Benki ya Biashara ya Mkombozi PLC, ni miongoni mwa benki ya biashara hapa
nchini inayokua kwa kasi. Imetashatangaza kutoa gawio la faida kwa wanahisa wake
wote ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Mkurugenzi mtendaji wa benki, Ndugu George R. Shumbusho amesema bank
itafanya malipo ya gawio kwa mujibu wa ratiba za hitaji la soko la hisa la DSM –
DSE. Na benki inatarajia wanahisa wote kupata gawio ndai ya mwezi Julai.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji. Tangangazo la siku ya gawio la faida ni
tarehe 26 mwezi Mei na kufuatiwa na mauzo ya hisa yatakayokua na gawio
yatakayofanyika kati ya tarehe 26 mwezi Mei hadi tarehe 15 mwezi Juni.
Ameyazungamza hayo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa
benki ya bishara ya Mkombozi, uliokutanisha zaidi ya wanahisa 100. Na kuongeza
kuwa mauzo ya hisa yasiyokuwa na gawio yataanza kuuzwa kuanzia tarehe 16
mwezi juni.
“kitabu cha wanahisa cha malipo ya marejesho kitafungwa rasmi mnamo tarehe 20
mwezi Juni, na kufunguliwa upya tarehe 21 mwezi Juni mwaka huu”. Alisema.
Mkurugenzi mtendaji ameongeza kuwa baada ya hatua zote hizi kukamilika
Wanahisa wanatarajiwa kuanza kupokea gawio la faida kuanzia tarehe 6 mwezi
Julai mwaka huu.
“Gawio la hisa kwa mwanachama litagawiwa moja kwa moja kupitia akaunti ya
benki ya mteja. Pia kupitia huduma za pesa kwa njia ya simu kama vile m-pesa,
airtel pesa na tigo pesa” alisema ndugu Shumbusho. Shumbusho ameongeza kuwa
kwa mwaka huu gawio limeongezeka hadi kufikia shilingi 25 kwa kila hisa kutoka
shilingi 20 ilivyokua mwaka jana.
Upanuzi wa huduma za kisasa zinazofanywa na MKCB PLC zimefanya urahisi wa
utoaji wa huduma kwa wateja. Hii imesaidia banki kutoa huduma zinazoridhisha
wateja na kwa ufanisi wenye kutatua changamoto za huduma za fedha kwa mtu
mmoja mmoja, kampuni na wafanyabiashara.
Hadi ilivyofika tarehe 31 mwezi Disemba 2007, jumla ya thamani ya mali za benki
zimeongezeka na kufikia shilingi bilioni 150.67 ukilinganisha na ilivyokuwa shilingi
bilioni 128.17 mwaka 2016. Kisi hicho cha fedha ni sawa na ongezeko la 17.6%.
Amana za wateja pia zimengezeka na kufikia shilingi bilioni 121.12 hadi mwishoni.
0 comments:
Post a Comment