A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, December 18, 2019

Benki ya DCB yaziasa familia kushiriki mazoezi ya viungo

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya  DCB, pampja na wakimbiaji wengine wakipasha viungo wakati wa mashindano ya Familia Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni. DCB ilidhamini tukio hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki mbio za Familia Marathon wakionyesha medali zao mara baada ya mbio hizo katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hilo lilidhaminiwa na DCB.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB walioshiriki mbio za Familia Marathon pamoja na wakimbiaji wengine wakishangilia mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo katika viwanja vya Chumvi, Bahari Beach, Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio hilo lilidhaminiwa na DCB.

Na mwandishi wetu,

BENKI ya Biashara ya DCB imezihamasisha familia kujenga tabia ya kushikiri mazoezi ya viungo ili kuweza kuwa na taifa lenye watu wenye afya bora jambo muhimu katika shughuli za uzalishaji mali za kila siku.

Akizungumza na washiriki wa mbio zilizopewa jina la Familia Marathon katika viwanja vya chumvi, Bahari Beach, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa DCB, Rahma Ngassa alisema ni muhimu kufanya mazoezi ili kuupa mwili afya na nguvu na kuzalisha mali. 

“Ni ukweli usiopingika kuwa magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza  huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya maisha tunayoishi na uzito mkubwa, mazoezi ya mwili yanasaidia sana kupambana na hali hizo”, alisema.

Bi Rahma aliongeza kuwa ili tuweze kuendelea na pia kutimiza azma ya serikali yetu ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda, tunahitaji sana kuwa na rasilimali watu wenye nguvu na afya bora ya   kuweza kuzalisha mali kwa wingi.

Mkuu huyo wa mawasiliano alisema ndio maana DCB ilipopata maombi ya kudhamini Familia Marathon walipokea maombi hayo kwa mikono miwili kwani kutokana na umuhimu wa mazoezi kwa afya za wateja wao na watanzania kwa ujumla.

“Wateja wetu wakiwa na afya bora wataongeza kasi ya uzalishaji mali hivyo hata nasi benki tutanufaika kutokana na kuwa kwa wateja wetu wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara kwani biashara zao zikikua na benki inakuwa.

“Endapo tukiwa na watanzania wenye afya bora, tutapunguza mzigo wa ghara za matibabu kutoka ngazi ya familia hadi kwa serikali, natoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kuwa na utamaduni wa kushiriki mazoezi ya mwili ili kujenga afya bora ya miili yao”, aliongeza Bi Rahma.

Sambamba za hayo  Bi Rahma alisema licha ya kujali afya ya wateja wao na watanzania kwa ujumla, DCB imeendelea kutoa fursa na bidhaa mbalimbali kwa wateja zinazolenga kutoa suluhisho la mahitaji ya kifedha kwa wateja wao. “Bidhaa hizi zinawalenga wateja wetu wote wakubwa kwa wadogo, wafanyabishara wakubwa na wadogo, wakulima pamoja na wateja katia makundi mengine”,alisema.

Alizitaja bidhaa hizo kama DCB Sokoni inayolenga kumkomboa mkulima na mfanyabiashara wa kilimo  katika mnyororo wake wa thamani,  DCB Skonga, ikilenga kuwasaidia wazazi katika suala zima la ada za watoto wao, DCB Lamba Kwanza ambayo mteja huanza hupata riba nzuri mara anapoamua kuwekeza, DCB kibubu ambayo mteja hujiwekea akiba mwenyewe kidogo kidogo huku ikianzisha huduma ya DCB Digital ambayo pamoja na mambo mengine humuwezesha mteja kufungua kaunti mahali alipo na kweza kupata huduma nyingi za kibenki za DCB kwa njia ya kidigitali.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive