Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maximillian Iranghe.
Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel.
Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha Dkt. Christina Ngereza.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara Dkt.Noelia Myonga.
Mdau wa maendeleo hapa nchini Dkt.John Lucian anatarajiwa kuwepo kwenye kongamano hilo.
Wasanii kutoka Cultural Arts Center Makumira University ni miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani kwenye kongamano hilo.
Wasanii kutoka Cultural Arts Center Makumira University ni miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani kwenye kongamano hilo.
Na Dotto Mwaibale, Arusha | MSTAHIKI Meya wa jiji la Arusha Maximillian Iranghe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Fursa katika Sekta ya Muziki na Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru ambayo yameandaliwa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha kwa kushirikiana na Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO).
Kongamano hilo litakuwa la siku tatu na kufanyika katika makumbusho ya Taifa ya Elimu Viumbe Arusha kuanzia Desemba 7, 2021 hadi Desemba 9, 2021.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwa wanamuziki wataimba nyimbo mbalimbali za zamani na za sasa uliotumika katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru ambao ulichangia kuhamasisha maendeleo.
Alisema Mstahiki Meya amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo ambalo baadhi ya watu maarufu kutoka ndani na nje ya jiji la Arusha wamealikwa.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Elimu Viumbe Arusha Dkt. Christina Ngereza alisema wameandaa kongamano hilo ili kutoa elimu na fursa mbalimbali zilizopo katika urithi wa muziki wa Tanzania ambao umebadilika sana katika miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania.
Mlezi wa TAMUFO Dkt. Frank Richard alitaja fursa zitakazo patikana siku hiyo kuwa ni kutolewa Bima ya Afya NHIF kwa gharama nafuu kwa ajili ya vipimo na matibabu kwa wanamuziki ambavyo vitatolewa kwenye Hospitali za Serikali na za binafsi.
Alisema kutakuwa na fursa lukuki kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na fursa za kibenki na nyingine nyingi.
Richard alisema Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na COSOTA watakuwepo kutoa elimu na usajili wa wanamuziki.
Joel alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali wa muziki kufika kwenye kongamano hilo na kuwa huduma ya chakula na vinywaji itapatika kwa gharama nafuu.
Wadau wengine walioalikwa kwenye kongamano hilo ni pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara Dkt.Noelia Myonga na mdau wa maendeleo hapa nchini Dkt.John Lucian.
0 comments:
Post a Comment