Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko
(wapili kushoto) akizungumza na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) pamoja na wakazi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya
kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Vijana wajasiriamali waosha
magari wa Kikundi cha Msingi Mikwanja
Car Wash yenye thamani ya shilingi milioni 1 iliyotoka katika fedha ya mfuko wa
jimbo la Ukonga.Ni mwendelezo wa kutimiza ahadi ambazo Mbunge wa Jimbo la
Ukonga,Mwita Waitara aliziahidi kwa wakazi wa jimbo hilo.Kushoto ni Mkurugenzi
wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema),John Mrema.
Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa
mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema
(kushoto) akizungumza jambo na wakazi wa Mtaa wa Guruka Kwalala uliopo katika
kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katika mtaa huo
leo kwa ajili ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa vijana wajasiriamali
waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash ikiwa ni mwendelezo wa
kutimiza ahadi za Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko,Diwani wa Kata
ya Gongo la Mboto,Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la
Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto),Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas
Rukiko, Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa
Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo wakikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki
yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana
wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash, Ally Mfaume
(Wapili kulia) na Katibu Wake,Yasini Omary jijini Dar es Salaam leo.Uongozi wa
Kata na mtaa pamoja Viongozi kutoka Chadema wamekabidhi mashine mbili za kuosha
magari kwa Vikundi vya Vijana
wajasiamali waosha magari wa Mtaa wa Guruka Kwalala.
Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko
(kushoto) akizungumza jijini Dar es Slaam leo na Vijana wa Kikundi kingine cha
Vijana wajasiriamali kitwaacho Nyamachoma kinachofanya kazi ya kuosha magari maeneo
ya Gongo la mboto Mwisho wa lami katika
hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya
shilingi Milioni 1 iliyotoka katika fedha ya Mfuko wa jimbo la Ukonga
ikiwa ni Mwendelezo wa kutimiza ahadi
alizoahidi Mbunge wa Jimbo hilo,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa
Kikundi cha Nyamachoma Car Wash,Juma Sungamizi,Katibu wa kikundi,Jimmy Vitalis
na Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano
wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema.
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi(watatu
kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.
Mashine ya Kuosha magari iliyokabidhiwa leo kwa
Kikundi cha Nyamachoma Car wash kilichopo Gongo la Mboto mwisho wa lami jijini
Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la
Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akizungumza jijini Dar es
Salaam leo na Vijana wajasiriamali wa Kikundi cha Kuosha magari kiitwacho
Nyamachoma Car Wash katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na
pikipiki kwa kikundi hicho yenye thamani ya shilingi Milioni 1 kutoka katika Mfuko
wa Jimbo la Ukonga.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la
Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akikabidhi mashine ya
kuosha magari na pikipiki kwa Katibu wa Kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha
magari kiiitwacho Nyamachoma Car Wash,Jimmy Vitalis (wapili kulia) na
Mwenyekiti wa kikundi hicho,Juma Sungamizi jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la
Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akipeana mikono ya
pongezi na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo baada ya kukabidhi
mashine mbili za kuosha magari na pikipiki kwa Vikundi viwili vya waosha magari
Nyamachoma Car Wash na Msingi Mkwanja Car Wash vilivyopo katika Mtaa wa Gruruka
Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo.
0 comments:
Post a Comment