Meneja Masoko Airtel Tanzania Aneth Muga akitoa Maelezo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa blog mbalimbali kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’
Airtel yafanyia kazi changamoto za watanzania.
Ikiwa na lengo lakurahisisha mawasiliano kwa watanzania kote nchini.
Moja ya makampuni ya mawasiliano yanayokuwa kwa kasi zaidi nchini, Airtel imesema kwamba itaendelea kutoa huduma zake kwa wateja wake kwa ubora zaidi na kwa bei nafuu
Akiongea na waandishi wa habari za mitandaoni (Blogers) Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kwamba maboresho ya vifurushi vya intaneti vimefanywa ili kukidhi hali ya kiuchumi na mahitaji ya watanzania.
Tumeamua kuongeza kiwango cha Baadhi ya GB mara mbili ya kile tulichokuwa tukitoa mwanzo kwa bei ile ile ili kumuwezesha mtanzania kufurahia thamani ya pesa yake alisema Mmbando.
aliongeza kwakusema kwamba kwa mara ya kwanza kampuni hiyo imekuja na kifurushi cha shilingi mia mbili (200)Kifurushi hiki kinamwezesha mteja wetu kupata MB 40.
kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Anethy Muga, alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bando za gharama nafuu na kabambe za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”
0 comments:
Post a Comment