A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, May 29, 2018

NBC yatoa udhamini wanafunzi vyuo vikuu

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE), Prof. Godliving Mtui (kutoka kushoto), Mkuu wa Chuo cha Uhifadhi Wanyama Pori, Prof. Jaffari Kideghesho, Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emmanuel Mjema na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dr. Imanueli  Mnzava wakisaini mikataba ya ufadhili wa wanafunzi 60 kutoka Benki ya NBC utakaowanufaisha wanafunzi hao katika mwaka wa kwanza wa masomo wa 2018/19 katika hafla iliyofanyika jijini  Dar es Salaam  hivi karibuni. Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa tano kushoto waliosimama), Kaimu Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kassim Hussein (wa sita kushoto) na baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo wakishuhudia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa program ya ufadhili ya NBC ambapo wanafunzi 60 watapata ufadhili katika vyuo vikuu vinne chini. Ufadhili huo wenye thamani ya shs milioni 300 utavihusu  Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo cha Uhifadhi Wanyama Pori Mweka (CAWM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), na  Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Kulia ni wakuu wa vyuo hivyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein (katikati). akishikana mikono na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Elimu  Dar es Salaam (DUCE), Prof. Godliving Mtui katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha CBE, Dk. Emanuel Mjema.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dr. Imanueli  Mnzava akzungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa programu ua ufadhili ya benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Michael Mniko akiishukuru NBC kwa kutoa ufadhili huo akisema utaisaidia serikali katika azma yake ya kuinua kiwango cha elimu nchini.
Share:

Monday, May 28, 2018

RESPECT BARBER SHOP YAFUTURISHA WAKAZI WA DAR


Ukizungumzia moja  ya mameneja wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na Dansi hapa nchini, huwezi kuacha kutaja jina la Mohamed  Kiumbe ‘Chief kiumbe’ jana amefuturisha jijini Dar es salaam katika ofisi za Respect Barber Shop Kinondoni ambapo mamia ya watu walihudhuria katika futari hiyo wakiwemo wasanii. mbalimbali wa bongofleva na filamu.

Pia  Respect Barber Shop imeamua kuandaa futari hiyo kwa wakazi wa jiji hilo ili kuonesha upendo pia  kama moja ya sadaka katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani. 

Baadhi ya wasanii waliohudhuria Iftari hiyo ni pamoja na Khadija Kopa, Mwajuma Abdul ‘Queen Darling’ na Bonge la Nyau na wengine wengi wakiwepo wasanii wa dansi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Iftari hiyo, Msemaji wa saluni ya Respect, Dakota Delavida amesema kuwa huu ni mwanzo tu ila Mungu akiwapa uzima wataongeza wigo wao kwani ni kitendo cha kurudisha fadhila kwa jamii.

“Chakula ni sadaka  na huwezi kupanga kiishie hapa tulijipanga vya kutosha, hii ni mara yetu ya kwanza mwenyezi Mungu akitujaalia uzima tutafanya tukio kama hili tena kwani ni kurudisha fadhili kwa jamii tunayoihudumia” alisema Dakota.


Wasimamizi wa shughuli hiyo wakiendelea kuhakikisha mambo yanakuwa sawia muda wote,
Msanii sheta akikaribia katika viwanja vya  Respect Barbar Shop kwaajili ya kupata futari iliyoandaliwa na ofisi hiyo.

Msanii kutoka kundi la Tiptop Tunda Man akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Respect Barbar Shop kwakuandaa futari hiyo pia kama moja yakuwaweka watu karibu.


Dakota akigawa Chakula kwa wakazi waliohudhulia futari hiyo
Share:

MKOMBOZI BENKI YATOA GAWIO KWA WANAHISA.

Benki ya Biashara ya Mkombozi PLC, ni miongoni mwa benki ya biashara hapa
nchini inayokua kwa kasi. Imetashatangaza kutoa gawio la faida kwa wanahisa wake
wote ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Mkurugenzi mtendaji wa benki, Ndugu George R. Shumbusho amesema bank
itafanya malipo ya gawio kwa mujibu wa ratiba za hitaji la soko la hisa la DSM –
DSE. Na benki inatarajia wanahisa wote kupata gawio ndai ya mwezi Julai.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji. Tangangazo la siku ya gawio la faida ni
tarehe 26 mwezi Mei na kufuatiwa na mauzo ya hisa yatakayokua na gawio
yatakayofanyika kati ya tarehe 26 mwezi Mei hadi tarehe 15 mwezi Juni.

Ameyazungamza hayo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa
benki ya bishara ya Mkombozi, uliokutanisha zaidi ya wanahisa 100. Na kuongeza
kuwa mauzo ya hisa yasiyokuwa na gawio yataanza kuuzwa kuanzia tarehe 16
mwezi juni.

“kitabu cha wanahisa cha malipo ya marejesho kitafungwa rasmi mnamo tarehe 20
mwezi Juni, na kufunguliwa upya tarehe 21 mwezi Juni mwaka huu”. Alisema.

Mkurugenzi mtendaji ameongeza kuwa baada ya hatua zote hizi kukamilika
Wanahisa wanatarajiwa kuanza kupokea gawio la faida kuanzia tarehe 6 mwezi
Julai mwaka huu.

“Gawio la hisa kwa mwanachama litagawiwa moja kwa moja kupitia akaunti ya
benki ya mteja. Pia kupitia huduma za pesa kwa njia ya simu kama vile m-pesa,
airtel pesa na tigo pesa” alisema ndugu Shumbusho. Shumbusho ameongeza kuwa
kwa mwaka huu gawio limeongezeka hadi kufikia shilingi 25 kwa kila hisa kutoka
shilingi 20 ilivyokua mwaka jana.

Upanuzi wa huduma za kisasa zinazofanywa na MKCB PLC zimefanya urahisi wa
utoaji wa huduma kwa wateja. Hii imesaidia banki kutoa huduma zinazoridhisha
wateja na kwa ufanisi wenye kutatua changamoto za huduma za fedha kwa mtu
mmoja mmoja, kampuni na wafanyabiashara.

Hadi ilivyofika tarehe 31 mwezi Disemba 2007, jumla ya thamani ya mali za benki
zimeongezeka na kufikia shilingi bilioni 150.67 ukilinganisha na ilivyokuwa shilingi
bilioni 128.17 mwaka 2016. Kisi hicho cha fedha ni sawa na ongezeko la 17.6%.
Amana za wateja pia zimengezeka na kufikia shilingi bilioni 121.12 hadi mwishoni.
Share:

Sunday, May 27, 2018

GSM YAJA NA BANDO LA NGUO.


Kufuatia kauli iliyotolewa na serikali siku chache kabla ya mfungo wa ramadhani ya kutaka wafanya biashara wote nchini kutopandisha bei bidhaa kampuni GSM inatekeleza agizo kwa kutoa punguzo la bei kwa bidhaa zake katika maduka yake yote hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es salaam, Meneja wa  GSM Pugu Mall, Simon Kais,  juu ya punguzo hilo kwa bidhaa zao zinazo patikana katika maduka yao amesema kuwa kutokana na wito uliotolewa na serikali wameamua kufuata maelekezo hayo ya kutopandisha bidhaa bei kwa msimu huu wa sikukuu

Aidha imetoa punguzo  hilo kwa wateja wake ikiwa ni sehemu ya kuwanufaisha wateja katika msimu huu wa sikukuu lengo nikutaka kila mtanzania ambae anakipato cha chini  aweze kutumia kilicho bora kulingana na kipato chake alisema Kais.
Upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza, amesema katika ofa hiyo pia kutakuwa na Bando la Nguo ambalo litamnufaisha mteja kupata nguo mara mbili atakaponunua Nguo kuanzia elfu ishirini pia bei ni nafuu sana ukilinganisha na ubora wa bidhaa hizo.

Pia GSM wameandaa ubao maalum ambao Mteja ukienda pale anaweza kupika picha selfie ukapost kwenye mtandao wakijamii wa facebook au istagram ukipata like mia moja zinaweza zikakusababisha ukapata zawadi nono kuanzia laki moja nakuendelea kutaka GSM
Share:

Friday, May 25, 2018

TMRC launches its 5 years Corporate Bonds issuance program

IMG_3113
The 5 year corporate bond issuance program is worth TZS 120 billion
TMRC will issue its first tranche of TZS 12 billion immediately in June 2018
tmrccccTanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) launched its 5 year corporate bond issuance program to the public today.  The launch took place today at the Serena Hotel and it was witnessed by potential investors, regulators and other financial sector stakeholders.  TMRC bond issuance launch took place after TMRC received all the necessary approvals for the 5 years corporate bond issuance program worth TZS 120 billion. 

 The program received the green light from both the Capital Markets and Securities Authority (CMSA) as well as Dar-es-salaam Stock Exchange (DSE).  TMRC corporate bonds will be listed on the DSE.The CMSA and DSE approval also included the go ahead for TMRC to issue its first Tranche of the corporate bond which will be TZS 12 billion.  TMRC CEO Oscar Mgaya said “we have received all the necessary approvals and we intent to go to the market with our first tranche immediately”.
TMRC is a specialized private sector financial Institution that provides long-term funding to financial institutions for the purposes of mortgage lending. It has the objective of supporting financial institutions to do mortgage lending by refinancing Primary Mortgage Lenders' (PMLs') mortgage portfolios. This type of lending is also known as wholesale or secondary market lending. TMRC is neither taking deposits nor lending directly to individuals. It refinances mortgage loan portfolios rather than individuals mortgage loans and caters to banks rather than individual borrowers.  TMRC is raising the funds to support its operations of mortgage refinancing.  “It was envisioned from its inception that TMRC will source funds from the capital markets through bond issuance among other sources” said Mgaya.  “It was just a matter of time and now is the right time given the declining interest rates environment” added Mgaya.
TMRC Shareholders:



Untitled 
Share:

Wednesday, May 23, 2018

WANAWAKE WAJAWAZITO WAPEWA SOMO KUHUSU FISTULA.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto), akizunguza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kulia kwake ni Mgeni rasmi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi Jacqueline Mahon.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline Mahon  akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wakati akitoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Amref Afrika Dkt. Floriance Temu akiongea na waandishi wa habari wakati maazimisho ya siku ya ugonjwa wa fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.




WANAWAKE wajawazito wamepewa manufaa na umuhimu wa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.




“Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40 tu ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.




Aidha, Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.




Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea kwa wanamke kupata fistula.




Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma za Fistula zinapatikana Bure nchini  kote hasa kwenye hospitali za CCBRT,Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata ushauri.




Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linayoshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi walioko Hospitali za Wilaya na Mkoa.




Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA Bi. Jacqueline Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma za afya wapatao elfu nne ili kupamabana na ugonjwa huo.

“Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” alisema Bi. Mahon.




Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji hospitali ya CCBRT inashirikkiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”
Share:

Monday, May 21, 2018

Balozi Ambokile kutangaza chakula cha Kitanzania Afrika Kusini


01
Balozi wa Tanzania  nchini  Afrika Kusini, SylvesterAmbokile , (kulia) akifurahia jambo pamoja na Mmiliki wa mgahawa huo.
02
Msanii wa bongo fleva sheta akipiga msosi katika Mgahawa huo.

BALOZI wa Tanzania  nchini  Afrika Kusini,Sylvester Ambokile ,  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mgahawa wa kisasa  wa chakula cha Kitanzania uitwao  Grill House Take Away  jijini Johanesburg nchini humo.

Mgahawa huo unalengo la kutangaza chakula asili cha kitanzania  kimataifa  pamoja na kuwapa huduma hiyo watanzania waishio nchini humo.

Akizungumza  na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, jana kwa niaba ya Mmiliki wa Mgahawa huo ,  Christopher Robert, mwakilishi wa mkurugenzi huyo hapa nchini, Frank Koko alisema sherehe za ufunguzi rasmi zimepangwa kufanyika  Juni 21 mwaka huu.

“Dhima yetu ni kukitangaza chakula asilia cha kitanzania kimataifa. Wapishi wote ni kutoka Tanzania na chakula kinasafirishwa kutoka Tanzania hadi nchini humo,”alisema Koko.

Alisema, kwa miaka mingi chakula cha kitanzania hakijapewa nafasi kubwa katika soko la  hoteli na migahawa duniani  kiasi cha kuwafanya hata watanzania wakiwa nje ya nchi kulazimika kula chakula ambacho si asili yao.

“Tuliona kwamba hata hoteli za kitanzania zinapika zaidi  chakula cha  utamaduni wa nje, watu wanalazimika kula tu.Ukifika Johanesburg ni changamoto kubwa kupata chakula cha nyumbani.

Watanzania wanahangaika kupata chakula cha asili yao jambo ambalo lilitusukuma kuja na wazo hili la kuwa na sehemu ambayo mtanzania akitua Johanesburg atapata huduma zote kama za nyumbani,”alisema.

Aliongeza; “ Tunaomba watanzania watakaotembelea Johanesburg watemelee Grill House Take Away , Mtaa wa 
51 Regent ili  waweze kutuunga mkono,”alisema Koko.

Picha mbalimbali muonekano wa Mgahawa huo.
IMG-20180521-WA0041

IMG-20180521-WA0036

IMG-20180521-WA0042

IMG-20180521-WA0043%2B%25281%2529

IMG-20180521-WA0037%2B%25281%2529
IMG-20180521-WA0036

IMG-20180521-WA0038

IMG-20180521-WA0045

IMG-20180521-WA0048

IMG-20180521-WA0038

sssss

IMG-20180521-WA0050
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive