu wakishirikiana na timu kubwa ya wahudumu takribani 500 inaunga mkono juhudi hizi, na ushirikiano huu unasisitiza umuhimu wa upendo na umoja katika kukabiliana na mahitaji ya afya ya jamii.


Diamond Carvalho, , ameeleza, kuwa “Rotary Tanzania, kwa kushirikiana hasa na Klabu ya Rotary ya Oysterbay, imekuwa ikiandaa kambi za matibabu kwa ushirikiano na Klabu ya Rotaract ya Kairiuki tangu mwaka 2012, lengo likiwa kutoa huduma za afya msingi kwa jamii ya Dar es Salaam. Kampeni ya afya ya leo inaadhimisha hatua muhimu sana, ikiwa imeongezeka mara tatu ukubwa wa kambi za matibabu zilizofanywa hapo awali na klabu yetu.


“Tunapenda kuwashukuru sana Vilabu vya Rotary na Rotaract washirika wetu, vilevile washirika muhimu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Awamu ya Sita Ikiongozwa na Raisi Doctor Mama Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya, Bill & Melinda Gates Foundation, Guaranty Trust Bank, Pepsi, SGA Security, Jollie Pads, Agha Khan Health Service, Manufaa Media, Bakhressa Group ,Chemi Cotex, Hitech Sai Hospitals, Afya Intelligence na Management and Development for Health (MDH).” Amesema Calvalho


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Mehreen Khatri amesema maandalizi yote yamekamilika na amewashauri wakazi wa Dar es Salaam kutumia fursa hii adhimu kuja na kupima afya zao Pamoja na kupata ushauri na elimu ya afya. “tunashukuru maandalizi yote yamekamilika. Hii ni kutokana na ushiriki mkuwa wa wanachama wa Rotary Tanzania Pamoja wafadhili wetu. Tunaamini watu wengi watajitokeza kupima afya zao siku hiyo” alisema Mehreen.


Naye Abdulrahman Hussein Rais wa Rotary Club ya Osterbay Dar es Salaam amesema Jumla ya wakazi 5000 kutoka Bunju na maeneo ya jirani watapata huduma za afya na elimu bila malipo wakati wa tukio la siku ya Afya ya Rotary inayofanywa kwa ushirikiano na Vilabu vya Rotaract vya Kairuki, Muhimbili, KIUT, Alpha, na Kwanza
Share:

WASHINDI WA DROO YA SITA YA Y9 MICROFINANCE WAPATIKANA

Meneja masoko wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi. Sophia Mang’enya (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya sita  kwa njia ya simu Baraka Barazae mkazi wa Dar es Salaam ambaye amejishindia pikipiki na Robert Keraryo mkazi wa Butiama ambaye amejishindia simu janja. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bi. Pendo Mfulu.


Washindi wa Droo ya sita ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Baraka Barazae mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam na mshindi wa simu Robert Keraryo Mkazi wa Butiama mkoani Kagera.


Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Masoko ya taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi Sophia Mang'enya ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.


Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma za kifedha popote alipo, hilo ndio lengo kuu la kuanzishwa kwa Y9 microfinance".


Aligusia kuwepo kwa wimbi kubwa  matapeli wa mtandaoni na amewasihi wateja wa Y9 microfinance kuwa makini na wizi huo wa mitandaoni, amewasihi watanzania kuitumia Tehama  kwa maendeleo sio kutumia Tehama kufanya uhalifu. 


Alieleza namna ya kushiriki ni rahisi hakikisha umepakua app ya Y9 microfinance kisha kujisajili na kuanza kukopa na moja kwa moja utaingia kwenye droo hii baada ya marejesho.  


Kwa upande wake afisa  kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Pendo Mfulu ameeleza "kama bodi ya michezo ya kubahatisha nchini tumeridhishwa na namna ya uchezeshwaji wa droo hii na upatikanaji wa washindi.

Share:

Takwimu sahihi nyenzo muhimu mapambano dhidi ya Ukimwi

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa (USAID) Bw. Craig Hart (katikati) akiangalia, wakati mmoja wa wenye VVU akijisajili katika mfumo wa alama za vidole mara baada ya mkurugenzi huyo kukabidhi msaada wa kifaa hicho kwa hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Mfumo huo unasaidia kupata takwimu sahihi za wenye VVU, jambo ambalo ni muhimu katika kufanikisha utoaji wa huduma bora. Hafla hiyo iliyofanyika mkoani humo jana inakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) unaofadhili miradi ya kupabana na Ukimwi inayosimamiwa na (USAID)
Mkurugenzi wa mradi wa USAID Afya yangu kanda ya Kusini unaoendeshwa na Shirika la Deloitte, Dk Marina Njekela, akielezea utendaji na mafanikio ya mradi huo katika kutoa huduma bora kwa wenye VVU katika hafla hiyo Mjini Iringa jana.
Mwakilishi wa mabinti wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Lucy Michael Mpwage, aliyezaliwa na maambukizi ya ugonjwa huo akitoa ushuhuda pamoja na changamoto za unyanyapaa alizokumbana nazo katika vipindi tofauti vya maisha yake na jinsi huduma za miradi ya USAID inayoendeshwa na Shirika la Deloitte ilivyookoa maisha yake. Ilikua ni wakati wawakilishi wa mfuko PEPFAR, USAID, mashirika yanayosimamia utoaji wa huduma kwa wenye VVU pamoja na waandishi wa wabari wakitembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa jana, kuangalia mafanikio ya miradi hiyo .
Baadhi ya wanawake waliowezeshwa na Mradi wa Hebu tuyajenge unaoendeshwa na Shirika la NACOPHA wakishangilia wakati wa ziara ya wawakilishi wa PEPFAR, USAID wakitembelea katika ofisi za shirika hilo mjini Iringa jana.

Na Zuhura Rashidi, Iringa.

UWEPO wa takwimu sahihi za wenye VVU unachangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya mipango mikakati katika uratibu wa miradi ya kupambana na ukimwi imeelezwa mkoani Iringa jana.

Hayo yalisemwa na Maganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dk. Mohamedi Mang’ula wakati wa ziara ya wawakilishi wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na ukimwi (PEPFAR), pamoja na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) hospitalini hapo ili kuangalia huduma mbalimbali za utoaji tiba kwa wenye VVU zinazofadhiliwa na mfuko huo kupitia USAID.

Dk Mang’ula alisema hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa msaada wa kifaa cha kufanyia usajili wa wenye VVU kwa kutumia mfumo wa alama za vidole kilichokabidhiwa na Mkurugenzi Mkazi wa USAID, Bwana Craig Hart akishukuru ufadhili wa USAID uliochangia uboreshaji wa huduma za afya kwa wenye VVU hospitalini hapo.

Tunaipongeza Kampuni ya Deloitte inayoendesha miradi hii inayofadhili na Mfuko wa PEPFAR katika mkoa wetu kwani imeweza kutusaidia kupata mafanikio makubwa katika kufikia malengo ya 95;95;95 katika kutambua wenye VVU, waliotambuliwa kuanza kupata tiba na suala la kufubaza virusi vya ukimwi”, alisema.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Afya Yangu Kusini, Dk. Marina Njelekela alisema wamekuwa na safari ndefu ila yenye mafanikio lukuki katika kutekeleza miradi inayofadhiliwa na PEPFAR kwa kupitia USAID.

Alisema misaada inayotolewa na PEPFAR kupitia Shirika la USAID imesainia kuokoa maisha ya watanzania wengi katika kipindi hiki cha miaka 20 huku kukishuhudiwa uimarikaji mkubwa wa huduma kwa wenye VVU katika vituo mbalimbali nchini.

USAID Afya Yangu Kusini tunasharehekea miaka 20 kwa kuboresha miradi ya PEPFAR USAID, tukipitia hatua mbalimbali za kimaendeleo moja ikiwa ni kuwajengea uwezo watoa huduma za afya katika vituo mbalimbali."

Tumeboresha ubora wa utoaji huduma bora za VVU na Kifua Kikuu katika ngazi ya jamii, mwaka 2004 tukiwa na vituo vya kutolewa huduma 33 lakini kwa msaada wa PEPFAR kwa hadi mwaka 2023 tumeweza kufikisha vituo 676."

Deloitte pamoja na washirika wake wa kiufundi wa MDH na T-marc tunajivunia sana kusimamia miradi inayofadhiliwa na PEPFAR, mwaka 2004 aina ya wagonjwa tulioanza nao kwa sasa imebadilika kabisa, sasa wapo na furaha na matumaini, wamewezeshwa, hawajisikii unyanyapaa”, alisema Dk. Marina.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraa la Taifa la Watu Wanaoishi na UVVU Tanzania (NACOPHA), Bwana Deogratius Rutwatwa wanaoendesha mradi wa ‘Hebu Tuyajenge’ alisema moja ya mikakati ya malengo ya mradi huo ni kuhakikisha pamoja na mambo mengine watu wenye maambukizi ya VVU wanatambua hali zao.

Ofisa mtendaji huyo alizungumzia suala la unyanyapaa kuwa moja ya changamoto inayosababisha watu wengi wenye VVU kushindwa kujitokeza kupata huduma za upimaji na kuunganishwa kwenye vituo vya tiba.

Baadhi ya huduma tunazozitoa ni pamoja na elimu kwa wenye VVU kuhusu namna bora ya kujzuia maambukizi mapya, kutambua wenza na watoto wenye VVU hivyo kuwaunganisha kwenye huduma za upimaji na kutoa usaidizi juu ya matumizi sahihi ya dawa za ARV’s."

Kwa namna ya kipekee niupongeze Mfuko wa PEPFAR kupitia USAID kipindi hiki unapotimiza miaka 20 kwa mafanikio na jitihada zake katika kupambana na janga la ugonjwa wa ukimwi hapa Tanzania”, alisema.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

 • ()
 • ()
Show more

Labels

Blog Archive