A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, November 16, 2023

BARAZA LA FCT LARIDHIA UUNGANISHWAJI WA KAMPUNI YA SARUJI YA TANGA CEMENT NA TWIGA

 Mwenyekiti wa bodi wa kampuni ya Tanga cement PLC, Patrick Rutabanzibwa (katikati), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam jana.Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wa pili kulia) na Raymond Mbilinyi, ye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa Tanga Cement pamoja na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement , Quresh Ganijee

Mkurugenzi Mtendaji  wa  Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (wapili kushoto), akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam Wengine ni Mkuu wa Divisheni ya Fedha wa Tanga Cement PLC, Pieter De Jager (kushoto) Mwenyekiti wa bodi ya Tanga cement, Patrick Rutabanzibwa, (wa tatu kulia) na Raymond Mbilinyi, ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa Tanga Cement na Katibu wa kampuni ya Tanga Cement Quresh Ganijee

Baraza la ushindani nchini FCT limeridhia mchakato wa uunganishaji kampunu ya saruji ya tanga na ile ya twiga huku wanahisa wa kampuni ya saruji ya tanga nao wakipitsha maamuzi ya kuruhusu uuzaji hisa asilimia 73 za kampuni hiyo kwenda kwa mwekezaji heidberg ambaye ndiye mmiliki kiwanda cha twiga cement.

Maamuzi hayo yamepitishwa jijini Dare esl saam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka na mkutano maalum wa wanahisa  hisa wa kampuni ya saruji ya tanga Cement ambapo akizungumza Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo patrick rutabanzibwa amesema maamuzi ya wana hisa hao yametokana na hali ngumu inayo ipitia kampuni ya tanga cement ambayo imeshindwa kutoa gawio kutokana na deni ambalo lipo kwenye kampuni hiyo.

Kampuni hiyo pia ilielemewa na gharama kubwa za uzalishaji hivyo kujikuta wakihitaji zaidi uwekezaji kutoka kampuni ya heidelberg inayo miliki kampuni ya scancem ambaye ndie mmiliki wa kiwanda cha twiga cement ili kuingiza nguvu nakuhakikishia wateja kuwa na uhakika wakupata bidhaa hiyo bila kuwa na mashaka.

Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya african mauritus ambaye anamiliki hisa zaidi ya asilimia 73 ya kiwanda cha tanga cement reinhardt swart ambaye ndie mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha tanga cement amesema mchakato wa upatikanaji wa mwekezaji huyo utakamilika haraka iwezekanavyo ili kuongeza nguvu ya uzalishaji wa saruji ambapo pia ameiomba serikali kuimarisha upatikanaji wa nishati kwa uhai wa viwanda nchini

Hata  baadhi ya wana hisa wa kiwanda cha tanga cement ambao wameeleza kusikitishwa na kukosa gawio kwa muda mrefu huku wakibariki kuuzwa kwa hisa hizo na kuunganishwa kwa kiwanda cha tanga cement na twiga cement ili kuwa kiwanda kimoja kitakacho kuwa imara.


WARAKA WA MWEYEKITI
Utangulizi
Wanahisa,
Tuko hapa kuwasilisha taarifa ya biashara iliyokaguliwa ya Tanga Cement Public Limited Company (“Tanga Cement” au “Kampuni”) na kampuni zake tanzu (kwa pamoja “Kundi”) kwa mwaka unaoshia tarehe 31 Disemba 2021.

 Licha ya athari za janga la kimataifa la UVIKO-19, kundi limefanya vizuri kwenye viashiria vyake muhimu vya utendaji wa kifedha kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Disemba 2021 kama ilivyofafanuliwa kwenye eneo la mapitio ya Kifedha na Kiutendaji hapo chini.

Tunathibitisha kujitolea kwetu kwa wadau wote kupitia simenti yetu yenye ubora wa hali ya juu na klinka na pia usambazaji wetu ambao ni mchango wetu katika ukuaji endelevu na maendeleo ya Tanzania, kama ilivyo kauli mbiu yetu, “STRENGTH WITHIN”. 

Kampuni imeweka viwango vya juu sana vya afya na usalama katika maeneo yake yote ya utendaji na inaendelea kutekeleza sera za usalama katika sehemu ya kazi ili kulinda wafanyakazi wake na wakandarasi.

Mapitio ya Uchumi.
Ukuaji wa kampuni (Kundi) unaendelea kujikita kwenye ukuaji wa mahitaji ya simenti kwaajili ya soko la ujenzi Tanzania.

Wastani wa kiwango cha mfumuko wa bei kimeongezeka na kufikia asilima nne nukta mbili (4.2%) mwaka 2021 kutoka asilimia tatu nukta tatu (3.3%) mwaka 2020. Makadirio ya ukuaji wa pato ghafi la taifa la asilimia nne nukta tatu (4.3%) kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia nne nukta nane (4.8%) iliyorekodiwa mwaka 2020 (kama ilivyochapishwa na shirika la takwimu la taifa). 

Japo ongezeko la pato ghafi la taifa linaridhisha, uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na uimarishaji wa msingi wa wateja, vinabaki kuwa vichocheo vya msingi vya ufanisi wa biashara. Mpango wa Serikali wa kati wa sera za kifedha wenye lengo la asilimia tano (5%) umesaidia kuongeza uhitaji wa bidhaa zetu. 

Kampuni (Kundi) inabaki kuwa na matumaini chanya ya maendeleo chini ya mipango ya maendeleo ya miundo mbinu iliyopo kwenye dira ya Mpango wa Maendeleo wa Serikali wa mwaka 2025 na inategemewa
miradi itashika kasi mwaka 2022. 


Kampuni inaimani na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19 na imedhamiria kufanya kazi pamoja na Serikali kwenye kukuza uchumi. Kampuni inao uwezo wa kufikia kiwango maalum cha mahitaji ya simenti nchini na kuendelea kujizatiti na uzalishai wa bidhaa za simenti zenye ubora wa hali ya juu. 

Mapitio ya Fedha na Utendaji Mapato ya kampuni kutokana na mauzo yaliongezeka kwa kiasi cha asilimia tisa (9%) na kuwa TZS 231bn kutoka TZS 213bn iliyopatikana mwaka 2020.

Sambamba na ongezeko la mapato, faida ghafi iliongezeka kwa asilima kumi na nne (14%) na kufikia TZS61.7bn kutoka TZS 54.2bn iliyopatikana mwaka 2020.

 Licha ya miradi mikubwa ya matengenezo ya mitambo yaliyofanyika
mwaka 2021 na kukatika kwa umeme mara kwa mara
kulikopelekea ongezeko la gharama za uzalishaji, pato la jumla
liliongezeka kufikia asilimia ishirini na saba (27%)
ikilinganishwa na asilimia ishirini na tano (25%) ya mwaka
2020.


Kampuni (Kundi) iliingia gharama za mara moja za
marekebisho yaliyosababisha kupungua kwa pato linalotokana
na uendeshaji kwa asilimia kumi na tatu (13%) na kufikia TZS
15bn kwa mwaka 2021 kutoka TZS 17bn kwa mwaka 2020.
Marekebisho hayo ni pamoja na kurekebisha Tanuri (Kiln) na
gharama zilizoambatana na marekebisho hayo ili kurudisha
uzalishaji katika hali ya kawaida.


 Gharama za kuachana na
operesheni za machimbo/migodi na kuanza kukodi huduma
hizo kutoka kampuni nyingine pia zimechangia kwenye
gharama hizo. 


Mapato kabla ya Riba, Kodi, Gawio na
Uchakavu (EBITDA) yalipungua kwa asilimia mbili (2%) kufikia
TZS 40.8bn kutoka TZS 41bn iliyopatikana mwaka 2020
iliyosababishwa haswa na gharama za kusitisha mikataba ya
wafanyakazi na gharama za matengenezo ya mitambo.


Kampuni (Kundi) ilirekodi faida kabla ya kodi ya TZS 3.8bn
mwaka 2021 ambayo imeongezeka kutoka hasara iliyopatikana
kabla ya kodi ya TZS 0.63bn iliyopatikana mwaka 2020.


Kuongezeka kwa faida kabla ya kodi ilitokana na kuongezeka
kwa faida ghafi na kupungua kwa hasara zitokanazo na
ubadilishaji wa fedha za kigeni na hasara ya thamani ya fedha
ambazo zinahusiana na deni la mkopo wa ujenzi wa kiln mpya
kuthaminishwa kwa Dola ya Kimarekani (USD) na riba
itokanayo na kukodisha vifaa na mali mbalimbali.

 Kampuni iliingia kwenye mkataba mpya uitwao ‘Standstill agreement’
kwenye mkopo wa PIC ambao ulizuia hasara zitokanazo na
ubadilishaji wa fedha za kigeni.


Matokeo hayo mazuriyamechagizwa na kuboreka kwa usimamizi wa hazina, mikakatiya ununuzi wa fedha za kigeni na viwango vya udhibiti wa mitaji
ya kazi. Kampuni (Kundi) ilipata faida baada ya kodi ya TZS
3.5bn mwaka 2021 ambayo imeboreka kutoka hasara baada
ya kodi ya TZS 2.1bn iliyopatikana mwaka 2020.


Fedha taslimu zilizotokana na shughuli za biashara zilipungua kwa asilimia
hamsini na nane (58%) kutoka TZS 48bn zilizorekodiwa mwaka
2020 na kufikia TZS 20bn mwaka 2021.

 Mtiririko wa fedha zilizotokana na shughuli za uendeshaji pia ulipungua kwa
asilimia hamsini na saba (57%) na kufikia TZS 18bn kutoka
TZS 43bn iliyo rekodiwa mwaka uliopita. 

Mapungufu yamtiririko wa fedha yamechangiwa na kushuka kwa faida ya
uendeshaji kwa asilimia kumi na tatu (13%) kutokana na
gharama za mara moja kama zilivyoainishwa hapo juu.


Kuongezeka kwa wadaiwa kwa TZS 5bn, kuongezeka kwa
malighafi kwa TZS 11bn, kupungua kwa madeni ya kibiashara
na madeni ya kimkataba kwa TZS 4bn na TZS 1bn kwa mwaka
2020 na 2021 mtawalia.

Kampuni inaendelea kujitoakuhakiksha mauzo, ufikishaji bidhaa sokoni na mipango yake ya kupunguza gharama za uendeshaji vinaendelea kuwa
suluhisho la kuongeza thamani ya wadau wake.

 Kampuni inabaki kuwa na matarajio chanya kwa mwaka 2022 licha ya
ushindani mkali na athari za UVIKO-19.

Mipango ya Serikali yakukuza uchumi kupitia maendeleo ya miundombinu na ukuzajiwa viwanda vya ndani vinatarajiwa kuchochea uzalishaji wa
ndani wa simenti na matumizi huku ikiendelea kuzuia utitiri wa
uingizaji wa simenti kutoka nje.
Gawio.


Kampuni haikutangaza gawio la muda mfupi au la mwisho wa
mwaka kwa wanahisa kwa mwaka 2021 na 2020. Maamuzi
hayo yamefanyika kwa kusudi la kua makini na rasilimali fedha
zilizopo ili kampuni iweze kujikimu na mahitaji mbalimbali katika
kipindi hiki cha kujikwamua kiuchumi kutoka kwenye athari
zilizosababishwa na UVIKO-19.


 Bodi imeamua kuendelea kutenga fedha zilizopo kwa ajili ya uendeshaji wa kampuni Bodi pia itafanya tathmini ya mwenendo wa kifedha katika
kipindi chote cha mwaka wa fedha wa 2022 kabla ya kufanya
uamuzi wa kutangaza gawio.

Pendekezo la kununuliwa kwa
kampuni na Scancem International DA Wanahisa
wanakumbushwa kuhusu tangazo la tarehe 27 Oktoba 2021 la
pendekezo la Scancem International DA kununua asilimia
68.33% ya hisa za Tanga Cement PLC kutoka Afrisam
Mauritius Investment Holdings Limited.

Taratibu zote zinazohusisha mamlaka mbalimbali zimekwisha fanywa. Pande
zote mbili zinasubiri maamuzi ya mamlaka hizo. Wanahisa
wataendelea kupewa taarifa za mchakato huu kadiri muda
unavyoenda.

Hitimisho
Katika kufanyia kazi malengo yake ya muda mfupi na mrefu,
kampuni inaendelea kuwashukuru wafanyakazi wake kwa
mapenzi yao na kujitoa walikokuonesha katika kipindi hiki licha
ya kuwepo kwa changamoto, na pia kwa wateja wake kutokana
na uaminifu wao kwa chapa yetu ya Simba simenti. Pamoja na
Tanzania kubaki kuwa mshirika mkuu katika Jumuia ya Afrika
Mashariki kwenye soko la ujenzi, uzalishaji wa simenti
unategemewa kuongezeka na Kampuni imejiweka tayari
kuchukua fursa hizo za ukuaji wa soko kwenye kanda.
Kwaniaba ya Bodi ya Wakurugenzi
Patrick Rutabanzibwa
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive