Thursday, October 1, 2026
AaDKT.YONAZI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UTURUKI
Monday, September 28, 2026
MIXX BY YAS YAONGEZA NGUVU JUHUDI ZA SERIKALI KUIMARISHA KILIMO NA VYAMA VYA USHIRIKA TANGA
TANGA: Mixx by Yas imeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha sekta ya kilimo na vyama vya ushirika kwa kutoa vitendea kazi kwa vyama vya ushirika mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuongeza matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali na kuchochea maendeleo ya wakulima.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Meneja wa Uhusiano wa Biashara na Serikali na Taasisi zake wa Mixx by Yas, Suleiman Asilia Khamis, alisema kampuni hiyo inalenga kujenga ushirikiano unaokwenda zaidi ya kuwezesha malipo kwa wakulima.
Katika hafla hiyo, Mixx by Yas ilikabidhi pikipiki na freezer kwa Tanga Dairy Cooperative Union (TDCU), vitakavyosaidia katika ukusanyaji wa maziwa kutoka kwa wakulima pamoja na shughuli za uuzaji wa maziwa.Kwa upande wa Tanga Rural Cooperative Union (TARECU), inayoshirikiana na wakulima wa mazao mbalimbali yakiwemo kakao, ufuta, mbaazi na korosho, Mixx by Yas imetoa guta litakalosaidia kusafirisha mazao kutoka mashambani kwenda katika vituo vya ukusanyaji.“Mixx by Yas tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya kilimo, vyama vya ushirika na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kufanya malipo kwa wakulima. Dhamira yetu ni kuhakikisha teknolojia na huduma za kifedha zinakuwa sehemu ya kuongeza ufanisi katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo,” alisema Khamis.
Khamis alisema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya Mixx by Yas ya kuunganisha huduma za kifedha za kidijitali na mahitaji halisi ya wakulima, ili kuongeza ufanisi, kurahisisha malipo na kuimarisha shughuli za vyama vya ushirika.
“Hatuangalii malipo pekee. Tunataka mkulima aione Mixx by Yas kama mshirika anayekuwa naye kuanzia shambani, katika ukusanyaji wa mazao hadi anapopokea malipo yake. Huu ni mchango wetu katika kujenga kilimo chenye tija, vyama vya ushirika imara na uchumi wa kidijitali unaomfikia mkulima moja kwa moja,” alisema.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa TDCU, TARECU na Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Wakulima (AMCOS), huku makabidhiano yakiongozwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga, Bi. Enikia Wilfred.
Kwa upande wake, Bi. Wilfred aliipongeza Mixx by Yas kwa kuendelea kushirikiana na vyama vya ushirika na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha sekta hiyo.
“Tunapongeza Mixx by Yas kwa ushirikiano huu. Vitendea kazi vilivyotolewa kupitia kampeni ya Vuna na Mixx vitasaidia vyama vyetu kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na usafirishaji wa mazao na maziwa, na hatimaye kuongeza tija na kipato kwa wakulima,” alisema Bi. Wilfred.
Hatua hiyo inaendelea kuonyesha nafasi ya teknolojia na huduma za kifedha za kidijitali katika kusaidia shughuli za kilimo, kuimarisha vyama vya ushirika na kuongeza ufanisi katika mnyororo wa thamani wa mazao nchini.
Endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari na uchambuzi zaidi kuhusu biashara, benki, fedha, teknolojia na maendeleo ya sekta mbalimbali nchini Tanzania
ABSA BANK TANZANIA REAFFIRMS COMMITMENT TO WOMEN IN TECHNOLOGY AT GIRLCODE HACKATHON 2026





Sunday, September 27, 2026
KASI kubwa ya mabadiliko ya teknolojia inaendelea kuongeza chachu katika sekta mbalimbali za uzalishaji na biashara,
Wadau mbalimbali wanasema kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia, hususan akili mnemba (AI), zinachochea uzalishaji wa bidhaa zinazoleta suluhisho na kukidhi matarajio yanayobadilika ya watumiaji, hivyo kufanya uhitaji wa kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia kuwa muhimu kwa kampuni zinazotaka kuendelea kuwa na nafasi katika soko.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji, alisema biashara zitakazoshindwa kuendana na maendeleo ya kiteknolojia zinaweza kuachwa nyuma, kutokana na ubunifu kuendelea kuwa na nafasi kubwa katika uuzaji, usambazaji na uundaji wa bidhaa.
“Wakati maendeleo na mabadiliko ya teknolojia yakiendelea kushika kasi, matumizi yake yanazidi kuchochewa hususani kwenye maeneo ya uzalishaji na endapo kama kuna biashara ambazo haziko tayari kukabiliana na haya mabadiliko, zitaachwa mbali sana,” alisema Fatema kwenye hafla ya mashirikiano baina ya MeTL group na Haier Tanzania yaliyofanyika wikiendi hii.

Ushirikiano huo unakuja wakati ushindani katika soko la vifaa vya matumizi ya nyumbani ukizidi kutegemea uwezo wa biashara kuunganisha ubunifu wa kiteknolojia na ubora wa bidhaa ili kutimiza mahitaji ya walaji.
Hata hivyo, aligusian juu ya mitazamo ya watu kuhusu AI ambapo wengi wanaitazama kama ni tishio kwenye soko la ajira ambapo alisema licha ya nguvu yake, bado ubunifu na mawazo ya binadamu vitaendelea kuwa muhimu hata wakati biashara zikiongeza matumizi ya teknolojia mpya.
“Teknolojia hii haiwezi kuchukua nafasi ya mawazo au watu wenye ubunifu na fikra,” alisema, akiongeza kuwa inaweza badala yake kuwasaidia wafanyakazi, wakiwemo wanaohusika katika uzalishaji.
Kwa upande wake, Meneja wa Haier-Tanzania, Liu Chi, alisema soko la vifaa vya matumizi ya nyumbani hapa nchini linaendelea kubadilika, ambapo watumiaji wengi sasa wanaangalia zaidi ubora wa bidhaa, hivyo kama kampuni zinawajibu wa kuhakikisha zinazalisha bidhaa zenye tija ili kufikia mahitaji ya walaji.
Wednesday, September 23, 2026
ABSA REAFFIRMS LONG-TERM COMMITMENT TO TANZANIA AS SITOYO LOPOKOIYIT HIGHLIGHTS GROWTH POTENTIAL


Thursday, September 17, 2026
KCB BANK TANZANIA LAUNCHES ZED 360 DIGITAL SYSTEM TO STREAMLINE SCHOOL FEE COLLECTION













Tuesday, September 8, 2026
WHY AFRICA IS EMERGING AS A STRATEGIC GLOBAL CONNECTOR?
Friday, September 4, 2026
OTR STAFF RECEIVE TRAINING ON QUALITY MANAGEMENT SYSTEM

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Thursday, September 3, 2026
VODACOM CUTS CARBON EMISSIONS BY 24% AS NETWORK MODERNISATION REACHES 27.7 MILLION CUSTOMERS



Wednesday, September 2, 2026
OTR, ANGLOGOLD ASHANTI SEEK STRONGER LONG-TERM PARTNERSHIP

.jpeg)


Saturday, August 29, 2026
TANZANIA U-19 WOMEN’S CRICKET TEAM TARGETS WORLD CUP TICKET AS AFRICA QUALIFIER BEGINS

Saturday, August 22, 2026
DKT. YONAZI AWAKUMBUSHA VIJANA KULINDA AFYA ZAO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

















