Wakandarasi wa Kampuni za CHICCO Engineering na Nyanza Road Work leo wamekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam kwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae ameagiza kukamatwa kwa wakandarasi hao kwa kosa la Kushindwa kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Mto Ng'ombe na Barabara ya Kivule kwa wakati na kuleta usumbufu Mkubwa kwa wananchi ukiwemo wa Mafuriko, Nyumba Kubomoka, Uharibifu wa Mali, Ajali na Magari kuharibika huku wakandarasi hao wakila Maisha mitaani.
Kwa mujibu wa RC Makonda Mkandarasi wa Kampuni ya CHICCO amekamatwa kwa kushindwa kuanza Mradi wa ujenzi wa Mto Ng'ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ambapo licha ya Kusaini Mkataba Mkandarasi huyo hajaanza kazi kwa zaidi ya Miezi minne na hadi sasa amelipwa zaidi ya Shilingi Bilioni 4.8 huku wananchi wakiteseka na kero ya Mafuriko.
RC Makonda amesema jambo hilo ni uzembe na hujuma inayoweza kuchonganisha Wananchi na Serikali yao ambayo tayari imetoa fedha za ujenzi wa Mto huo ili kuwaondolea kero lakini Mkandarasi amekuwa akisuasua kuanza kazi.
Kwa upande wa Kampuni ya Nyanza RC Makonda ameagizwa kukamatwa kwa Mkandarasi huyo kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kivule na Daraja licha ya Kupokea fedha zaidi ya Shilingi Milioni 800 jambo linalopelekea wakazi wa Kivule kuteseka na kero ya ubovu wa Barabara na wakati mwingine kusababisha Ajali na Kuharibika kwa Vyombo vya usafiri.
Kwa Maelekezo ya RC Makonda Wakandarasi hao waliokamatwa watakuwa Wakilala Polisi Central na asubuhi watatokea polisi kwenda kufanya kazi ya Ujenzi hadi hapo atakapojiridhisha kuwa kazi inaenda vizuri huku akieleza kuwa zoezi hilo la ukamataji litakuwa endelevu kwa Wakandarasi wote wanaokwamisha miradi ya serikali.
0 comments:
Post a Comment