Kufuatia kauli iliyotolewa na serikali siku chache kabla ya mfungo wa ramadhani ya kutaka wafanya biashara wote nchini kutopandisha bei bidhaa kampuni GSM inatekeleza agizo kwa kutoa punguzo la bei kwa bidhaa zake katika maduka yake yote hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es salaam, Meneja wa GSM Pugu Mall, Simon Kais, juu ya punguzo hilo kwa bidhaa zao zinazo patikana katika maduka yao amesema kuwa kutokana na wito uliotolewa na serikali wameamua kufuata maelekezo hayo ya kutopandisha bidhaa bei kwa msimu huu wa sikukuu
Aidha imetoa punguzo hilo kwa wateja wake ikiwa ni sehemu ya kuwanufaisha wateja katika msimu huu wa sikukuu lengo nikutaka kila mtanzania ambae anakipato cha chini aweze kutumia kilicho bora kulingana na kipato chake alisema Kais.
Upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza, amesema katika ofa hiyo pia kutakuwa na Bando la Nguo ambalo litamnufaisha mteja kupata nguo mara mbili atakaponunua Nguo kuanzia elfu ishirini pia bei ni nafuu sana ukilinganisha na ubora wa bidhaa hizo.
Pia GSM wameandaa ubao maalum ambao Mteja ukienda pale anaweza kupika picha selfie ukapost kwenye mtandao wakijamii wa facebook au istagram ukipata like mia moja zinaweza zikakusababisha ukapata zawadi nono kuanzia laki moja nakuendelea kutaka GSM
0 comments:
Post a Comment