A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, December 30, 2019

Washindi Wa Ibuka Kidedea Na NBC Malengo Wapaa

Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa Benki ya NBC, Dorothea Mabonye (kushoto), pamoja na Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), wakiagana na mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Ramdhani Saidi (kulia) muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo akielekea Seychelles pamoja na mwenza wake. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu (Toyo).
Meneja Masoko wa benki ya NBC,  Alina Maria Kimaryo (kulia), akikabidhi tiketi ya ndege ya kwa moja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Esther  Ndunguru muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo akielekea Arusha kufanya utalii katika Mbuga za Wanyama za Serengeti akiwa na mwenza wake. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu (Toyo).
Mshindi wa safari ya kwenda Mbuga za Wanyama za Serengeti wa Ibuka kidedea na NBC Malengo, Esther Ndunguru (kushoto) akikaguliwa tiketi yake kabla ya kupanda ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Safari hiyo pamoja na mwenza wake inalipiwa na NBC. Washindi wanne wameibuka kidedea na kushinda safari ya kwenda Serengeti pamoja nma wenza wao huku gharama zote zikilipiwa na NBC.
Washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakifungua shampeni muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo wakielekea Seychelles. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, kila mwezi washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki za miguu mitatu (Toyo).
  
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakitakiwa heri ya safari yao na wawakilishi wa NBC waliowasindikiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla hawajaondoka.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakipozi kwa picha pamoja na  wawakilishi wa NBC waliowasindikiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kabla hawajaondoka huku wakiwa wameshika glasi zenye shampeni ikiwa ni ishara ya kuwatakia safari njema.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakiwa katika hatua ya mwisho ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Share:

Saturday, December 28, 2019

NBC yawapongeza na kuwaaga Washindi wake wa Kampeni ya “IBUKA KIDEDEA”

Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (katikati) akimkabidhi tiketi ya ndege  mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Jocelyne Rwechungura aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mshindi huyo pamoja na mwenza wake aliyemchagua.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tatu kushoto) akimkabidhi tiketi ya ndege, mwenza wa mshindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Kijakazi Mohamed aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles  wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond na  Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za  safari ya mwenza huyo pamoja na mshindi mwenyewe Ramadhani Saidi (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke akimkabidhi tiketi ya ndege, mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Prof. Lettice Rutashobya (kulia),  aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.  Kutoka Kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond na  Meneja Masoko wa Benki hiyo, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mshindi huyo pamoja na mwenza wake aliyemchagua.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na maofsa wa NBC katika hafla hiyo.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond akizungumza katika hafla hiyo ambapo alitoa hamasa kwa wateja na wasio wateja kuitumia kampeni ya  akaunti ya Malengo ya NBC ili kutimiza malengo yao.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke akizungumza katika hafla ya kuwapongeza na kuwaaga washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo walioshinda safari za kwenda Sychelles na katika mbuga za wanyama za Serengeti.
Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo akizungumza kuhusu kampeni hiyo akisema Ibuka Kidedea imekuwa ikitoa zawadi kila mwezi na hadi sasa jumla ya pikipiki tano zimeshatolewa tangu mwezi Oktoba ilipozinduliwa.

Dar es Salaam 27 Disemba, 2019.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imefanya hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwaaga wateja walioibuka washindi katika  Kampeni yake ya Ibuka Kidedea na akaunti ya NBC Malengo. Washindi hao wamejishindia safari za  kitalii ambapo baadhi watazulu  Mbuga ya Wanyama ya Serengeti na wengine visiwa wa Sychelles.

Kampeni ya Ibuka Kidedea ilizinduliwa mwezi Okotoba mwaka huu ikiwa na lengo kuu la kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kwa wateja ambapo zawadi mbalimbali zikiwemo zikiwemo bodaboda zimekuwa zikitolewa kwa washindi walioingia kwenye droo maalum inayosimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha nichini.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga washindi hao  iliyofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton (zamani New Africa), jijini  Dar es Salaam Mkurugenzi wa wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke aliwashukuru wateja wote waliojitokeza  kushiriki kampeni hii tangu kuzinduliwa kwake .

“Ibuka Kidedea imefanyika kwa mafanikio makubwa, tumeshuhudia idadi kubwa ya wateja wetu wakishiriki katika kampeni hii, lakini pia wateja wanashuhudia kuongezeka kwa amana zao kutokana na faida za kila mwezi.

"Natoa pongezi kwa washidi wetu wote na tunaamini mtaendelea kuwa mabalozi wetu wakati mkifurahia safari hizi katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka”, kampeni hii bado inaendelea hivyo tunatoa wito kwa wateja wengine kushiriki katika kampeni hii kwa kuendelea kuweka akiba ili kupata nafasi ya kushinda zawadi”,  aliongeza Bwana Masuke.

Naye Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond alisema ni matumani ya NBC kuwa kampeni hii inatoa hamasa kwa watanzania kuwa na utamaduni endelevu wa kujiwekea akiba ili kutimiza mahitaji yao ya kifedha lakini zaidi ni kuwa na uhuru wa kifedha.

"Tunahamasisha wateja wetu na wasio wateja kuitumia akaunti ya Malengo ya NBC ili kutimiza malengo yao, iwe ni nyumba, gari nzuri, pikipiki, kwenda mapumzikoni, ada za shule na mengineyo.

"Tunajua kila mtu ana ndoto yake, jiunge na NBC Malengo na tutafurahi kukusaidia kutimiza ndoto zako", aliongeza.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo, Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo alisema Ibuka Kidedea imekuwa ikitoa zawadi kila mwezi na hadi sasa jumla ya pikipiki tano zimeshatolewa tangu mwezi Oktoba.

Ili kujishindia pikipiki (bodaboda) mteja anachotakiwa kufanya ni kuweka akiba kwa kiwango kinachoanzia shs 100,000 katika akaunti yake ya Malengo, na kwa safari ya Serengeti kiwanngo kinaanzia shs 1,000,000 na kiwango kinachoanzia 50,000,000 kwa safatri ya Sychelles.

"Pamoja na zawadi hizi katika kampeni hii, wateja watakaoweka akiba katika akaunti zao za Malengo kwa kiwango kinachoanzia shs 1,000,000 wanapata nafasi ya kujishindia pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo  katika droo kubwa ambayo jumla ya pikipiki za kubebea mizigo (Toyo) tatu zitatolewa”, alisema. 

Mmoja wa washindi aliyejishindia bodaboda, Daudi Patrick Majani, mstaafu na mfanyabiashara anayeishi Tabata Segerea jijini Dar es Salaam alisema atatumia bodaboda yake kumuingizia kipato na kuitumia kwa usafiri utakaosaidia kuiwezesha biashara yake.

Washindi walioshinda safari ya Serengeti ni Christopher Mgote kutoka Nzega, Makongoro Makongoro kutoka Arusha, Bi. Jocelyine Rwechengura na Bi.Esther Ndunguru wote kutoka Dar es Salaam.

Washindi walioshinda safari ya Sychelles ni, Wambura John Wambura kutoka Tarime mkoani Mara, Ramadhan Saidi, Lettice Rutashobya na Sylevester Ambokile wote wa jijini Dar es Salaam.
Share:

Saturday, December 21, 2019

NBC yazindua Kampeni ya Bima ya magari kipindi hiki cha sikukuu kwa kushirikiana na SANLAM



Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni iliyozinduliwa na NBC kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka, Meneja Masoko wa Sanlam, Marco Yambi na Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow (kushoto kwake), wakionyesha kadi ya kuwekea mafuta ya Total wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayofanyika kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka, Meneja Masoko wa Sanlam, Marco Yambi, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total, Marsha Msuya na Meneja Mahusiano Kitengo cha Bima cha NBC, Kuruthum Mwaluwinga.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kushoto), akikabidhi kadi ya kujazia mafuta ya Total kwa  mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Danford Robert Buguru wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoangalia ni wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
Mkuu wa Kitengo cha Bima cha Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kushoto), akikabidhi zawadi mbaimbali kwa  mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert Danford Buguru, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoangalia ni wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (katikati), akisaidia kuweka mafuta ya ofa katika gari la mteja wa kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert Danford Buguru (kulia), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Nyuma yake ni Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC, David Raymond (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ambapo NBC ilizindua kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana.  

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Sanlam imezindua kampeni ya bima ya magari itakayojulikana kama “Ifurahishe gari yako”.

Kampeni hiyo inayoanza Desemba mwaka huu hadi Januari mwakani ni sehemu ya malengo ya benki kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja kwa kuwapa mahitaji muhimu kupitia huduma bora zilizoandaliwa mahsusi kwa ajili yao.

Kwa kutambua umuhimu wa usalama kwa wasafiri na watumiaji wote wa vyombo vya moto kwa ujumla, katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, NBC imemrahisishia mteja kupata kifurushi kizuri cha bima kwa ajili ya magari kikiambatana na nyongeza kadhaa za kuvutia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Kituo cha Mafuta cha Total, Mbezi jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema kampeni hiyo imezinduliwa katika kipindi sahihi cha mwaka ambapo kwa kawaida huwa na idadi kubwa ya wasafiri.

NBC imedhamiria kuboresha huduma za bima na kufanya kasi ya matumizi ya bima nchini kuongezeka, kwa kupitia kampeni hii, wateja watakaonunua bima katika matawi ya NBC watapata ofa kadha wa kadha zikiwemo huduma ya bure ya mafuta ya kilainishi cha injini na mafuta ya bure kutoka vituo vya mafuta vya Total pamoja na bima ya bure ya ajali ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu kutokana na ajali.

Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo, Meneja Mahusiano wa Bima kutoka NBC Bi. Kuruthum Mwaluwinga alisema, wamiliki wa magari yenye thamani ya TZS 50,000,000 na zaidi watanufaika na mafuta bure pamoja na bima ya bure ya ajali, ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu kutokana na ajali.

Aliongeza kuwa kwa wateja wenye magari yenye thamani ya kuanzia TZS 15,000,000 hadi 49,900,000, watapata lita 10 za mafuta bure katika kituo chochote cha Total nchi nzima, bima ya ajali ama ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu.

Mwisho, kwa wateja wenye magari yenye thamani ya kuanzia TZS 7,000,000 hadi 14,900,000, watapata lita tano za bure za mafuta katika kituo chochote cha Total nchini, bima ya ajali ya bure ama ulemavu wa kudumu na gharma za matibabu. Wateja wote kwenye vipengele tajwa watapata kadi ya Total kwa ajili ya kujazia mafuta.

Alimaliza kwa kusema: "NBC kupitia Sanlam na kampuni nyingine za bima hutoa huduma bora za bima za aina mbalimbali kwa wateja wetu zikijumuisha bima za maisha na za kawaida. Huduma hizi tayari zipo katika matawi yetu yote yanayopatikana kote nchini.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke, alisema kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni ishara wazi ya dhamira NBC kutoa huduma bora za kifedha  kwa wateja wake hapa Tanzania.

"Pamoja na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 ya kutoa huduma za kuvutia, siku zote NBC inajivunia kuzindua huduma zenye viwango vya juu kwa manufaa ya wateja wetu. Tunawakaribisha wote kutumia na kufurahia huduma hizo za kibenki.”

NBC imeendelea kuwa kinara katika ubunifu ambapo kwa mwaka huu pekee imefanikiwa kuzindua huduma na bidhaa kadhaa za kufurahisha, kama Klabu ya Biashara ya NBC inayolenga kuwapa maarifa muhimu ya biashara wafanyabiashara wa kati na wadogowadogo ili waweze kuendeleza biashara zao kwa ufanisi; NBC Kiganjani ambayo ni suluhisho rahisi kwa watumiaji kwani ni huduma za kidijitali zinazotembea. Bidhaa nyingine mpya ni Akaunti ya Fasta inayowezesha kufunguliwa kwa akaunti haraka na mteja kupewa kadi ya Visa papo hapo.

Kwa muktadha huo huo, NBC imeendelea kukuza mtandao wa mawakala wa huduma zake (NBC Wakala) nchini. Zaidi ya mawakala 2,200 wanawezesha huduma za kibenki kupatikana kwa urahisi hata katika maeneo pasipokuwa na matawi ya benki.
Share:

Friday, December 20, 2019

Benki ya DCB yazindua Mkopo wa Ada ya Shule

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James Ngaluko (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa DCB Skonga, Zamaradi Mketema, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB, Fortunata Benedict (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko.
Balozi wa bidhaa ya DCB Skonga ya Benki ya Biashara ya DCB, Zamaradi Mketema (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.

Dar es Salaam 19 Disemba, 2019. BENKI ya Biashara ya DCB imezindua huduma ya mkopo maalumu wa Ada ya Shule ikiwa ni fursa nyingine tena itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kulipa ada za watoto wao kwa wakati na uhakika.

Mkopo wa ada wa DCB ni mwendelezo wa mkakati wa benki kubuni huduma na bidhaa bora zinazowanufaisha wateja. Benki imekuja na bidhaa hii ya mkopo wa ada katika harakati ya kuwaondolea hofu wazazi linapokuja suala zima la elimu kwa watoto wao hii ni sambamba na akaunti ya DCB Skonga inayomuwezesha mtoto kusomeshwa pindi mzazi anapopata ulemavu wa kudumu ama kifo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa mkopo huu, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bi Rahma Ngassa alisema ‘’DCB inaendelea kuleta kwenye soko bidhaa zinazo kidhi maisha ya watanzania, benki hii ni ya watanzania hivo ni lazima kuja na fursa inayowawezesha wateja wetu kunufaika na benki yao.

Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Bwana James Ngaluko aliongeza ‘’mkopo huu ni wa dharura na ni suluhisho kubwa kwa wateja wetu, siku hazilingani na kama Benki tunataka watoto wetu wasome, elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunampa mzazi fursa ya kupata mkopo wa dharura ndani ya masaa 48 kwa ajili ya ada ya mtoto  pindi amekwama.

Alisema wakati tunaendelea kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kukaribisha mwaka 2020, Benki tumeona tuwazawadie zawadi ya kipekee kabisa wateja wetu kwani ni jambo lililo dhahiri kuwa suala la ada ni moja ya changamoto kubwa inayowakabili wazazi wengi kila ifikapo mwanzoni mwa mwaka. Mkopo wa Ada wa DCB una riba ya chini sana na utalipwa moja kwa moja kwenye shule ya mtoto. Mkopo huu unakupa fursa ya kukopa hadi shilingi milioni tano ndani ya masaa 48 na muda wa marejesho unachagua mwenyewe hadi miezi sita.

Nae Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi Bi Fortunata Benedict alisema ‘’Wazazi wengi kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao wamejikuta wakihangaika kutafuta fedha za ada kwa njia zozote hivyo kujikuta kuingia katika matatizo. Mzazi sasa huna haja ya kupata stress za kulipa ada, acha DCB ikufikirie masuala ya elimu ya mtoto wako hii ni suluhisho la uhakika la kifedha.

Ikumbukwe kua mwaka wa 2019 DCB imetoa fursa mbalimbali kwa wateja ikiwemo:

§  DCB imewapa maelfu ya watanzania fursa ya kuwekeza kwa kununua Hisa na kua wamiliki halali wa benki hii kupitia mfumo wa hisa za upendeleo.

§  DCB kibubu inampa fursa mteja kuweka akiba mwenyewe kidogo kidogo kupitia simu ya mkononi (DCB Digital) na kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.

§  DCB ilizindua DCB Sokoni inayolenga kumkomboa mkulima na mfanyabiashara wa kilimo  katika mnyororo wa thamani.

§  DCB Lamba kwanza inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14% papo hapo na kila mwanzo wa mwezi.

§  DCB Skonga, ikilenga kuwasaidia wazazi katika suala zima la elimu ya watoto wao pindi watakapopata majanga ya ulemavu wa kudumu au kifo.
  
Share:

Thursday, December 19, 2019

ATE yatoa Tuzo kwa Mwajiri Bora 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB)akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB)akitoa juzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 Mwakilishi kutoka kampuni ya TBL David Magese wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho Jayne Nyimbo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa (katikati), akitoa tuzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 kwa nafasi ya mshindi wa pili Mwakilishi kutoka  Geita Gold Mine Elizabeth Karua, wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. anaeshuhudia (kulia), ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Jayne Nyimbo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB)akitoa Cheti kwa Kaimu Mkurugenzi Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Edna Chogo (kulia), wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho Jayne Nyimbo.


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini, kuhakikisha wanawawezeshewa fanyakazi waokwenda kuhudhuria mafunzo mbalimbali ili waweze kupata ujuzi unaohitajika nautakaokidhi ushindani katika mazingira ya kibiashara.

Mhagama ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya utoaji tuzo za waajiri bora wa mwaka kwa mwaka 2019, tuzo zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Waziri alisema wafanyakazi wakipata mafunzo hayo watajiongeza ujuzi, watafanyakazi kwa bidii na kuongeza uzalishaji mahali pakazi kwa lengo la kupambana na manadiliko ya teknolojia.

"Sisisote ni mashahidi mabadiliko ya teknolojia ni makubwa kwelikweli, kwahiyo kama hatutawashirikisha wafanyakazi wetu kupata ujuzi mpya na mafunzo endelevu katika maeneo yetu ya kazi ambayo yatawasaidia kuendana na  mabadiliko hayo yateknolojia katika ulimwengu, tunaweza tukajikuta hatupigi hatua kwenda mbele na hatutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea ndani ya taasisi zetu na taifa kwa ujumla," alisema.

Alisema pia anawakumbusha waajiri kuendelea kuchangia katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwani umekuwa ukiwakinga waajili na madhala na majanga wanayoyapata mahali pa kazi.'

Uchangiaji katika mfuko huu unamanufaa makubwa situkwawafanyakazi hata kwa waajiri kwani utamsaidia mwajiri kuwa na nguvukazi yenyeafya njema itakayofanyakazi kwa kujiamini," alisema

Aidha alisema wanapoendelea kuijenga nchihasa katika kuwekeza kwenye sekta ya viwanda wanategemea kwa kiasi kikubwa mchango wa sekta binafsi kama injini ya kujenga uchumi hivyo maamuzi ya ATE ya kutambua na kuwekeza katika rasilimali watu nikuongeza tija kwenye maeneo ya kazi.


Aidha alisema wao kama serikali, waajiri na Chama cha wafanyakazi nchini (Tucta) watahakikisha kwamba tuzo hizo zinaendelea kilamwaka bilakukoma kwani nichachu kwa waajiri katika kuleta mabadiriko mahala pa kazi.

Naye Naibu Waziri Ofisiya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa amewataka waajiri kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia watu wenye ulemavu vifaa visaidizi
"Vifaa visaidizi kwa watu wenye ulemavu nikama chakula maana vinahitajika kila siku.

Unapomnunulia mtu mwenye ualbino mafuta yataisha na atahitaji mengine baada ya muda hivyo ni muhimu sana kwa wadau kujitokeza kwawingi kununua vifaa hivyo vikiwamo fimbo kwa wasiona na Wheel Chair (vitivyawalemavu),"alisema

Kwa upande wake Ofisa Mtendajiwa ATE, Agrey Mlimuka alisema tuzo hizo zilianza kutolewa mwaka 2005 zimekuwa zikihamasisha kampuni wanachama kuweka juhudi katika masuala ya ajira na usimamizi warasilimaliwatu kama msingi na mkakati wa kujenga nguvu kazi yenye ujuzi, furaha na ushindani.

Alisema kutokana na mapendekezo yaliyotolewa,  kwa mwaka huu tuzo hiyo ya mwajiri  bora imeongeza vipengele vipya vitatu hivyo kufanya kuwa na jumla ya vipengele 38 kutoka 35 vilivyokuwepo mwakajana.

Vipengele vilivyoongezeka ni mwajiri bora anayeendeleza mafunzo ya ujuzi kwa Kazi kwa wahitimu, mwajiri bora anayetoa mafunzo ya uwanangezi pamoja na tuzo ya mwajiri bora anayezingatia haki rasilimali, haya yaliku wamaagizo ya waziri mwakajana na tumeyatekeleza.

Alisema lengo la kuongeza vipengele hivyo nikuendelea kuboresha tuzo hizo, kuongeza ushindani miongoni mwawashiriki pamoja na kugusa kila eneo ambalo litaleta tija katika ukuzaji na uendelezaji warasilimaliwatu katika maeneo ya kazi.


"Tunatambua bila rasilimali watu hatuwezi kupiga hatua wala kwenda kwenye uchumi wa viwanda tunao usema, hivyo tuzo hizo mpya ni nyongeza katika zile zinazotolewa ambazo ni utawala na uongozi, ubora na usimamizi warasilimaliwatu, bidhaa na huduma, uwajibikaji katika mwenendo wa biashara, pamoja na usalama wa mwajiri wakati eneo la kazi”

Alisema wameendelea kuwa na tuzo ya mshindi wa jumla na kuongeza kuwa ushiriki wa kampuni katika tuzo hizo umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na ukweli kwamba ni jambo muhimu kwa ustawi wa wafanyakazi.

Kwa upande wake Mwenyekitiwabodiya ATE, Jayne Nyimbo alisema wanaomba wapate fursa ya kukutana na Rais John Magufuli kwani tangu aingie madarakani hajapata nafasi ya kukutana na waajiri ili kujua changamoto wanazo kumbananazo.

Alisema  ATE wanaamini kuwa iliwafikie mafanikio hasa katika Nyanja za kiuchumi na kijamii ni muhimu kuzingatia mgawanyo sawa warasilimali zao nchini kwa watu wote.

"Kwa kuzingatia hilo waajiri tunaendelea kutekeleza program maalum ya Female ambayo inalengo kuwajengea uwezo wanawake na hicho kuwawezesha kushika nafasi za uongozi katika Nyanja mbalimbali katika taifa letu, natoa wito kwa waajiri waendelee kushiri kikatika mpango huu ili kujenga mazingira yanayo jail usawa wa kijinsia hasa katika ngazi za maamuzi," alisema.

Share:

Wednesday, December 18, 2019

Benki ya DCB yaziasa familia kushiriki mazoezi ya viungo

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya  DCB, pampja na wakimbiaji wengine wakipasha viungo wakati wa mashindano ya Familia Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni. DCB ilidhamini tukio hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki mbio za Familia Marathon wakionyesha medali zao mara baada ya mbio hizo katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hilo lilidhaminiwa na DCB.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki mbio za Familia Marathon pamoja na wakimbiaji wengine wakishangilia mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach, Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hilo lilidhaminiwa na DCB.

Na mwandishi wetu,

BENKI ya Biashara ya DCB imezihamasisha familia kujenga tabia ya kushikiri mazoezi ya viungo ili kuweza kuwa na taifa lenye watu wenye afya bora jambo muhimu katika shughuli za uzalishaji mali za kila siku.

Akizungumza na washiriki wa mbio zilizopewa jina la Familia Marathon katika viwanja vya chumvi, Bahari Beach, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa DCB, Rahma Ngassa alisema ni muhimu kufanya mazoezi ili kuupa mwili afya na nguvu na kuzalisha mali. 

“Ni ukweli usiopingika kuwa magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza  huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya maisha tunayoishi na uzito mkubwa, mazoezi ya mwili yanasaidia sana kupambana na hali hizo”, alisema.

Bi Rahma aliongeza kuwa ili tuweze kuendelea na pia kutimiza azma ya serikali yetu ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda, tunahitaji sana kuwa na rasilimali watu wenye nguvu na afya bora ya   kuweza kuzalisha mali kwa wingi.

Mkuu huyo wa mawasiliano alisema ndio maana DCB ilipopata maombi ya kudhamini Familia Marathon walipokea maombi hayo kwa mikono miwili kwani kutokana na umuhimu wa mazoezi kwa afya za wateja wao na watanzania kwa ujumla.

“Wateja wetu wakiwa na afya bora wataongeza kasi ya uzalishaji mali hivyo hata nasi benki tutanufaika kutokana na kuwa kwa wateja wetu wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara kwani biashara zao zikikua na benki inakuwa.

“Endapo tukiwa na watanzania wenye afya bora, tutapunguza mzigo wa ghara za matibabu kutoka ngazi ya familia hadi kwa serikali, natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kuwa na utamaduni wa kushiriki mazoezi ya mwili ili kujenga afya bora ya miili yao”, aliongeza Bi Rahma.

Sambamba za hayo  Bi Rahma alisema licha ya kujali afya ya wateja wao na watanzania kwa ujumla, DCB imeendelea kutoa fursa na bidhaa mbalimbali kwa wateja zinazolenga kutoa suluhisho la mahitaji ya kifedha kwa wateja wao. “Bidhaa hizi zinawalenga wateja wetu wote wakubwa kwa wadogo, wafanyabishara wakubwa na wadogo, wakulima pamoja na wateja katia makundi mengine”,alisema.

Alizitaja bidhaa hizo kama DCB Sokoni inayolenga kumkomboa mkulima na mfanyabiashara wa kilimo  katika mnyororo wake wa thamani,  DCB Skonga, ikilenga kuwasaidia wazazi katika suala zima la ada za watoto wao, DCB Lamba Kwanza ambayo mteja huanza hupata riba nzuri mara anapoamua kuwekeza, DCB kibubu ambayo mteja hujiwekea akiba mwenyewe kidogo kidogo huku ikianzisha huduma ya DCB Digital ambayo pamoja na mambo mengine humuwezesha mteja kufungua kaunti mahali alipo na kweza kupata huduma nyingi za kibenki za DCB kwa njia ya kidigitali.

Share:

Monday, December 16, 2019

Swissport yatoa msaada wa machine mbili zenye thamani ya Sh.Milioni 12.6 katika Hospitali ya Temeke

Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dk. Serafini .K. Patrice (kushoto) akipokea moja ya mashine zenye thamani ya shilingi milioni 12.6 ijulikanayo kwa jina la Patient Monitor inayofuatilia muenendo wa afya ya mgonjwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Swissport Tanzania, Nd. Yassin Mrisho.

KAMPUNI ya kuhudumia mashirika ya ndege, abiria na mizigo katika viwanja vya ndege ya Swissport imetoa msaada wa mashine mbili za kufatilia afya ya mgonjwa anapokuwa katika hali isiyo ya kawaida, zenye thamani ya Sh. Milioni 12.6 kwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kukabidhi msaada huo hospitalini hapo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Mrisho Yassin alisema wamesukumwa kutoa msaada huo ili kuweza kuokoa maisha ya mama na mtoto wanaofika katika hospitali hiyo kupata huduma.

Alisema kampuni yao imekuwa na sera ya kusaidia jamii hasa katika maeneo ya afya na elimu hivyo wakati huu wa kumaliza mwaka wameamua kutoa msaada huo ambao utakwenda kupunguza baadhi ya changamoto zilizokuwa zinaikabili hospitali hiyo.

“Tumekuja katika hopsitali hii kwa sababu tunataka kuisaidia jamii hivyo mashine hizi mbili ambazo kwa jina la kitaalamu zinajulikana kama Patient Monitor zitakwenda kusaidia watoto ambao mara nyingi si rahisi kutambua wanaumwa nini pia itawasaidia kinamama,” alisema Yassin na kuongeza.

“Tutaendelea kushirikiana zaidi na hospitali hii ili kuweza kutatua  baadhi ya changamoto zingine zilizopo, lakini pia jambo hilo limefungua mlango kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia,” alisema.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Serafini Patrice alisema pamoja na kupokea msaada huo bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na wod, hivyo wanawaomba wadau wengine kujitokeza kuweza kusaidia.

“Licha ya kwamba Serikali imekuwa ikijitahidi kwa kiasi kikubwa kuisaidia hospitali hiyo ambayo inamadaktari bingwa zaidi ya 10, lakini bado peke yake haiwezi kumaliza changamoto zilizopo katika hospitali hii hivyo basi tunawaomba  wadau wengine wajitokeza kusaidia,” alisema.


Aidha alisema hospitali hiyo imekuwa ikiwahudumia wagonjwa zaidi ya Milioni 1.6 ila magonjwa waliomengi ni yale ya kinamama pamoja na ya upasuaji wa mifupa.
Share:

Saturday, December 14, 2019

KAMPUNI YA VISA YAWAFANYIA MAKUBWA WATEJA WAKE

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo fleve wanaounda kundi la NAVY KENZO Emmanuel Mkono pamoja na Aika Marealle ambao ni Mabalozi wa Visa,  wakipiga picha ya pamoja na  mmoja ya wateja na familia yake alipokwenda kufanya manunuzi kwakutumia  kadi ya Visa katika maduka yaliyopo katika jengo Msasani Mall jijini Dar es Salaam leo. ambapo mteja aliweza kulipiwa nusu ya gharama ya manunuzi yake na mabalozi hao
Balozi wa VISA kadi ambae  ni msanii wa musiki wa kizazi kiPya anaeunda kundi la NAVY KENZO   Emmanuel Mkono almaarufu kama Nahreel (kulia), akionesha kadi yake ya Visa ambayo mteja anaweza kuitumia kufanya manunuzi badala yakutembea na pesa mkononi anaweza kutumia kadi hiyo (katikati), ni msanii wa kundi hilo pamoja na mteja anaetumia kadi ya Visa kufanya manunuzi
Balozi wa VISA kadi ambae  ni msanii wa muziki wa kizazi kipya anaeunda kundi la NAVY KENZO   Emmanuel Mkono almaarufu kama Nahreel (kushoto),akifanya kwakutumia kadi yake ya Visa kwakumlipia Evetha Sebastian (kulia), ambae huwa anatumia kadi yake ya visa  kufanya manunuzi (katikati), ni msanii wa kundi hilo ambaye  pia ni Balozi wa Visa Aika Marealle
Balozi wa VISA kadi ambae  ni msanii wa muziki wa kizazi kipya anaeunda kundi la NAVY KENZO   Emmanuel Mkono almaarufu kama Nahreel (kushoto), akifafanua jambo juu ya matumizi ya Visa kadi kwa Mteja anaetumia kadi hiyo kufanya manunuzi, Hussein Bashiru (katikati) mwengine pichani ni Balozi wa Visa Balozi ambae ni mmoja ya wasanii wa kundi la NAVY KENZO  Aika Marealle PICHA ZOTE NA Brian Peter
Share:

Benki ya NBC yakutana na wateja wake kuwashukuru kwa mahusiano bora kwa mwaka 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Abdallah Mwaduga katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi wa NBC, Rehema Chonde.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akifurahi pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Kampuni G4S Cash Solutions Tanzania, Hassan Nuru na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya G4S Secure Solutions Tanzania, Barry Hogg.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akisalimia na Mkurugenzi wa Kampuni ya Enterprises Business Department, Tony Wu huku Ofisa Fedha Mkuu wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Mao Jinbao akiangalia katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kulia), akisalimiana na baadhi ya wateja waliohudhuria  hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Benki ya NBC, Linley Kapya (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Abdallah Mwaduga katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi wa NBC, Rehema Chonde.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Anga Tanzania, Hamza Johari, huku Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe (katikati), akiangalia,  katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis ndunguru (katikati), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi (kushoto), huku Mwenyekiti wa Kampuni ya Chelsea Starway Group, Martin Mbwana akisikiliza, katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive