A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, August 13, 2020

NBC yasaidia ujenzi wa madarasa shule ya Kizimkazi mjini Unguja

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (katikati), akiwasalimia baadhi ya maofisa wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), katika hafla ambayo NBC ilimkabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shs 29,200,000 kumalizia ujenzi wa madarasa manne ya Shule ya Awali ya Kizimkazi Mkunguni katika hafla iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi, jana, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar. Kutoka kushoto ni, Mkuu wa Huduma za Kibenki Kitengo cha Kiislamu wa NBC Zanzibar, Mohamed Nuh, Meneja Mahusiano  Serikalini wa NBC Tanzania, William Kallaghe, Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar, Ramadhani Lesso na Ofisa Mauzo, Mussa Waziri.  
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia), amkimsikiliza Meneja Mahusiano Serikalini wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), William Kallaghe baada ya kupokea msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shs 29,200,000 vilivyotolewa na NBC kumalizia ujenzi wa madarasa manne ya Shule ya Awali ya Kizimkazi Mkunguni katika hafla iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi, jana, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar. Kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar,Ramadhani Lesso na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki za Kiislamu wa benki hiyo Tawi la Zanzibar, Mohamed Nuh.   
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (katikati), akipokea moja ya vifaa vya ujenzi kutoka kwa Meneja Mahusiano Serikalini wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), William Kallaghe (wa tatu kushoto), vyenye thamani ya shs 29,200,000 vilivyotolewa na benki hiyo kumalizia ujenzi wa madarasa manne ya Shule ya Awali ya Kizimkazi Mkunguni katika hafla iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi, jana, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar. Kutoka kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar, Ramadhani Lesso na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki za Kiislamu katika tawi hilo,  Mohamed Nuh.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (katikati), akipokea shukurani maalumu kutoka NBC kupitia kwa kwa Meneja Mahusiano Serikalini wa Benki hiyo, William Kallaghe mara baada ya kupokea msaada wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shs 29,200,000 vilivyotolewa na benki hiyo kusaidia ujenzi wa madarasa manne ya Shule ya Awali ya Kizimkazi Mkunguni katika hafla iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi, jana, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar. Wanaongfalia kushoto ni Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar, Ramadhani Lesso na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki za Kiislamu katika tawi hilo,  Mohamed Nuh.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive