Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (katikati) akimkabidhi tiketi ya ndege mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Jocelyne Rwechungura aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mshindi huyo pamoja na mwenza wake aliyemchagua.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tatu kushoto) akimkabidhi tiketi ya ndege, mwenza wa mshindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Kijakazi Mohamed aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond na Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mwenza huyo pamoja na mshindi mwenyewe Ramadhani Saidi (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke akimkabidhi tiketi ya ndege, mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Prof. Lettice Rutashobya (kulia), aliyejishindia safari ya kwenda Sychelles wakati wa hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka Kushoto ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond na Meneja Masoko wa Benki hiyo, Alina Maria Kimaryo. NBC inalipia gharama za safari ya mshindi huyo pamoja na mwenza wake aliyemchagua.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na maofsa wa NBC katika hafla hiyo.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond akizungumza katika hafla hiyo ambapo alitoa hamasa kwa wateja na wasio wateja kuitumia kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC ili kutimiza malengo yao.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke akizungumza katika hafla ya kuwapongeza na kuwaaga washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo walioshinda safari za kwenda Sychelles na katika mbuga za wanyama za Serengeti.
Meneja Masoko wa NBC, Maria Alina Kimaryo akizungumza kuhusu kampeni hiyo akisema Ibuka Kidedea imekuwa ikitoa zawadi kila mwezi na hadi sasa jumla ya pikipiki tano zimeshatolewa tangu mwezi Oktoba ilipozinduliwa.
Dar es Salaam 27 Disemba, 2019.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imefanya hafla maalumu ya kuwapongeza na kuwaaga wateja walioibuka washindi katika Kampeni yake ya Ibuka Kidedea na akaunti ya NBC Malengo. Washindi hao wamejishindia safari za kitalii ambapo baadhi watazulu Mbuga ya Wanyama ya Serengeti na wengine visiwa wa Sychelles.
Kampeni ya Ibuka Kidedea ilizinduliwa mwezi Okotoba mwaka huu ikiwa na lengo kuu la kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kwa wateja ambapo zawadi mbalimbali zikiwemo zikiwemo bodaboda zimekuwa zikitolewa kwa washindi walioingia kwenye droo maalum inayosimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha nichini.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga washindi hao iliyofanyika Hoteli ya Four Points by Sheraton (zamani New Africa), jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa wateja Binafsi wa NBC, Elibariki Masuke aliwashukuru wateja wote waliojitokeza kushiriki kampeni hii tangu kuzinduliwa kwake .
“Ibuka Kidedea imefanyika kwa mafanikio makubwa, tumeshuhudia idadi kubwa ya wateja wetu wakishiriki katika kampeni hii, lakini pia wateja wanashuhudia kuongezeka kwa amana zao kutokana na faida za kila mwezi.
"Natoa pongezi kwa washidi wetu wote na tunaamini mtaendelea kuwa mabalozi wetu wakati mkifurahia safari hizi katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka”, kampeni hii bado inaendelea hivyo tunatoa wito kwa wateja wengine kushiriki katika kampeni hii kwa kuendelea kuweka akiba ili kupata nafasi ya kushinda zawadi”, aliongeza Bwana Masuke.
Naye Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond alisema ni matumani ya NBC kuwa kampeni hii inatoa hamasa kwa watanzania kuwa na utamaduni endelevu wa kujiwekea akiba ili kutimiza mahitaji yao ya kifedha lakini zaidi ni kuwa na uhuru wa kifedha.
"Tunahamasisha wateja wetu na wasio wateja kuitumia akaunti ya Malengo ya NBC ili kutimiza malengo yao, iwe ni nyumba, gari nzuri, pikipiki, kwenda mapumzikoni, ada za shule na mengineyo.
"Tunajua kila mtu ana ndoto yake, jiunge na NBC Malengo na tutafurahi kukusaidia kutimiza ndoto zako", aliongeza.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo, Meneja Masoko wa NBC, Alina Kimaryo alisema Ibuka Kidedea imekuwa ikitoa zawadi kila mwezi na hadi sasa jumla ya pikipiki tano zimeshatolewa tangu mwezi Oktoba.
Ili kujishindia pikipiki (bodaboda) mteja anachotakiwa kufanya ni kuweka akiba kwa kiwango kinachoanzia shs 100,000 katika akaunti yake ya Malengo, na kwa safari ya Serengeti kiwanngo kinaanzia shs 1,000,000 na kiwango kinachoanzia 50,000,000 kwa safatri ya Sychelles.
"Pamoja na zawadi hizi katika kampeni hii, wateja watakaoweka akiba katika akaunti zao za Malengo kwa kiwango kinachoanzia shs 1,000,000 wanapata nafasi ya kujishindia pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo katika droo kubwa ambayo jumla ya pikipiki za kubebea mizigo (Toyo) tatu zitatolewa”, alisema.
Mmoja wa washindi aliyejishindia bodaboda, Daudi Patrick Majani, mstaafu na mfanyabiashara anayeishi Tabata Segerea jijini Dar es Salaam alisema atatumia bodaboda yake kumuingizia kipato na kuitumia kwa usafiri utakaosaidia kuiwezesha biashara yake.
Washindi walioshinda safari ya Serengeti ni Christopher Mgote kutoka Nzega, Makongoro Makongoro kutoka Arusha, Bi. Jocelyine Rwechengura na Bi.Esther Ndunguru wote kutoka Dar es Salaam.
Washindi walioshinda safari ya Sychelles ni, Wambura John Wambura kutoka Tarime mkoani Mara, Ramadhan Saidi, Lettice Rutashobya na Sylevester Ambokile wote wa jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment