Meneja masoko wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi. Sophia Mang’enya (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya sita kwa njia ya simu Baraka Barazae mkazi wa Dar es Salaam ambaye amejishindia pikipiki na Robert Keraryo mkazi wa Butiama ambaye amejishindia simu janja. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bi. Pendo Mfulu.
Washindi wa Droo ya sita ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Baraka Barazae mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam na mshindi wa simu Robert Keraryo Mkazi wa Butiama mkoani Kagera.
Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Masoko ya taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi Sophia Mang'enya ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.
Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma za kifedha popote alipo, hilo ndio lengo kuu la kuanzishwa kwa Y9 microfinance".
Aligusia kuwepo kwa wimbi kubwa matapeli wa mtandaoni na amewasihi wateja wa Y9 microfinance kuwa makini na wizi huo wa mitandaoni, amewasihi watanzania kuitumia Tehama kwa maendeleo sio kutumia Tehama kufanya uhalifu.
Alieleza namna ya kushiriki ni rahisi hakikisha umepakua app ya Y9 microfinance kisha kujisajili na kuanza kukopa na moja kwa moja utaingia kwenye droo hii baada ya marejesho.
Kwa upande wake afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Pendo Mfulu ameeleza "kama bodi ya michezo ya kubahatisha nchini tumeridhishwa na namna ya uchezeshwaji wa droo hii na upatikanaji wa washindi.
0 comments:
Post a Comment